Hii ni hatari kwa Muungano na inavyoelekea ,huenda mambo yakabadilika na kuifanya kura ya maoni kuwa ni maoni ya kuendelea na CCM ambayo ndio inayoonekana kuilalia Zanzibar kimabavu ,na lazima CUF watalikubali hilo kwani na wao watalitilia nguvu lisimamiwe na vyombo vya Umoja wa kimataifa kwa kila kipngee ,na hapo ndipo patakapobadili muelekeo wa kura ya Maoni ya muafaka na kuwa kura ya maoni ya Muungano ambayo imekuwa ikipigiwa makelele muda mrefu na Wazanzibar wakidai Muungano uliokuwepo si wa kuridhiana bali ni wa watu wawili.CUF walijua wazi kwamba makubaliano yaliofikiwa CCM hawana ubavu wa kuyakubali ila waliwaweka CCM kwenye mtego mkali sana ambao unaonekana umefyetuka na kunasa.
 
CCM inaweza kupandikiza wapiga kura toka bara na wakashinda kura ya maoni au hata kuiba uchaguzi huo. Kura ya maoni ikiwa huru na wakaamua wao ni kura ipi ya maoni wanayoitaka basi ndio utakuwa mwisho wa Muungano.
 


Mkuu kama ukikumbuka harakati za Bw Anaf kutoka Ghana unaweza kujua ni nini hasa huu mwafaka. Kwa wanaojua ukweli wa mambo ni kuwa mara zote tatu kwenye chaguzi zilizofanyika CUF walishinda uchaguzi, lakini kutokana na sababu mbalimbali katiba ikiwa moja wapo, hali ya sasa na dunia, na historia ya Zanzibar na mambo nyeti yanayohusu Mapinduzi, na mambo ya kikatiba haikuwa sahihi kisiasa kwa CUF kuunda serikali Zanzibar. Kwa hiyo ulifanywa ujanja, zikatumika nguvu na mambo mengine ili kuwapora CUF ushindi.
Lakini wenye busara na wenye akili walijua na wanajua kuwa hii sio long term solution, na waliona kuwa move ya mwisho ya CUF haikuwa ndogo, na huenda baadaye itakuwa move ya kutisha zaidi. Kwa kuwa siku zote haki hainyimwi huwa inachelewshwa tu, wenye busara ndani ya CCM wakaanza kuangalia utaratibu wa kutafuta suluhisho la kudumu, ambalo hata kama CUF ikishinda itawale bega kwa bega na CCM, ndio maana issue za muafaka zikaanza kuwepo. Vilevile watu wa nje walioshuhudia ujanja uliofanyika huko Zanzibar nao walianza kuchoka wakaona ni afadhari mambo yashughulikiwe kistaarabu, hapo ndio mwafaka ukaanza.
Lakini kama unavyojua kuna manunda ndani ya CCM zanzibar wanasiasa za chuki, hawataki mwafaka, wanaona kuwa hawawezi kukaa na CUF, hapo ndipo kwenye tatizo!
 
nimeipokea habari hii kwa mshtuko mkubwa na kuemewa, siamini nilichokisoma japo yaonekana ndio ukweli wenyewe.


zanzibar ina safari ndefu zaidi ya kuelekea mafanikio na kuboresha hali za watu ambao wanaonekana wamechoka au kuchoshwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao.


hivi kabla sijatoa mawazo yangu niulize

mbona ndugu zetu kenya wao walifanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi na kikatiba pasipo kufanya kura za maoni na ss watanzania ikiwa rais ni kinara wetu alienda kutia msukumo?


au ss waafrika hatuoni umuhimu wa jambo mpaka tuone watu wanauwana wanachomeana nyumba, wanaharibu mali za umma ndio tuhisi kunahitajika suluhu la haraka?


zanzibar kwa mazingira yaliopo ni vigumu kuitisha kura ya maoni ilio huru.

malalamiko ambayo kila siku yanalalamikiwa na pande zote kuwa kuna mamaluki hutumika kuwakilisha wazanzibari ambao si wazanzibar na huo ndio msingi wa matatizo.

ccm muda mrefu tunaamini pemba kuna vitendo vinafanywa ili kuhakikisha ccm isipate kiti hata kimoja ikiwemo kuandikwa watu mara mbili mbili, wengine hutoka tanga na mombasa kuja kuandikishwa ili cuf washinde, na pia hutumia baadhi ya watendaji wa tume ya uchaguzi kufanikisha hayo.


