mie nnakubali kua shy anaandika kwa kupenda bila ya kujua akiandikacho.


anasema ZPPP ilikuwa ya waarabu? huyu kweli hajui lolote kuhusu sh Ali Ameir na Mohammed Shamte uwaarabu waliupatia wapi?

anajua kutofautisha baina ya ZNP na ZPPP?

jee anajua asili ya wazanzibari na mchanganyiko wake?

au ndio muandishi wa makala nyingi kwa kupenda kuandika.

ukome hasidi na mwana mabuje weee kuzungumzia jambo usilolijua
 


The boy is only 20yrs plus few months anaweza kujua mambo haya wapi ?Akili yake imekaa kama mabavu ya CCM, China na dailama, Russia na Zimbabwe so unategemea nini ?
 
The boy is only 20yrs plus few months anaweza kujua mambo haya wapi ?Akili yake imekaa kama mabavu ya CCM, China na dailama, Russia na Zimbabwe so unategemea nini ?

ikiwa hivyo kumbe tumuache, baleghe inamsumbua. na aende kule brazameni keshawawekea mambo yao.


kujibizana na mwehu na wewe huitwa mwehu sasa sijibizani tena na mkosa haya
 

Nimeisoma hii story hadi mwisho na sijaona mgogoro wowote. Kinacho onekana hapa ni hofu na ubinafsi mkubwa wa viongozi wa CCM ambao wako tayari kufanya kila kinachowezekana ili kutetea maslahi yao binafsi. Naamini katika suala hili- maslahi ya wananchi wa Zanzibar ndio yanapaswa kuwekwa mbele bila kujali nani atapoteza au atapata nini!
 
Chama cha Mapinduzi hakijaridhia mapendekezo yote ya kamati ya muafaka na hivyo kwa kupitia kikao chake cha kamati kuu kimerudisha mjadala tena kwa wajumbe wake ili wazungumze tena na CUF kwa kufuata maelekezo hayo.

Mojawapo ya mapendekezo hayo ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Zanzibar wanapewa nafasi ya kuamua mwelekeo wa kisiasa visiwani humo kwa kutumia kura ya maoni.

Na pia CCM imeazimia kuitisha kikao maalum (angalia makala yangu ya leo kwenye Tanzania Daima) kwa kuwa kuna mambo mazito ambayo yanalihusu Taifa na kikao hicho agenda yake imetajwa kuwa ni "siri" kubwa.

Baadaye leo tutaweletea KLHN Exclusive ripoti nzima ya maazimio kama ilivyosikika live kupitia klhnews na Bongoradio na pia hotuba ya mwisho ya Rais Kikwete.

We set the Standard, others follow...

Pia wametoa maagizo kadhaa kuhusu suala la maadili, Richmond, nidhamu n.k
 
Kwa maana hiyo CUF wamepigwa chini kama baadhi ya JF members walivyosema. Usanii at its best. Aluta continua.
 
Kimsingi, suala la Mseto wajumbe toka Zanzibar walilikataa jinsi lilivyo bila kuwasikiliza wananchi. Kimsingi huo ndio msimamo ambao ungeweza kutolewa hata bara kama wajumbe wao wangekuwa na misimamo. wale wa Zanzibar waliingia wakiwa wameshaweka mguu chini na wameondoka wakiwa na ushindi na imechukua masaa nane ya leo kufikia uamuzi usiokuwa uamuzi.

Lakini wameamua kuitisha kikao maalum ambacho sisi wengine tuliona ipo haja ya kufanya hivyo kwani kikao hiki hakikuwa muafaka kufanya maamuzi mazito ambayo watu wengi walikuwa wanayazungumzia
 
Lakini wameamua kuitisha kikao maalum ambacho sisi wengine tuliona ipo haja ya kufanya hivyo kwani kikao hiki hakikuwa muafaka kufanya maamuzi mazito ambayo watu wengi walikuwa wanayazungumzia
Kamanda nakuona kama uko Mara vile...🙂 Anyway kura ya maoni kama ipo ipigwe katika muda muafaka, kwani hili tatizo sasa ni la muda mrefu. Sijui upande wa CUF watareact vipi na maamuzi haya ya NEC.
 


Mbwe mbwe zote zile hawakuwa na muafaka wala maamuzi ? Haya wananchi wenzangu tuendelee kuvumilia .Wamesema kura za maoni je zitaendeshwaje ili kufikia makubaliano ?Hakuna watu walio jiandaa kwamba hakuna MSETO huko kweli ?
 
Je, hii sio njama ili wapate nafasi ya kufanya rigging ya kura hiyo ya maoni pale itakapokuwa imekubaliwa?
 
Kimsingi, suala la Mseto wajumbe toka Zanzibar walilikataa jinsi lilivyo bila kuwasikiliza wananchi.

Sounds to be a very wise democratic political idea, na ndio demokrasia yenyewe kuwasikiliza wananchi wanataka nini, sasa sio tena kuanza ujanja ujanja kwenye kutafuta maoni ya wananchi on the ishu,

Halafu hii tabia ya kutafuta maoni ya wananchi CCM waitumie kila kona muhimu za maamuzi ya taifa letu, sio iishie kwenye muafaka tu!

Bravo NEC kwa hili!
 
