Na Ndimara Tegambwage



SITAKI Zanzibar itumbukie katika mgogoro mwingine mkubwa, mpana na mzito kuliko yote iliyowahi kushuhudiwa Tanzania kutokana na ukaidi wa wachache wasiopenda mabadiliko.

Kamati ya Rais Jakaya Kikwete imekamilisha kazi ya kuleta makubaliano kati ya vyama viwili vikubwa vya siasa – Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

Tayari Baraza Kuu la CUF limekubaliana na mapendekezo ya kamati iliyofanya kazi kwa miaka miwili ikiwa na wajumbe kutoka vyama hivyo viwili.

CCM ilitarajiwa kuridhia makubaliano hayo jana au leo katika kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kinachoendelea katika viunga vya Butiama, kijiji alikozaliwa Mwalimu Julius Nyerere.

Lakini hapa katikati kumezuka vineno. Hivi vinahusu tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa muafaka mpya, unaolenga kuundwa kwa serikali ya umoja kati ya vyama vikubwa ambavyo ni CCM na CUF; na baadaye vyama vingine kwa mujibu wa marekebisho ya katiba na sheria husika.

Hadi jana, hakukuwa na taarifa yoyote juu ya tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa muafaka mpya unaoleta serikali ya umoja. Taarifa zilizopo ni kwamba baada ya CCM kuridhia kazi ya Kamati ya Rais, basi kamati itaketi tena kuweka utaratibu, ikiwa ni pamoja na tarehe ya kuanza utekelezaji.

Habari kutoka Zanzibar zinasema utawala wa CCM visiwani Unguja na Pemba umeanzisha kampeni ya kutaka muafaka huu utekelezwe baada ya uchaguzi mkuu wa 2010.

Hoja zimeanza kujitokeza kwamba wakati rais anaweza kuendelea kuwa yuleyule kutoka CCM, Waziri Kiongozi wa sasa atapoteza nafasi yake. Hili, hoja hizo zinasema, litamdhalilisha Waziri Kiongozi na ofisi yake.

Hoja hizo zinadai pia kwamba, baadhi ya mawaziri waandamizi huenda wakapoteza nafasi zao katika serikali ya umoja, jambo linaloelezwa kuwa litawaondolea utukufu wa kisiasa waliokwishachuma.

Ni hoja hizohizo ambazo zinadai kuwa kuja kwa serikali ya umoja kutadhalilisha baadhi ya viongozi wa CCM ambao kwa ushabiki wa siasa za kitoto, wamekuwa wakitunisha vifua na kutambia CUF kwa kauli: “Ikulu mtaisikia kwenye redio na kuiona kwenye televisheni…hamtakanyaga kule!”

Hizi ni hoja za woga. Zinaletwa alfajiri wakati kazi pekee iliyo mbele yao kwa siku hii ni kuwa na “serikali ya ushirika” au “serikali ya ubia,” kabla haijaanza kuitwa serikali ya “umoja wa kitaifa.”

Hatua ya CUF ya kukubaliana haraka na mapendekezo ya Kamati ya Kikwete inaweza kueleweka haraka pia. Kwamba wamechoka na biashara ya maneno kati ya chama chao na CCM.

Kwamba wamechoka kupokonywa ushindi au hata kunyimwa ushirika katika utawala wakati wana wanachama, wapenzi na wafuasi wengi katika Unguja na Pemba.

Kwamba wamechoka kutawala wakiwa kivulini; sharti sasa watambuliwe na katiba na sheria za Zanzibar, na jumuiya ya kimataifa.

Hili la kuwa watawala kivulini limeipa shida kubwa Serikali ya CCM Visiwani, kwani imeshindwa kujiamini; imekalia tako moja kwa woga; imeshindwa kupeleka huduma palipostahili, ama kwa kutaka kukomoa au kushindwa kupenya ngome ya wapinzani.

Kwa CUF kukubaliana haraka na mapendekezo ya Kamati ya Kikwete, inaonyesha imechoka kupigwa rungu na risasi; wafuasi wake kuuawa na wengine kuwa wakimbizi nchi za nje; na kuishi maisha ya woga siku hadi siku.

