Mkandala mkuu heshima yako!
Mkuu mimi kama kijana wa miaka ya 80 nisiyejua lolote kuhusu zanzibar zaidi ya simulizi za hapa na pale nina hamu hasa ya kujua historia ya zanzibar japo yale muhimu tu.Kwa mfano hilo swali ulilouliza mkuu kama itawezekana ningependa ujijibu mwenyewe ili na sisi wengine tuelimike.Na kabla ya hapo kama unavyosema chaguzi za nyuma zilikuwaje,sasa embu tueleze basi.
Halafu naskia Karume baba mtu ni mtu wa malawi kuna ukweli wowote?je alifikaje zanzibar?Kama yeye siye muhusika mkuuwa Mapinduzi nani ndiye alihusika zaidi?Kwanini uhuru wa 1963 ni halali/si halali?Pia chama cha hizbu kilikuwa cha nani na nani na kwanini Dr.Salim A.Salam alihisishwa nacho kama tuhuma za kumchafua 2005?Kwanini pia Nyerere alimpenda sana Dr.Salim hata kumpa vyeo vikubwa wakati akiwa na umri mdogo tu na ilifikia hata(kama kweli),kumuomba kama mara mbili hivi awe Rais wa Muuungano ilhali wajumbe wa CCM zanzibar hawamkubali Dr.Salim?
Kwanini Nyerere kama inavyosemekana alifanya hizo hila ili Tanganyika iungane na zanzibar kwa gharama yoyote ile,faida yake kwake ilikuwa nini hasa?
Mkuu ukinijibu haya utakuwa umenisaidia sana
Shukrani mkuu
 
Mtarajiwa,
Bila shaka mkuu nadhani site hii itakusaidia zaidi yangu mimi. Nitakushauri kitu kimoja tu Usome historia yenyewe badala ya mawazo ama dhana za mwandishi kwani pale panaposema INASEMEKANA ina maana hakuna uhakika...
http://www.zanzinet.org/zanzibar/history/historia.html

Swala La Karume kuwa alitoka Malawi?.. well, nambie Kiongozi Mzanzibar ambaye hana asili ya nje!
Kuhusu Salim A. Salim, soma kipande kinachohusu Umma Party wale waliokuwa wakiitwa wacommunist.. kina Abraham Babu.
Kwa nini Zanzibar hawamkubali hilo nadhani waulize Wazanzibar wenyewe - pengine hilo la Ukommunist (fagio la mafisadi) ni zaidi ya rangi yake kwani wapo wengi CCM wenye rangi na asili kama yake..
 
uhuru tuliopewa 63 na muingereza ss huiita uhuru bandia na nnaamini mbunge hafidh alishtuka kutokuwekwa neno hilo bandia.

maana uhuru huu ilikuwa ni kujiondoa muingereza na kuhamishia mamlaka kwa sultan wa zanzibar kwa fupi kwa mwaraabu.

mapinduzi ya zanzibar yamekuja kumkomboa mtu mweusi au muafrika na kumpatia utawala kitu ambacho muingereza hajakifanya


sasa uhuru wa kweli kwa wananchi ni mapinduzi ya 64 na ccm wa zanzibar ndivo tuaminivyo ama ndugu zetu wa cuf wanaamini kinyume
 


wiki ijayo mola akipenda zamu yangu kutoa khutba ktk sala ya ijumaa,so ngojea nimalizie kutunga then nitakujibu.
 

siku hizi hawaendi tena GUANGZHOU wamehamia KUALA LUMPUR,wanadai china vitu bei ghali sana siku hizi.
 
Hakuna maana ya serikali ya umoja wa kitaifa sehemu moja ya muungano...

Vyama vyote vya upinzani visubiri kitu kama hicho uchaguzi unao fuata....

Muafaka wa zanzibar ni matokeo ya mabadiliko ya siasa Za Tanzania...

CUF...sijui mmenielewa..
 
