Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mawazo finyu hayo, Mkishamaliza na hao unaowaita Watanganyika haitachukua muda, mtaanza muunguja na mpemba, na kwa wale mliokwisha bahatika kuishi unguja na pemba, Waunguja wanaaamini mpemba hawezi watawala hakuna mpepmba anaweza kuwa rais, wapemba wanaamini waunguja wamewaonea kwa miaka mingi, na ilikhali chakula na karafuu nyingi inatoka pemba, Wazanzibari Muungano ndo unawafanya mjiite Zanzibar Bila huu muungano hakuna na wala halitakuwepo taifa la watu wa Zanzibar, TIME WILL TELL

Sema basi umetoa quote kutoka kwa genius wako "Nyerere" the failure na mbaguzi to the maximum ..aagh..umekariri..sasa kama watagawanyika wewe unalalamika nini si waache kahudumia watu wako huko musoma wasio na maji..zenj inakuhusu nini unajidai uko concern sana nao!
 
Narrow mind,

Tatizo lako unafikiria leo tu hufikirii na kesho nimeargue kwa sababu nimeshakaa Pemba na Unguja,watu wenyewe nawajua nakutokana na hilo muungano ukivunjika hilo ndo litakalo tokea, Hakuna ubishi kwenye hilo. Na yote Nyerere aliyowatendea leo unajitokeza wazi wazi kumtukana, kwahapo naona kama unajitakia laana itakayokuangamiza wewe na hayo mambo ya kipuuzi unayoyatetea, shame on you
 
Kwani Jamhuri ya Muugano ya Tanzania maanake nini,jamani acheni ulevi wa kisiasa watakao imia ni wenzangu mimi akina pangu pakavu na si Maalimu Seifu wala Karume,hivi fikirieni enyi watu muungano ukivunjika ni ipande upi utapata hasara,kwanza nina hakika Upemba na Uunguja utarudi na pia tabaka fulani kujiona bora kuliko lingine kutajitokeza na sijui ndugu zangu kutoka Zanzibar waliofurika bara sijui kama wataweza kuishi na kufanya biashara zao huko kisiwani kwani sio siri Zanzibar ina wabara wachache wanaoishi na kufanyabiashara Zanzibar kulinganisha na watu kutoka Zanzibar walivywengi hapa bara.Na mwisho hizo bakora mlizoziona You tube wa kulaumiwa si watu wa bara bali ni Maalimu na Karume wake,kwani walishindwa nini kupatana wakati huo na sasa waweze.Alamsiki uchezeeni huu muungano lakini mtakuja ukumbuka na pia hatutakuwa tayari watu wa bara kupokea tena wakimbizi mkishajitenga
 
Ha ha ha

Ni vizuri ungesema ni qoute kwa nyerere kuliko kujidai ni mawazo yako hii ndiyo hoja yangu

Kuhusu kupata laana kwasababu ya hicho kibaguz chenu utaomba mpaka mwisho wa dunia ..alipofariki milango ya neema ilikuja Tanzania ikiwemo mimi amelaaniwa hicho kibabu chenu...kwasababu ya ubaguzi wake..shame on you
 
Kwani Jamhuri ya Muugano ya Tanzania maanake nini,jamani acheni ulevi wa kisiasa watakao imia ni wenzangu mimi akina pangu pakavu na si Maalimu Seifu wala Karume,hivi fikirieni enyi watu muungano ukivunjika ni ipande upi utapata hasara,kwanza nina hakika Upemba na Uunguja utarudi na pia tabaka fulani kujiona bora kuliko lingine kutajitokeza na sijui ndugu zangu kutoka Zanzibar waliofurika bara sijui kama wataweza kuishi na kufanya biashara zao huko kisiwani kwani sio siri Zanzibar ina wabara wachache wanaoishi na kufanyabiashara Zanzibar kulinganisha na watu kutoka Zanzibar walivywengi hapa bara.Na mwisho hizo bakora mlizoziona You tube wa kulaumiwa si watu wa bara bali ni Maalimu na Karume wake,kwani walishindwa nini kupatana wakati huo na sasa waweze.Alamsiki uchezeeni huu muungano lakini mtakuja ukumbuka na pia hatutakuwa tayari watu wa bara kupokea tena wakimbizi mkishajitenga

