Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Visa sasa vyaanza Zanzibar

na Mwandishi Wetu

UPEPO wa kisiasa visiwani Zanzibar umeanza kuchafuka na kuonyesha dalili za kuibuka vitendo vya uvunjifu wa amani, iwapo viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), hawatachukua hatua za haraka na za makusudi za kuafikiana kuhusu namna ya utekelezaji wa makubalino ya muafaka.

Hali hiyo inadhihirishwa na kuibuka kwa kasi kwa siasa za chuki na uhasama, zinazoambatana na maneno ya kukashifiana na kutukanana baina ya makundi ya wafuasi wa vyama vya CCM na CUF, siku chache baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kutoa tamko la kupigwa kura ya maoni itakayoamua uanzishwaji wa serikali ya mseto visiwani humo.

Aidha, uamuzi huo wa CCM umesitisha pia kuanza kutekelezwa kwa rasimu ya muafaka kati ya vyama hivyo viwili, ambao katika maazimio yake ulikuwa ukitaka kuanzishwa kwa nafasi za Makamu wa Rais wa kwanza na wa pili kwa Zanzibar, huku nafasi ya Waziri Kiongozi iliyopo sasa ikifutwa.

Kwa mujibu wa rasimu hiyo ya makubaliano ya vyama hivyo viwili iliyochapwa kama ilivyo ndani ya gazeti hili leo, Kamati ya Muafaka ya CCM na CUF ilifikia makubaliano ya kufungua ukurasa mpya wa kimahusiano kati yao ambao ungemaliza uhasama uliodumu visiwani kwa miaka mingi sasa.

Taarifa zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili kutoka Zanzibar jana, zilieleza kuwa, hali ya wasiwasi imetanda miongoni mwa wananchi, baada ya kuanza kusambazwa kwa vikaratasi vinavyowataka Wazanzibari wenye asili ya Pemba, kuondoka katika Kisiwa cha Unguja kwa madai kuwa hakuna tena uundwaji wa serikali ya mseto.

Taarifa zilieleza kuwa, limeibuka kundi la vijana katika kisiwa hicho wanaozunguka mitaani wakiwa katika malori huku wakitoa maneno ya kuipongeza CCM kwa kutaka kuwepo kura ya maoni juu ya serikali ya mseto Zanzibar.

Mbali na kundi hilo la vijana, kundi jingine linalopongeza uamuzi wa chama hicho ni la wazee wa CCM wakieleza kuwa hiyo ndiyo demokrasia.

Baadhi ya wananchi kutoka kisiwani hapo walieleza kuwa, vijana hao wamekuwa wakipita mitaani katika malori hayo, huku wakiipongeza CCM kwa uamuzi wake huo sambamba na kutoa maneno ya maudhi kwa wapinzani wa hoja ya kura hiyo ya maoni.

Wanaodaiwa kulengwa zaidi na vijana hao ni wafuasi wa CUF ambao wamekuwa wakikashifiwa wakati wakiwa katika mabaraza ya nyumba zao.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, mmoja wa watu waliopata viperurushi vyenye maneno ya vitisho yanayowataka Wapemba kuondoka katika Kisiwa cha Unguja ni Mwakilishi wa Jimbo la Mkanyageni, Dadi Faki Shaali (CUF).

Malalamiko mengine ya kuibuka vitendo vya ubaguzi visiwani humo yametolewa na baadhi ya wasafiri wanaotoka Unguja kwenda Pemba kuwa, wanasakamwa na kupekuliwa isivyostahili.

Wakati hali ikiwa hivyo katika Kisiwa cha Unguja, taarifa zilizopatikana kutoka Kisiwa cha Pemba zilieleza kuwa, vijana wa Pemba wamesema wapo tayari kubaki kwao na baadhi wameapa kutokanyaga tena Unguja.

Wachambuzi wa siasa za Zanzibar wameeleza kuwa, ‘fitna’ za kisiasa zenye lengo la kuonyesha kuwepo kwa mwenendo mbaya wa hali ya mambo kila unapotokea utata wa kisiasa baina ya vyama vya CCM na CUF zimekuwa jambo la kawaida.

