Mote humo CUF walishindwa. Lakini asilimia zao za kura zilikuwa kubwa walipata kati ya 30-42percent.mNa yapo majimbo Pemba ambako CCM ilishindwa lakini ilipata kura za zinazofikia asilimia 30 (Mkanyageni, Wawi, Mkoani, Mtambile ) na mengineyo.
Zanzibar ni Nchi lakini sio Taifa... Zanzibar is a Country but not a Nation!
Tuendelee kuchangia...
Definitions:
Nation: a large body of people, associated with a particular territory, that is sufficiently conscious of its unity to seek or to possess a government peculiarly its own; The government of a sovereign state; A relatively large group of people organized under a single, usually independent government; a country.
Country: the land of one's birth or citizenship; the territory of a nation; a tract of land considered apart from any geographical or political limits; region; district; any considerable territory demarcated by topographical conditions, by a distinctive population, etc.: mountainous country; the Amish country of Pennsylvania.
sovereign state: Self-governing; independent; Having supreme rank or power
Nadhani definition hapo juu zinasaidia... haya tukate issue!!!
ONCE A CROOK ALWAYS A CROOK,
Kikwete anafanya crooked politics hivyo ndivyo nchi inakwenda,
Yaani kwa kifupi mhuni ni mhuni tu irrrespective of his status.
Yapi nikumbushe walilolisema CCM na linalohusu Muafaka nimeliandika na zaidi kuhusu Muafaka walisema hakuna Mseto hapa ladda wa Choroko na mchele (NWK Ali J. Shamhuna) nafikiri unakumbuaka sasa tueleze walichosema CUF kuhusu Muafaka na sio utaje viwanja wanavyofanyia mikutano.
Tuombe Mungu busara ichukue mkondo wake na watu wapime mambo kwa kuumia kichwa na kusikiliza mioyo yao lakini hali hii ni mbaya kwa anayejua hali ya Zanzibar na kama anaishi kule basi hali sio shwari na wengi wa watu wameshafikia katika hali ya kusema hawana cha kupoteza zaidi tena kwani kama ni utu hawanao tena.
"Hakuna mseto wa mawe na chooko" Komandoo Salmin Amour
Bw.Kitila sadakta. Nilitaka kusema thanks ya jumla kwa hii yako, lakini sikubaliani na uliyoandika kuhusu Rais Kikwete. Hivyo nakushukuru hapa kwa haya niliyo ya "quote". Wafahamishe wengine waelewe. Mungu Ibariki Zanzibar Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wapemba na Waunguja ni watu wamoja. Koo na familia zao zimeingiliana (wameoleana), Ni watu wanaofanya kila kitu pamoja.Mkamate Muunguja atakwambia sijahusiana na Wapemba (kwa sababu ya kuzongwa na vitna) lakini mwite pembeni zaidi atakwambia girl friend wangu (mwandani) ni binti wa Kipemba. Na kwa Mpemba hivyo hivyo mwisho atakwambia wa ubani ni Mtumbatu au Mhadimu wa Makunduchi. Ni dhambi kubwa kuwachonganisha. Wao ni mseto Bwana, wa asili. Si deal kubwa kuwa pamoja (mseto) katika Baraza la Mawaziri.(Kwani si wameshawahi kuwa huko nyuma) Yanawezekana Bwana.. Lakini sasa ni lazima tuzibe mwanya ili kina Seif wasije wakawachafua tena Wazanzibari.Kasheshe: watu wenye mawazo kama yako haya ndiyo yanafanya baadhi ya wazanzibari watuchukie sisi wabara na muungano wetu uyumbe. Ni hivi: a country or a nation (as you call it) does not become a country or nation simply by the virtue of the population or a mere geographical positioning. A country is rather a result of a history and struggles for self-determination. Wazanzibar hawakupewa taifa lao na wabara, walilipigania kutoka kwa wakoloni. Tunapaswa kuwaheshimu kama nchi na taifa pia lililohuru na hatupaswi kabisa kuwaamuliwa mambo kama vile wao ni watoto.................... Kinachogomba Zanzibar ni kikundi cha watu fulani kufikiri kwamba wana entitlement to power kuliko wengine. Kwa sababu ya mentality hii wamekuwa wakipindisha maamuzi wanayoamua wananchi kwenye sanduku la kula. Sasa tatizo kama hili haliwezi kutatuliwa kwa kura za maoni; linapaswa kutatuliwa kwa kujenga imani kati ya makundi yanayopingana ambayo ni wapemba na waunguja first, and CUF and CCM,second. Nafasi ya muungano hapa ni ushauri tu na kusaidia raslimali za kuwawezesha wenzetu hawa kujenga imani. Sasa kitendo cha kamati ya mwafaka kushirikisha wanasiasa wa CUF na CCM pekee bila kuwashirikisha other prominent and respected citizens wa Pemba na Unguja was a fake move whose endresult couldn't be difficult to predict.
Halafu pamoja na uelewa mdogo wanaonyesha, kuna baadhi ya watu hapa wanataka kutufanya tuamini kwamba NEC ya CCM inaweza kusaidia kuiponya Tanzania, please someone out there stop me from thinking!
