Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
JK aliweka nguvu zake zote kwenye muafaka wa Zanzibar, kama ameshindwa kutekeleza sasa atafanikiwa kwenye nini?
Ni dalili mbaya sana kwake kama NEC ambayo yeye ana nguvu kubwa imeshindwa kukubaliana na ushauri wake. Hiyo ni weakness kubwa sana kwa JK.
Ingelikuwa nchi za wenzetu, angelazimika hata kujiuzulu kwa hilo.
CCM inabidi watambue kwamba Tanzania ni kubwa kuliko wao na amani ya nchi ni bora kuliko pride ya CCM.
Udanganyifu wa kila siku hauwezi kuwasaidia kabisa.
Kweli kabisa Mtanzania,
Unajua inachosha sana kuona kuwa kila linalofanyika Tanzania huyu Kikwete hana habari kabisa au hataki kuhusishwa hata kidogo.
Alisema kuwa hakuhusika Buzwagi, Richmonduli, na mengine mengi watu tukajaribu kumwelewa. Haya yaliyotokea Butiama nayo akisema kuwa hakuhusika ila watu wengi tu (ambao hawatajwi) ndio wamehusika basi hii itakuwa too much!