ON THE DREAM OF FREEDOM (1963): "So even though we face the difficulties of today and tomorrow, I still have a dream. I have a dream that one day this nation will rise up and live out the true meaning of its creed . . . that all men are created equal.
Martin Luther King, Jr
 
Maelfu wajitokeza Zanzibar kupinga matamshi ya CCM kuhusu muafaka
*Wabeba mabango yenye ujumbe kuwaonya mahafidhina
*Mvua kubwa yashindwa kuvunja maandamano yao
* Maalim Seif ataka uchaguzi 2010 usimamiwe na UN
* Mbowe awataka wasilale mpaka kieleweke



Na Salma Said, Zanzibar
MAELFU ya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) jana walijitokeza katika maandamano ya kupinga tamko la kura za maoni, lililotolewa Butiama na Chama Cha Mapinduzi (CCM) juu ya mazungumzo ya kutafuta Mwafaka wa visiwani Zanzibar.Wanachama hao waliovalia nguo za rangi nyekundu, nyeupe na bluu huku wakiloweshwa na mvua kubwa iliyonyesha asubuhi mjini hapa wakiwa na viongozi wao walibeba mabango mbalimbali yenye ujumbe wa kuwaonya wahafidhina wasioitakia mema Zanzibar na Tanzania.

Baadhi ya mabango yalikuwa na ujumbe ufuatano: "Wahafidhina nchi mnaisukuma, vizazi vitawasema…, tunahitaji kura ya maoni juu ya muungano"... Kenya na Comoro ni kama wenzako, Zanzibar ni kwako"..."ikiwa Makamba wewe huelewi ni nani basi Seif ni Katibu Mkuu wa CUF"... Zanzibar hakuna amani na utulivu kuna imani na ustahamilivu"... "kura ya maoni hii ni janja ya nyani tu tumeng'amua. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliongoza maandamano hayo akiwa na viongozi wenzake wa vyama vya upinzani, wakianzia viwanja vya Maisara karibu na nyumba ya Fatma Karume, Mama wa Rais wa Zanzibar, Abeid Amani Karume. Waandamanaji hao walijipanga mapema asubuhi katika Barabara ya Maisara wakapitia eneo la kwa Raju, Miembeni, Komba Wapya, Mwembeladu hadi Kibanda Maiti, ambapo walifanya mkutano mkubwa wa hadhara uliohutubiwa na viongozi wao.

Wakati maandamano hayo yakifanyika gari la polisi lenye nambari T198AMV lilikuwa mbele ya viongozi wa maandamano hayo.Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad alisema, chama chake kitaendelea kudai haki yake kwa njia za kidemokrasia bila ya fujo, hadi itakapopatikana lakini alisisitiza hatarejea katika mazungumzo ya mwafaka.

"Wakati umefika sasa sisi kuingia uwanjani sisi hatutaki fujo, tutachukua njia za kidemokrasia hadi haki ipatikane," alisema.Maalim Seif alisema kitu cha kwanza ambacho wanakihitaji kuliko yote ni kutia saini makubaliano kwa kuwa, katika miafaka ya huko nyuma CCM wamekuwa wakikataa kutekeleza makubaliano ya vikao baina ya vyama hivyo. "Kwanza kuweka saini, then (halafu) kuendelea maana wenzetu wana historia hiyo ya kutoheshimu na kukataa kutekeleza. Tukimaliza kuzungumza wanaitikia, lakini hawatekelezi sasa hivi sisi tumesema hapana tuweke saini kwanza," alisema Maalim Seif. Katibu Mkuu huyo alisema iwapo CCM watakataa kutia saini makubaliano ya kuunda kwa serikali ya mseto Zanzibar, basi wafahamu kwamba CUF haitokubali kuingia tena katika uchaguzi wa mwaka wa 2010 na watazunguka dunia nzima, kutaka uchaguzi huo usimamiwe na Jumuiya za Kimataifa. Maalim Seif alipinga kauli ya wanaomuona yeye kuwa ni laini na kusema kwamba, kama wangelijitoa katika Mwafaka ule, dunia nzima ingewaona ni watu wa ajabu.

"Mimi jamani sio mlaini, watu wengi wananiambia mlaini kwani najua siku za mwongo ni 40 na sasa imefika siku yao, tungejitoa siku ile dunia nzima ingetulaumu," amesema.

Maalim Seif alisema wanaofikiria kwamba CUF inataka kuingia madarakani ili yeye awe Waziri Kiongozi, wanajidanganya kwani hana haja na ukubwa kwa kuwa tayari ameshawahi kuwa na nafasi hiyo huku akijihesabu kuwa yeye ndio rais wa Zanzibar tangu mwaka 1995 ulipomalizika uchaguzi kwa kuwa alishinda.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alisema aliwataka CUF kutumia nguvu ya umma kukataa kuonewa.

