Kweli kabisa Mtanzania,

Unajua inachosha sana kuona kuwa kila linalofanyika Tanzania huyu Kikwete hana habari kabisa au hataki kuhusishwa hata kidogo.

Alisema kuwa hakuhusika Buzwagi, Richmonduli, na mengine mengi watu tukajaribu kumwelewa. Haya yaliyotokea Butiama nayo akisema kuwa hakuhusika ila watu wengi tu (ambao hawatajwi) ndio wamehusika basi hii itakuwa too much!
 
SISIEMU ni wasanii, Mie nashangaa watu kupoteza fedha za walipa kodi kwa kupanda ndege kwenda kusuluhisha Mgogoro wa Kibaki na Odinga lakini wa hapa nyumbani unawashinda. Ina maana hicho kilichowapeleka Kenya walitaka kujionyesha kuwa wenyewe ni wana diplomasia kwa mambo ya nje tu lakini ndani hawawezi kushughulikia. Jamani wananchi tuwe macho na usanii huu wa SISIEMU, sasa huko Butiama mlienda kufanya nini kama mmeshindwa hata kuwashughulikia MAFISADI??? Pum**$# kabisa. SISIEMU nchi imewashinda na siamini kama JK anastahili kipindi kingine. Mafisadi bado wanatesa na mnakaa nao meza moja, JK anawatoa wasiwasi kuwa hatataifisha mali zao, Bulls*****. Huu mpasuko wa Zanzibar utakuja leta balaa na hili balaa litaenea na kwingineko.
Watu hapo (CCM) wako kwa ajili ya kuangalia maslahi yao. Waliona wakiunda serikali ya umoja then Nahodha atapoteza nafasi yake pamoja na baadhi ya mawaziri. Jamani kwani nyie ni nani???????? Hamkuchaguliwa kuwaongoza watanzania/wanzibari maisha. Afterall nyie mmeteuliwa tu na Rais wa Zanzibar kushika hayo madaraka. Kila kitu na wakati wake, weka maslahi ya Taifa mbele. Damu ikianza kumwagika ndo mshituke kuwa mnahitaji kuwa serious (Siko hapa ku-promote umwagaji damu) Hatutaki yaliyotokea Kenya hapa, mkishindwa kuwa waungwana basi hata Watanzania watashindwa kuwa waungwana kwenu kwa kuwanyima kura wote na nyie nao mtaanza kulilia MUAFAKA.
 
mnakumbuka kwenye kikao cha NEC waliwatimua waandishi "wote" kutoka ndani ya ukumbi wao? Itakuwaje basi kama yule nzi siyo "mwandishi"? Hakikisha unasoma Raia Mwema la Kesho...

Lakini kwa kudokeza mjiulize swali hili, ni kitu gani kiliwafanya CCM wabadilishe maamuzi licha ya kujua mapema kile kilichopendekezwa na kamati ya Makamba? Wajumbe wa Zanzibar walikuja na kitu gani mkononi ambacho kiliwafanya NEC wasalimu amri?

Ule usiku wa jumamosi wajumbe wawili mashuhuri toka Zanzibar waliwasili kuwapa nguvu wenzao na wakaondoka jumatatu mapema kuwahi kikao cha Baraza la Wawakilishi.. Walikuja na hoja gani?

Hii nguvu ya kuikatalia NEC CCM Zanzibar imeitoa wapi? Kwanini Bara hawana?
 
Mwafrika wa Kike,

Nilitaka kwenda kwenye mkutano wa JK London, Lakini sasa siendi tena.

Jamaa mbabaishaji na msanii tu. Afadhali niendelee kubeba mabox yangu siku hiyo.

Aangalia, asije akawa Mugabe mwingine 2010.

Watu wameiba pesa EPA anashindwa kuwashughulikia. Muafaka unapatikana baada ya mazungumzo ya miezi 14, wanakuja na usanii mwingine, hivi huyu JK ni rais kweli?

Tutaendelea kuongozwa mpaka lini na watu wasiojali maslahi ya nchi?
 
Kikwete ni mwenyekiti wa chama, na ni mkuu wa majeshi. Alishindwa nini kufanya kama alivyofanya Kenya? Au alishindwaje kufanya kama Nyerere alivyofanya kwa Hamad na Jumbe kule Zanzibar?

Kwa nini hiki kikundi kidogo cha madikteta pale Zanzibar watuchafulie siasa ya nchi yetu yote kiurahisi hivi jamani? Ukimbizi, umwagaji damu yote haya yametokea kwa ajili ya hawa waroho wachache wa madaraka wakisaidiwa na dikteta Mkapa.