Sasa upemba na uunguja utarudi hanakuhusu nini? wewe si waache wenyewe waamue

Au wewe ndio utaenda kupandikiza huo upemba na uunguja aagh! watu wengine bana

Shughulikeni na watu tabora, ruvuma etc njaa na barabara hakuna huko pemba na uunguja ni pilipili....
 
point chief - baada ya kufikiria mafuriko huko kilosa watu wanazama na maji nyie wote masikio juu eti Rais karume kateta nini na Maalim, kwani hamkujua wale ni ndugu? na ndiyo maana wakaitana wawili tu - na walichoongea bado hamtakijua.

Watu wengine na heshima zao eti kukurupuka katiba katiba - we katiba ya zanzibar inakuhusu? oooo muungano - kwa hiyo mkiungana hadi uvunguni unaingia? kwa taarifa yenu zanzibar ni jamhuri na ndiyo maana ina Rais wake, ule siyo mkoa kama singida ndugu zangu.

Walivyokufa mwaka 1995, 2000 sijaona mtu anaandamana kulaani vifo watu mkabakia kwenye TV zenu tu mnajifanya mna manjonzi, wangekufa shangazi zenu leo hii na nyie mngesaport maridhiano haya...

acheni acheni wafikie maridhiano - mtalaaniwa mkiingilia suala hili, na dhambi hiyo itawatafuna.

Ni wale tu wasio na uwelewa wa kawaida ndiyo wanapinga kitu hiki - nina wasiwasi na uwezo wa kufikiria wa watu wengi.
 
Na Salim Said Salim

KWA kawaida binaadamu yoyote yule mwenye akili timamu huwa hapendi kupoteza kiungo chake chochote kile, iwe cha mguu au mkono. Lakini hufika wakati mtu huyo huyo huridhia kwa tabasamu na kusisitiza kiungo chake kimoja kinachomsumbua kikatwe haraka.

Wakati mwingine mtu huyo anakuwa tayari kiungo hicho kikatwe hata kama hapana sindano ya ganzi, kama kufanya hivyo kutamsaidia kunusuru maisha yake ambayo yapo hatarini.

Ni kutokana na hali kama hii ndio wazee wetu wakasema na kutunasihi kwamba baadhi ya wakati “Lisilo budi hutendwa”.

Hivi sasa pamezuka jambo baada ya kusikika kauli za kutaka uchaguzi wa Zanzibar uliopangwa kufanyika Oktoba, usogezwe mbele ili kujenga mazingira sio tu ya kuwa na uchaguzi huru na wa haki, bali wa amani ya kweli na utaokuwa hauna mauaji, watu kupigwa mapanga na nondo na kuwa vilema.

Wengine wengi katika chaguzi ziliopita za vyama vingi walibakwa, nyumba zao ziliporwa na wengine walilazimika kukimbia nyumba zao na kuishi msituni au kwenda nje ya nchi kuwa wakimbizi na wengine hivi leo wapo Somalia kwa vile wanaona huko kuna afadhali kwao kuliko waliyoyashuhudia visiwani.

Hakuna mtu aliyefikishwa mahakamani kwa kuhusika na orodha ya maovu yote haya. Sijui mambo kama haya yangefanyika Kisarawe, Mzee Pius Msekwa angelisemaje.

Baada ya kikao cha kihistoria cha miezi miwili iliyopita kati ya Rais Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, watu wa Zanzibar wameanza kupumua na kuona ipo kheri usoni. Hata hivyo, wapo pia walionuna.

Ni kwa kutaka hali hii ya amani iendelee na pajengeke mazingira yatakayoyafanya yaliopita kuwa sehemu ya historia na sio kurudiwa baadhi ya watu, hasa kutoka bara, nasisitiza kutoka bara, wanaoonekana hawapendi na wamekasirishwa na kuwa watetezi wakubwa wa Katiba ya Zanzibar.