Mkuu Masatu,
inaonekana hii statemement imekuwa kweli hasa ukichukulia yaliyotokea Butiama. Dissapointment nyingine toka kwa Kikwete na serikali yake. Naona sasa tuendelee tu na mambo ya nchi zingine kwani inaonekana Zimbwabwe nayo inaweza kuelekea huko huko ambako itabidi Kikwete atume majeshi ya "kulinda amani" kwani haya ya ndani yamemshinda kabisaaaaa!!!!
NITAINGIA IKULU-wakitaka wasitake- sawa, sawa? Sasa hii kubembejea mseto ya nini tena? Si ni kusubiri Uchaguzi 2010 ili uingie IKULU sawa,sawa?. Watu wanabadilika (2010 kuna sura mpya inaingia kugombea Urais kwa tiketi ya CCM ) Bwana Mkubwa yupo tu. mpaka lini? Ni kheri aburutwe na Mseto. Lakini la msingi- ni huo mseto hauwezi ukafanyika kiholela. Lazima kuwe na nguvu za Kikatiba, kuwe na sheria zinazoruhusu kufanyika hivyo, kuwe na taratibu za kusimamia madaraka ya viongozi wakuu (Rais na Waziri Kiongozi ili kudhibiti mgongano na kufanikisha uwajibikaji kwa wananchi), kuwe na taratibu za kudhibiti conflicting interests. na kuwe na ridhaa ya wale ambao tunahitaji kwa nia njema kuwaletea maafikiano na harmony katika maisha yao ya kila siku. Haiwezekani watu wakurupuke na mseto tu. Haya, Seif, kuwa Waziri Kiongozi, halafu atuletee tafrani zake kati. Wewe hukumbuki visa vyake? (kikiwemo kile babu kubwa cha PLO)alichoanza nacho alipokuwa Waziri wa Elimu katika utawala wa Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.
Sasa hapo ndipo kutakapokuwa na kidonge ambacho mtu akimeza au akitema itakuwa hsauri yake. CCM yenyewe haina maafikiano kuhusu issue hiyo ya kuupiga chini muafaka, na CUF will no longer accept to play fool again and again, na kuua watu haitakuwa suluhisho, Mbona Kenya wameaua na hawakupata jibu????
Sawa, sawa. You a real think BIG. Na hapa ndipo pa kuanzia katika kutafuta lasting solution ya mgogoro huu wa Zanzibar, ambao ni wa kutengenezwa.Mimi kwa mawazo yangu ya haraka haraka, Ni ah. Sizungumzii mseto. Wazanzibari (wapemba na Waunuguja tayari ni mseto - tena wa asili). Napenda kuzungumzia hawa watu anaozungumza think Big (tena kwa pande zote CUF, CCM, Pemba Unguja). Sasa, kama kuwarudisha wafanyekazi pamoja lazima wawekewe misingi ambayo itahakikisha kuwa hawatatumia mwanya wowote kuwachonganisha Wazanzibari, misingi itakayohakikisha kuwa wanafanyakazi kwa manufaa ya mseto ambao Wazanzibari "naturally" wanao. Tusiwe na jazba za kukurupuka.Tutafute dawa ya kweli.Matatizo ya ZNZ si siasa (yaani u-CUF na u-CCM), bali ni watu! u-Unguja na u-Pemba ulikuwepo tangu wakati wa chama kimoja. Leo hii tunafikiri kuwa tatizo ni siasa za vyama tunakosea!
Kuna watu (esp Unguja) wanaamini kuwa wao ndio ZNZ, na wapemba ni sehemu tu ya ZNZ hawatakiwi kuwa kwenye madaraka. Na hata kwenye NEC imedhibitisha wajumbe kutoka Pemba waliafiki muafaka huu (kuwa na serikali ya mseto) maana wanafahamu matatizo si siasa bali watu, na iwapo watu hawa wakifanikiwa kufanya kazi pamoja basi wataelewana.
Tunaporudisha kwa wananchi ili watoe maoni yao, tunarudi kule kule kwa "watu", "wa-Unguja", "wa-Upemba", na sio wa "u-CCM" na "u-CUF".
Ikumbukwe wakati wa sherehe ya Maulid iliyoandaliwa na Rais Karume (mwaka uliopita) kuna viongozi wa kitaifa ZNZ walikataa kupigwa picha wakiwa na Sherif Hamad na hata wengine kukimbia, kisa wanaogopa kuletewa "zongwe!" Tutafika??
Kuna watu (esp Unguja) wanaamini kuwa wao ndio ZNZ, na wapemba ni sehemu tu ya ZNZ hawatakiwi kuwa kwenye madaraka. Na hata kwenye NEC imedhibitisha wajumbe kutoka Pemba waliafiki muafaka huu (kuwa na serikali ya mseto) maana wanafahamu matatizo si siasa bali watu, na iwapo watu hawa wakifanikiwa kufanya kazi pamoja basi wataelewana.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UDP, John Cheyo ameshauri vyama hivyo viendelee kukaa chini ili vikubaliane. "Sisi tulishangalia matamshi ya CUF tukadhani tumepata utawala wa aina yake wa Serikali ya Mseto ya vyama viwili Zanzibar, sasa kama sivyo basi warudi kwenye meza moja waendelee na Mazungumzo"
Amesema suala la mazungumzo hayo kuchukua muda si la msingi kwani mambo ya kijamii hayahitaji haraka. "Wakati mwingine mnaweza kufanya haraka matokeo yakawa si mazuri," alisema Cheyo