Nchi nzima inawashindwa hawa majambazi wachache kweli? Nafikiri ni wakati sasa wa kuwashughulikia kwa njia ya kimabavu kama mazungumzo hawataki tena kwa haraka kabla hawajaleta uasi mwingine kwenye chama chao.
 

Hili ni swali kubwa sana ndugu.

Kinachoumiza moyo zaidi ni kuwa wanaahidi mambo makubwa na watu tunakuwa na matumaini mengi kabla ya kupata tukiwa crashed kwa big tyme dissapointments!

Hii sasa inatia aibu. Haimsaidii Kikwete kuhamisha lawama kila wakati. Inabidi ifikie wakati afanye maamuzi mazito au afanye ushawishi ili hoja zake zikubaliwe. Otherwise, anakuwa kama everyother fisadi out there!
 
Nianze kwa kusema nawashangaa sana watu wanaotoa hoja kwanini suala la muafaka znz liwe la ccm na cuf peke yao. Watu hawa either akili zao zimeganda au they are not belonging to Tanzania. Kwanini nasema hivyo?upo ushahidi wa wazi kabisa kuwa CUF ilishinda uchaguzi mara zote lakini CCM imekuwa ikifanya Ghilba na Hadaa kama zile za ECK ya Kivuitu. Wale watu wazima ambao bongo zenu zipo sawa esp medulla mtakumbuka DTV walivyo pewa karipio kumtangaza Seif kashinda 1995 na wengi wenu mtakuwa bado mnakumbuka gaazeti la majira lilipigwa marufuku znz na ilikuwa ni kosa la jinai ukikutwa na gaazeti hilo! Hamkumbuki?Eti mwanakijiji na mwafrika wa kike hamkumbuki hivi vitu?

Tumeshuhudia yaliyotokea Kenya, tumeona jinsi ODM walivyofanya na muafaka wao ulipofikiwa ulifikiwa baina ya ODM na PNU kwanini na kuna vyama vingi sana tena idadi yake inaweza hata kuwa mara nne ya vyama vyetu? jibu ni rahisi sana. PNU ya kibaki kupitia kwa Kivuitu waliiba kura za ODM na hii ndio iliyofanywa na CCM mara zote! Msijadili mambo kisiasa hapa! tujadili mambo kwa maslahi ya ustawi wa taifa letu kwani matatizo yakitokea znz tanzania bara pia tunaingia dowa.

Umefika wakati watu waelewa historia sio wanavamia mambo na kusema sijui WAASI sijui WADINI hivi hakuna anaekumbuka kuwa mwakilishi mmoja kwenye moja ya vikao vya uwakilishi alisema "sisi tumefanya mapinduzi tumemwaga damu tukaipata hii nchi iweje leo hii tuitoe nchi hii kwa vipande vya karatasi" yaani ana amanisha kwa kupiga kura. Kwa mtazamo wa kawaida watakuwa tayari kuitoa nchi kwa kura za maoni ikiwa kura za kuchangua viongozi wanazibaka!Hawa ni watu waovu watu amabao wapo tayari waue ili wawe madarakani hawa sio watu wakuwachekea najua ma spy mpo wengi humu na na nyie ndio manao iua hii nchi! maana hampeleki taarifa za kweli mnawadanganya mabasha zenu si muwaeleze kuwa watu hawana imani nao?kuliko kuwaambia kuwa watu wanawapenda?waambieni wanalitengeneza bomu wajue znz ikilipuka bara hakutakalika pia!

Napenda nimalize kwa kusema JK hawezi kufanya kitu kwani hata zile mo than 80% za kura yalikuwa mambo ya kichina china yaani mazingaombwe kura zilizidi kila sehemu leo hii wenye akili ndio tumeanza kujua baada ya kufanya chaguzi ndogo mbili watu waliojitokeza kupiga kura hawatimii hata 50% sasa homework muifanye kila jimbo toeni 50% mtapata JK alipigiwa kura asilimia ngapi!

