Mimi naomba nisirudie mambo ambayo hayatabadilika hata nikifanya nini!

Kura ya Maoni naunga mkono. Na pia Naunga Mkono Kwa kamati ya muafaka kufika hapo... hii ndio maana ya Process... Kamati hii imekaa na kuchambua mambo matano... na mojayapo ni hili la serikali ya mseto, ambayo wanaJF kwa makusudi kabisa mnataka kupotosha umma kwamba ndilo lililokuwa linajadiliwa tu... na Kama halijapita basi hakuna lililofanyika... This is wrong.

Kwa hakika ili uite kura ya maoni ni maoni kweli ya Wananchi wa Zanzibar ni muhimu basi kuwe na formula... yaani tuseme kwa mfano... ili serikali ya mseto iuundwe kule Zanzibar... basi kuwe na at least 50% ya wakaazi wa Pemba na 50% ya wakaazi wa Unguja. Bila hivyo tutapa mgawanyiko ule ule wa CCM na CUF ambao sio mzuri kwa Zanzibar.

Na lazima basi kuwe na chombo Huru(yaani kisiegemee CUF au CCM) cha maridhiano ambacho ndicho kitakacho tangaza na ku-promote maridhiano na ndicho kitakacho tangaza na kuendesha Kura. Chombo hiki chaweza Kuwa Tume ya Uchaguzi, au hata kamati maalumu ya Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar.

Lini kura zinafanyike!!! Kwa hakika zifanyike kabla ya Uchaguzi wa 2010, Lakini implementation ya Serikali ya Mseto ifanyike baada ya 2010... muda huu mrefu kwa kubalisha utawala wa nchi.

Haya si mambo marahisi sana kama tunavyodhani, angalia Kenya Kibaki na Raila bado walikuwa hawajakubaliana kuhusu muundo wa Serikali hiyo ya Mseto mpaka jana at least....

Muhimu ni kuweka processes and structure and framework into implementation of "Serikali ya Mseto";

Tupeane matumaini kuliko ku-raise hali ambayo sio lazima itokee tena Zanzibar.
 
hebu nisiadieni wana JF

HIVI KWELI CCM ZANZIBAR WANA UBAVU KUITIKISA CCM NZIMA pamoja na JK?
sijui wajumbe wa zanzibar wapo wangapi ktk huo mkutano.

Wacha uvivu. Kama kweli unataka kuwa mchambuzi wa mambo na mfuatiliaji wa mambo tafadhali nenda katika Website ya CCM hapo utaona muundo mzima na utajua kuna wajumbe wangapi katika NEC na CC kutoka Zanzibar tena kwa majina na vitongoji wanavyotoka. Halafu iangalie Historia ya Zanzibar. angalia chimbuko la Seif Sharif Hamad, Utawala wa Alhaj Aboud Jumbe na masahibu yaliyomfika. Vurugu za Seif Sharif Hamad na kufukuzwa kwake CCM na SMZ. Hasira za Seif Hamad uongo na vitimbwi vyake dhidi ya wananchi wa Pemba. Njama na propaganda za Seif Hamad dhidi ya SMZ. Malumbano na mapambano kati ya Seif Hamad na kikundi chake (upande mmoja) na CCM-Znz na SMZ upande mwengine.Angalia Zanzibar chini ya uongozi wa Marehemu Idriss Abdulwakil, Komandoo Salmin Amour na Mhe. Amani Karume na jinsi gani Seif na Kikundi chake walivyoshiriki kuparaganya system ya utawala. Angalia chaguzi zote za 1995, 2000, na 2005 na vitimbwi vyake (bila ya upendeleo). Uangalia na ufuatilie kwa makini huu muafaka wa hivi sasa. KITANDA USICHOKILALIA HUWAJUI KUNGUNI WAKE. Unataka Wajumbe wa CC na NEC Tanzanaia Bara waamue kuhusu mstakbala wa Zanzibar? katika mazingira hayo?
 

