Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mkuu muungano ni kero nyingine inayokumbatiwa na CCM.

Watu wako tayari kujadili muungano kwa Uhuru, lakini CCM kwa matakwa yake haitaki na inalazimisha masharti kwenye mjadala kana kwamba nchi ni ya wana CCM peke yao.

Mi naamini hata ndani ya CCM watu hawataki huu muungano wa kinyonyaji.

Watanganyika wameuvumilia kwa manufaa ya wenzao wazanzibari, lakini kwa bahati mbaya anayepata upendeleo mkubwa kwenye muungano ndie mlalamikaji mkubwa.

Sasa hivi ni muda MUAFAKA muungano ujadiliwe bila shinikizo la chama tawala, Vinginevyo basi tutauvunja tuanze upya
 
a stupid man is the one who never know an old phenamenon.zanzibar came into union in 1964,before that date every thing was right in zanzibar and well known social welfare.after union no any change in zanzibar took place.realy u a stupid my pal for this and u a numb,blind and deaf.if u dont know ask your fellow who know and u fail to do that u wil continue to be more like stupid.
what do you mean everything was right?
 
Zanzibaries have their own constitution, you stupid!! We don't need to give our views on this constitutional review. Warioba get hell out of Zanzibar, its not our thing its Tanganyikans constitution. Again...we have our own constitution.
Bring Tanganyika on the table first then we can talk,....hali ndio hiyo!

You are behaving as if constitution is a god. what good has that inactive constitution of yours done so far?
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekuja na pendekezo la kuunda serikali Tatu ikiwa ni njia ya kutatua kile kinachoitwa "Kero za Muungano".

Kuanzia viongozi wa serikali,chama na wananchi wa kawaida,wamekuwa wakitoa maoni yao.Wengine wanaunga mkoni pendekezo la serikali Tatu,wengine wanataka serikali moja (mfano mimi) na wengine (mfano CCM) wanataka mfumo wa serikali mbili uendelee.

Pamoja na kwamba napendekeza uwepo wa serikali moja,natambua ugumu wa suala hili.Upande wa Zanzibar hawako tayari kuwa na serikali moja,na wala hawako tayari kuendelea na mfumo wa serikali mbili.Hata mfumo wa serikali tatu,wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Kimsingi,sitaki Muungano uvunjike.Lakini dalili za kuvunjika kwa Muungano zinaonekana,hata kama sio sana.
Desmund Tutu,wiki mbili zilizopita,aliwambia viongozi wa serikali ya Afrika Kusini na wananchi wote kufanya maandalizi ya msiba wa Nelson Mandela.Akaonya kwamba,sio kwamba anaombea Nelson Mandela kufariki,lakini hilo halikwepeki.Hivyo ni vema kufanya maandalizi ili kuepuka kadhia na mfadhaiko kwa Taifa.

Nami najiuliza,tumejiandaaje kuuvunja Muungano?
 
Habari wakuu.

Wadau,watanzania hatujawahi kupewa fursa ya kupiga kura ya maoni ili kwa ujumla wetu tuamue hatima ya muungano.Ni wazi kabisa kuwa muungano huu umejaa kero na manung'uniko mengi kutoka kwa watanzania wa pande zote mbili za muungano huu.

Hata hivyo,watawala wamekuwa wakikwepa kuwapa wananchi fursa ya kupiga kura ya maoni ili waamue kama muungano huu uendelee au uvunjwe.

Vile vile hata walioasisi muungano huu hawakuwashirikisha wananchi ili kupata maoni yao kama wanakubali au wanakataa kuanzisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwasababu hizo basi,sisi wana JF tutumie mtandao huu kueleza hisia zetu juu ya muungano huu na itasaidia kupeleka ujumbe kwa watawala ni namna gani umma wa watanzania wanavyouchukulia muungano huu.

Hivyo basi,kama unaona muungano uendelee kuwepo sema "NDIO" na kama unaona muungano usiendelee kuwepo sema "HAPANA".

NB:Hii ndio Demokrasia na inaweza kuanzia hapa JF sio lazima kuisubiri serikali ifanye kila kitu.
 
Naanza kwanza kwa kutangaza maslahi,mimi ni mtanzania kutoka bara.

Kura yangu ni HAPANA(usiendelee).
 
Uendelee ila kuwe na serikali 1 tu siyo 2 kama ilivyo sasa wala zisiwe 3 kama wanavyopendekeza wengine.
 
Habari wakuu.

Wadau,watanzania hatujawahi kupewa fursa ya kupiga kura ya maoni ili kwa ujumla wetu tuamue hatima ya muungano.Ni wazi kabisa kuwa muungano huu umejaa kero na manung'uniko mengi kutoka kwa watanzania wa pande zote mbili za muungano huu.

Hata hivyo,watawala wamekuwa wakikwepa kuwapa wananchi fursa ya kupiga kura ya maoni ili waamue kama muungano huu uendelee au uvunjwe.

Vile vile hata walioasisi muungano huu hawakuwashirikisha wananchi ili kupata maoni yao kama wanakubali au wanakataa kuanzisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwasababu hizo basi,sisi wana JF tutumie mtandao huu kueleza hisia zetu juu ya muungano huu na itasaidia kupeleka ujumbe kwa watawala ni namna gani umma wa watanzania wanavyouchukulia muungano huu.

Hivyo basi,kama unaona muungano uendelee kuwepo sema "NDIO" na kama unaona muungano usiendelee kuwepo sema "HAPANA".

NB:Hii ndio Demokrasia na inaweza kuanzia hapa JF sio lazima kuisubiri serikali ifanye kila kitu.
uvunjwe ili tuwe majirani waaminifu kama tulivyo na Kenya
 
muungano usiendeleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, wanzanzibar warudi kwao tumechoka kunyonywa na midebwedo
 
However kipindi Karume na Nyerere wanaungana Tanganyika na Zanzibar zilikua sio nchi za kidemokrasia, na kwa vile walitumia White paper! Kuendelea na muungano huu ni unafiki mkubwa!
...
Nasikitika viongozi waliopo (Kikwete na Sheni) kuendeleza Muungano kwa hoja za kitoto!!!
...
Eti kila mmoja (Kikwete na Karume) hataki Muungano uvunjike ktk utawala wake!!!!!
...
Hizi kero za Muungano kwa wananchi zimekua hazisilizwi!
...
Maoni yangu: Muungano uvunjwe na kila upande uchukue mbao zake!
Just tutashirikiana kama nchi na nchi nyengine tu!
...
Viongozi muache unafiki!
 
Huu muungano wa kihuni haukubaliki?

TANGANYIKA kwanza,muungano baadae!
 
Back
Top Bottom