Alamsiki.
Sokomoko Bin Mloboko
 
--------------------------------------------------------------------------------

Mie nafikiri CUF wasikubali kuchezewa hivi. Hivi jamani CCM wanafikiri watanzania wa 1922 ndio wa sasa?? Tatizo la Zanzibar ni uendeshwaji wa jinsi ya kupata KURA HALALI, leo hii unasema upeleke hili suala tena kwa wananchi, Bulls***. Wananchi wa Pemba na Unguja (Zanzibar) walishasema na kuamua kupitia kwenye masunduku ya kura ambayo mnataka muendeshe: Wanahitaji kile ambacho wali-indicate kwenye kura zao. Sasa leo mje na usanii wenu na kuiweka AMANI yetu rehani, mmhh mmh hatukubali ujinga huu. Sasa kama suala lilikuwa kura ya maoni kwa nini mlipoteza hela za walipa kodi kuendesha hivi vikao kwa muda wote???? Yaani hakuna ambaye alikuwa na Busara ya kusema hili suala tulipeleke kwa wananchi wenyewe KWA WAKATI HUO??? Huo nao naweza kuuita UFISADI. Wape wananchi wanachostahili, hii nchi si ya SISIEMU peke yake bali ya watanzania wote. Kumbukeni kuwa CUF inawakilisha wananchi vilevile. Acheni U-ROHO wa MADARAKA na mtangulize maslahi ya Taifa mbele.

Kikwete jaribu kuwa serious for a minute, kama nchi imekushinda kwa nini usiwe jasiri na wazi wa kusema kazi imekushinda? Mmepewa dhamana ya kuongoza nchi kwa kipindi fulani na si maisha. Wananchi ambao wamekupeni hiyo dhamana wanahitaji serikali yenye mshikamano, walishatamka tangu kipindi cha Dr. Salmin lakini mnataka kupindisha ooh mrudishe kwa wananchi wenyewe. Jamani pesa zinazidi tu kutumiwa ovyo wakati wenye nchi walishaonyesha hiyo dhamira ya serikali ya umoja.
Mkuki kwa nguruwe bwana kwa binadamu mmmh sijui ni mtamu. Ilipoibuka gasia huko Kenya, watu wakapanda ndege kwenda kusuluhisha huo mgogoro na matokeo yake Katiba ya Kenya ikafanyiwa marekebisho na amani ikarejea nchini Kenya, That was really good kwa sababu sisi hatupendi machafuko nchini au kwa majirani na duniani. Ndiyo maana JK ulidiriki kupeleka majeshi yetu Comoro bila taarifa kwa Watanzania. Sasa leo hapa Zanzibar yanakuwaje magumu??????????????????????? Watu kama akina MKAPA walishindwa kwenda Butiama kujadili suala kama hilo lakini walikuwa wa kwanza kwenda Kenya kuwapatanisha Kibaki na Odinga. Nini tofauti ya Kenya na Zanzibar?? Kenya wananchi waliamua kupitia masanduku ya kura kuwa wanahitaji mabadiliko. Waliamua kwa njia halali tena na ya kiungwana, lakini Kibaki na genge lake walibatilisha maamuzi ya wananchi matokeo yake mnayajua. Sasa Zanzibar nako walishatamka kwa njia halali na ya kiungwana lakini sisi hatutaki kuona hili suala linapewa utatuzi baada ya watu kupoteza maisha yao ingawa tulishuhudia (Mimi kwa macho yangu maana nilikuwa mtumishi wa serikali) watu wakipoteza maisha kwa kudai haki zao.

Mnatakiwa kusoma alama za nyakati na kutumia Busara. Tulisikia mambo mengi eti ooh isingekuwa busara za Kingunge na Makamba hayo majadiliano yasingefika huko. Sasa hizo busara zimeishia wapi??? Au wenyewe hawakuwa katika hivyo vikao vya Butiama. Mie nafikiri umefika wakati sasa mnatakiwa mkae pembeni maana kazi imewashinda.
ACHENI USANII KWA HAYA MAMBO MAZITO. MMLETA USANII NA PESA ZA EPA SASA MNALETA USANII KWENYE AMANI AMBAYO TUMEBARIKIWA UKILINGANISHA NA NCHI ZINGINE. PLS BE SERIOUS FOR A MINUTE FOR THE SAKE OF OUR UNITY.
 
Jitahidi na tamko tuweze kupitia kila neno maana hawakawilii kusema CUF ni wa waarabu na wapenda madaraka .Hawa akina mtambo.


CUF ni chama cha kihuni ambacho kinakosa dila na msimamo. Sasa kuna kitu gani ambacho hakieleweki katika kauli zilizotolewa na CCM kuhusu muafaka?. Kuwarudishia wananchi ridhaa hiyo hamwoni kama ni jambo zuri?. Mlitaka CCM ikubali tu matakwa ya CUF bila ya kulitafakari suala hilo vizuri?. Mnafikiri CCM imejaa watu wajinga na wasio soma kama walivyojaa CUF?. BE REAL acheni kupewa vichwa na majibu na hao waarabu wenu, yatawashinda na kuwatokea puani.

