Ahaa! Sasa nimekuelewa...kumbe suala la wizara ya mambo ya nje pia lilichomekwa kinyemela...then ina maana huu wa sasa uko so diluted...ule original uko wapi?

Sasa ndio hujaelewa kabisa nilikwambia suala la Mashirikiano ya KImataifa ndio limechomekwa kinyemela kwani mwanzo ilikuwa ni Mambo ya nje tu na hapo Zanzibar walikuwa na uhuru wa kushirikiana na Mashirika na nchi rafiki hasa katika masuala ya uchumi na ndipo wakati huo Zanzibar iliweza kushiikiana na nchi yeyote au Mashirika yeyote ta Kimataifa bila ya ruhusa kutoka serikali ya Muungani ilimradi masuala hayo hayahusu siasa - ndio lilipoonekana hilo ikabidi kichomekwe kipengele cha Mashirikiano ya Kimataifa. Wizaera ilikuwa ya Mambo ya Nchi za Nje tu na sasa imekuwa Mambo ya Nje na Mashirikiano ya KImataifa.
 
...Hakuna haja ya kusoma soma huo mkataba mambo yalisha isha

...Nyerere alichanganya Udongo ... sijui uo mchanganyiko upo wapi..?Labda ulimwagwa baharini ... ...

...lakini kwenye kuvunja muungano haito wezekana

Unajua ishu sio kutaka kuvunja muungano. Isitoshe, nadhani usiri uliotanda juu ya hiyo hati ndio unanazorotesha Muungano. Mambo yamepita, ndio, lakini na sehemu ya historia. Sio kwa sababu ni hadithi za kujifurahisha bali ni muhimu hata katika kuulewa na kuutetea huu muungano kujua nini kilitokea. Moja ya giza nene lililofunika huu muungano ni kwamba hakuna mwenye nakala ya hati ya Muungano. Hiyo iliyotundikwa hapa sio original document. (Angalia hata ilivyo jaa mi - typo! Nyaraka ya Muungano, iliyo andikwa na wanasheria, ikapitiwa na Bunge haiwezi kuwa na mi typo.)

Kwenye kesi ya Muungano iliyosikilizwa Zanzibar mwaka 2003 Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alishuhudia kwamba hajawahi kuiona hati ya Muungano. Na inasemekana haipo. Nyerere ndio anajua ilipokwenda, na aliamua kufa nayo. Kina Kawawa, na marehemu Kambona na Hanga na wengine wachache wanasemekana waliiona hii hati siku ya kwanza. Zaidi ya hapo hakijulikani.

Kwa hiyo huu usiri unachangia kudhoofisha muungano, na kutafiti ukweli hapa sio sawa na kutaka kuvunga Muungano.
 

asante, labd akwa hapo sasa unanifunua macho na akili kuona kuwa je, suala la OIC lilikuwa haliingilii siasa ya nchi? Si Muungano wa nchi za kiislamu duniani, na kwa mujibu wa katiba yetu hilo suala lingekuwa kwenda kinyume na katiba kwa sababu inatamka wazi kuwa serikali haina dini...

Najua hili suala ni tete na limeshajadiliwa kwa kina sana hapa lakini naliangalia katika muktadha wa mkataba wa muungano....kwa maoni yangu hata bila ya kuwepo neno ushirikiano, bado ilikuwa ni kukiuka mkataba wa muungano na katiba ya nchi
 

Hapo siwezi kujua kama walitaka kuingia kwa sababu za kisiasa lakini walivyosema ni kwa ajili ya kupata misaada ya kiuchumi kama wenzao wengine mojawapo ikiwa ni Uganda nchi yenye idadi kubwa ya raia walio Wakiristo kumbuka hapa Tanzania tuna Ubalozi wa Vatican ambao uwakilishi wake unatambuliwa na serikali yetu jee hapo tutasema Serikali ina dini au haina?

Kama ulivyosema tusilijadili hili suala kwani linaweza kugusa hisia za imani zetu za dini na sio lengo hapa. Kama utanikubalia kuwa mkataba wa Muungano umekuwa tampered sawa kama hukubali pia ni sawa - kuna uhuru wa mawazo na mimi naheshimu hilo.
 