Hata hivyo, kusambazwa kwa karatasi hizo za vitisho kumezua wasiwasi na hofu ya nini kitafuata baada ya vitisho hivyo, huku baadhi ya watu wakifanya matayarisho ya kuwahamisha wazee, ndugu na watoto wao kutoka Pemba kwa hofu ya kuibuka vurugu zinazoweza kusababisha Wapemba kuanza kupigwa.

Hali hiyo imechochewa zaidi na uvumi unaoenezwa sasa kuwa, serikali imepanga kupeleka vikosi vya askari polisi visiwani humo kutoka Tanzania Bara ili kuimarisha ulinzi kutokana na vitisho hivyo.

Wakati hilo likiendelea, wafuasi wa CCM wamekuwa wakieneza uvumi kwamba Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa amekimbilia nje ya nchi kukwepa upinzani mkali kutoka kwa vijana wa chama chake, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipinga kufanyika kwa mazungumzo kati ya vyama hivyo viwili.

Uvumi wa Maalim Seif kukimbia, ulifikishwa katika chumba cha Tanzania Daima Jumapili majuzi kutoka kwa mmoja wa wasaidizi wakuu wa kiongozi mmoja wa juu serikalini.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Ismael Jussa Ladhu, ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa Maalim Seif aliyapuuza madai ya kiongozi wake huyo kutoroka nchi, akisema alikuwa ameenda nje ya nchi katika kikao muhimu cha watu mashuhuri duniani, ambako Afrika imetoa watu wawili, Maalim Seif na Dk. Salim Ahmed Salim.

Source:Tanzania Daima Jumapili
 
Ah. Fundi Bwana, Be realistically, katika Population ya Wazanzibari wapatao Milioni Moja wakiristo ni wangapi Mheshimiwa? (Hivi wanafikia angalau 50 Elfu)?

Mimi sijui. Kwani wangazija wako wangapi? Na wangapi wako serikalini?

Kilichonistua ni kuwa hii idadi inaelekea ni katika viongozi wakuu wote wa serikali. Huyo Mwakanjuki ni miaka nenda rudi. Kweli hakuna wakristu wengine wanaostahili? Ninachojua mimi ni kuwa katika jamii ya wakristu Zanziba kuna dhana kuwa wanabaguliwa na wanafanywa second class citizen. Hii dhana ni ya hatari na serikali yeyote iliyo makini inabidi iiangalie kwa undani. Ili waweze kutoa mchango wao kikamilifu katika jamii, serikali ni vizuri kama ikiwahakikishia wao na minorities wengine (wangazija, wahindi n.k) kuwa wana nafasi katika nchi yao. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa sehemu zilizomuhimu ( sehemu za kuabudia n.k)katika jamii na uwakilishi katika serikali vinapewa kipaumbele. Sijui kama hili linafanyika. Ni rahisi sana kwa walio wengi kuwasahau ndugu zao walio wachache. Ni vyema kuwasikiliza wakina Mukombosi na sio kutoa majibu ya mkato. Avaae kiatu ndiye anayejua wapi kinambana.
 
