Sasa ndugu yangu Makaimati, kazi yenu mbona ni rahisi? Wamobilize Wazanzibari wote mtoe waraka wa azimio lenu kwa rais wa muungano kwamba Wazanzibari wanataka waondoke kwenye muungano. Hakuna atakayewazuia kama hayo ndiyo matakwa ya majority.Sisi hatutaki tatu wala mbili wala moja.
Zanzibar irudi kwa wenyewe, mengine tutajuana baadae.
Wakuu zangu msitake kuingiza uislaam ktk maswala ya Osama na huyo Turabi kwa sababu hamjui Uislaam ni nini.. na zaidi ya hapo hamjui kwa nini Osama alikuwa mpinzani wa Marekani na vibaraka wake..Kwa maneno haya simuungi mkono Osama kwa hatua alizochukua dhidi ya Marekani na dunia kwa ujumla isipokuwa sababu za msingi ambazo yeye aliziona kuwa cheche za mageuzi aliyoyataka..
Osama kama Osama alichukia nguvu ya Marekani ktk uchumi wa Saudia na hasa jinsi shirika la mzee Bush lilivyoweza kucukua mabillioni ya fedha kama mbia wa baba yake. Ni chuki ambayo hata wewe unaweza kuwanayo kwa Barricks au shirika lolote la nje isipokuwa tofauti inaweza kuwa maamuzi yako ktk kuitekeleza hiyo chuki..
Sisi wote tunamchukia Osama na wala hakuna mtu anayefurahia hawa kina Turabi jinsi wanavyowanyanyasa waislaam wenzao chini ya utawala wa huyo Bashir, na inaongezea nguvu zaidi kumwona mwandishi wetu hapa akijisifia sana kuonana na watu kama Osama na Turabi kisha kujiweka nao kundi moja kifikra na kuelezea maswala ya Muungano wa Tanzania.
Mtu huyu ni hatari na uhatari wake hauna Uislaam isipokuwa chuki na ghadhabu kubwa walokuwa nayo hawa member wa Al qaeda kiasi kwamba ananipa mashaka makubwa zaidi kuwepo hotelini siku ambayo huyo Osama anaingia Hotel hiyo hiyo pasipo yeye kuwekewa kashaka. Ina maana moja tu ni mwenzao hivyo kwa utangulizi wake tu tayari kisha nipa shaka kubwa dhamira yake kuhusiana na Muungano na yawezekana moja ya agenda za mkutano ulompeleka Sudan ilikuwa kuzungumzia Muungano wetu.
Isije kuwa huyu ni mshirika wa mabomu yaliyolipuka ubalozi wa Marekani nchini hivyo chuki yake haikuanzia ktk swala la Muungano ila inarudi nyuma zaidi ktk mahusiano baina ya Nyerere na Qaboos..Dhahiri mwandishi anatuonyesha jinsi Uoman wake unavyoweza kuathiri Muungano wetu kutokana na chuki zake binafsi au washirika wenzake, kisha utawasikia watu wakisema hizi vuguvugu za madai ya Muungano hayana mikono ya watu wenye nia mbaya na Zanzibar..Watu kama hawa ndio wanafanya Muungano ulindwe kwa nguvu zote kwa sababu Zanzibar kwao ni koloni ambalo watajaribu kwa kila njia kuonyesha uhalali wao kulitawala..
Nitaruidia tena kwenu watu wa kitabu (Wakristu), kuhusisha Uislaam na matendo wa watu waovu ni sawa na kuhusisha Ukristu na kulawiti watoto wadogo wakati mkijua fika kwamba Ukristu na vitu hivyo havihusiani ila ni akili mbovu ya wahusika wanaotumia dini kufanya maovu yao..
Sasa ndugu yangu Makaimati, kazi yenu mbona ni rahisi? Wamobilize Wazanzibari wote mtoe waraka wa azimio lenu kwa rais wa muungano kwamba Wazanzibari wanataka waondoke kwenye muungano. Hakuna atakayewazuia kama hayo ndiyo matakwa ya majority.
