Wakati tunaungana na Zanzibar idadi ya watu walikuwa si zaidi ya laki 4 sisi tukiwa 12m. Kwa idadi hii ya watu ili nchi ya Zanzibar isimezwe ilitumika busara Tanganyika ipoteze identity yake kuiinua Zanzibar. Ni kawaida sana kwa nchi za visiwa vinapoungana na nchi kubwa. Huko nyuma hata wajumbe wa NEC wa CCM kutoka kila Mkoa, Bara ilitoa mjumbe mmoja kuwakoliaha Mkoa lakini Zanzibar Mkoa mmoja walipewa nafasi ya wajumbe 4. Lakini Tanganyika tu iliyopoteza, Kisiwa Cha Dominica ina watu wasiozidi laki 3. General Assembly Yao haijazi ukumbi wa Karemjee Hall lakini wana kiti Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo kusema Tanganyika imepoteza si kweli. Na kwa kukusaidia zaidi nakupa assignment ujue Zanzibar ni nchi ilhali Tanzania ni TAIFA. Panua ubongo.
 
Hakuna Mtanganyika mwenye akili timamu anaweza kuukubali huo muungano wa hovyo kabisa.

Ni ccm pekee na serikali yao ndiyo wanaupigania huo muungano kwa gharama yoyote ile.
Nyie ambao sio CCM mmetoa mchango gani katika kujitoa na muungano huu?

Na mmefikia wapi?
 
Hakuna manufaa yoyote.
 
Wewe mpuuzi unajua nini wanaposema ULINZI NA USALAMA? Zanzibar ikiachwa haichukui round inakuwa kama Dubai... ni hatari sana
Hizi ndoto za kijiweni, Zanzibar iwe kama Dubai?πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

Dubai, Saudi Arabia na U.A.E ni vibaraka wa Marekani kupitia OPEC+.

Mtaishia tu kuwa kama Mauritius na Comoros na msipokaa sawa kama Yemeni.

Hamna sababu za kiuchumi kuwa kama Dubai.

Hata watu wenye critical and creative thinking kama Wayahudi hawapo Zanzibar. Angalau Watanganyika wanajitahidi kama Professor Ndulu wa Economics.
 
Wewe mpuuzi unajua nini wanaposema ULINZI NA USALAMA? Zanzibar ikiachwa haichukui round inakuwa kama Dubai... ni hatari sana
Huo ndio uongo mnaojazwa 🀣,mpemba kwa % ndio hataki muungano na ndie mbaguzi,waunguja wako half half kwenye suala maana muunguja hata huko pemba anabaguliwa ila mpemba anapeta tu akiwa unguja,siku muungano ukivunjika mpemba tamaa yake achukue visiwa vyote unguja na pemba na ndio tumbatu,kunduchi,kojani nk watakapoukumbuka huu muungano
 
Kile kiwanda hakizalishi sukari ya kutosha mahonda wanaimport sukari bei rahisi kutoka uarabuni halafu wanafanya packaging kwa label zao, hiyo ilifanya serikali ikawapiga bann kuingiza aina hiyo ya sukari huko bara,
Huo ni mfano tu sio lazima iwe sukari, chochote unachochukua Znz kikija Hapa Kodi inakuhusu.

Kwa perspective ya mlaji kama mimi na wewe ukichukua Kitu Znz kulipishwa unaona kama unAonewa ila vaa viatu vya Wauzaji wa Znz ambao wanategemea tu Soko la Ndani kuuza Bara ama hata nje ya Nchi Mazingira sio rafiki.

Kuna kipindi tulienda kule kusajili bidhaa ila masharti Yakawa magumu kama una bidhaa Zanzibar huruhusiwi kuuza nje ya Nchi, ila ukisajili huku kwetu rahisi kabisa kuuza nje.
 
Wewe mpuuzi unajua nini wanaposema ULINZI NA USALAMA? Zanzibar ikiachwa haichukui round inakuwa kama Dubai... ni hatari sana
Kwani wanaomwagwa na Dp world si ni hao hao ?!. Na mmekabidhi rasilimali muhimu. MtawadhibitiJe ?! Kama lengo lilikuwa ni usalama!!
 
Zitapigwa pale balaa mpemba na muunguja,kingine hata ule utalii unaoringiwa utakua wa masharti sana kwa watalii,bara kuna sehemu nyingi za blue safari tourism attract kama kilwa kuna beach nzuri kushinda hata znz na ukizingatia pia kuna selous ambapo mtalii akienda pale atajidai na utalii wa bahari na vile akitoka kidogo atawaona wanyama ila serikali kama imeacha ile sehemu sababu ikiwa itaua utalii wa znz
 
Hawajui wanajidanganya kwenye vijiwe vya Kahawa.
 
Mbona tunabishana madesa ya shule ya Msingi hapa?


Soma mambo 22 ya Muungano hapo, Masuala ya Viwanda na Nishati yapo kwenye Muungano, hivyo ni Serikali ya Tanzania iliokua inasimamia sio Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…