Lakini muhimu pia ni kwamba, CUF imeona hakuna sababu ya kuendelea kuwanyima wananchi wa Unguja na Pemba, fursa ya kujitawala, hata kama ni kwa ushirikiano na waliokuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

Kingine muhimu ni kwamba, CUF imetambua kuwa hakuna sababu ya kuchelewa kuasisi utamaduni wa maridhiano kisiasa ili kuweka msingi wa siasa za uvumilivu kwa vitendo.

CUF pia imejifunza na sasa imehitimu. Inaelewa vema kwamba siasa za kukaa na kulalamika, au kwenda mahakamani; au kusubiri “mkono wa binadamu udondoke” ndipo fisi auokote, hazitaweza kuifikisha mbali.

Kwa ufupi imekubali na kutamka: “Tutawale pamoja. Nchi ni yetu sote.” Kwa yeyote aliyekuwa anafuatilia vituko vya serikali katika chaguzi zote Visiwani, tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi, atakubali kuwa CUF imekubali kumeza ndoana, lije na lijalo!

Viongozi wa CUF waliona CCM ndio serikali na wakapata fursa ya kukaa na serikali kupitia CCM. Leo kuna muafaka wa kuwa na serikali ya ubia kati ya CCM na CUF. Nani anasema serikali hiyo isije leo?

Hatua sababu yoyote ile ya kutaka kuchelewesha utekelezaji wa makubaliano kupitia Kamati ya Kikwete, kwa visingizio vya Waziri Kiongozi na baadhi ya mawaziri kupoteza “hadhi,” ni adui mkubwa wa amani na usalama wa nchi hii.

Kwamba wafadhili wametishia kusita kutoa misaada kwa Zanzibar katika bajeti ya mwaka huu hadi muafaka wa sasa utekelezwe, si hoja kubwa sana ya msingi.

Wafadhili wana malengo yao na wanatumia miwani tofauti; kwani wamekuwepo kwa miaka yote na uchafu huu umefanyika mbele ya macho yao mwaka hadi mwaka.

Inabidi watawala wafikie mahali wachoke kutenda jinai na uhalifu mwingine, hata bila kuambiwa na wafadhili au yeyote kutoka nje. Katika hili, kusubiri ni kujidhalilisha.

Sitaki kusikia Serikali ya Kikwete ikikubali mawazo ya kuahirisha utekelezaji wa muafaka mpya hadi 2010. Kufanya hivyo ni kukiri utoto kisiasa. Ni kuomba wananchi waiondoe madarakani kwa ukosefu wa uwezo. Ni kuleta mgogoro mwingine mkubwa.
 
Niliandika humu kuwa CCM wananunua muda na CUF ni wasanii - kuna kila dalili kuwa maandiko yangu yatatokea, lakini la kujiuliza matokeo yake ni nini?
 
Niliandika humu kuwa CCM wananunua muda na CUF ni wasanii - kuna kila dalili kuwa maandiko yangu yatatokea, lakini la kujiuliza matokeo yake ni nini?

CUF wasanii kwa kukubali haraka matokeo ya majadiliano ama wasanii kivipi ? CCM wanaogopa ku share madaraka wakidhani Tanzania ni mali yao na si Watanzania wote .Hapa ndipo inakuwa kazi nzito zaidi .Naomna ufafanuzi juu ya hoja yako ya CUF kuwa wasanii.
 
Pia Watambue Kwamba Ccm Ni Baba Na Mama Yao Na Hakuna Mwingine Zaidi Ya Huyo

Kwahiyo Ni Wao Wenyewe Cuf Kuamua Wanataka Muafaka Au La Na Huo Muafaka Wanataka Kwa Masilahi Yao ( Waarabu ) Au Yetu ( Ccm Na Afrika Kwa Ujumla )

Kama Jibu Ni Wao ( Waarabu ) Watambue Kuanzia Sasa Na Hata Milele Hatutoweza Kufikia Muafaka Nao - Mpaka Warekebishe Msimamo Wao Na Wafute Mawazo Ya Zpp Kurudi Tena Katika Siasaza Visiwani Pamoja Na Wajomba Zao Wa Oman

