Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 129
Visa sasa vyaanza Zanzibar
na Mwandishi Wetu
UPEPO wa kisiasa visiwani Zanzibar umeanza kuchafuka na kuonyesha dalili za kuibuka vitendo vya uvunjifu wa amani, iwapo viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), hawatachukua hatua za haraka na za makusudi za kuafikiana kuhusu namna ya utekelezaji wa makubalino ya muafaka.
Hali hiyo inadhihirishwa na kuibuka kwa kasi kwa siasa za chuki na uhasama, zinazoambatana na maneno ya kukashifiana na kutukanana baina ya makundi ya wafuasi wa vyama vya CCM na CUF, siku chache baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kutoa tamko la kupigwa kura ya maoni itakayoamua uanzishwaji wa serikali ya mseto visiwani humo.
Aidha, uamuzi huo wa CCM umesitisha pia kuanza kutekelezwa kwa rasimu ya muafaka kati ya vyama hivyo viwili, ambao katika maazimio yake ulikuwa ukitaka kuanzishwa kwa nafasi za Makamu wa Rais wa kwanza na wa pili kwa Zanzibar, huku nafasi ya Waziri Kiongozi iliyopo sasa ikifutwa.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo ya makubaliano ya vyama hivyo viwili iliyochapwa kama ilivyo ndani ya gazeti hili leo, Kamati ya Muafaka ya CCM na CUF ilifikia makubaliano ya kufungua ukurasa mpya wa kimahusiano kati yao ambao ungemaliza uhasama uliodumu visiwani kwa miaka mingi sasa.
Taarifa zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili kutoka Zanzibar jana, zilieleza kuwa, hali ya wasiwasi imetanda miongoni mwa wananchi, baada ya kuanza kusambazwa kwa vikaratasi vinavyowataka Wazanzibari wenye asili ya Pemba, kuondoka katika Kisiwa cha Unguja kwa madai kuwa hakuna tena uundwaji wa serikali ya mseto.
Taarifa zilieleza kuwa, limeibuka kundi la vijana katika kisiwa hicho wanaozunguka mitaani wakiwa katika malori huku wakitoa maneno ya kuipongeza CCM kwa kutaka kuwepo kura ya maoni juu ya serikali ya mseto Zanzibar.
Mbali na kundi hilo la vijana, kundi jingine linalopongeza uamuzi wa chama hicho ni la wazee wa CCM wakieleza kuwa hiyo ndiyo demokrasia.
Baadhi ya wananchi kutoka kisiwani hapo walieleza kuwa, vijana hao wamekuwa wakipita mitaani katika malori hayo, huku wakiipongeza CCM kwa uamuzi wake huo sambamba na kutoa maneno ya maudhi kwa wapinzani wa hoja ya kura hiyo ya maoni.
Wanaodaiwa kulengwa zaidi na vijana hao ni wafuasi wa CUF ambao wamekuwa wakikashifiwa wakati wakiwa katika mabaraza ya nyumba zao.
Habari zaidi zinaeleza kuwa, mmoja wa watu waliopata viperurushi vyenye maneno ya vitisho yanayowataka Wapemba kuondoka katika Kisiwa cha Unguja ni Mwakilishi wa Jimbo la Mkanyageni, Dadi Faki Shaali (CUF).
Malalamiko mengine ya kuibuka vitendo vya ubaguzi visiwani humo yametolewa na baadhi ya wasafiri wanaotoka Unguja kwenda Pemba kuwa, wanasakamwa na kupekuliwa isivyostahili.
Wakati hali ikiwa hivyo katika Kisiwa cha Unguja, taarifa zilizopatikana kutoka Kisiwa cha Pemba zilieleza kuwa, vijana wa Pemba wamesema wapo tayari kubaki kwao na baadhi wameapa kutokanyaga tena Unguja.
Wachambuzi wa siasa za Zanzibar wameeleza kuwa, fitna za kisiasa zenye lengo la kuonyesha kuwepo kwa mwenendo mbaya wa hali ya mambo kila unapotokea utata wa kisiasa baina ya vyama vya CCM na CUF zimekuwa jambo la kawaida.
Hata hivyo, kusambazwa kwa karatasi hizo za vitisho kumezua wasiwasi na hofu ya nini kitafuata baada ya vitisho hivyo, huku baadhi ya watu wakifanya matayarisho ya kuwahamisha wazee, ndugu na watoto wao kutoka Pemba kwa hofu ya kuibuka vurugu zinazoweza kusababisha Wapemba kuanza kupigwa.
Hali hiyo imechochewa zaidi na uvumi unaoenezwa sasa kuwa, serikali imepanga kupeleka vikosi vya askari polisi visiwani humo kutoka Tanzania Bara ili kuimarisha ulinzi kutokana na vitisho hivyo.
Wakati hilo likiendelea, wafuasi wa CCM wamekuwa wakieneza uvumi kwamba Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa amekimbilia nje ya nchi kukwepa upinzani mkali kutoka kwa vijana wa chama chake, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipinga kufanyika kwa mazungumzo kati ya vyama hivyo viwili.
Uvumi wa Maalim Seif kukimbia, ulifikishwa katika chumba cha Tanzania Daima Jumapili majuzi kutoka kwa mmoja wa wasaidizi wakuu wa kiongozi mmoja wa juu serikalini.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Ismael Jussa Ladhu, ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa Maalim Seif aliyapuuza madai ya kiongozi wake huyo kutoroka nchi, akisema alikuwa ameenda nje ya nchi katika kikao muhimu cha watu mashuhuri duniani, ambako Afrika imetoa watu wawili, Maalim Seif na Dk. Salim Ahmed Salim.
Source:Tanzania Daima Jumapili