Sijui watu hawa walikuwa wapi na kushindwa kutetea Katiba pale suala la mafuta lilipoingizwa katika orodha ya mambo ya Muungano bila ya ridhaa ya Zanzibar na hatukuwaona kutetea maslahi ya Zanzibar na watu wake?

Kichekesho ni kwamba aliyekuwa Spika wa Bunge, Pius Msekwa, na sasa Makamu Mwenyekiti wa CCM alikuwa kimya wakati mabadiliko mengi ya Katiba yalipofanywa akiwa Spika, lakini leo ndio kawa mtetezi mkubwa wa kutaka Katiba ya Zanzibar iheshimiwe na isirekebishwe wakati alikuwa kimya Katiba ya Muungano ilipoongezwa kiraka kimoja baada ya chengine.

Zipo hisia hapa Zanzibar kuwa labda Msekwa na wengine kama yeye wangelielewa uchungu wa mauaji kama waliouawa na kuwa vilema ni watu wa kisiwa cha Kisarawe na sio Pemba.

Baadhi ya waandishi wa habari wa Dar es Salaam ambao hata Zanzibar hawajafika na kuona harakati za uchaguzi ambapo watu kutoka Bunju, Kawe, Bagamoyo huja kupiga kura wamekuwa wataalamu wa masuala ya Zanzibar.

Ni vyema wakaelewa wanapaswa kufahamu kilichotokea kinachoendelea na kinachopangwa kutokea visiwani kabla hawajawa na ujabari wa kuzungumzia habari za Zanzibar.

Ukweli ni kwamba mazingira ya kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu ni machafu na ya hatari. Zaidi ya nusu ya watu wenye haki ya kupiga kura wamenyimwa haki hio, hasa katika sehemu ambazo ni ngome za chama cha CUF, kama Mji Mkongwe, ingawa takwimu zinaonyesha ni zaidi ya asilimia 90 ya wapiga kura wameandikishwa.

Takwimu za Tume ya Uchaguzi hazitoi sura yoyote ile isipokuwa kuonyesha namna uwongo unavyoshadidiwa ili ukubalike kuwa kweli. Kama Tume ya Taifa Uchaguzi Zanzibar (ZEC), inasema kweli, basi ingeacha kuendesha shughuli zake kwa siri na kuliweka hadharani daftari la wapiga kura ili wale walioandikishwa zaidi ya mara moja wakaeleweka.

Huu mchezo mchafu wa maelfu ya watu kunyimwa haki ya kupiga kura, ndio unaoleta wasi wasi juu ya uchaguzi ujao.

Zipo taarifa za kuandaliwa kambi za vijana wanaoitwa Janjaweed na maeneo yanayotajwa kuwepo kambi hizi ni kama Tungu na Pangatupu, Unguja.

Waliofanya vijana hawa katika chaguzi ziliopita na Jeshi la Polisi kuonekana halikuwa na habari za matukio ya watu kupigwa mapanga na nondo katika vituo vya uchaguzi.

Matukio kama haya, kutokana na mazingra yaliopo yanaonekana kutaka kurejewa katika uchaguzi ujao. Hii ni hatari ambayo akina Msekwa wanafaa waione na waelewe kuwa maisha ya watu wa visiwani nayo yana thamani kama ya ndugu zao wa bara.

Kwa ufupi hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi ujao Zanzibar ni mbaya na inatisha, lakini inaoenkana baadhi ya wakubwa bara huenda wakawa wanafurahia vurugu hizi zilizoshuhudiwa Zanzibar.

Kama wanawapenda ndugu zao wa Zanzibar kwa nini wasifurahie maelewano haya na kuona amani ni muhimu kuliko uchaguzi?

Linalonishangaza ni kuwa kinachojadiliwa ni Katiba ya Zanzibar na sio ya Muungano. Kwa maana nyingine hili ni suala la Wazanzibari na sio la bara au Muungano. Au tunataka kuambiwa Wazanzibari hawana haki ya kujiamulia mustakbali wao au Zanzibar ni mali ya CCM na sio ya wananchi wake?

Wazanzibari wamekuwa wakijizuia kujadili kasheshe za Richmond, EPA na nyingine kwa vile masuala haya hayamo katika orodha ya Mambo ya Muungano.