"Nazungumza kwa uchungu kabisa kwa sababu tunajua Zanzibar ni chemchem ya mageuzi ya demokrasia, mmevumilia sana tangu 1995 mmechukua subira, sasa uvumilivu ufikie kikomo, ajenda hii sio ya CUF bali ni ya kitaifa," alisema Mbowe huku akishangiliwa.

Mbowe alisema hakuna kulala hadi serikali ya mseto ipatikane na hakuna jeshi la polisi ambalo litakuwa na mabomu na risasi za kuwamaliza Wazanzibari wote, kwani wameshawahi kufanya hivyo na wakashindwa kuwamaliza. Aliwasihi viongozi wa CUF kutokubali kufanywa watumwa na CCM na kuwataka kuacha kuwasilikiza na kurejea kwenye meza ya mazungumzo, kwani kufanya hivyo ni kukidhalilisha chama na taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema alisema, ili kupatikana suluhu ya mgogoro wa Zanzibar atafutwe hakimu wa kimataifa atoe hukumu juu ya nani mkweli katika hilo.

"Kuna mgogoro mkubwa sana kati ya CCM na CUF Zanzibar, sasa tutafute mahakimu wasikilize pande zote mbili mlalamikiwa na mlalamikaji kisha atwambie pumba ni zipi na mchele ni upi," alisema.

Mwenyekiti huyo alisema CCM ni watu wanafiki na hawana nia wala dhamira ya kumaliza mgogoro na wanachokifanya ni kuonyesha umoja wa mataifa na nchi jirani kwamba wanaweza kuleta suluhu Zanzibar.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed alisema, watakapomaliza maandamano watarejea bungeni na kama Spika atakataa kuwapokea hilo halitakuwa jambo kubwa kwao, kwani kitu muhimu ni kuangalia maslahi ya taifa kwanza kuliko kitu chochote.
 
CUF ukweli ni kuwa kikulacho kinguoni mwako wahenga walisema, hata mkiandamana usiku na mchana haisaidii kwa sababu wanaowaangusha ni hao viongozi wenu ambao ni wazi kuwa ni waroho wa madaraka.
ninachowaonea huruma tu ni kuwa mkiendelea kuandamana mtalambwa virungu na FFU huku viongozi wenu wakikimbilia ughaibuni.

waswahili wanasema dawa ya jino ni kung'oa, so ondoeni viongozi wenu mamluki hao kisha ingieni kwenye uchaguzi muone matokeo yatakuwaje.
 


Swali kwa wadau mnisaidie: Hivi hawa akina Mrema, Lipumba, Maalim Seif n.k ndiyo watu pekee kwenye vyama vyao wanaoweza/stahili kushika madaraka ya Urais kiasi kuwa ni lazima kila kipindi wagombee wao tu?
 
.....Game, ni kweli kabisa, tukipata watu wengi kutoka visiwani kutaleta balance makiri. Tatizo ni kuwa wakiona traffic nyingi zinaelekea kwenye JF servers, hawacheleweshwi kuanza kukatiwa umeme kila kukicha...... be it metaphorically.

Aaa kule wana web yao wanaiita zanzibarwebsite humo ni mawaidha tu sasa kama munataka JF iwe kiriri cha citation ya vitabu vitakatifu wakaribisheni bila hivyo inabidi muwaelimishe kuwa kuna maisha ya hapaduniani na ya akhera.
 

CUF wanaamini hivyo hivyo ila wanataka kuboresha ili uwe kwa faida ya Waafika wote sio leo serikali nzima ina Waziri mmoja, Mkatibu wakuu wawili, Wakurugenzi/Mameneja wa idara au mashirika ya serikali watatu nk kutoka sehemu nyengine ya Zanzibar au ndio ilikuwa lengo ndio lengo la Mapinduzi au kule hakuna WAFIRIKA?
 

Itakuwa vema ukifafanua zaidi hapo kwenye rangi nyekundu
 
Waombe hao CUF wasipate huo MKATABA WA MUUNGANO baina ya TANGANYIKA na ZANZIBAR ambao ni siri kubwa kuliko siri zote Tanzania

Mkataba original uliosainiwa au makubaliano kwa ujumla kwa maana kama ni makubaliano haya hapa.

The Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar

--------------------------------------------------------------------------------
THE ARTICLES OF UNION

between

THE REPUBLIC OF TANGANYIKA AND THE PEOPLES' REPUBLIC OF ZANZIBAR

WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar being mindful of the long association of the peoples of these lands and of their ties of kinship and amity, and being desirous of furthering that associatio! n and strengthening of these ties and of furthering the unity of African peoples have met and considered the union of the Republic of Tanganyika with the Peoples Republic of Zanzibar:

AND WHEREAS the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples'Republic of Zanzibar are desirous that the two Republics shall be united in one Sovereign Republic in accordance with the Articles hereinafter contained:-

It is therefore AGREED between the Governments of the Republic of Tanganyika and of the Peoples' Republic of Zanzibar as follows: -

(i) The Republic of Tanganyika and the Peoples' Republic of Zanzibar shall be united in one Sovereign Republic.

(ii) During the period from the commencement of the union until the Constituent Assembly provided for in Article (vii) shall have met and adopted a Constitution for the united Republic (hereinafter referred to as the interim period) the united Republic

(i! ii) to (vi).

shall be governed in accordance with the provisions of Articles

(iii) During the interim period the Constitution of the united Republic shall be the Constitution of Tanganyika so modified as to provide for-

(a) a separate legislature and executive in and for Zanzibar from time to time constituted in accordance with the existing law of Zanzibar and having exclusive authority within Zanzibar for matters other than those reserved to the Parliament and Executive of the united Republic;

(b) the offices of two Vice-Presidents one of whom (being. a person normally resident in Zanzibar) shall be the head of the aforesaid executive in and for Zanzibar and shall be the principal assistant of the President of the United Republic in the discharge of his executive functions in relation to Zanzibar;

(c) the representation of Zanzibar in the Parliament of the United Republic;

(d) such other matters! as may be expedient or desirable to give effect to the united Republic and to these Articles.

(iv) There shall reserved to the Parliament and Executive of the united Republic the following matters-

(a) The Constitution and Government of the united Republic.

(b) External Affairs.

(c) Defence.

(d) Police.

(e) Emergency Powers.

(f) Citizenship.

(g) Immigration.

(h) External Trade and Borrowing.

(i) The Public Service of the united Republic.

(j) Income Tax, Corporation Tax, Customs and Excise.

(k) Harbours, Civil Aviation, Posts and Telegraphs.

And the said Parliament and Executive shall have exclusive authority in such matters throughout and for the purposes of the united Republic and in addition exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika.

(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject-

(a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

(b) to such provision as may be made by order of the President of the united Republic for the extension to Zanzibar of any law relating to any of the matters set out in Article (iv), and the revocation of any corresponding law of Zanzibar;

(c) to such amendments as may be expedient or desirable to give effect to the union and to these Articles.

(v) (a) The first President of the united Republic shall be Mwalimu Julius K. Nyerere and he shall carry on the Government of the united Republic in accordance with the provisions of these Articles and with the assistance of the Vice-Presidents aforesaid and of such other ministers and officers as he may appoint from Tanganyika and Zanzibar and their respective public services.

(b) The first Vice-President from Zanzibar to be appointed in accordance with the modifications provid! ed for in Article (iii) shall be Sheikh Abeid Karume.

(vii) The President of the united Republic: in agreement with the Vice-President who is head of the Executive in Zanzibar shall-

(a) Appoint a Commission to make proposals for a Constitution for the united Republic.

(b) Summon a Constituent Assembly composed of Representatives from Tanganyika and from Zanzibar in such numbers as they may determine to meet within one year of the commencement of the union for the purpose of considering the proposals of the Commission aforesaid and to adopt a Constitution for the united Republic.

(viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

IN WITNESS WHERE Julius K. Nyerere, the President of the Republic of Tanganyika, and Abeid Karume the President of the Peoples' Republic of Zanzibar have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April, 1964.

Passed in the National Assembly on the twenty-fifth day of April, 1964.

Watu wakipata huu mkataba wanapata chao wanakaa kimya, jamaa mmoja alivyosema hapo juu.
 