Amani Upendo Na Mshikamo Udumu
 


Kibaraka mkubwa wewe .Unawezaje kuwaita wenzio waarabu ? This si too low na ndiyo maana unahisiwa kuwa mamluki .Tanzania is not for CCM ni yetu Watanzania wote .Who are you kuwaita CUF waarabu can you hold on your claims and all those stupud allegations? Unastahili kufungwa jiwe utoswe baharini wewe ni hatari kwa jamii ya wapenda amani .Yaani leo unakuja open kwamba wewe ni CCM ? Poa
 
Lunyungu

Nahisi Sasa Kuna Watu Wanataka Kutengeneza Wakina Dalai Lama - Mawazo Hayo Yafuteni Kabisa Kama Mpango Wenu Ni Huo Kama Wa Dalai Lama Kuchochea Vurugu Na Mambo Mengine Ukiwa Nje Sio Lazima Nje Ya Nchi Ukiwa Nje Ya Nyumba.

Ni Kweli Ndio Na Inajulikana Cuf Na Zpp Lao Ni Moja Wale Wajomba Zao Wa Oman Na Nchi Zingine Za Waarabu Na Walishapinduliwa Sasa Hivi Wanatumia Cuf Kudai Marhaba Zao .

Sasa Nawaambia Zpp Haitakaa Irudi Visiwani Na Wala Cuf Haitoweza Kutawala Visiwani Labda Ije Damu Nyingine Sio Hii Damu Ya Sasa Inayofadhiliwa Na Waarabu .

Kwa Wale Wanao Tumia Jina La Tanzania Kama Kampeni Zao Kama Lunyungu Anavyofanya - Tunawapa Warning Kwamba Tanzania Ni Nchi Huru Yenye Amani Upendo Na Umoja Na Ndio Maana Tulimkubali Karume Toka Hapo Mwanzo

Hatataweza Kuzungushwa , Kuchonganishwa Na Watu Kama Lunyungu Wasiojua Chochote Wala Lolote Kuhusu Muungano Huu Au Mambo Ya Visiwani

Mwisho Ni Kwa Wana Cuf Wenyewe Kama Mkikataa Mapendekezo Yoyote Toka Kwa Viongozi Wa Juu Basi Tuko Tayari Kuirudisha Zanzibar Kuwa Mmoja Wa Mikoa Ya Tanzania Na Sio Nchi Kama Ilivyo Sasa Hivi
 



NO wonder Mike na De Mello walikamatwa .
Siamini kwamba mtoto ambaye anaganga njaa anaweza kuwa na mawazo mufilisi kama hivi .Nawaachia wengine waseme .
 

Husituletee siasa za Mugabe kuwa mpinzani hawezi kutawala. Husifikiri kuwa Tanzania ni CCM tu bali ni ya watanzania wote. Umamluki huu sijui unakufaidisha nini, hatuwezi kujua si ajabu wanakulipia rent, karo za shule for ur kids. Yaani ina maana wewe hata huwezi kusoma alama za nyakati?? Mie siamini kama hilo linahitaji kwenda darasani, na kama kweli unahitaji kwenda darasani basi naamini CCM waliku-overdose maji yale ya kijani(Maji ya bendera yao). Walikuchanganyia na JIKI.
 


Indume haka ni ka bwana mdogo hapa Dar kana hangaika na njaa zake .Kanajifanya informer na kaandishi .Hakana mke wala nini ni ujanja ujanja anatuletea hapa na kuwachoma watu na kuwatishia akina Mike kila kukicha .

watu wanaacha hoja wanaleta vioja , viroja na unazi .Unawaita watu wa Tanzania kwamba watumwa wa Waarabu .Ongea hoja na si kuleta ujinga na kupapalia kibarua chako .Pesa ya aina hii ni ya laana na kwa umri wako nadhani you need to be careful utaishia pabaya .
 
Lunyungu

Naweza Kumwambia Mike Aje Online Sasa Hivi Kutoka Msn

Aje Kusema Mimi Nimemtisha Lini Na Wapi

Usiwe Mzushi Na Uwongo

Kitu Usicho Kijua Ni Zaidi Ya Usiku Wa Giza

Lunyungu Usidharau Watu Hata Siku Moja Na Usijaribu Kuonyesha Dharau

Wenzako Walioonyesha Dharau Wako Wapi?
 