1. Sitapenda kujadili historia ya Zanzibar, asili ya mtanziko wa kisiasa huko; lakini mimi naomba nichangia suala la principle tu hapa- kwamba pande mbili zimekaa zimajadiliana na kukubaliana mambo Fulani Fulani; baadaye upande mmoja umeanza kwenda tofauti. It’s a political problem, that needs a political solution.
2. Nimesoma neno kwa neno rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM ambayo ilishakubaliwa na kamati zote mbili. Suala la serikali ya pamoja linapaswa kutekelezwa kabla ya mwaka 2010.
3. Nimesoma ripoti ya Kamati ya CCM iliyopeleka Butiama kwa ajili ya Kamati Kuu na baadaye halmashauri Kuu; ukweli ni kuwa hoja ya kura ya maoni haikuzuka kikaoni- iliandaliwa kabla kwa pendekezo la Karume na kukubaliwa na wanakamati. Pamoja na uzuri wa dhana ya kura za maoni, lakini nia(motive) yake hapa si nzuri! Kwa serikali ambayo haifanyagi referendum katika masuala muhimu kihistoria kama Muungano, Katiba, Mfumo wa Vyama vingi, kumuundoa Rais wa Zanzibar kama makamu wa Rais(ambalo lilikuwa ni suala katika makubaliano mama ya muungano); inatia shaka serikali kama hiyo itakapo suala la kura za maoni Zanzibar. Ni Kikwete huyu huyu ambaye alipokwenda Kenya hakutaka wakina Raila na Kibaki wafanye kura za maoni, akata wasaini makubaliano na kuyatekeleza. Wakati wa kuibwa kwa kura hakuitishwa kura za maoni, kosa moja haliwezi kuhalalisha kosa, lakini kosa moja linaweza kutoa ishara ya kosa lingine! Kwa ujumla ukiisoma ripoti hii ya Kamati ya CCM; ukisoma na Barua ya Mwisho ya Makamba; utagundua kuwa Makamu Mwenyekiti Msekwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete- hawakusema kweli wakati wakieleza mchakato wa Maazimio ya NEC ya CCM na Matokeo yake!
4. Nilikuwepo Diamond Jubilee jana na nimemsikiliza Lipumba toka mwanzo mpaka mwisho. Nilichokielewa ni kwamba CCM imekuwa ikiwatapeli CUF toka baada ya uchaguzi, ikiwafanyia unafiki wa hali ya juu- CUF nayo kwa upande wake ilikuwabali ku-give in too much; ikakubali ghilba za aina zote ikiwa na matumaini makubwa kwamba Kikwete yuko genuine! Na kwa kiasi kikubwa mambo yote haya yalifanyika kwa siri ya pande mbili; kwa mategemeo makubwa ya CUF kwamba pengine serikali ya mseto ingetokea. Kumbe CCM wakati wote ilikuwa ikiweka kadi chache mezani na nyingine nyingi zaidi kuzificha chini ya meza.Ukiangalia mtiririko wa matukio katika hii miaka mitatu kuhusu Zanzibar utagundua ama Rais Kikwete anafanya unafiki wa hali ya juu wa kisiasa, au ni kiongozi dhaifu katika CCM kama mwenyekiti anayezidiwa nguvu na makundi mengine ndani ya chama chake. Kwa vyovyote vile, hali hii ikiachwa bila panga kuitwa panga na si kisu kikubwa ni ishara mbaya kwa utangamano wetu kama taifa haswa kwa kuwa kwa sasa CCM ndicho chama tawala!
5. Tunaungana mkono na CUF katika hili, kwani kitisho cha demokrasia mahali Fulani ni kitisho cha demokrasia mahali pote. Maandamano ya jumamosi, hayapaswi kuwa maandamano ya CUF, yanapaswa kuwa maandamano ya umma! Ama hakika, uwongo una mwisho- lakini ukweli unapaswa husimama milele, na ukweli hauna itikadi. CUF wanaweza kuwa walijikwaa mahali Fulani katika mchakato huu; lakini sasa ni wakati wa kutazama mbali zaidi, kutazama picha kubwa zaidi- CCM ikiwachwa ikapita katika hili, itandelea kuacha na ufisadi mwingine ukatawala kwenye RICHMOND, BOT nk na hatimaye kuweka misingi ya ufisadi wa kudumu zaidi katika uchaguzi mkuu 2010. Hatupaswi kuacha utadamuni wa ufisadi, usanii wa kisiasa, uchezeaji wa haki, na wananchi kukaaa pembeni kama watazamaji na wanyooshaji vidole kuendelea katika taifa letu. Ni wakati mwingine wa kuandelea kuchukua hatua!
JJ

PS:
• Mwenye Hotuba ya Jana ya Lipumba atuwekee hapa tafadhali
• Mwenye rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM iliyokubaliwa na kamati za pande mbili aiweke hapa pia tafadhali
 
Hivi ni kweli tunataka makubaliano ya CCM na CUF ndio yabadilishe katiba?
 