Kubwa zaidi ambalo litateka fikara za waandishi wengi wiki hii inayokuja ni kuitishwa kwa kikao maalum mwezi wa tano... ambapo Kikwete kawaambia wajumbe "agenda yao ya siri waliyokubaliana jana..

Pia wamekubaliana kuwa Butiama itakuwa ni makao makuu ya wilaya mpya itakayoundwa..
 

Mkuu ES, bravo tena?? Maoni si code name tu kuwa the issue is dead?? Kwani since 1995, breakdown ya votes huko Zenj si inajulikana?? (I'm pretty sure unajua hilo)

Yaani hapa mkuu wa kaya ameleta aibu ya mwaka!! He can't even decide and get consensus on an issue that he knew for the last 8 weeks.

anyways, stalemate kwenye kila kitu itafuata maana I can see precedent from this.

Also nilikuwa naomba legal opinion humu ndani, is this thing even legal???

Maoni ni kwa CCM members au wananchi wa Zanzibar?? Je kama ni CCM mbrs, ni ccm mbrs wa Zanzibar tu au nchi nzima?? Maoni ni wananchi wa Tanzania au Zanzibar tu??

Discussion btn CUF/CCM, wamekubaliana kitu, CUF wamekubali, CCM inaonekana wamekataa, so how does it then go to maoni ya wananchi?? What if Chadema, TLP also want to field candidates in Zanzibar how does all this play out??

When U start talking about maoni ya wananchi how does that not include the constitution??

Halafu why did CUF/CCM waste all the taxpayers money in discussion for over 2 yrs, kumbe issue itakuwa solved na maoni??

Sorry guys, I'm just thinking out loud.
 
Pia katika kumuenzi baba wa Taifa wameamua.

Imeazimia kuondoa upungufu wa mgongano wa maslahi kwa viongozi wake wa dola ili watenganishe biashara na uongozi. Wamesema "viongozi watakaobainika kuvunja miiko ya uongozi watachukuliwa hatua mara moja".

Kuhusu suala la Richmondd wamesema "HKT imeona kuwa wananchi wanachukia sana maovu"....
 
Mkuu MO,

Unajua ndugu yangu katika taifa kama letu na mazingara ya uongozi wetu na siasa kwa ujumla, unapopata angalau kidogo kinacho-make sense, basi unashukuru, maana kumbuka wangeweza kunyamaza kimyaaa, au wangeweza kuleta mauza uza kibao,


Lakini kwa kusema watatafuta maoni ya wananchi, angalau sisi wananchi tunaweza kuwafuatilia kwa makelele, si unakumbuka Hosea alivyosema kuwa Richimonduli haikuwa na noma, sasa si unajua kuwa anasubiri hukumu ya Waziri Mkuu, kutokana na mapendekezo ya wabunge kuwa aondolewe, pole pole mkuu, as a nation we are making progress, ingawa sio kwa kasi ambayo wengi hapa tungeitaka!
 

Mkuu, you're absolutely right.

Unajua hata katika nchi zilizoendelea wakati mwingine wananchi wenyewe ndio wanalazimisha kwamba kupigwe kura ya maoni.

Kitakachotoka hapa ni mawazo halisi ya wananchi.

Sasa kama CCM na serikali wameamua kuwasaidia wananchi wa Zanzibar kufanza hivo ni jambo zuri, mambo polepole.
 

....as if there was a time when they liked them....
 
Kuhusu Muafaka:

"Imeyakubali kimsingi mapendekezo yaliyomo kwenye taarifa" ya kina Makamba lakini imetaka marekebisho yafanyike. Hivyo warejee kwenye mazungumzo na watu wa CUF. Imeazimia.(nanukuu)

- Iwapo mapendekezo hayo yatakubaliwa basi yataleta mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala wa Zanzibar, hivyo kwa kuzingatia hivyo basi wananchi wa Zanzibar wahusishwe katika kuamua kwa njia ya kura ya maoni juu ya jambo hilo.

- HKT imeoneshwa kusikitishwa kwake na tabia ya CUF ya kutangaza makubaliano kinyume na makubalianao kuwa jambo hilo litafanyika kwa pamoja "kadhia" hii inaifanya kazi ya kujenga mazingira ya kuaminiana kuwa ni ngumu sana. HKT inaipongeza kamati ya muafaka kwa kuamini kuwa mazungumzo hayo ni hatua muhimu huko Zanzibar.

Katika kuhitimisha kikao hicho Rais Kikwete alisema hivi:

"tumefanya mambo mengi sana, kwa siku ya leo kwa siku hizi tulizofanya kikao hapa, na hasa leo; na ajenda hii moja imetuchukulia zaidi ya saa nane kuzungumza mpaka kufikia tulipofikia"..

"kazi imekamilika... iliyobakia ni kwenda kutekeleza tuliyoyaamua, kwa sababu tumeamua wenyewe.. naamini tutaenda kufanya hivyo"...

"Nimesema sana kutwa nzima ya leto katika kuongoza kikao hiki, sina mengine ya kusema bali kuwashukurani, asante sana"..

"tutakiane safari njema, turejee makwetu salama, tufanye mambo yetu salama, tukutane tena mwezi mei kwenye kikao maalum kwa lile jambo maalum tulilokubaliana jana au siyo jamani, hiyo maalum hatumuambii mtu ni siri yetu" (makofi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…