Sijuwi wapi baadhi ya viongozi wa bara wamepata ujabari wa kutaka kuwaamulia watu wa Zanzibar mambo yao. Labda walitakiwa ushauri na kama ni hivyo ni nani hao waliowapa kazi hiyo?

Ninachowasihi ndugu zangu wa bara waliachie suala hili liamuliwe na Wazanzibari ambao wamechoshwa na mauaji na kuona askari wanaletwa kwa mamia kutoka bara wakati wa uchaguzi.

Ni kweli katiba haifai kuchezewa, japokuwa Katiba ya Muungano ina historia ndefu ya kuchezewa na ndio maana sasa imejaa viraka. Lakini inaonekana kutaka kubadili Katiba ya Zanzibar ndio nongwa. Maajabu haya.

Hili ni suala la Zanzibar na kinachotaka kufanywa na Wanzibari na lile niliolieleza kama lisilo budi hutendwa, kama kukubali mtu kukatwa kiungo ili anusuru maisha yake.

Lakini pia tukumbuke mtu ambaye hajala pili pili hastahiki kudai inamuwasha, yaani pilipili usioila wewe inakuwashiani? Katiba ya Zanzibar haiwahusu watu wa bara sasa kwa nini hawawaachii watu wa Zanzibar kuamua wanachotaka au hawana haki hiyo?

Kama viongozi wa Bara walishindwa kuwasaidia watu wa Zanzibar kuelewana walipokuwa wanakwaruzana sasa wasifunge njuga kuwarejesha walipotoka. Wanaokufa ni watu wa visiwa vya Unguja na Pemba na sio Mafia au Kisarawe na wanaopata vilema ni watu wa Mji Mkongwe na sio Nguvumali, Tanga.

Suala la kama Rais Karume aongezewe muda ili astawishe mazingira ya amani au la, waachiwe Wazanzibari kuamua na wenye haki kwa niaba ya watu wa visiwani kulifanyia maamuzi ni Baraza la Wawakilishi na sio Msekwa, Makamba na wenzake au Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Katiba ya Zanzibar ni ya Wanzibari wenyewe na tuiachie ibaki hivyo kwa maslahi ya Zanzibar na ya Muungano. Tuache dhana potofu ya kusema Wazanzibari wanapotaka umoja basi lengo lao kuu ni kuvunja Muungano. Hii ni hoja ya kipuuzi.

Kama Wazanzibari hawataki Muungano hawataona taabu kueleza hivyo na mara kadhaa walipokerwa walitamka hivyo. Hakuna anayeogopa kusema hivyo.

Hata Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati mzee Abeid Amani Karume, aliweka wazi kwamba Muungano ni kama koti. Ukiona linakubana sana na huwezi tena kulivaa, unalivua na kutafuta jengine.

Sio vizuri kuburuzana na kutishana.

Kama Wazanzibari wanafanya makosa kwa kutafuta maelewano, kuachana na siasa za chuki na uhasama na kuwa na mshikamanao waachieni wafanye hivyo.

Kama wanakosea huko usoni watakuja kujuta wenyewe na historia itawahukumu kwa kosa hilo. Kama wanayoyafanya yana maslahi na wao na vizazi vijavyo historia itatuonyesha siku za mbele.

Lakni jambo lingine la kuzingatia ni kwamba kinachoonekana Zanzibar sasa ni historia kujirudia. Katika mwaka 1964 mzee Abeida Karume na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nerere, walifanya mazungumzo wao wawili na kuunganisha Zanzibar na Tanganya na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivi sasa mwanawe, Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad, wamekutana watu wawili kwa lengo la kuwaunganisha Wazanzibari. Sasa kwa nini mkutano wa watu hawa wawili uwe nongwa?

Vile vile, baadhi ya viongozi wa Serikali ya Zanzibar na ya Muungano wanataka Baraza la Wawakilishi lisifanye uamuzi wowote wa masuala ya Katiba na badala yake waachiwe wananchi kuamua.

Hapa tujiulize kazi ya Baraza ni ipi na kama ni wananchi kuamua mbona mambo mazito huamuliwa bila ya wao kushirikishwa moja kwa moja?

