Uislam wa Tanzania is not synonymous with Zanzibar. Huwezi sema lengo la kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika lilikuwa kuua uislam. That is political crap. Naamini wakati nchi hizi zinaungana, Jumla ya waislam zanzibar walikuwa si zaidi ya laki 5. At any time, Waislam walioko Bara ni wengi saaaaana kuliko wanzanzibari wote. Tatizo ni kwa wazanzibari kujipa ujiko kuwa wao ndio kitovu cha uislam afrika mashariki. So what? Je kila mzanzibari ni muislam safi kuliko waislam wote wa ujiji, upareni, na bukoba, kyela, kondoa, tabora, lindi, tunduru? Sasa utauuaje uislam wa watu laki 5 zanzibar wakati Tanganyika wako zaidi ya 13M?. Ni mawazo ya kichovu hayo uliyonayo bwana Abusahaf na Turabi wako.
Nikirejea kwenye swala zima la muungano, ninaungana na mtazamo wa Baba wa Taifa wa kuwa na serikali hizi mbili tukitazamia kuwa na serikali moja. Ila kama nyie wazenji hamtaki, basi sawa tu. Tuvunje muungano. Swala la serikali tatu linawezekana kimantiki. Lakini ukitazama mbali na kwa kutilia maanani asili yenu wazenji ya ulalamishi, muungano wa serikali tatu utakufa haraka. Nasema hivi kwasababu, kwenye muungano wa namna hiyo, nchi hizi mbili zitatakiwa kuchangia gharama kwa usawa katika serikali ya muungano. Na jinsi mlivyo wabinafsi na wabishi, kuna siku mtakataa kuchangia serikali ya muungano na ndipo huo muungano wa serikali tatu utakuwa mwisho wake.