Kwa historia ni kwamba Pemba hakuna hakuna CCM ila Unguja .CUF iko kote kote na sasa wakisema haya basi Seif ataingia mjini kumwaga sumu mamb yatakuwa kama uchaguzi mkuu na CCM itaangukia pua vibaya sana .Kama hawaamini ngoja utaona kama hawatapeleka FFU na majeshi mengine kuongezea maoni yao .
CUF kaeni macho muda kabla mtaona wageni wengi toka bara hao watakuwa wamekuja kuleta maoni ya CCM .Wakabeni koo bila ya aibu .
 
JK is leading in playing sanaa hakuna lolote .Hawako tayari kuona CUF wanakuja madarakani maana wote akina Makamba wanaamini vyama vingine havina haki hii .No political will tunaimbishana bure hapa .

CCM WASHUKURU;

NINGEKUWA MKULU WA CUF NINGESEMA NENO LISILOPENDWA NA WANASISIEM, NA NINGETENDA JAMBO LINALOPENDWA NA WANAJAMBO.
 
Kura ya maoni ya nini ? Huu ni ujinga kabisa...

CUF imeshinda majimbo yote Pemba PERIOD pia imeshinda baadhi ya majimbo ya Unguja . Kwa nini tunataka kupoteza hela za walipa kodi ? why are these people so scared to make tough decisions ?

Mkuu Rufiji,

Kwa hekima zako ulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu unafikiri NEC ya CCM au/na Baraza Kuu la CUF. lina uwezo wa kuamua maamuzi hayo bila kuwashirikisha wasiokuwa na vyama, wananchama wachache wa CHADEMA, NRA, JAHAZI ASILIA, TLP...? Are you kidding my friend? Wamepewa mandate hiyo na nani? na Katiba ipi? Ya bara, ya SMZ, ya wapi mkuu?

In fact hii nchi ingekuwa na informed society/community kwa hakika watu wangesema CCM wameamua uamuzi wa Busara kuliko CUF.

Kamati ya Muafaka ilikuwa ya muhimu kwa kuwa wameweka framework ya utelekelezaji this is by all chances an important milestone.
 
hebu nisiadieni wana JF

HIVI KWELI CCM ZANZIBAR WANA UBAVU KUITIKISA CCM NZIMA pamoja na JK?
sijui wajumbe wa zanzibar wapo wangapi ktk huo mkutano.

Zanzibari ni nchi ati! kwa nini wasiwe na uwezo? na ni wakorofi kwelikweli. mara nyingi wanasema kuwa wabara wanayavamia masuala la zenji bila ya kujua wanachokifanya. na kuna uwezekano katika hili wanamcheka pia Jk kuwa aliyavamia masuala hayo buila kuyaelewa sawasawa
 

Natamani Sana Zanzibar ihakikishe kwamba kwenye issue ya Serikali ya Mseto... isiwagawe waZanzibar kiitikadi tena... iwagawe ki-uwananchi wao na ki-uzalendo wao...

Kwa hiyo hoja kama ya kwako natamani isipandikizwe kwenye mambo haya... wananchi waamue kama wananchi na sio kama CUF au CCM... ndio maana kwenye Kura ya Maoni natamani sana... issue isiwe ya ki-Chama.
 
Kura ya maoni ya nini ? Huu ni ujinga kabisa...

CUF imeshinda majimbo yote Pemba PERIOD pia imeshinda baadhi ya majimbo ya Unguja . Kwa nini tunataka kupoteza hela za walipa kodi ? why are these people so scared to make tough decisions ?