Nakubaliana na wewe Bikirembwe kuwa hili suala ni tete ijapokuwa sikubaliani na mfananisho wa ubalozi wa vatican nchini na suala la Zanzibar kujiunga na OIC...pia maadamu sijaona mkataba original inakuwa vigumu kukataa kuwa huu tulio nao haujatiwa mikono na wajuaji kama kawaida
 

Jamani Kawawa si yuko hai tukipata nafasi ya kumhoji atajibu maswali mengi tu kuhusiana na serikali yetu miaka ya mwanzoni.
 

Mapato ya Dhahabu, Tanzanite, na Uranium itapotoka... Zanzibar inapata haya mapato kwenye gawiwo lake lile la 4.5%
 
Katika dunia hakuna muungano wa NCHI isipokuwa huu uliokuwepo hapa East Africa ,nakumbuka ulijaribiwa Misri na Syria haukufika mbali.
Hivi kuna mtu aneweza kuniambia kama ziko nchi zimeungana kama hizi za Tanganyika na Zanzibar ? Nasubiri jibu ?
 
Katika dunia hakuna muungano wa NCHI isipokuwa huu uliokuwepo hapa East Africa ,nakumbuka ulijaribiwa Misri na Syria haukufika mbali.
Hivi kuna mtu aneweza kuniambia kama ziko nchi zimeungana kama hizi za Tanganyika na Zanzibar ? Nasubiri jibu ?

Mimi najua United Arab Emirates. Pia kuna zile zenye muungano wa tofauti kama vile United States of America na United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland. sina uhakika na muungano wa visiwa vya Comoro wanaita The Union of comoros.

Spirit ya Umoja/Muungano naiunga mkono. Ningependa hata tuungane na Comoro, Malawi, Zambia, Kenya, Ugandaetc. Ila ule Muungano kama wa US.
 

US hakuna muungano hivi uliwahi kusikia kuna nchi inaitwa Chicago au Texas ,tazama hiyo ramani hapo juu halafu niambie kama unaiona Tanganyika ,sasa Tanganyika inaweza ikafananishwa na US unataka muungano upi tena umeiona Urundi ,Unyamwezi ,Uhehe hizo ni baadhi ya States za Tangayika au Changanyika(United)ila wameiita Tanganyika kwa kutumia lugha ya Kigunya.Utaona hata jina hatuna.Kwa kuwa maana ya tanganyika ni states wenzetu wana America .Bora tungeitwa United States of Zanzibar kidogo ungelikuwpo mshiko.
 
Katika dunia hakuna muungano wa NCHI isipokuwa huu uliokuwepo hapa East Africa ,nakumbuka ulijaribiwa Misri na Syria haukufika mbali.
Hivi kuna mtu aneweza kuniambia kama ziko nchi zimeungana kama hizi za Tanganyika na Zanzibar ? Nasubiri jibu ?


Nasikia muungano wa namna hii uko UK!!! mimi sio mfuatiliaji wa siasa za huko!!! mlioko huko tuelezeni.
 


Mkataba original kuupata hutoupata hata siku moja kwa hivyo baki na imani yako hiyo hiyo kuwa hali ya Muungano ulivyo sasa hivi ndio hiyo hiyo iliyokuwa kabla - hakuna kilichozidishwa wala kupunguzwa , huoni hata nafasi ya Makamo wa rais mwanzo ilikuwa ni mbili yaani Rais wa Zanzibar alokuwa anajulikana kama Makamo wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye alikuwa anajulikana kama Makamo wa Pili wa Rais. Sasa jee iko vipi? au hilo hulioni pia.?
 