Uislam wa Tanzania is not synonymous with Zanzibar. Huwezi sema lengo la kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika lilikuwa kuua uislam. That is political crap. Naamini wakati nchi hizi zinaungana, Jumla ya waislam zanzibar walikuwa si zaidi ya laki 5. At any time, Waislam walioko Bara ni wengi saaaaana kuliko wanzanzibari wote. Tatizo ni kwa wazanzibari kujipa ujiko kuwa wao ndio kitovu cha uislam afrika mashariki. So what? Je kila mzanzibari ni muislam safi kuliko waislam wote wa ujiji, upareni, na bukoba, kyela, kondoa, tabora, lindi, tunduru? Sasa utauuaje uislam wa watu laki 5 zanzibar wakati Tanganyika wako zaidi ya 13M?. Ni mawazo ya kichovu hayo uliyonayo bwana Abusahaf na Turabi wako.
Nikirejea kwenye swala zima la muungano, ninaungana na mtazamo wa Baba wa Taifa wa kuwa na serikali hizi mbili tukitazamia kuwa na serikali moja. Ila kama nyie wazenji hamtaki, basi sawa tu. Tuvunje muungano. Swala la serikali tatu linawezekana kimantiki. Lakini ukitazama mbali na kwa kutilia maanani asili yenu wazenji ya ulalamishi, muungano wa serikali tatu utakufa haraka. Nasema hivi kwasababu, kwenye muungano wa namna hiyo, nchi hizi mbili zitatakiwa kuchangia gharama kwa usawa katika serikali ya muungano. Na jinsi mlivyo wabinafsi na wabishi, kuna siku mtakataa kuchangia serikali ya muungano na ndipo huo muungano wa serikali tatu utakuwa mwisho wake.
Sisi hatutaki muungano wa moja, mbili wala tatu, tunaitaka Zanzibar yetu mlioipora na kuikalia kwa mabavu mpaka leo.
Zanzibar for Zanzibaris and we cant wait to see your backs.
View attachment 29568
Sisi hatutaki muungano wa moja, mbili wala tatu, tunaitaka Zanzibar yetu mlioipora na kuikalia kwa mabavu mpaka leo.
Zanzibar for Zanzibaris and we cant wait to see your backs.
View attachment 29568
Kumbu kumbu zangu zinaonyesha ulishawahi kuongelea serikali tatu!! Leo umebadilika ndugu yangu!!!! Tulishawahi kujadili na nikakuuliza unataka seriakli ya Tanganyika ili iweje? Kama mumebadilika na hamtaki serikali tatu ambayo sisi wengine tumeikataa kila thread(ushahidi ni maswali hapo juu ya thread yangu) ambayo hakuna anayejibu. Basi kuna njia rahisi ya kuirejesha nchi ya neema ya asali na maziwa.
Anzeni maandamano kushinikiza kuvunjwa muungano, tena muanzie hapa Dar maana ndipo mlipo wengi kuliko sehemu nyingine duniani.
Halafu sambazeni sumu znz na Uingereza mumalizie marekani.
Wakati haya yakiendelea pelekeni mswada BLW mpitishe kama mlivyofanya wimbo wa taifa, bendera, mlivyojitoa shirikisho la mpira, bandari n.k. Wakati BLW likifanya hayo, nanyi kuonyesha hasira zenu fungeni virago, acheni ajira huku bara, fungeni biashara rejeeni nyumbani.
Haya yanawezekana ndani ya mwezi mmoja. Hakika atakayewafuata huko katika nchi ya kanaani atakuwa mgonvi.
Nanren safi sana, kweli Zanzibar kuna fikra zilizotokana na BRAINWASH za kiarabu, unakuta kila mwenye kijirangi anaitwa mwarabu na kupishwa siti pa kukaa popote pale, na hao waarabu wa kweli hawakai foleni hata siku moja, kuna siku mimi nimemtoa nishai mmoja bank, znz wanamwabudu mwarabu... mara nyingine hata mweusi kama mkaa anaijiita mwaarab na ukitaka muelewane mwiite mwaarab...
Umeongelea options nne zilizopo: kubaki na Muungano kama ulivyo, kuunda serikali moja, au tatu au kuuvunja. Umesahau moja nyingine: muundo mwingine wowote ambao hatuujui bado....Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaweza tu kuokolewa endapo katiba ya Muungano itafanyiwa marekebisho ili pawepo mfumo wa serikali tatu.
Utakuwa ulilala na mpemba kitanda kimoja,
hembu jitazame vizuri maungoni mwako.
Mkuu inaamana mpemba ni mcameroon au?