Sawa. Na CCM imeshinda majimbo yote ya Unguja (unajua hivyo). CUF imeshinda jimbo moja tu la Mji Mkongwe. Na sababu unaijua? Huko Mji mkongwe ni sehemu ya Biashara na Makaazi. Waliokuwa wakikaa huko ni Wahindi na Waarabu ambao wengi wao walihama. Hivyo kukawa kuna nyumba za biashara na majengo mengi matupu amabayo yalihamwa, baadae yakajazwa na Ndugu zetu wengi kutoka Pemba waliohamia Zanzibar Mjini. Hivyo Mji Mkongwe una wakaazi ambao wengi wao ni wahamiaji kutoka Pemba na vijana wengi wa Kipemba ambao ni (Blue Guards). Watu hawaogopi kuchukua tough decisions. lakini wanataka kuhakikisha kuwa any tough decision itakuwa kwa faida ya kweli ya hao wanaopaswa kutetewa , na sio kundi la watu wachache (wababaishaji) wanaoongozwa na jazba, tamaa na chuki Ukitaka kulielewa suala la Zanzibar angalia both sides of the coins. Wewe unaangalia Pemba tu na CUF. Jee kwa nini hutaki kuangalia Unguja na CCM-Zanzibar. Ndiyo maana basi tunakwambia tuzingatie demokrasia. Itisha kura ya maoni na usikilize maoni. halafu fuata mkondo wa demokrasia. Huko si kupoteza fedha za walipa kodi hata kidogo.
 

Zanzibar ni Nchi lakini sio Taifa... Zanzibar is a Country but not a Nation!

Tuendelee kuchangia...


Definitions:

Nation: a large body of people, associated with a particular territory, that is sufficiently conscious of its unity to seek or to possess a government peculiarly its own; The government of a sovereign state; A relatively large group of people organized under a single, usually independent government; a country.

Country: the land of one's birth or citizenship; the territory of a nation; a tract of land considered apart from any geographical or political limits; region; district; any considerable territory demarcated by topographical conditions, by a distinctive population, etc.: mountainous country; the Amish country of Pennsylvania.

sovereign state: Self-governing; independent; Having supreme rank or power

Nadhani definition hapo juu zinasaidia... haya tukate issue!!!
 

Mheshimiwa Jakaya hakuyavamia. Unaelewa kuwa Mhe. Kikwete alikaa Zanzibar kwa kipindi kinachopindukia miaka mitatu akiwa Afisa Mkuu katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. Anaielewa ZNZ vizuri. Anawaelewa Wazanzibari vizuri, kwani alichanganyika nao katika kila kitu. Anawaelewa CUF vizuri na viranja wao kwa majina, na ndiyo maana akapiga kifua kusema atasaidia kwa nguvu zake zote na kutumia kila kilicho katika uwezo wake (ikiwa ni pamoja na Urais wa Jamhuri na Uenyekiti wa CCM) kutafuta usuluhisho wa mgogoro uliopo sasa ambao umetengenezwa na kikundi cha Seif lakini unawaathiri innocent people (Pemba na Unguja)watu ambao yeye (Kikwete) anawaelewa vizuri utiifu wao na unyenyekevu wao. Endelea na nia yako nzuri Mh. Kikwete sisi tuna matumaini makubwa nawe, katika hili.
 
Kwa hakika anaiyeponda maamuzi ya NEC ya CCM na Mwenyekiti wake Mh. JM Kikwete sijui ana-promote demokrasia ipi? Ni vyema akaja na kutueleza vizuri!!!

By the way; CCM haijawahi kupata mwenyekiti ambaye anaendesha chama kwa matakwa ya wananchama wake kama ilivyo sasa!!! ndio maana mijadala inachukua muda kuhakikisha mawazo mengi yanazingatiwa.
 

Hiyo historia yako Mheshimiwa imeandikwa wapi? au umeinukuu wapi?Angalia takwimu za uchaguzi uliopita majimbo kwa majimbo. Jee wagombea wa CCM ambao walishindwa huko walipata au hawakupata kura? Kwa mtizamo wako basi na Unguja hakuna CUF? Tafuta facts halafu ujenge hoja. Usiwe mvivu Bwana.
 
 

Haya ni mawazo finyu kabisa, halafu tunawashangaa WTZ walioko vijijini kuipigia kura CCM - wanafanya hivyo kwa sababu ya njaa na wanapopewa vijisenti kidogo hao wanauza kadi ya kupigia kura.

Na wewe Mkuu umeshadumazwa kimawazo na unashukuru kwa uamuzi uliotoka bila ya kujiuliza walikuwa wapi muda wote huo wa miaka 2 bila kuitisha hiyo kura ya maoni , kupotza muda na fedha za WTZ tu.