Mkataba original upo na tazama hiki kipande nimekumegeeni tu ili mjue kuwa kilichopo kipo na ndio wenyewe maana una saini ya Mwalimu Nyerere na mtumishi wa Bunge ambae ni Msekwa na Spika ambae ni Adam Sapi Mkwawa.:-
N WITNESS WHERE Julius K. Nyerere, the President of the Republic of Tanganyika, and Abeid Karume the President of the Peoples' Republic of Zanzibar have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April, 1964.
Passed in the National Assembly on the twenty-fifth day of April, 1964.
Clerk of the National Assembly
I hereby certify that the Bill for this Act was passed by the National
Assembly in accordance with the provisions f Constitution.
on 35 of the 25th April, 1964
----- - Printed by the Government Printer, Dar es Salaam.
Speaker
Msekwa
Fungueni hiyo file hapo muone ndio yenyewe au nimeikosa.
 

Attachments

Kero za Muungano zinapotikisa Umoja wa Kitaifa

Joseph Mihangwa
Aprili 16, 2008



KIASI cha mwaka au hata miwili, kabla ya Uhuru wa Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere, alinukuliwa kwenye karamu moja ya chakula cha jioni mjini Dar es salaam akisema maneno yafuatayo kuhusu Zanzibar:

“Kama ningeweza kukivuta kisiwa kile mpaka katikati ya Bahari ya Hindi ningefanya hivyo”.

Huku akionyesha wasi wasi dhahiri na kukerwa kwake na Zanzibar Mwalimu alisema:

“kwa kweli sitanii kuna wasiwasi mkubwa kitatuletea matatizo makubwa huko mbele”.

Miaka mitano baadaye Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, April 26, 1964.

Kwa Watanzania, Aprili unabeba matukio matatu makubwa ya kihistoria. Tukio moja ni hili la nchi mbili, (Tanganyika na Zanzibar) kuungana; la pili ni kuuawa kwa mmoja wa waasisi wa Mungano huo, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, mzee Abeid Amani Karume, miaka minane baadaye, Aprili 7, 1972.

Na tukio la tatu ni kufariki katika ajali ya gari kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambaye rekodi yake haijavunjwa, Aprili 12, 1984. Yote haya yaligusa kwa namna moja au nyingine mustakabali wa Muungano.

Miaka 48 ni muda mrefu kwa uhai wa Muungano kama wetu, ikizingatiwa kwamba Muungano kama huu ulijaribiwa na nchi nyingine barani Afrika, kama vile kati ya Senegal na Gambia uliojulikana kama Sene-gambia, na ukafa katika kipindi kifupi sana pengine kutokana na kukosekana kwa utashi madhubuti wa viongozi wa nchi hizo, au kutokana na mifumo ya miungano hiyo kutokidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi wa nchi husika.

Vivyo hivyo, licha ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutimiza miaka 48 mwezi huu, hatuwezi kusema kwamba umesafiri kwenye barabara iliyonyooka siku zote kufika hapa ulipo, wala hatuwezi kujitapa kwamba Muungano huu umekidhi utashi (wa viongozi) na matarajio ya wananchi walio wengi kuweza kuitwa “Muungano maridhawa” asilimia mia kwa mia.

Tumeshuhudia mawimbi na tufani na meli yetu bado inaendelea kusukwasukwa. Tunapoadhimisha miaka hiyo 48 ya Muungano, siku kumi na moja tu zijazo kuanzia leo, yatupasa kutazama nyuma kuona wapi tumejikwaa, wapi tumelegea, wapi tujisahihishe ili tuweze kwenda mbele. Yote haya yataka utashi na uzalendo wa kweli.

Hatutaweza kufanya hivyo bila kutazama nyuma kuona na kubaini ukweli juu ya utashi uliozaa Muungano, misingi na mihimili ya Muungano; utekelezaji wake na mitafaruku iliyojitokeza na kuzua tufani.

Je, kifo cha Karume au kung’atuka kwa Mwalimu Nyerere kumebakiza au kumepunguza utashi na usimamizi wa Muungano? Nini hatima ya Muungano?

Aprili 21, 1964 Rais Karume alipokea simu kutoka kwa Rais Nyerere akimwomba wakutane mjini Dar es Salaam kesho yake. Kweli, siku iliyofuata, Karume aliruka kwa ndege kwenda Dar Es Salaam, akakutana na Mwalimu na kuzungumza mengi ambayo hatujapata kuambiwa. Karume alirejea Zanzibar siku hiyo hiyo adhuhuri.

