Hapa ndipo wanasiasa wetu wanapokosea. Anaenda ulaya ili iwaje? Watakaopiga kura si anawajua? Kwa nini asizunguke nchi nzima kuwafahamisha kinagaubaga vile ambavyo anaona wameonewa?
 

Samahani, Nilisha kuambia huko nyuma. Please check kwanza ulichoandika kabla ya kutuma. Sasa sisi tunakuwa tunahisi kuwa kama tunaongea na mtoto mdogo kwenye issue nyeti kama hizi.

samahani kama wewe ni under 18 kwa sababu una haki ya kuchemsha hivyo Consistently, lakini kama ni li baba pole sana
 
Una matatizo wewe, au unataka kuvuruga tu bandiko hili linalo onyesha kwa jinsi gani Madevu aka Maalim alivyochemsha!
 
Sasa ina maana ukiwa kiongozi wa upinzania huruhusiwa kwenda Ulaya, sijaelewa kabisa mnachokisema akina Kada. Halafu kuna ubaya gani wapinzani kutafuta support ya wanasiasa wenzao huko Ulaya na America mbona wale wa vyama tawala kila siku wapo Ulaya na hatuwashangai badala yake tunawaandalia tafrija?
 

Tatizo ni huku kuiga kila kinachofanywa na chama tawala. Wao kutokana na historia wamejijenga sana katika jamii ambayo sehemu kubwa iko huko vijijini. Vyama vya upinzani ili viweze kupata credibility inabidi vieende huko kwenye grassroots. Hizo nchi za nje zina balozi zao ndani ambao bila shaka kila siku wanawapelekea taarifa. Mimi naamini ingekuwa bora zaidi kuwasiliana na balozi zao badala ya kuingia gharama ya kuzunguka dunia kukutana na desk ofisaz kwenye wizara zao za mambo ya nje. Ni nzuri kipropaganda kama ilivyo kutumia helikopta lakini I doubt effectiveness yake. Maalim angetangaza kuzunguka nchi nzima kama walivyofanya wenzake kwenye suala la madini ningemuelewa. Hii inatengeneza headline nzuri lakini wangapi katika jamii yetu wanasoma hayo magazeti?
 
"Katika mkutano huo, Maalim Seif awali alipanga kuelezea mafanikio ya mwafaka, lakini sasa ataeleza jinsi CCM ilivyowahadaa wapenda amani katika suala hilo," alisema Ismail Jussa ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu CUF.

Hivi si inaonekana alikuwa ahudhurie mkutano huo hata kabla ya maamuzi ya Butiama? Sidhani kama amejipeleka
 
Huyu jamaa anapata ruzuku ya kuwa Waziri Kiongozi mstaafu anapata posho zote za serikali. Sasa anachotaka yeye ni kinyume kwa sababu zake binafsi sitaki kumbagua kwa rangi yake au itikadi yake alitakiwa kuangalia maslahi ya Taifa hili muafaka utawasaidia wananchi na sio viongozi kutumia migongo ya wavuja jasho. Aka Wananchi
 
Maalimu Seif wewe nenda tu kawachome kwa Blair maovu wanayoyafanya kwa makusudi yajulikane.Jamani suala la ZNZ tusilifanyie mzaha hata kidogo,na kweli kama kuna mtu atakua kwa njia moja ama nyingine atakua amechangia kwa machafuko ambayo mimi naona yanaweza kutokea basi ake akijua hukumu yake ni shortcut(Death by Hanging)

Harufu inayonukia ZNZ jamani sio nzuri kabisa,Jk fanya hima juu ya hili na kama ingekua maoni basi utekelezaji wake ungekua umeanza hata leo,sasa nyie mmesema tu wananchi wahusishwe,sawa,lini sasa.Kauli hii ukiichambua kweli utagundua kuna usanii ndani yake

JK nadhani ungesimamisha shughuli zingine ukalimaliza hili,harufu yake sio nzuri President.Kama usipo yasikia haya ipo siku utakatisha ziara zako za nje.Limalize hili kwanza.
 
Hivi si inaonekana alikuwa ahudhurie mkutano huo hata kabla ya maamuzi ya Butiama? Sidhani kama amejipeleka

Kama ni hivyo, inaeleweka. Ninachopinga ni hii kusema ati anafunga safari hususan kwenda kushitaki. Waendeleze kampeni yao humu humu nchini kama walivyoanza.
 
Maalimu Seif wewe nenda tu kawachome kwa Blair maovu wanayoyafanya kwa makusudi yajulikane.Jamani suala la ZNZ tusilifanyie mzaha hata kidogo,na kweli kama kuna mtu atakua kwa njia moja ama nyingine amechangia kwa machafuko ambayo mimi naona yanaweza kutokea basi akae akijua hukumu yake ni shortcut(Death by Hanging)

Harufu inayonukia ZNZ jamani sio nzuri kabisa,Jk fanya hima juu ya hili na kwa maoni yangu nadhani utekelezaji wake ungekua umeanza hata leo,sasa nyie mmesema tu wananchi wahusishwe,sawa,lini sasa.Kauli hii ukiichambua kweli utagundua kuna usanii ndani yake

JK nadhani ungesimamisha shughuli zingine ukalimaliza hili,harufu yake sio nzuri President.Kama usipo yasikia haya ipo siku utakatisha ziara zako za nje.Limalize hili kwanza.
 