Kwa kukumbushana tu, CuF imewahi kufanya yafuatayo:-
  • Kupaka vinyesi katika shule
  • Kuweka vinyesi vya binadamu katika visima vya maji
  • Kulipua mtambo wa ugawaji umeme Zanzibar(kidatu)
  • Kutoa talaka kwa wake zao ambao ni ccm
  • kugoma kushiriki katika shughuli za maziko
  • kugoma kushiriki katika shughuli za arusi
  • Na pengine kuanzisha hadithi za popo bawa 😀

Unaposema CUF walifanya inamaana CCM hawakuusika hata kidogo. lakini ninavyojua ni kuwa hata CCM played the same fujo kwa CUF populated areas. kwahiyo ni matatizo ya wote na sio CUF tu.
 
Mimi nasuport kura ya maoni kama inasimamiwa na wasimamizi kutoka nje maana wa kwetu ni manyangau wanaoiba kura kila siku hatuwezi kuwaamini tena. CCM hawana nia ya kweli kutekeleza muhafaka bali ni kubuy time mpaka uchaguzi wa 2010 utakaoleta majadiliano ya miaka 3 mingine.
 
CUF sio chama Kizuri kwasababu Tanzania Nzima hakuana Chama Kizuri!!!..Lakini kwenye Muafaka lazima wasikilizwe..CCM..JK Umekosea hapo...!!serikali ya mseto ni muhimu..japo kwa kuhaidi itategemea Uchaguzi unao fuata...
 
Kwa kukumbushana tu, CuF imewahi kufanya yafuatayo:-
  • Kupaka vinyesi katika shule
  • Kuweka vinyesi vya binadamu katika visima vya maji
  • Kulipua mtambo wa ugawaji umeme Zanzibar(kidatu)
  • Kutoa talaka kwa wake zao ambao ni ccm
  • kugoma kushiriki katika shughuli za maziko
  • kugoma kushiriki katika shughuli za arusi
  • Na pengine kuanzisha hadithi za popo bawa 😀

Niksoma post kama hizi huwa nakumbuka thread ya Rev. Kishoka jamaa JF tumeingiliwa maanake kwa mtu mwenye akili timamu anajua hayo yaloandikwa hapo juu yote yalikuwa ni propaganda za CCM au yawe ya kweli yanazidi mauaji ya makumi ambayo ulimwengu mzima unajua yalifanywa na CCM na katika waliouawa ilikuwa hata maandamano hayajaanza. Au kijana alopigwa risasi Kilimahewa halafu Marehemu Dr. Omar akasema risasi ilitungwa hewani halafu ikashuka chini ikauawa mtu.

Walimwengu tuwe na haya tunapoelezea jambo lolote na ikiwa ni ushabiki uwe mioyoni mwetu.
 
Siku zote JF itakuwa imevamiwa pale muziki unaopigwa unapokuwa sio mzuri katika masikio yako...
 
Tarehe ya uhuru wa Zanzibar yazua mtafaruku Bungeni
Ramadhan Semtawa said:
Dodoma

MKANDA unaotumika katika kompyuta, ambao umeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, umeibua mkanganyiko katika Bunge la Muungano jana, baada ya kuonyesha kwamba Zanzibar ilipata uhuru wake mwaka 1963. Akitafuta mwongozo wa Spika baada ya kipindi cha maswali na majibu jana asubuhi, Mbunge wa Dimani Hafidh Ali Tahir (CCM), alisema mkanda huo unaeleza muungano ulifanyika baada ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961 na Zanzibar mwaka 1963.