Siku moja au mbili nyuma kabla ya ziara ya Karume, Mwalimu alikuwa amemwagiza Mwanasheria Mkuu wa Tanganyika, Roland Brown, kuandaa rasimu ya Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar “bila mtu mwingine kujua”.

Naye Karume, aliporejea Zanzibar kutoka Dar Es Salaam, aliwaagiza wasaidizi wake kuandaa mapokezi ya Mwalimu Nyerere aliyetarajiwa kufika Zanzibar (Unguja) kesho yake asubuhi, Aprili 22, 1964. Mwalimu (na ujumbe wake) waliwasili Unguja siku hiyo kama ilivyopangwa akiwa na rasimu ya Mkataba wa Muungano mkononi, na kumkabidhi Karume aupitie na kuutia sahihi Mkataba huo ulioandikwa kwa Kiingereza.

Mkataba huo ulitiwa sahihi siku hiyo hiyo na Nyerere na Karume na kushuhudiwa na wasaidizi wao.

Nyerere alirejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo baada ya kutiwa sahihi kwa Mkataba wa Muungano, maarufu kwa jina la “Hati ya Muungano” au kwa lugha ya kigeni “Articles of Union”. Mkataba uliofikiwa na viongozi hao wawili ulikuwa na hadhi ya kimataifa. Na ili Mkataba wa kimataifa upate nguvu, utambuliwe na kutumika katika nchi husika ni sharti uridhiwe (to ratify) na mabunge ya nchi husika.



NYERERE na Karume siku ya Muungano

Kwa hiyo, Bunge la Tanganyika na lile la Zanzibar (Baraza la Wawakilishi) yaliitishwa haraka haraka na kuridhia Mkataba huo, Aprili 25, 1964, na Aprili 26, 1964 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitangazwa rasmi.

Tutazame kwa ufupi tu maswali yaliyoibuka juu ya uhalali wa Muungano na jinsi ulivyofikiwa, kero na mitafaruku inayousibu Muungano tangu mwanzo hadi sasa.

Imeelezwa mara nyingi na duru za Muungano kwamba, Nyerere alitoa wazo la Muungano kwa Karume, naye (Karume) akakubali sawia. Kuna ukweli gani kwa taarifa hiyo?

Ni mambo yapi yalikuwamo katika Mkataba wa Muungno? Kuna hoja pia kwamba Mkataba wa Muungano haukuwa na ridhaa ya wananchi; na hivyo si halali. Watetezi wa hoja hii wanakwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa, ili mkataba huo uwe halali, ilitakiwa kura ya maoni (referendum) kama ambavyo mapendekezo ya muafaka wa Zanzibar kati ya CCM na CUF umerejeshwa kwa Wazanzibar kupata kura ya maoni. Hoja hii ni sahihi kiasi gani?

Kumbukumbu zilizopo (na imeandika mara nyingi juu ya hili) zinaonyesha kwamba kabla na baada ya Uhuru wa Tanganyika, kisiwa cha Zanzibar kilimnyima usingizi Mwalimu Nyerere kiasi cha kutamani “kukivuta hadi katikati ya Bahari ya Hindi”, kama angekuwa na uwezo wa kufanya hivyo; lakini hakuwa na uwezo huo kwa sababu yeye hakuwa Mungu.

Kwa hiyo, pengine njia pekee aliyoona Nyerere inafaa, ni “kukidhibiti” kisiwa hicho na kukisogeza karibu kwa njia ya Muungano. Hakuna ushahidi kuonyesha kwamba Karume alikubali sawia pendekezo la Mwalimu la Muungano, lakini kuna ushahidi kuonyesha kuwa, mwanzoni Karume alikuwa mzito kupokea au kujadili pendekezo la Mwalimu.

Kwanza, Mwalimu aliwatuma Oscar Kambona na Bibi Titi Mohamed kwenda kumshawishi Karume juu ya nchi zao Kuungana, lakini yaelekea Karume hakuweza kutoa jibu lililonyooka.

