Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekuja na pendekezo la kuunda serikali Tatu ikiwa ni njia ya kutatua kile kinachoitwa "Kero za Muungano".
Kuanzia viongozi wa serikali,chama na wananchi wa kawaida,wamekuwa wakitoa maoni yao.Wengine wanaunga mkoni pendekezo la serikali Tatu,wengine wanataka serikali moja (mfano mimi) na wengine (mfano CCM) wanataka mfumo wa serikali mbili uendelee.
Pamoja na kwamba napendekeza uwepo wa serikali moja,natambua ugumu wa suala hili.Upande wa Zanzibar hawako tayari kuwa na serikali moja,na wala hawako tayari kuendelea na mfumo wa serikali mbili.Hata mfumo wa serikali tatu,wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili.
Kimsingi,sitaki Muungano uvunjike.Lakini dalili za kuvunjika kwa Muungano zinaonekana,hata kama sio sana.
Desmund Tutu,wiki mbili zilizopita,aliwambia viongozi wa serikali ya Afrika Kusini na wananchi wote kufanya maandalizi ya msiba wa Nelson Mandela.Akaonya kwamba,sio kwamba anaombea Nelson Mandela kufariki,lakini hilo halikwepeki.Hivyo ni vema kufanya maandalizi ili kuepuka kadhia na mfadhaiko kwa Taifa.
Nami najiuliza,tumejiandaaje kuuvunja Muungano?