Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Sasa ina maana ukiwa kiongozi wa upinzania huruhusiwa kwenda Ulaya, sijaelewa kabisa mnachokisema akina Kada. Halafu kuna ubaya gani wapinzani kutafuta support ya wanasiasa wenzao huko Ulaya na America mbona wale wa vyama tawala kila siku wapo Ulaya na hatuwashangai badala yake tunawaandalia tafrija?

tatizo sio kwenda ulaya, lakini intention ya trip yake kwenda ulaya ndio tatizo ! ama kweli waafrika KAMWE hatutoweza kuwa independent kwenye masuala ya maendeleo yetu wenyewe na hilo hamad seif amethibitisha !

Hao viongozi wa chama tawala sidhani na sijawahi kusoma kokote kwamba wanaenda kuwasemea wapinzani nje, lakini viongozi hao hao wa chama tawala huwasemea wapinzani kwa wananchi wao maana wanajua ndio wapiga kura zao ! i CANT expect huyu jamaa kusolve mambo ya muafaka haki ya mungu !
 
Mhhhh!!!!!!!!!!!!
Nashauri wakristo woooote hii kazi ya kupindua wawaachie waislamu kwani hata serikali yenyewe imejaa waislamu au siyo wakulu?

Hakuna haja ya mkristo kushiriki hapo.tutahamia bara woooote wakati wakipindua pindu.

pindua pindu pindu pinduuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Tatizo letu wabongo uoga umezidi,badala ya kuwatoa jamaa kwa njia ya kura watu wanaogopa,njia ya mtutu si nzuri kabisa kwa sababu mtutu unakula hata wasio jua kinachoendelea kama watoto.
 
1.Sifagilii mapinduzi ya mtutu

2. Kupindua Zanzibar katika set up ya sasa ni upunguani, utapindua Zanzibar na kuacha bara unafikiri itakuwa nini kama si mbio za sakafuni?

3.Naamini katika uhuru wa kujieleza kwa hiyo kila kitu kinaruhusiwa kama tupo ndani ya sheria.Tatizo swala la mapinduzi huwa linachukuliwa vingine kabisa hata kuweza kuwapa the powers that be uwezo wa ku suspend "civil liberties" chache tulizo nazo kwa kutumia clauses za sedition na national security.

Tusiwape msemo, wanaotaka kupindua seriously hawaongelei hilo kwenye internet boards, wanaoongelea hilo katika internet boards hawawezi kuwa serious kuhusu kupindua.

Kasheshe za uhaini waulize The Ngaizas,Banyikwas,McGhee and that Lakha lawyer kama wao au familia zao wapo watakuelezea.
 
Hawa Wazanzibari naona wameamua kuharibu dili zima!

Tunarudi kwenye siasa za jino kwa jino; ukimwaga ugali namwaga mboga tukose wote.

babu !!wee hizo si ndio siasa zao akina Seif na Mashambenga wao. Akirudi Ulaya twamsubiri Haile-sellasie tumpakulie kipya cha sabri-bachani. Mipasho roho juu-juu- mseto oyee.
 
babu !!wee hizo si ndio siasa zao akina Seif na Mashambenga wao. Akirudi Ulaya twamsubiri Haile-sellasie tumpakulie kipya cha sabri-bachani. Mipasho roho juu-juu- mseto oyee.

Karibu sana Sabri

😀 😀
 
Kwanini Maalim Seif asihamie tu huko majuu na kujifunza namna ya kuwa mpinzani?

Kwani si amekwenda mara nyingi(kwa safafi fupi) na hakuna kinachotokea?

CUF inahitaji "PURIFICATION" na kibadilishe jina lake, kwa sasa jina hilo halifai.
 
babu !!wee hizo si ndio siasa zao akina Seif na Mashambenga wao. Akirudi Ulaya twamsubiri Haile-sellasie tumpakulie kipya cha sabri-bachani. Mipasho roho juu-juu- mseto oyee.

haaaaaaaaaaaaa,

SABRI-BACHANI???????????? yakhe jibadilishe jina.

KM,MTU WA PWANI na KIBUNANGO.........hivi huyu ndio yule jamaaa wa kuleeeee au MACHO YANGU tu.
 
Kwanini Maalim Seif asihamie tu huko majuu na kujifunza namna ya kuwa mpinzani?

Kwani si amekwenda mara nyingi(kwa safafi fupi) na hakuna kinachotokea?

CUF inahitaji "PURIFICATION" na kibadilishe jina lake, kwa sasa jina hilo halifai.

Waafrika sisi bana yani kwakweli inasikitisha sana kukataa kujifunza kutokana na historia si kwamba hatujui ila kwa makusudi tu hatutaki kuelewa.