Alipowatuma tena Kambona na Bibi Titi Mohamed na kuwatumia pia baadhi ya viongozi wa Zanzibar – Kassim Hanga na Salehe Sadallah kumshawishi Karume akubali hapo ndipo Karume alipoanza kuuona “mwanga”. Hilo ni jibu la kwanza.

Itakumbukwa pia kwamba, wakati Nyerere akijaribu kuzima hofu yake juu ya kisiwa hiki kama alivyosema mwanzo, Marekani nayo ilijawa na hofu kwa kisiwa hicho kuendelea kuserereka kwenda (kutekwa) kambi ya Ukomunisti (Urusi) kifikra na kimahusiano kiasi cha kuitwa “Cuba ya Afrika".

Kwa hiyo, wazo la Nyerere la Muungano lilishabikiwa vile vile na Marekani kwa kuamini kwamba kama Zanzibar ingemezwa ndani ya “tumbo pana la Tanganyika”, harakati za Kikomunisti zikiongozwa na kina Abdulrahman Babu na vijana wengine kama Kassim Hanga, wenye fikra za mrengo wa kushoto, zisingefurukuta. Hilo ni jibu la pili.

Wakati huo huo Karume na Serikali yake alikuwa anakabiliwa na changamoto ndani na nje ya Serikali yake mwenyewe, kwamba alikuwa ameshindwa kutetea na kuendeleza dhana ya “Mapinduzi” iliyofanikisha Mapinduzi ya Januari 12, 1964, na hivyo alikabiliwa na tishio la kupinduliwa wakati wowote.

Kwa wana harakati wengi, Karume alionekana kuyaasi au kuyauza Mapinduzi. Kwa hiyo, Karume aliingia katika Muungano ili kujiponya mwenyewe na mahasimu wake ndani ya serikali waliomsakama na kutaka kumpindua. Hii ni sababu ya tatu.

Kwa sababu hizo tatu, na ile hofu ya Nyerere juu ya Zanzibar kuwa karibu na Tanganyika, tunaweza kusema kwamba Muungano huu ulifikiwa kwa msukumo wa “hofu” na kwa pande zote mbili mmoja kutaka “kujiponya” na tishio lake la kufikirika. Hii haikuwa ndoa ya hiari, bali ilikuwa ndoa ya kulindana (marriage of convenience) na kujiponya.

Chini ya Mkataba wa Muungano, Tanganyika na Zanzibar zilikubali kushirikiana katika mambo kumi na moja tu, ambayo ni Katiba, mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Polisi, Mahakama, hali ya hatari na Uraia.

Mengine ni Uhamiaji, Mikopo na biashara ya nje, utumishi, kodi ya mapato na Bandari. Orodha ya mambo ya Muungano imekuwa ikiongezwa kila mara kwa utaratibu ambao Wanasheria wa mambo ya Katiba wanadai ni kinyume cha Mkataba wa Muungano. Mambo hayo sasa yamefika 22.

Profesa Issa Shivji, katika kitabu chake “The Legal Foundation of the Union in Tanzania’s Union and Zanzibar’s Constitution” anabainisha kuwa Bunge la Tanzania halina mamlaka ya kuongeza au kupunguza mambo yaliyokubaliwa kwenye Mkataba wa Muungano. Kufanya hivyo ni kukiuka ibara ya 5(i) ya Mkataba.

Msomi huyo anaeleza kuwa marekebisho kama hayo yanaweza kufanywa tu kwa njia ya kura ya maoni (referendum), ambao ndio utaratibu pekee unaojulikana duniani kwa nchi zenye Muungano kama wetu.

Anayosema Profesa Shivji yamefafanuliwa vizuri na Mahakama ya Rufaa ya Canada, katika shauri la A.G of Canada for Nova Scotia Vrs A.G. Canada (1951) S.C.R 31.

Ni maoni pia ya mtaalamu wa Katiba za nchi mbali mbali, K. C Wheare, katika kitabu chake, “Modern Constitutions (Edition 1966), London, Oxford University Press – Uk. 84, kama alivyoelezea Profesa Shivji.