Mungu inusuru Zanzibar na watu wake na iwakinge na wale wasioitakia mema na iwabariki wote wanaoitakia kheri.
 
Ukishasema Zanzibar itakuwa vipi Tanzania?

Kijana MrFroasty, Tanzania kirefu chake ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (United Republic of Tanganyika and Zanzibar). Jina Tanzania lilipatikana baada ya mchakato uliohusisha mapendekezo mengi tu yalitolewa na wadau mbali mbali. Hata hivyo majina matatu yaliweza kupita katika hatua za awali na kubaki matatu yaliyoonekana kupendwa zaidi, nayo ni Tanzan, Tangibar, na Tanzania. TanganyikaZanzibaria iliweza kuyapiku majina mengine kwa vile ilishabihiana na lugha zetu za Kibantu na rahisi kutamkika. Hivyo huwezi kuwa na Tanzania bila Tanganyika kama vile usivyoweza kuwa na Tanzania bila Zanzibar. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania kama vile Tanganyika ilivyo sehemu ya Tanzania ila Zanzibar ilipewa upendeleo maalumu wa semi-autonomy kwa sababu ya udogo wake (eneo pamoja na watu).

Mungu inusuru Zanzibar na watu wake na iwakinge na wale wasioitakia mema na iwabariki wote wanaoitakia kheri.

Mungu inusuru Tanzania na watu wake na uwakinge na wale wote wanaoitazama kwa macho ya husuda na, kwa kuwatumia watu kama MrFroasty, wanataka kuisambaratisha.
 
Ndugu mleta hoja,
Ulichoongea kina 95% ya ukweli na bila shaka wewe kama Mzanzibar una kila sababu ya kupata uchungu.

- Nyie kama vijana wa kizanzibar mna kila sababu ya kuoneshwa mikataba iliyokuwepo ama iliyowekwa mpaka kutokea muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hilo lingeweza kusaidia sana katika kupata ukweli.

Mimi ni kijana wa Tanzania Bara na bila kuficha naona wazi kwamba muungano uliopo una kasoro, hivyo ilikuwa ni busara na hekima kuzishughulikia kasoro hizo ili kuimalisha muungano na wala si vyema kuvunja muungano.

Dunia ya leo mataifa yanaungana ili kuwa na nguvu. Sisi kama watanzania bara na visiwani hatuna sababu ya kuvunja muungano, tuna kila sababu ya kuuimarisha muungano ila tuzishughulikie kasoro zilizopo ndani ya muungano bila ya kuchelewa wala kuona woga kwa lengo la kuepusha machafuko huko mbeleni.
Mimi kama kijana wa Tanzania Bara siwezi kuruhusiwa kununua ardhi na kujenga Zanzibar, lakini wazanzibar wanaruhusiwa kununua ardhi na kujenga Tanzania Bara. Hapa naona wazi kwamba hii si haki hata kidogo. Huo ni mfano mdogo tu wa kasoro za muungano wetu.

Ni muhimu kushughulikia kasoro zilizopo haraka kadri iwezekanavyo.
Suala la ardhi ya Zanzibar ni logics, watanganyika mukiachiwa mununue ardhi Zanzibar ni sawa na kusema unauza nchi...muna uwezo wa kuvinunua visiwa vyote 😀

Mbona Kenya na nchi zengine haziunganishwi...acha mizengwe hiyo, uvunjwe tuu huu muungano hewa...haurekebishiki!
 