Ingawa tamko lenyewe limetolewa siku ya wajinga lakini kama inavyojulikana kwamba hata hao wajinga hawakupewa siku nzima,wameishia saa nne asubuhi! Na hata hivyo wakati mwingine stupid questions make sense kwa hiyo hatuna budi kuisheherekea siku ya wajinga!

CCM walidhani watanzania wataendelea kuwa wajinga lakini kumbe hatimaye watanzania wameamua kusomea demokrasia ukubwani na kwa kuazima maneno ya mwalimu "elimu ni kama bahari na elimu haina mwisho!

manufaa ya kujua demokrasia na kuitumia manufaa yake ni yaleyale hata kama itaonekana kama ni kuchelewa kwa baadhi ya watu. CUF walipaswa mapema kabisa kufahamu kwamba wanachofanyiwa na CCM ni sawa na mchezo wa kuigiza wenye hadithi ya Alfu ulela ulela isiyo na mwisho!

kuna baadhi ya watu humu wanaogopa vita lakini hawaogopi viashiria vya vita. kuishibikia CCM na mbinu zake za mwituni ni kupoteza muda na kuusaliti umma wa watanzania. CCM lazima iwajibishwe kwa kuielekeza nchi yetu kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe

walitaka CUF watoe nini zaidi ya hiki walichojitolea, yaani heshima yao kwa wanachama wao na wananchi kwa ujumla?
 
Kwa sababu Serikali ya Zanzibar haikuingia Madarakani kwa ridhaa ya wananchi badala yake kwa Mapinduzi yaliyoongozwa na Field Mashal John Okelo (wahafidhina naomba mnisamehe kwa kutokumtaja Abeid Amani Karume)jee na hawa kina Karume na wahafidhina wenzao kama kina Shamhuna wanaong'ang'ania madaraka kama luba nao waondolewe madarakani kwa mapinduzi?
 
Ipinduliwe na nani? Sasa naona unataka kutupeleka ambako wengine hatutaki kwenda! Hili si jambo la kufanyia mzaha hata kidogo.
 
kama mnaweza pindueni.

ila jueni kile si kikombe cha kahawa kama kinapinduliwa kwa mguu au kupigwa pute
 

Jamani hii thread imakaa vibaya kwa mtizamo wangu, jamaa anaistigate coup de tat hii inaweza kusabababisha umwagikaji wa damu hata za wasio na makosa....Wanzazibara watumie kupiga kura kuwaondoa hao akina Shamhuma, Zimbambwe wameonyesha nyia kumtoa jimbi, pamoja na kuiba kura imeshindikana...sauti za wengi ni sauti ya MUNGU
 
Haya yaliyoitwa Mapinduzi YA ZANZIBAR kipindi cha mwaka 1964 YANATOSHA!!Kwa nini tutafute mapinduzi mengine?
Hivi kweli unafikiri nchi kama hii mapinduzi ya kijeshi yatafanyika??Yatatusaidia nini wananchi wa leo??
 
""Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Mwananchi, akiwa nchini Uholanzi, Maalim Seif atajumuika na viongozi 40 mashuhuri duniani katika mkutano ambao unazungumzia masuala ya utatuzi wa migogoro.


""Maalim Seif katika mkutano huo, anatarajia kuwaeleza wajumbe hao jinsi ambavyo mwafaka wa chama chake na CCM ulivyokwama. Mjumbe mwingine kutoka Tanzania anayeshiriki kakika mkutano huo, ni Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Afrika (AU), Salim Hamed Salim.



""Katika mkutano huo, Maalim Seif awali alipanga kuelezea mafanikio ya mwafaka, lakini sasa ataeleza jinsi CCM ilivyowahadaa wapenda amani katika suala hilo," alisema Ismail Jussa ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu CUF.




Ukisoma vizuri hapo juu utagundua kuwa amekwenda kwenye mkutano sasa mngetegemea aseme nini kwenye huo mkutano,Hapa nafikiri tuwe wakweli hata kama unatofautiana na CUF au Maalimu Seif lakini ukweli unabaki palepale.
 
chama chake si kimejiondoa kwenye muafaka, sasa anaenda kusema nini ? heheee, nilidhani ataisemea CCM kwa wananchi kumbe anaenda ulaya ! Sasa sijui wapiga kura wake wapo ulaya, au vipi, i dont get it !

Statement from a Foolish person!!!
 
Mimi sina tatizo na yeye kwenda kuzungumzia hii hali katika huo mkutano. Itashangaza kama hatozungumzia hasa ukizingatia mada ya mkutano wenyewe. Nilipotoshwa na kichwa ambacho kilinifanya nidhani kuwa ametunga safari BAADA ya yaliyotokea Butiama kwenda kushitaki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…