Kwa hiyo, Bunge, hata kama litakaa kama Bunge la Katiba (Constituent Assembly), haliwezi kubadili Mkataba wa Muungano wa 1964. Huu ndio msimamo na mwongozo wa kisheria (wa mahakama) kama inavyobainishwa na Mahakama ya Mamwinyi ya Uingereza, katika shauri la A.G for Canada Vrs A.G for Ontario: (1973) A.G. 326 (PC); na katika hukumu za Mahakama ya Rufaa ya India, katika shauri la Kesavananda Vrs State of Kerala (1973) S C. 1461; Smt Indira Gandhi Vrs Raj Narain (1976) 2 S.C.R 3475 na katika kesi ya Minerva Mills Vrs Union of India: AIR (1980) SC 1789.

Kitendo cha Bunge la Muungano cha kubadili mambo ya msingi yale 11 yaliyomo katika mkataba kinyume cha utaratibu, kimekuwa ni moja ya sababu za Wazanzibari kurejea hoja ya “kutaka kumezwa”: na pale wanapojiamlia kutenda watakavyo, kinyume na baadhi ya marekebisho kiasi cha kuitwa “wakorofi”, serikali ya Muungano imekosa nguvu wala kauli inapobaini hayo; kero za Muungano huibuka, mitafaruku kuzuka, Muungano huyumba na utatuzi huwa mbali kwa imani kwamba suala la Muungano ni nyeti na lisilozungumzika.

Muungano uliofikiwa na waasisi wake, Mwalimu Nyerere na Karume mwaka 1964 ni halali na hauwezi kubatilika kwa sababu tu haukufikiwa kwa njia ya kura ya maoni (referendum) ya wananchi. Utaratibu wa kura ya maoni ni mpya kwa mfumo wa sheria za nchi za Jumuiya ya madola. Ulianza kutumika miaka ya 1970 (1976). Kwa hiyo wakati Nyerere na Karume wanafikia Muungano wa nchi zao walikuwa sahihi walivyofanya kwani Katiba iliruhusu.

Hapa nchini, utaratibu, uhalali na umuhimu wa kura ya maoni ni matokeo ya marekebisho ya Katiba ya 1984 pale Katiba hiyo ilipoingiza ibara ya 8(i)(a) inayosomeka: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo, wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi”. Tangu sehemu hiyo ya Katiba itungwe 1984, ni lazima wananchi watoe maoni yao kwa kura ya maoni, ni muundo gani wa Muungano wanataka.

Mengine yaliyokubaliwa katika mkataba huo ni pamoja na Rais wa Serikali ya Muungano, kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar, kuteua Tume ya kupendekeza Katiba ya Muungano na kuitisha Bunge la Katiba ndani ya mwaka mmoja tangu tarehe ya Muungano, kupitisha Katiba ya Muungano.

Itakumbukwa kuwa pia Muungano wetu ulifikiwa haraka haraka bila maandalizi ya kutosha kiasi kwamba serikali ya Muungano ilianzishwa bila kuwa na Katiba ya nchi. Kwa sababu ya uharaka huo aina ya “zima moto”, ilibidi Katiba ya Tanganyika ya 1962 itumike pia kama Katiba ya Muungano kwa kuifanyia marekebisho madogo, hadi hapo Muungano utakapopata Katiba yake.

Hadi muda wa mwaka mmoja unamalizika, si Tume ya Katiba iliyoteuliwa, wala si Bunge la (kutunga) Katiba lililoitishwa. Ukimya huo ulifuatiwa na kutungwa kwa sheria Na. 18 ya 1965 ya kuongeza muda huo “hadi hapo hali itakaporuhusu”, huku kero za Muungano zikiibuka kwa kasi.

Mbali na kuongezwa kwa mambo ya Muungano kinyume cha Mkataba wa Muungano, mengine ni pamoja na kufutwa kwa nafasi za Makamu na Makamu wawili wa Rais, kuingizwa kwa mfumo wa chama kimoja ndani ya Muungano, na uteuzi wa Tume ya kupendekeza Katiba mwaka 1976, tofauti na aina ya Tume iliyotajwa ndani ya Mkataba na mengine. Yote haya na mengine yamezidisha badala ya kupunguza kero za Muungano.