Siku zote JF itakuwa imevamiwa pale muziki unaopigwa unapokuwa sio mzuri katika masikio yako...

Muziki mzuri ni ule wa sera ya mtoto wa nyoka ni nyoka kamata chinja - hii ndio "slogan" ya CCM Zanzibar na wewe unaorodhesha habari za Alinacha.
 
CUF watangaza kudai haki kwa nguvu ya umma

*Lipumba awataka vijana kuanza mazoezi
*Seif:Butiama yalifanyika mazingaombwe
*Prof. Othman ahoji kura ya maoni ya nini?
*Asema Karume angekuwa hai, angesikitika

Na Masau Bwire, Zanzibar

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimefanya maandamo makubwa kupinga uamuzi wa NEC-CCM kutaka iitiswe kura ya maoni juu ya kuunda Serikali ya mseto Zanzibar na kuwataka vijana wa chama hicho kote nchini kujiandaa kwa mazoezi tayari kudai hatma yao kwa njia ya amani kwa nguvu ya umma.

Maandamano hayo yalifanyika jana kuanzia viwanja vya Maisara na kumalizikia katika viwanja vya Kibanda Maiti ambapo ulifanyika mkutano wa hadhara.

Maandamano hayo yaliyoambatana na mvua kubwa kupitia maeneo ya Kilimani, Miembeni, Kariakoo, Biziredi na Mikunguni pia yalishirikisha vingozi wa vyama vya siasa vya TLP, CHADEMA na NCCR-Mageuzi, wabunge na wawakilishi wote wa CUF na wageni wengine mbalimbali.

Akihutubia umma wa wananchi waliofurika viwanjani hapo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad alisema CCM wamekiuka mazungumzo ya muafaka yaliyovikutanisha vyama hivyo mara 21 kwa kipindi cha miezi mitatu na kutumia pesa za watanzania sh. milioni 210.

Aliuita uamuzi wa CCM katika kikao chake cha Butiama kuwa ni mazingaombwe ya kisiasa yanayolenga kuvuruga amani visiwani humo.

Maalim Seif aliongeza kuwa kura ya maoni katika suala la muafaka haihitajiki kwani katika muafaka walikubaliana juu ya mambo matano likiwemo la kuunda Serikali ya mseto lakini hakuna mahali walipopatana kufanya kura ya maoni.

Alisema CCM imeanzisha hoja hiyo mpya kwa lengo la kuchelewesha utekelezaji wa muafaka ambao ulitakiwa kutiwa saini tu na kuanza kutekelezwa. Alisema kitendo hicho kimelenga kufikia uchaguzi mkuu ujao bila kuwepo serikali ya mseto ili watu wapate nafasi ya kuiba kura.

Aliipinga kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa saini ya Katibu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba na yake kuwa haziwezi kuamua matatizo ya Zanzibar ni kujidhalilisha na inaonesha dalili kuwa CCM haiuamini uwezo wa Katibu Mkuu wake.

Naye Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba alimtaka Rais Kikwete atumie nafasi yake katika kuliweka sawa jambo hilo kwani alisema pamoja na makosa yaliyofanyika Butiama bado anayo fursa ya kuufanya muafaka usainiwe na kutekelezwa.

Alisisitiza kuwa Rais Kikwete asipofanya hivyo heshima yake itashuka katika jumuiya za kimataifa kwani CUF wako tayari kuzunguka duniani kote kuzungumzia suala hilo iwapo CCM itaendelea kuwa 'kichwa ngumu.'

Alisema maandamano hayo ni mwanzo tu, kwani CUF inaandaa maandamano mengine katika mikoa ya Morogoro, Dar es salaam, Mwanza, Bukoba, Tabora na kisiwani Pemba.

Naye kiongozi wa upinzani bungeni ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazungumzo upande wa CUF na mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid Mohamed alisema wao hawatatishika kwa kunyimwa posho bungeni, wataendelea kudai haki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw. Freeman Mbowe alisema Zanzibar ni chemchem ya mageuzi na demokrasia ya kweli, na ikiwa serikali ya mseto itaundwa Zanzibar na Bara pia itafuata.

Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augustine Mrema alisema CCM hawana dhamira ya kweli juu ya muafaka Zanzibar na kwamba wanafanya mchezo wa kuigiza wakifikiri watu hawana akili ya kuwang'amua.

Alisema wazo la kuundwa kwa serikali ya mseto halikuibuliwa na CUF bali lilianzishwa na marehemu Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1995 mara baada ya matokeo ya urais wa Zanzibar kutangazwa na kuwepo tofauti ya kura kidogo kati ya Maalim Seif na Salmini Amour Juma.

Bw. Mrema amemtaka Rais Kikwete afanye kama alivyofanya nchini Kenya, awakutanishe Maalim Seif na Rais Karume, wafikie makubaliano na waunde Serikali ya mseto Zanzibar.

Naye Hassan Abbas anaripoti kuwa msomi mahiri nchini ambaye pia ni manju katika siasa za Zanzibar, Profesa Haroub Othman Miraj wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ameukosoa msimamo na tamko la CCM lililotolewa hivi karibuni Butiama akisema haoni kama kuna dhamira ya kweli ya kulitatua tatizo la kisiasa visiwani Zanzibar.

Profesa Othman ameyasema hayo katika mahojiano maalum na gazeti hili ambapo ameeleza pia kusikitishwa kwake na msimamo huo mpya wa CCM na kushauri kuwa jamii ishinikize kupatikana kwa mwafaka huo haraka.

" Rais Jakaya Kikwete alipoliarifu Bunge kwamba ana azma ya kilipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo la mpasuko wa kisiasa Zanzibar, wananchi wengi wa Bara na Visiwani walifurahi. Ilipoundwa kamati ya pamoja ya CCM na CUF matumaini ya wengi yalikuwa kwamba sasa mambo yatanyooka.

"Kwa wengi tuliokuwa tukifuatilia mazungumzo hayo kulikuwa na wasi wasi baadhi ya wakati kwamba labda yalikuwa hayapewi kipaumbele inachostahiki; lakini bado tulikuwa na imani kwamba Rais atatimiza ahadi yake. Sasa kusema kweli sidhani kwamba ipo dhamira na utashi wa kisiasa wa kulimaliza tatizo hili," alisema.

Akizungumzia kitendo cha CCM kuna na mapendekezo mapya likiwemo la kutaka maamuzi yafanywe na wananchi kupitia kura ya maoni, Prof. Othman amepinga suala hilo akisema hiyo ni staili ya kulikataa jambo hilo.

"...Sidhani kwamba viongozi wakuu wa CCM na wa CUF walikuwa hawajui nini kimekubaliwa. Nataka kuamini kwamba walikubaliana nayo. CUF waliyakubali hadharani. Ikiwa katika CCM viongozi wa juu walikuwa na mashaka nayo, haikuwa na haja kuyaharakisha kwenye Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa," alisisitiza na kuongeza:

"Kwa maoni ya mtu wa kawaida, kusema kwamba viko vipengere vizungumzwe upya au kuleta dondoo jipya ni njia ya kistaarabu ya kusema huyakubali."

Prof. aliunga mkono haki ya wananchi kuhojiwa katika masuala ya msingi kitaifa lakini akasema: "Wananchi kuulizwa juu ya mambo mbali yanayowahusu na yanayohusu taifa ni wajibu. Lakini katika hili wananchi waulizwe nini?

"Ilipobadilishwa katiba ya Tanzania na kumuondosha Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais na badala yake kuwepo na mgombea mwenza, wananchi waliulizwa? Kwa hakika badiliko lile liligusa msingi wa Makubaliano ya Muungano (Articles of Union), lakini hatua ilichukuliwa na Bunge!"

Akaonesha wasiwasi wake kuhusu muelekeo wa hali ya amani iliyoanza kurejea visiwani humo na kugusia kuwa mwafaka wa kisiasa si jambo la kudumu la kuumaliza mpasuko uliotokea lakini lingesaidia kuepusha maafa zaidi.

Akizungumzia mwenendo wa sasa wa siasa za Zanzibar na visheni aliyokuwa nayo awali aliyekuwa Rais wa kwanza wa visiwa hivyo hayati Abeid Aman Karume, Prof. Haroub anaeleza kuwa kuna kukinzana.