Tahir alifafanua kwamba, kutokana mkanda huo kupotosha historia, baadhi ya wabunge wa CUF bungeni wamekuwa wakiutafuta kwa udi na uvumba ili waonyeshe dunia kwamba kumbe historia ya visiwa hivyo inapotoshwa. “Mheshimiwa Spika naomba mwongozo wako, hapa kuna Disk ambayo imesambazwa kwa wabunge na wenzetu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, lakini disk hii imepotosha historia ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,” alisema na kuongeza;

''Sasa hivi mkanda huu unasakwa na wenzetu wa CUF, wanataka kuutumia kuonyesha dunia kwamba, historia ya Zanzibar inapotoshwa. Ninavyojua mimi, Zanzibar ilipata uhuru baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, mwaka 1964. " Tahir, alisema Bunge ni chombo nyeti, hivyo kitendo cha wizara kuandaa mkanda kama huo bila kuuhakiki kwa makini kisha kuupeleka bungeni, ni makosa hivyo akaomba mwongozo wa Spika katika hilo .

Alisema ndani ya mkanda huo pamoja na mambo mazuri ya kueleza vivutio vya utalii, lakini kuna mwanamke mmoja anajitokeza na kuzungumzia historia hiyo ambayo inapotosha historia halisi.
Baada ya kuomba mwongozo, Tahir pia alitaka kanda hizo zikusanywe na zirudishwe wizarani zikafanyiwe marekebisho kuliko kuendelea kuzisambaza. Kutokana na ombi la mbunge huyo, Spika alisimama na kukiri ofisi yake kusaidia mawasiliano na wizara ili kanda hizo zisambazwe kwa wabunge.

Sitta alifafanua kwamba, atamuita Waziri wa Maliasili na Utalii kwa ajili ya kupata maelezo ya kina. Alisema suala hilo halitapaswa kufika wiki ijayo, hivyo litazungumzwa wiki hii.
“ Sisi tulisaidia mawasiliano na Wizara ya Maliasili na Utalii, lakini nitakutana na waziri,” alisisitiza Spika. Historia ya Visiwa vya Zanzibar ambayo kwa sehemu kubwa imetawaliwa na Sultan, imejaa utata kuhusu lini hasa uhuru wa kweli ulipatikana.

Wachambuzi wanaamini historia hiyo ndiyo inayotesa visiwa hivyo hasa Pemba na Unguja, huku sehemu kubwa ya Wapemba wakiamini uhuru kamili ulipatikana mwaka 1963 chini ya Waziri Mkuu, Mohamed Shamte kutoka Zanzibar National Party (ZNP). Hata hivyo, Waunguja wengi ambao wana asili ya Afrika, wanaamini mapinduzi ya Januari 12, 1964 ndiyo halali kwani yaliondoa utawala wa Shamte, ambaye wanadai alikuwa kibaraka wa Waarabu ambao walikuwa na ngome zaidi Pemba .

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya Wapemba wanaamini uhuru kamili ulipatikana mwaka 1963 hivyo kilichofanyika mwaka 1964 ni mapinduzi haramu dhidi ya utawala halali.

Source: Mwananchi.
 
Ndio maana wengine wanfikia kulia na kusema CUF wakijumuishwa kwenye Serikali Historia itafutika! Lakini ukweli ni kwamba wao ndio wamefuta historia si kweli kwamba Karume baba ndie alieendesha mapinduzi! na ukweli unaojulikana ambao CCM hawautaki ni uhuru uliopatikana 1963 Zanzibar wangekuwa wanauwezo wangewatoa watu kumbukumbu hiyo kweny vichwa vya watu.

Hawa ndio watawala anaowasema Mzee Mwanakijiji kuwa tuwazirie nchi. Hawa ni viongozi wanaotaka kuandika historia ya upande mmoja! huo uhuru ulikuwa na mazuri na mabaya yake na haya mapinduzi yana uzri na ubaya wake na ubaya ni kuwa waliuawa watu wengi sana wengi wao waarabu wasiokuwa na hatia. Na mpaka leo wanapindua tu ile kadhia ya Jan 26 na 27 2001 ni muendelezo wa Mapinduzi Zanzibar.
 
Waombe hao CUF wasipate huo MKATABA WA MUUNGANO baina ya TANGANYIKA na ZANZIBAR ambao ni siri kubwa kuliko siri zote Tanzania
 
Sokomoko,
Umesema Uhuru halali ulipatikana 1963 na ndio historia halisi ya Uhuru wa Zanzibar, sasa nakuomba unijibu moja tu!...
Nani alikuwa rais? ama kwa lugha nyepesi akiyekabidhiwa kiti cha Ikulu..
Ikisha hilo pia fikiria chaguzi zilizopita kabla ya hiyo 1963 kulitokea nini hata isiwe ndio siku ya Uhuru wa Zanzibar!
 