Dunia inaungana na kusonga mbele kuelekea kua kijiji kimoja kiukweli, sisi tunazungumzia kutengana ili turudi nyuma..haha this is soo funny.
MY VIEWS NI KWAMBA KWELI DUNIA INABADILIKA NA MAHITAJI YANAONGEZEKA HUSUSANI TOKANA NA MAENDELEO YA TECNOLOGY DUNIANI NA VIJANA TUNAMITIZAMO MINGI NA ITIKADI TOFAUTI NA WAASISI WETU WA MUUNGANO HIVYO POINT YANGU NI KWAMBA NINGEPENDA SANA SERIKALI YA MUUNGANO ITOE NAFASI YA KUPATA MAWAZO HUSUSANI TOKA KWA VIJANA WA VISIWANI NA BARA YA JINSI YA KUUBORESHA HUU MUUNGANO NA SIO KUUVUNJA ILI KUTOA MAJIBU YENYE TIJA KWA JAMII YA WATANZANIA WOTE....DHUMUNI KUU LA MWANADAMU KUZALIWA NI ILI AISHI SALAMA NA KWA MATUMAINI YA BADAAYE NA AMANI HIVYO INATUPASA KUJENGA MUUNGANO UNAOENDANA NA WAKATI NA UTAKAOTUFANYA SOTE TUISHI KWA KIWANGO KINACHOENDANA NA UTILIZATION ZA MALIASILI TULIZONAZO PAMOJA NA MAZINGIRA YETU..VIPENGERE VYA MKATABA WA MUUNGANO WA KARNE YA 20 SI VYOTE VITAKUA BADO APPLICABLE KWA KARNE YA 21....
NOTE: VIONGOZI WETU SISI WANANCHI WENU NI BINADAMU SAWA KABISA NA NYIE NA TUNAHITAJI MAISHA BORA KAMA MYAPAYO NYIE HIVYO TUNACHOKITAKA KUKIONA SIO SIASA ZISIZOKUA NA TIJA BALI NI VITENDO VYENYE KUTULETEA MAISHA BORA KULINGANA NA UTAJILI WA MALIASILI ZETU..SIKILIZENI SAUTI ZETU NA FANYENI KAZI KWA MANUFAA YA JAMII NZIMA NA SIO KUANGALIA MASLAHI YENU AS IF NCHI NI PRIVATE COMPANY YA KUNDI LA WATU FULANI.....
 
Kijana MrFroasty, Tanzania kirefu chake ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (United Republic of Tanganyika and Zanzibar). Jina Tanzania lilipatikana baada ya mchakato uliohusisha mapendekezo mengi tu yalitolewa na wadau mbali mbali. Hata hivyo majina matatu yaliweza kupita katika hatua za awali na kubaki matatu yaliyoonekana kupendwa zaidi, nayo ni Tanzan, Tangibar, na Tanzania. TanganyikaZanzibaria iliweza kuyapiku majina mengine kwa vile ilishabihiana na lugha zetu za Kibantu na rahisi kutamkika. Hivyo huwezi kuwa na Tanzania bila Tanganyika kama vile usivyoweza kuwa na Tanzania bila Zanzibar. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania kama vile Tanganyika ilivyo sehemu ya Tanzania ila Zanzibar ilipewa upendeleo maalumu wa semi-autonomy kwa sababu ya udogo wake (eneo pamoja na watu).

Mungu inusuru Tanzania na watu wake na uwakinge na wale wote wanaoitazama kwa macho ya husuda na, kwa kuwatumia watu kama MrFroasty, wanataka kuisambaratisha.

..
Hiyo Tanganyika ikowapi?.
.
MUNGU INUSURU ZANZIBAR NA MKOLONI HUYU MTANGANYIKA ANAEIJIITA TANZANIA mwenye kufurahia unapopata matatizo
 
katiba ifanye kazi kwa maslahi ya wananchi na si wananchi wafanye kazi kwa maslahi ya katiba..katiba ihudumie wananchi..kwa hiyo nawa support wanzazibar kukutaa madai ya kina msekwa na makamba (wabara) kwa kujidai kutetea katiba..huo ni wivu, ujinga na ukoloni

Kama wazanzibar wataona kuna haja ya kubadili katiba yao wafanye bila kusumbuliwa na wabara it is high kuwa wamoja na kuangalia maslahi yenu kuliko kelele za bara..ujue viongozi wa bara wanataka kufanya kama huko zenj kuna issue sana ili kuhamisha public opinion huko ..tusiongelee tena uchaguzi wa unaokuja, ufisadi, barabara etc...