Katika sehemu ya pili ya makala haya, tutajibu maswali yafuatayo: kwa nini Rais Nyerere hakuteua Tume ya Katiba wala kuitisha Bunge la Katiba na kusababisha Muungano kuendeshwa kwa Katiba ya mpito kwa miaka 13? Je, Katiba ya 1977 ni halali chini ya mkataba wa Muungano?

Je, kifo cha Karume na kung’atuka kwa Mwalimu madarakani mwaka 1985 kuliathiri vipi utashi wa Muungano na kwa kiasi gani? Je, kitendo cha Zanzibar kuwa na bendera yake, wimbo wa taifa na ngao ya taifa ndani ya Muungano ni sehemu ya mkataba? Kwa nini haya yafanyike leo na si wakati wa enzi za waasisi wa Muungano huo?


Itaendelea wiki ijayo.
 
Mimi kwa kweli suala la Muungano linanichanganya sana.

Hii ni kwa sababu mpaka sasa wahusika wakuu waliobuni mambo haya hawapo na labda kama wameacha maagizo kwa kalamu kwamba kisiguswe kitu baxsi kutakuwa na matatizo makubwa baadaae.

Katika maelezo yafuatayo ambayo nimepekua mahala fulani, inaonesha kwamba pia kulikuwa na maongezo mengine ambayo yanafanza hizo articles kuwa ni nyingi na zinazojitosheleza.

19th March - 6th April 1962: A constitutional conference was held in London and was attended by all the political parties in the Legislative Council with the Colonial Secretary as chairman. At the conference the ZNP/ZPPP alliance and the ASP showed very diverged views on future constitutional development. The conference ended in a stalemate. ASP wanted the complete removal of means and literacy conditions in elections, a reduction of minimum voting age to 18, an increase of elected members from 23 to 31, and the holding of new elections before independence. While the ZNP/ZPPP coalition agreed on the removal of means and literacy conditions, they rejected the other demands.


24th June 1963: Zanzibar became an internally self-governing territory


8th to 15th July 1963: Elections were held for a legislature of 31 members. The ZNP/ZPPP alliance won 18 seats, and the ASP 13.


September 1963: The last constitutional conference was convened in London on the Independence Constitution. This conference agreed on the date of Zanzibar's formal independence from Britain as 10 December 1963.


10th December 1963: The British colonisation of Zanzibar ended after seventy-three years.


December 1963: Formal independence from Britain on December 10th, 1963, saw the Sultan as the Head of State, with power to nominate his successor




12th January, 1964: Barely a month after formal independence, Zanzibar experienced a revolution that overthrew the ZNP/ZPPP coalition government; immediately abolished the monarchy; the rule of Al-Busaidy dynasty and abrogated the Independence Constitution 1963.


1964: After the revolution, Abedi Amani Karume was declared the first African President of Zanzibar and the country became a one party state under the Afro-shirazi party.


26th April 1964: the People's Republic of Zanzibar and the Republic of Tanganyika announced a merger to form a United Republic of Tanzania.


December 1964: by an Act of the Union Parliament, a new name for the United Republic was adopted, i.e. Tanzania [Act No.61 of 1964].


December 1964: Immediately after the ratification of the ‘Articles of Union', the Constitution of Tanganyika was adopted as the first Constitution of the United Republic. The Interim Constitution of Tanganyika and Zanzibar, 1964, was to operate until a new Constitution was to be adopted.


The initial "Union Matters" included the following eleven areas as Union matters:

·The constitution and government of the United Republic;

· External affairs;

· Defense;

· Police;

· Emergency powers;

· Citizenship;

· Immigration;

· External trade and borrowing;

· The Public service of the United Republic;

· Income tax, corporation tax, customs and excise duties, and

· Harbours, civil aviation, posts and telegraph.



Between 1964-1977: through an amendment of the Interim Constitution which had reproduced the list of union matters and not an amendment of Acts of Union, new items were added to the list of Union matters giving the Union parliament and executive more powers.



