Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nipashe wametumia njia nzuri kuweka mambo sawa kwa Bw. Lowassa, manake AG wa bara angeona haya kusema ukweli...
Mwanasheria Mkuu wa SMZ said:Mwanasheria Mkuu alisema kwa mujibu wa sheria za viongozi wastaafu hutakiwa kutumikia serikali kwa miaka mitano na sio chini ya hapo, ili uweze kunufaika na mafao yote ya wastaafu.
..kama ni hivyo, Cleopa Msuya na Salim Salim wanapaswa kukatiwa mafao yao. they did not complete a 5 yrs term. pia hawastahili kuitwa Mawaziri Wakuu Wastaafu.
Hiyo kauli (bold) ya Mrema imeniacha sina mbavu...lakini ni kweli,kuna umuhimu wa kutumia panya kunasa panya wengi zaidi.
Asante mlalahoi.
Tumeona sasa umeamua kuingia mzima mzima. nakuomba usiweke michango yako itakuwa ni conflict of interests hatujui unachangia kumfurahisha bosi wako au ni mchango wako wa moyoni. hongera kwa kitengo kipya ulichoshika.
Hivi hiyo sheria ya mafao ya wastaafu haiwezi kupatikana ikawekwa hapa tuhangaike nayo?
Znz Kuwa Na Serikali Ya (makande) Mseto.......! One Step Forward!
Kama haijaundwa siamini,CCM hupenda kununua muda na CUF ni wasanii
Ah Balahau we (Balahau kwa kipemba maanaake Rafiki "Ndugu" Mpendwa-usishituke) Hili ni jambo zuri. Tusubiri CCM watasemaje, lakini mimi sioni tatizo kwao. Tatizo linakuja katika kutekeleza jambo hili. Mimi naona itakuwa gumu kutekelezeka kama Maalim hajacha tabia zake mbovu za ubinafsi na tamaaa zisizo na mwisho. CUF kuwemo Serikalini mbona ni jambo zuri tu, lakini Maalim Seif asilazimishe yeye ateuliwe katika nafasi anazozitamani (awe radhi nafasi hizo ziwe kwa wana CUF wowote wale ambao wana uwezo kama yeye au kupindukia yeye) hasa ukizingatia mazingira , mstakabala na maendeleo tunayohitaji hivi sasa Zanzibar.Si lazima Maalim awe Waziri Kiongozi au Waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hivi sasa, nafasi ambazo kina Juma Duni, Abubakar Bakari, Hamad Rashid, Salum Bimani, Miraji,Jussa, Najma Khalfan, Hariri, Dedes, Dk Muchi na wengi wengineo wanaweza kuzikamata vyema tu na kukidhi mahitaji na matarajio. Balahau, subiri. lakini ukisikia muafaka mwengine umevunjika asitafutwe mchawi, bali ni Seif kukosa uluwa. Kwani sidhani kama ameacha nadhiri yake na tabia yake chafu ya tamaa zisizo na mwisho.
CCM mbona haijatoa tamko kuhusu hili?????? Maana wale ni vigeugeu hawakawii kusema hiyo kitu haipo au kwamba bado majadiliano yanaendelea.
All in all huko ndiko tunakotakiwa kwenda!