Point of note: je wazanzibar wote mko pamoja! watu kama shamhuna wanatafuta ujiko na wachumia tumbo wa huko kwenu mnaweza kuwathibiti? maana hao ndio puppet wa watu bara watawagombanisha ili wapate vyeo ambavyo viko vingi ..ubalozi, ukuu wa mkoa etc..hiyo ndio challenge kubwa kuliko watu kama kina msekwa ambao wameshazeeka vibaya
 
Mimi siwaelewi kabisa Wazanzibari! CCM Zanzibar walikutana wenyewe na kuamua kwamba Karume hataongezewa muda na kwa upande wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (mseto?) walidai kwamba maamuzi ya Butiama yazingatiwe na hakuna mtu yeyote toka bara aliyehudhuria vikao hivyo wala kuwaamulia mambo yao! Na kama Wazanzibari wangeamua kwamba wangemwongezea Karume muda wa kukaa madarakani basi hakuna mtu yeyote kutoka bara ambaye angelazimisha maamuzi yao hata kama hawayapendi! Kama kuna mtu wa kulaumiwa basi ni Wazanzibari wenyewe kuhusu maamuzi waliyofanya bila kuingiliwa na mtu yeyote! Kwa kuwa Tanzania Bara imekuwa kama jalala la kutupia kila uchafu hata kama uchafu huo unastahili kutupwa kwenye jalala jingine, basi mwaka huu tutasikia mengi!
 
Ili kuinusuru Tanzania kwa sasa hivi ni lazima kuwasikiliza Wanzibar na sio CCM wanaolazimisha mambo kwa maslahi yao. Muungano ulopo una utata mwingi ambao nafikiri umefikia ukingoni sasa ni lazima tukubali ukweli, hakuwezi kuwa na muungano wa kulazimisha bila kumwaga damu. Hivyo basi kama Wanzazibar wamepata ujasiri wa kuweka mambo sawa, tuwape nafasi na sisi wabara ikibidi Tanganyika irudishwe na kuwe na Jamhuri ya Muungano inayoeleweka.

Mbona mnaogopa mabadiliko?
 
Utawaelewa vipi wakati nerve zote za fahamu umeshazifunga hutaki kuelewa?

Simple: Zanzibar for Zanzibaris, kina msekwa, JK waache wabadilishe katiba yao watakavyo..wao washughulikie richmond, buzwagi, trl etc...
 
..
Hiyo Tanganyika ikowapi?.
.
MUNGU INUSURU ZANZIBAR NA MKOLONI HUYU MTANGANYIKA ANAEIJIITA TANZANIA mwenye kufurahia unapopata matatizo

Yamekuwa hayo kuwa watanganyika ni wakoloni. Sidhani kama hayo ni mawazo ya wazanzibar. Lakini wazanzibar wanaweza kuamua kujitenga kama hizo jumuiya kubwa zaidi USSR, YUGOSLAVIA zilikwisha sembuse TANZANIA. Kama watanzania bara wamekuwa wakoloni basi wazanzibar mbona wanakosa courage yakusema muungano uvunjwe ili wapate uhuru wao.
 
Ili kuinusuru Tanzania kwa sasa hivi ni lazima kuwasikiliza Wanzibar na sio CCM wanaolazimisha mambo kwa maslahi yao. Muungano ulopo una utata mwingi ambao nafikiri umefikia ukingoni sasa ni lazima tukubali ukweli, hakuwezi kuwa na muungano wa kulazimisha bila kumwaga damu. Hivyo basi kama Wanzazibar wamepata ujasiri wa kuweka mambo sawa, tuwape nafasi na sisi wabara ikibidi Tanganyika irudishwe na kuwe na Jamhuri ya Muungano inayoeleweka.

Mbona mnaogopa mabadiliko?

Mkuu sidhani kama kuna anayeogopa mabadiliko bali wazanzibar ndiyo wanataka mabadiliko kwa kuwa huko kwao kumegundulika mafuta. Mbona kipindi kile hizi chokochoko hazikuwepo? Hawa jamaa ni wabinafsi sana.

Lakini yote heri kama wanataka usawa na uwekwe ili kila mmoja ajue mipaka yake. Hawa jamaa wamebebwa sana, lakini hawaridhiki siku hizi hata kazi hawafanyi KARAFUU iko wapi siku hizi? Wanabebwa na utalii. Wanaota mafuta tu.
 
Back
Top Bottom