Nani alikwambia Mzungu anakutakia mema?? Yani SEIF kwa ubongo wake wote anakataa kufahamu hilo Eti anaenda kushataki Hii mpya.

Ukiona Mtu mweupe ana ingilia swala ujue ana dili kubwa kuliko analokusaidia.Kuna theory ambayo inafanyiwa kazi nayo ni-Ukiona kiongozi anatafuta suluhu ama anamashwaiba wake kutoka ulaya huyo si kiongozi tunayemtafuta HAKIKA wala msijisumbue naye.

Pili yani Maalimu anakataa kufahamu kabisa kua ili asaidiwe na watu wa ulaya lazima ameet condition hii nayo ni-ushwaiba wake na hawa wazungu lazima uwe wa hali juu kuzidi ushwaiba alio nao JK kwa akina Bush na wazungu wa ulaya.Sasa maalimu akimeet hiyo condition unadhani ni kiongozi tunayemtafuta??
 
Tatizo ni huku kuiga kila kinachofanywa na chama tawala. Wao kutokana na historia wamejijenga sana katika jamii ambayo sehemu kubwa iko huko vijijini. Vyama vya upinzani ili viweze kupata credibility inabidi vieende huko kwenye grassroots. Hizo nchi za nje zina balozi zao ndani ambao bila shaka kila siku wanawapelekea taarifa. Mimi naamini ingekuwa bora zaidi kuwasiliana na balozi zao badala ya kuingia gharama ya kuzunguka dunia kukutana na desk ofisaz kwenye wizara zao za mambo ya nje. Ni nzuri kipropaganda kama ilivyo kutumia helikopta lakini I doubt effectiveness yake. Maalim angetangaza kuzunguka nchi nzima kama walivyofanya wenzake kwenye suala la madini ningemuelewa. Hii inatengeneza headline nzuri lakini wangapi katika jamii yetu wanasoma hayo magazeti?

JK alichukua Nchi akaanza kuzunguka Dunia nzima kujitangaza kwamba ndiye Rais baada ya Mkapa je hatukusema maneno haya hapa mkawa mnabisha ? Kamaliza pesa BoT kuzunguka akaja na style ya kuwatafuta wawekezaji kwa kwenda huko na misafara.Je Hakukuwa na bado hakuna mabalozi Tanzania ? Tuliuza kama Rais wa Liberia ama Kenya ama Ghana walizunguka kujiambulisha , leo CUF wanataka msaafa wa mgogoro mnasemaje ? Vijijini wanaelewa kweli kirahisi kama si kupokea amri ya Mwenuyekiti wa Kijiji ?
 
Kwanini Maalim Seif asihamie tu huko majuu na kujifunza namna ya kuwa mpinzani?

Kwani si amekwenda mara nyingi(kwa safafi fupi) na hakuna kinachotokea?

CUF inahitaji "PURIFICATION" na kibadilishe jina lake, kwa sasa jina hilo halifai.

Mmekuja na jina la CUF tena na si mgogoro wenyewe ? Jamani mie nashangaa yaani Butiama CCM wameacha kufanya ya maana kw ajina la CUF ? Mwandishi huyu hadui hamjaona kana kwamba yeye kaongeza chumvi.Kuna mkutano wa namna ya kutatua migogoro na Seif anaenda huko .Mkutano uliuwepo hata kabla ya NEC kujiandaa na CUF walialikwa huko .Haya mambo ya Butiama yamekuja wakati akiwa na safari hiyi nje ya Nchi .Mgogoro hata kama Seif asingalisema US na wengine walianza kukoroma mapema .Nadhani kuna ushabiki hapa na kuacha kujiuliza na ndiyo maana CCM wanachekelea maana wanajua mambo ya mana tutayajadili kama mpira wa Arsenal na Man U.
 
JK alichukua Nchi akaanza kuzunguka Dunia nzima kujitangaza kwamba ndiye Rais baada ya Mkapa je hatukusema maneno haya hapa mkawa mnabisha ? Kamaliza pesa BoT kuzunguka akaja na style ya kuwatafuta wawekezaji kwa kwenda huko na misafara.Je Hakukuwa na bado hakuna mabalozi Tanzania ? Tuliuza kama Rais wa Liberia ama Kenya ama Ghana walizunguka kujiambulisha , leo CUF wanataka msaafa wa mgogoro mnasemaje ? Vijijini wanaelewa kweli kirahisi kama si kupokea amri ya Mwenuyekiti wa Kijiji ?

Sasa mkubwa
Kwa vile JK alitembea dunia nzima basi na Maalimu afanye hivyohivyo??
sasa nini tofauti kati ya Maalimu na JK kama wote wanatumia staili ile ile kuna sababu gani ya kumbadirisha JK na kumweka Seif??
 
Back
Top Bottom