na cuf wana masikitiko hayo na zaidi kwa wenzao wa ccm wao wanasema na kuamini ccm kwa kushirikiana na smz wanajitahidi kupanga watendaji wakuu wa tume ili kuhakikisha wanaiba kura, wanaanzisha vikosi vingi vya ulinzi na usalama na kazi yao ni kuhakikisha ccm inabaki masarakani ama kwa kuiba kura au kwa kuwatisha na kuwapiga wananchi.


pande zote mbili kuna watu ambao hutumia nguvu zao kuwashawishi wananchi waamini na kubehave wanavyotaka wao.


tulifanya kura ya maoni kuhusu muungano au wengine wanasema white paper sio siri zanzibar watu walienda pale kwa mitizamo ya vyama vyao na sio huru.


pande zote kila siku zilikua zikipita na kuwakaririsha watu wao cha kusema au kuandika kwenye tume.

ukisema kinyume na msimamo wa chama chako au wanaokuhisi wewe mwenzao unahesabiwa msalit na unastahiki kuadhibiwa.


sasa ilikuwa busara kuunda serikali ya kitaifa ili itengeneze mazingira na kuwajengea uwezo wazanzibari wa kusimamia mawazo yao kisha ndio tufikirie hilo suala la maoni.


tunahitaji kwanza kujenga umoja wa wazanzibari ambao kila saaa inayoenda mbele humun'gunyuka.

hapa ndio shaka yangu huingia kwa ndugu zetu wa bara hivi kweli wanatutakia mema?
 
Mtu wa Pwani,

Kwani unadhani Kibaki na PNU yake walikubali kufanya hayo mabadiliko kwa hiari? Ama wewe hukuona damu za watu zilivyomwagika? Labda waulize CUF kama wako tayari kuwalazimisha CCM wafanye mabadiliko kama ilivyotokea Kenya.
 
Kuhusu suala la Richmondd wamesema "HKT imeona kuwa wananchi wanachukia sana maovu"....

Hili limenishangaza kuliko yote, hawa wakuu imewachukua siku nyingi sana kutambua kwamba wananchi wanachukia sana maovu, akili zao ngumu!! (granite brains).

No wonder why, they don't see poor and difficult life of Tanzanians MWENYE SHIBE HAMJUI MWENYE NJAA.
 

Mtu wa Pwani

Sijui una maana gani unaposema wenzetu wa bara hawatutakii mema, ukumbuke kwamba tarizo la Zanzibar ni wenyewe watu wa CCM (Unguja) ndio wanalikwamisha na sio watu wa bara hata hao so called "Wazanzibara" huwa mara nyingi wanakuwa muhimu wakati wa CCM (Unguja) kutafuta kura baada ya kura "waZanzibara" wanakuwa hawana hadhi ya kuwafanyia maamuzi wazanzibari na hapo ndipo inapojulikana kwamba wao si wazanzibari halisi.

Hali ya zanzibar kwa kweli inasikitisha sana na hiyo kura ya maoni haiwezi kuleta mabadiliko yoyote kwa sababu wenyewe CCM(U) wameshaamua, nadhani si busara kuiingiza nchi katika kupoteza pesa kugharamia maamuzi ambayo hayaamuliki
 

Mkuu kama hiii ndio maana hasa ya muafaka, basi ni doomed kabla hata ya kura za maoni kupigwa.
 

Simple. CUF na Seif wameshinda uchaguzi mara zote tatu wakanyang'anywa ushindi. Na hii ndio sababu CCM wamekuwa wakikubali kufanya mamifyaka kama njia ya kuwa-cool down CUF. Hatuna haja ya mwafaka bara kwa sababu CCM wamekuwa wakishinda kihalali kabisa katika sanduku la kura. Of course bara pia CCM wamekuwa wakiiba, lakini ni kuiba kwa lengo la kupata ushindi wa kishindo sio kubadilisha mshindi hasa katika ngazi ya urais.

Kuhusu muungano, I will come back later kwa sababu naamini tunahitaji a serious and separate discussion on this one.
 