Ukitaka Kuona Ukweli Wa Mtu Mchokoze Tu Mchokonoe Tu Siku Moja Utaanza Kujua Kidogo Kidogo Kuhusu Yeye

Kama Sasa Hivi Lunyungu Anavyojiweka Wazi

Masikini Ya Mungu Hajui Chochote Wala Lolote Zaidi Ya Umbea , Chuki Na Fitina Zisizo Kuwa Na Kichwa Wala Miguu

Lunyungu

Mie Kwa Moyo Mweupe Kabisa Nakusamehe Usipate Tabu Sana
 

Bwana mdogo .I know you better than anything .Matisho yako endelea nayo kwa hao hao .Look here hakuna atakaye baki akaishi milele na ukiua means utauawa so I take no crap from you .Utafundishwa kuheshimu mada na kuacha kutukana watu na kutoa madai mazito kwa njia hizo hizo unazotumia .Now let's go on.Mimi ni mkomavu na I have lived longer kuliko unayenuka maziwa bado .Haya nenda kashitaki.Kumbuka mie situmii nick names hapa .Majina nakupa tena Joseph Cleophas Lunyungu Mademla wa Matandula .Omba namba yangu ya simu najua unayo maana uliwahi kunipigia then ukajificha kwenye issue ya Muhimbili nikaamua kula nawe .Ninapo ishi ni Mtoni Kijichi je unataka kazini kwangu il iwe rahisi kwao kuniondoa kama unavyo tishia ? Sema I will furnish you with details then nikuone .
 
Hi lunyungu

Please review the website for suitable content for submission to thelist. This is a nice piece but not the type of information we post.

Regards
 

Shy
hujui unachozungumza. kasumba iliyopo juu ya kuwa CUF ni waarabu ni uzushi tu wa CCM. Na kwa kweli tumechoshwa na hawa CCM, nyiyi mnazungumza ufisadi wa bara lakini huko visiwani ndo wamezidi. Mimi si si mtetezi wa CUF.... nadhani watakuja wenyewe kusema, lakini kama mtanzania mwenye upenzi na zanzibar, Serekali ya mseto ni muhimu sana. kwa mtazamo wangu CUF inayo mapungufu yake lakini hauzidi ufisadi wa CCM amboa sio tu unahujumu uchumi bali pia unawagawa wazanzibar kwa kiasi kikubwa sana. Jamii ya Kizanzibari imegawanyika vibaya sana na sasa najua mambo yatazidi kuwa mbaya. Mi hata sielewi kwanini CCM wanang'ang'ania madaraka

any way bora niishie hapa
 


What a great way to end my sunday!

Thanks Lunyungu!
 
Huwa Napata Taabu Sana Kubishana Watu Wa Hit And Run Anaandika Kitu Hawezi Kukitetea Anakimbia Zake

Ulikuwa Mjini Internet Cafe Sasa Ndio Unarudi Kijichi Nini ?

Mzee Why Dont U Go Ttcl Mobile ??

Itakusaidia Kuendeleza Mada Na Sio Kukimbia Kimbia Kwenda Kutafuta Notes
 
Naandika Kwa Sababu Napenda Kuandika Siandiki Ili Nionekane Siandiki Kwa Ajili Ya Kushindana Na Kupigiwa Machepeo

Ahsante

Usiku Mwema
 
Maranyingi Huwa Natumia Watu Wengine Kupublish Vitu Vyangu Hata Wewe Naweza Kukutumia Tukikubaliana

Wengi Wamekubali Na Tupo Nao Kwahiyo Ukinikimbia Kwa Jina La Shy Then Mwingine Atakuja Namada Zangu Ataweka Utajadili Utazipenda

Hata Hivyo Wiki Hii Nimeandaa Seminar Pale Ifm

Karibu Sana Kaka/bibi

Nitaweza Kukupa Mwaliko Uje Uone Angalau Huwa Unaongea Na Watu Wa Aina Gani Sio Wale Unaohadisiwa Mitaani Na Katika Bar
 

Kwa maandiko pekee kwangu inatosha kwamba hiyo Seminar itakuwa ya aina gani .Haya nitafika na nitasema taja ukumbi na saa na tarehe na useme utakuwa na semina juu ya nini .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…