"Nadiriki kusema mengi yangemsikitisha. Mapinduzi ya mwaka 1964 yalikusudia kuondosha dhulma, uonevu, uhasama, na yalilenga kuleta usawa na kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida. Mzee Karume alielezea dhamira hizo katika tamko alilolitowa pale uwanja wa Maisara siku ya tarehe 8 Machi 1964."


majira
 

Prof Haroub Othman is my HERO ...... Tanzania imejaliwa kuwa na watu kama Prof Othman. CCM wasichukulie maneno na mitizamo kama hii kwa dharau. Wazanzibari ni binadamu na wanahitaji kuchukuliwa kama binadamu na kuheshimiwa kwa mitizamo na mawazo yao bila kuingiliwa na mamluki na watu wachache mabinafs.
 
Binafsi huu wote ni Upuuzi mtupu!.. mtanisamehe wakuu, kwani hawa viongozi walitegemea kitu gani haswa!...Ombi lolote lina majibu mawili...hakuna sheria.
Hili swala lilitakiwa kushughulikiwa baada tu ya matokeo ya Uchaguzi.. Hizi ahadi za kuunda serikali ya mseto ulikuwa mbovu toka mwanzo na haikutakiwa kuwepo suluhu yoyote ikiwa mshindi alikuwa CUF..
Kutegema matokeo ya Butiama miaka miwili baada ya uchaguzi tena kinyume cha sheria yaani rais ndiye kupewa uamuzi badala ya sheria ni upofu wa kutoona mbali...Tunazitukuza sheria za mtungo sisi wenyewe!..Kifungu gani cha sheria kinachosema rais anaweza kuunda serikali ya mseto ikiwa chama chake kitapendekeza hivyo!

CUF walikubali ku shake hand na Devil sasa hivi lawama zote ni bure kwa sababu walipotaka serikali ya mseto haikuwa matakwa ya wananchi waliopiga kura. Makubaliano yalikuwa kati ya CUF na CCM bila kuwashirikisha wananchi wala kufuata sheria ya uchaguzi. Leo imekuja shindikana CUF wanataka kurudisha swala hili kwa wananchi..
NGUVU ya UMMA ni kura walizopiga wananchi ambazo CUF wenyewe walikubali kutozipa uzito toka siku matokeo ya kura na wakachagua kuunda Muafaka nje ya sheria za kura..Imeshindikana basi wajifunze somo hilo.. kuomba nguvu ya UMMA ni kutafuta machafuko yasiyokuwa na msingi kwani wananchi waliwekwa nje na kizani siku zote wakati ahadi za Uongozi zilipokuwa mezani...Walichoambiwa ni Muafaka wa muundo wa serikali ya Zanzibar (Kikatiba) na sio sharing power na CCM baada ya ushindi wa CUF.
Morgan wa Zimbabwe pamoja na makosa yake madogo madogo mwanzoni, sasa hivi amekataa kurudia upiganji kura wala swala la Mseto ikiwa matokeo yanaonyesha wazi chama chake kimeshinda. Hakuna mazungumzo isipokuwa kesi hii amewaachia vyombo vinavyohusika pamoja na wananchi
 
wiki ijayo mola akipenda zamu yangu kutoa khutba ktk sala ya ijumaa,so ngojea nimalizie kutunga then nitakujibu.



Eng Mo umenifurahisha sana. Tafadhali usitunge tunge tupe ya ukweli ya kutunga tunga hayafai mheshimiwa.

Kuna mtu mmoja mkubwa sana aliwahi kusema Prof Abdulrahman Babu ndie anaeijua Historia ya Zanzibar vizuri na atakuwa hajaitendea haki jamii ya wazanzibari akifa bila ya kuiandika. Huyu bwana mkubwa alisema maneno hayo kwasababu Prof Babu alikuwa ni msomi! na mtu mwenye uweledi wa historia ya zanzibar. Historia tunayoijuia sisi sio ya kweli mambo mengi yamepikwa pikwa! historia inayopatikana kwenye tovuti ya zanzinet hamwongelei John Okelo na kuna watu wanadai wakati wa mapinduzi yenyewe mhe Karume sr alikuwa Dar msasani na mkewe wala sio yeye aliyeongoza mapinduzi! Tunahaja ya kuwasihi wazanzibari waingie JF watupe vipande vipande wanavyovijua ili tuunge tupate japo picha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…