Haya tena, usanii unaendelea. kama walijua kuwa suala hili linapaswa kuamuliwa na wananchi,m kwa ni ni wakafanya mazungumzo kwa zaidi ya mwaka mmoja? nashangaa cuf walishindwa kuuona mtego huu na kutangaza mambo ambayo ccm hawakuwa na nia ya kuyatekeleza. lakini hao waunguja wanaopinga inapaswa wawafikirie wenzao wa pemba wanavyofanya kazi katika mazingira magumu. wakiendelea kufikiria maslahi yao tu, ipo siku wataamua kuondoka na hivyo kukifganya kisiwa chote cha pemba kuwa cha cuf, tukifika hapo, hali itakuwa ngumu sana kwani hata huko unguja hakutakalika
 

kwanza nnashukuru sana mchango wa bara kwa zanzibar nnaamini bila ya muungano huenda tungelishapinduana zaidi ya mara 40 kama ndugu zetu wa comoro mara 20.

pia huenda unguja na pemba vingekuwa visiwa viwili visivyoiva pamoja.


ila bado nnaamini haijafanya jitihada za kuumaliza ule mzozo, kuna wakati kama ndugu tunahitaji jitihada za ziada ktk kumaliza lile suala.

ikiwa waliweza kuwachagulia wazanzibari rais wakati wana ccm wa zanzibar tulikuwa tukimtaka mwengine iweje kwa hili ambalo ni jepesi zaidi?
 
Ras-Nungwi,

Mimi nadhani tutoe ushirikiano wa nguvu ZOTE zinazotakiwa ktk hii kura ya maoni. Ni vizuri tukaangalia nchi nyingine duniani zilifanikiwa kwa kiasi gani kutatua migogoro ya kisia kwa mtindo huu wa kura za maoni. Ninaamini ya kuwa, vyama vyote vya siasa vinawawakilisha wananchi, hivyo basi, ni wakati muafaka wa wananchi kuamua mustakabali wa nchi yao. Remember, People's Power.
 

Hapa ndipo nauliza wapenzi wa Kkwete je hakujua hii nchi ilivyo kabla hajaamua kugombea ama yeye alitaka kutimiza jina na hesabu ya kuwa mmoja wa marais wa Tanzania ?
 

I support CUF kutangaza maan wali pre empty na sasa iko wazi nani mwenye matatizo maana kama wangalichelewa ingalikuwa spinned kwamba CUF wanaleta shida .Now kila mmoja anaona .
 
hebu nisiadieni wana JF

HIVI KWELI CCM ZANZIBAR WANA UBAVU KUITIKISA CCM NZIMA pamoja na JK?
sijui wajumbe wa zanzibar wapo wangapi ktk huo mkutano.
 
I support CUF kutangaza maan wali pre empty na sasa iko wazi nani mwenye matatizo maana kama wangalichelewa ingalikuwa spinned kwamba CUF wanaleta shida .Now kila mmoja anaona .
Naungana nawe cuf waligundua ccm watawachezea makida ndio mana wakawahi na sisi watz tushajua nani mkorofi kati yao.
 
hebu nisiadieni wana JF

HIVI KWELI CCM ZANZIBAR WANA UBAVU KUITIKISA CCM NZIMA pamoja na JK?
sijui wajumbe wa zanzibar wapo wangapi ktk huo mkutano.

JK is leading in playing sanaa hakuna lolote .Hawako tayari kuona CUF wanakuja madarakani maana wote akina Makamba wanaamini vyama vingine havina haki hii .No political will tunaimbishana bure hapa .
 
Kura ya maoni ya nini ? Huu ni ujinga kabisa...

CUF imeshinda majimbo yote Pemba PERIOD pia imeshinda baadhi ya majimbo ya Unguja . Kwa nini tunataka kupoteza hela za walipa kodi ? why are these people so scared to make tough decisions ?
 
Ngoja tuyasubiri haya maoni,lakini mimi naamini ni ucheleweshaji fulani ili sisiem wajipange vizuri kuiba kule visiwani kama hawataridhia serikali ya Mseto.Surely the oppressions drives the wise into to madness,Tulitegemea kutakuwa na jipya la kihistoria kuhusu huo muafaka wa ZNZ,kumbe ni kufunika mambo sirini.
Kama sisiem huwa haishindi ZNZ sijui kama hizo kura za maoni watazichukuwa kwa staili gani ili washinde,maana nakumbuka hata kibaki kule Kenya mwaka fulani aliwahi kuomba wananchi kutoa tamko la kura za maoni kuhusu uandishi wa katiba mpya kwa kivuli cha kuwa demokrasia ni kuacha wananchi waamue wenyewe,matokeo yake wengi walitaka katiba mpya,kwa hiyo sisiem wasidhani wananchi hapa ZNZ wamelala.woe to sisiem
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…