Waombe hao CUF wasipate huo MKATABA WA MUUNGANO baina ya TANGANYIKA na ZANZIBAR ambao ni siri kubwa kuliko siri zote Tanzania

Kunawakati Mzee Karume alisema "Muungano ni kama koti ukiona linakubana unalivua" Nyerere aka mind sana!!! hii ni baada ya mkumstukia Mzee mwenzie alivyokuwa akimpelekapeleka.

Na kwa taarifa yenu msiojua mambo Muungano ulifanikiwa kwasababu yale mapindizi ya 1964 yalikuwa haramu! Nyerer alitumia karata yake kufanikisha Muungano kwa hoja ya Mapinduzi!

Kuna wanaojua zaidi humu kwenye JF tunawaomba mtupe kwa kirefu zaidi.
 
......... nilifikiri nao huu uko wikileaks.org tayari !!! lol

Bado na nasikia wale jamaa waliofungua kesi kule Unguja sasa hivi wana multiple visa za kwenda Guangzhou, China na mwingine sasa hivi anataka kufungua shopping centre kubwa la maana kule Kariakoo (znz)

Engineer Mo atakuwa anajua zaidi kuhusu hili. In short hakuna anayejua kesi iliishia wapi
 
Kunawakati Mzee Karume alisema "Muungano ni kama koti ukiona linakubana unalivua" Nyerere aka mind sana!!! hii ni baada ya mkumstukia Mzee mwenzie alivyokuwa akimpelekapeleka.

Na kwa taarifa yenu msiojua mambo Muungano ulifanikiwa kwasababu yale mapindizi ya 1964 yalikuwa haramu! Nyerer alitumia karata yake kufanikisha Muungano kwa hoja ya Mapinduzi!

Kuna wanaojua zaidi humu kwenye JF tunawaomba mtupe kwa kirefu zaidi.

The only question kuwa tukianza kuujadili Muungano na fitna za Nyerere kuna watu hawatoweza kustomach Mwalimu akiwa criticized as if Mwalimu alikuwa Saint

cha muhimu ni kurecruit watu wa visiwani waje humu JF ili kupata balance

wazo lako ni zuri sana
 
Bado na nasikia wale jamaa waliofungua kesi kule Unguja sasa hivi wana multiple visa za kwenda Guangzhou, China na mwingine sasa hivi anataka kufungua shopping centre kubwa la maana kule Kariakoo (znz)

Engineer Mo atakuwa anajua zaidi kuhusu hili. In short hakuna anayejua kesi iliishia wapi

Engineer Mo tupe habari sio vizuri kukalia habari watu wanakalia makalio Yakhe hawakalii habari.

Hii ndio Afrika ikijifanya unajua unanunuliwa wengi tumewaona wakinunuliwa wakati wao ndio walikuwa wapinzani halisi kumbe walikuwa makada wapinzani! si mnawajua? kina Akwilombe, Tambwe, Ngawaiya, Chief Fundikira na wengine wengi... hata nyie mashushu wa JF mnaingia kwenye kundi hili. Lakini JF hamuiwezi huu ni moto wa gesi teh teh teh teh teh
 
The only question kuwa tukianza kuujadili Muungano na fitna za Nyerere kuna watu hawatoweza kustomach Mwalimu akiwa criticized as if Mwalimu alikuwa Saint

cha muhimu ni kurecruit watu wa visiwani waje humu JF ili kupata balance

wazo lako ni zuri sana
.....Game, ni kweli kabisa, tukipata watu wengi kutoka visiwani kutaleta balance makiri. Tatizo ni kuwa wakiona traffic nyingi zinaelekea kwenye JF servers, hawacheleweshwi kuanza kukatiwa umeme kila kukicha...... be it metaphorically.
 
Back
Top Bottom