Warioba aliwauliza maswali Kikwete na Pinda kwamba ni lini wameshakanyaga Zanzibar kukagua au kushiriki shughuli za kimaendeleo?Ikizingatiwa wao ni viongozi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba,hadi leo hakuna kati ya hao aliyejibu swali hilo tofauti na kuja na vioja na mipasho mipya kila siku.Kwakuwa hadi leo hawajajibu,Hivyo wao ni viongozi wa Tanganyika.Vilevile Zanzibar ina rais na viongozi wake wengine.SWALI LANGU NI JE RAIS WA TANZANIA NI NANI?.MUUNDO WA MUUNGANO:Wakati Tanzania haina Rais ila kuna rais wa tanganyika(JAKAYA M KIKWETE),CCM inatuambia tanganyika haipo bali kuna Tanzania na Zanzibar.KAMA TANGANYIKA HAIPO KWANINI TANGANYIKA INA RAIS? KAMA TANZANIA IPO,RAIS WAKE NI NANI?KAMA NDIYE HUYU JK,JE KWANINI HANA MAMLAKA YOYOTE KWA MAMBO YA ZANZIBAR?Hivi Prof SHIVJI we unaona hili ni sawa na uprofesa wako?CCM mnaliona hili sawa?HUU MUUNGANO UNA MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU,KARIBUNI KWA MJADALA!