Wameshatufikisha pabaya hadi kufikia kuwa ukitendewa haki yako unaona kama umefanyiwa ihsani - TUMEKWISHA - Niliandika humu na narudia tena kuwa CCM wananunua muda tu hadi 2010/20 na CUF ni wasanii tu kwa nini kila siku hewala bwana. Hali ya Zanzibar ni tete na wale waliokuwa hawaioni au hawataki kuelewa wajue kuwa ndio chanzo cha kuipeleka nchi hii pabaya kwani likitokea lolote inajulikana ulimwenguni kuwa ni Tanzania ..... wakimbizi wa Kitanzani, mauaji Tanzania nk - hakuna nchi inayoitwa Zanzibar.
 
Mbwe mbwe zote zile hawakuwa na muafaka wala maamuzi ? Haya wananchi wenzangu tuendelee kuvumilia .Wamesema kura za maoni je zitaendeshwaje ili kufikia makubaliano ?Hakuna watu walio jiandaa kwamba hakuna MSETO huko kweli ?
Bw. Lunyungu, wewe ni mmoja wapo ambaye huwa unachangia sana kuhusu suala hili la muwafaka, na nina imani kuwa una interest kubwa na masuala ya Zanzibar. Lakini kwa mara nyingi umekuwa na ushawishi kusikiliza sauti ya upande mmoja tu ambao ndiyo uikipgiwa kelele sana kupitia vyombo vya habari, wafadhili na propanda nyengine ambazo kule (CUF) kuna mabingwa wa kuzieleza. Sauti za wana CCM (Zanzibar) ni kubwa lakini zikivizwa na CCM yenyewe. Sasa CCM imesema wacha sauti hizo nazo na zisikike. Usione taabu kuzisikiliza, na labda tembelea Zanzibar uende vijijini Unguja uwasikie wenyewe wanasema nini. Nafikiri unaweza kupata picha ya hali hii tete ya mstakbala wa siasa za Zanzibar.
 

Hizo definition hazina maana kwa sisi huku Tanzania, Zanzibar si nci wala Taifa - kumbuka kipengele hicho ndio klichowatoa kina Seif Sharrif korokoroni katiaka kesi ya kutaka kuangusha serikali akaambiwa Zanzibar haipinduliki kama usivyoweza kusema nimepindua Rukwa kwani si Taifa hakuna dola - hii ni kwa mujibu wa wanasheria wetu.
 
hiyo ni chenga ya mwili CUF washapigwa tobo......anyway tuandamane masela wangu....
 

Hawana uwezo ila ni woga wa CCM bara, silaha ya CCM Zanzibar ni kutishia kuvunja Mungano ikiwa yao hayakukubaliwa na CCM Bara hawalitaki hilo, kwa vile CCM Znz wanajua udhaifu huo wanautumia. Nashanga kwa nini mbinu hiyo inafanikiwa kila siku kuna siri gani kuwangangania?
 
kitu ninachoshanga mie ni kuwa wakati wa kura wajumbe wa znz walimtaka DR BILALI awe awe mgombea urais wa znz,lkn ccm bara ilikuwa inamtaka AMANI,well ilivyofika dom ccm bara wakaweka chaguo lao fine ccm znz wakawa wamelizwa akina komandoo na wenzake.


leo nashangaa ccm znz hawataki muafaka/mseto/ugali etc na ccm bara wamekubaliana na hilo.
 

Hii ilikuwa zamani wapemba asilimia kubwa walihamishwa kule Mji mkongwe na Mkuu wa mkoa wa wakati huo (1995) Abdalla Rashid na wanaoishi mji mkongwe asilimia ndogo ni Wapemba na hasa mji mkongwe wenyewe sasa hivi nyumba za makazi ni chache nyumba nyingi zimegeuzwa mahoteli na maduka ya vinyago.

Ushindi wa CUF mji Mkongwe unatokana na kweli kuwa kama mahal popote pengine wakazi wa mjini wanakuwa mbele kujua mbivu na mbichi na si rahisi kuwadanganya kwa ahadi za uongo, na jengine ni mchanganyiko wa watu hakuna kuwa hapa sisis ni CCM au CUF hata aje nani hatumpi kura sipokuwa mtu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…