Mtambo Juma Mtambo (Jitu la Mahasira)
 

ROFLMAO!!!

Baada ya kura ya maoni kuhusu muafaka, ifanyike na ya kuhusu Muungano pande zote mbili.
 
Nchi Yetu Ni Huru Na Hawa Cuf Tutapambana Nao Kwa Hoja Na Nguvu Zote Lakini Suala La Muafaka Kwa Sasa Wasahau Tanzania Ina Mengi Ya Kujadili Na Kuyafanyia Kazi Zaidi Ya Huo Muafaka

..na hii nayo ni kwa ajili ya wajinga au?

..hivi unaweza kuwa serious ukasema muafaka ungoje kwanza!?

..ngoja mapinduzi ya pili visiwani yatakapofumuka ndio waliolala watakurupuka na kukimbia kama vichaa!
 
SASA TUTAKAAJE MEZA MOJA NA WAASI ?

Kiburi chako (na hicho chama chako) kina mwisho, tena mwisho wenye aibu!

Nadhani Muasi ni yule aliyeunda Kamati ya Muafaka (ikatumia pesa kibao za wahisani) kisha mapendekezo ya Kamati (iliyokuwa na wajumbe kutoka pande zote mbili) yakashindwa kufanyiwa kazi na upande mmoja (kwasababu ya kiburi, na usanii).

CCM bado hamjasoma alama za "nyakati"! Angalia aibu anayoipata Edo sasa, alikuwa na kiburi kama hicho, angalia sasa hata sehemu ya kuweka uso hana!!
 
Hivi waziri wa muungano na makamu wa rais kutoka Pemba ni nini hasa maana eti mimi nilidhani ndio muafaka wenyewe, duh jambo usilolijua ni usiku wa giza, wazee mnaolijua zaidi tuwekeni sawa tusijua kitu,

By the way, hivi idea ya makamu wa rais kutoka Pemba ililetwa na nani?
 
mkuu Es

waziri anayeshughulikia masuala ya muungano mheshimiwa mohammed seif khatib ni mtu kutoka kusini unguja kule MAKUNDUCHI.

mpendwa na wengi hapa JF(nikiwemo mie mwenyewe)dr ali mohd shein kweli ni mtu wa pemba.
mwengine ni mohd aboud(naafikiri ni n/waziri masuala ya EA)
 


ndugu zetu wazanzibar tuko pamoja kwenye hili janga la CCM la kizandiki.
 
Ushauri wangu ni kwa CUF na wao wafanye kura ya maoni kama Wapemba wanataka kuingia katika huo mseto au wanataka Kipande chao cha ardhi - matokea yake yatajulikana na kama CCM watayaheshimu - baadae kama wakisema wanataka kipande chao cha ardhi ndio itakuja suala la kujiunga na Muungano kama mdau mwengine au la.
 
Nasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa kati ya Unguja na Pemba. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 yamedhihirisha mpasuko huo ambao naamini chanzo chake ni cha kihistoria. Lakini historia hiyo ni ya wanadamu, na wanadamu hawalazimiki kuwa wafungwa wa historia yao.
Iweje Wapemba hawa ambao ni hodari wa kutumia fursa ya Muungano wetu kwa kuishi na kufanya biashara na kuwekeza katika pembe zote za Jamhuri yetu wawe hao hao wanaojitenga kisiasa kwa kiwango tulichoshuhudia kwenye Uchaguzi Mkuu?
Wakati umefika sasa wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mpasuko huo. Nategemea ushirikiano mzuri kutoka kwa wanasiasa wa Tanzania-Zanzibar. - JK

Haya ni maneno ya JK mwenyewe wakati alipolizungumzia suala hili Bungeni mwaka 2005. Hivi ushirikiano aliosema anautegemea kutoka kwa wanasiasa wa Zabnzibar ndio huu waliompatia?
 
Naona umeshikia bango suala la Pemba kujitenga... sijui umeshafikilia athari zake vilevile au ni ushabiki tu...! mawazo mengine ni ya hatari na wala hayajengi zaidi ya kubomoa tu
 
Naona umeshikia bango suala la Pemba kujitenga... sijui umeshafikilia athari zake vilevile au ni ushabiki tu...! mawazo mengine ni ya hatari na wala hayajengi zaidi ya kubomoa tu

anacheza huyoooo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…