Other issues added to the list to make the Union matters 22 were:

All matters concern coinage, currency for the purposes of legal tender (including notes), banks (including savings banks) and all banking business; foreign exchange and exchange control

Industrial licensing and statistics

Higher education

Mineral oil resources, including crude oil and natural gas

The National Examinations Council of Tanzania and all matters connected with the functions of that Council

Civil Aviation

Research

Meteorology

Statistics

The Court of Appeal of the United Republic

Registration of political parties and other matters related to political parties

Thus Zanzibar retains jurisdiction over issues which include: Information, Agriculture, Natural Resources, Environment and Cooperatives, Trade, Industry, Marketing, Tourism, Education, Culture and Sports, Health and Social Welfare, Water, Construction, Energy and Land, Communication and Transport and finally, youth, employment, women and children development, etc



7th April 1971: Zanzibar's founder President Sheikh Abeid Amani Karume was assassinated and was succeeded by Aboud Jumbe as President of Zanzibar and Vice President of Tanzania


1977: The Interim Constitution was repealed and replaced by the Constitution of Tanzania (1977).


1977: the two ruling parties : TANU and Afro Shirazi Party merged to form Chama Cha Mapinduzi (CCM)


1979: The first post-revolution Constitution of Zanzibar was enacted. It was modelled after the Union Constitution providing the same format and organization for government, dividing into executive, legislative and judicial branches and also endorsed all provisions in the Union Constitution relating to Zanzibar, with only modest modifications where appropriate.


5th October 1979, (fifteen years after the revolution): the Revolutionary Council passed the Zanzibar Constitution that established a House of Representatives as the country's legislature. It had only 10 directly elected members out of 109


14th January 1980: The House of Representatives established in 1979 started to function.


1984: as result of a "polluted political atmosphere" in Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe had to resign his state and party positions namely, as President of Zanzibar, Chairman of the Revolutionary Council, Union Vice-President and CCM Vice Chairman.


1984: Ali Hassan Mwinyi was elected to replace Aboud Jumbe in Zanzibar


1984: A new Constitution was adopted for Zanzibar under a one-party system. The

1984 Zanzibar Constitution differed very much from the 1979 one, for it had a bill of Rights, defined a Zanzibari, stipulated state directives and made a House of Representatives that consists mostly of elected members.


1984: The new Zanzibar Constitution Chapter V established the House of Representatives.


1985: The first elections after the 1964 Revolution were held.


1985: Idriss Abdul Wakil became President of Zanzibar, replacing Ali Hassan Mwinyi who became Head of State of Tanzania


Kwa hio hapa mambo bado ni magumu sana.

Source: Kituo Cha Katiba ( Eastern Africa Centre for Constitutional Development)
 

Mwiba;

Ulichoonyesha kwenye PDF sio Hati ya muungano (Articles of Union) ila ni Sheria ya Muungano (Act of the Union). Tazama haina saini ya Karume. Pia angalia tarehe: ilisainiwa tarehe 25, wakati mkataba ulisainiwa -inasemekana - tarehe 22. Hakuna utata kuhusu Bunge kupitisha Muungano. Ishu ni kwamba kiini, au mkataba wenye saini ya Karume na Nyerere uko wapi?. Achilia mbali karatasi yenyewe, inasemekana hata nakala hakuna. Hili hakuna mwana wa Adam aliyewahi kukataa, wala hakuna kuumizani vichwa. Ukisema mkataba upo unaambiwa tuonyeshe!

Katika kesi ya Muungano iliyofunguliwa Zanzibar mwaka 2003, mwanasheria mkuu wa Zanzibar alitoa ushahidi kwamba hajawahi kuiona Hati ya Muungano. Inasemekana haipo.
 
Ingawa nina malalamiko mengi na muungano wa sasa, lakini bado sidhani kama ni wazo zuri kuvunja muungano. Hii mipaka mingi iliwekwa na wakoloni. Waafrika kabla ya wakoloni wa kiarabu na kizungu, tulikuwa tukiishi pamoja.

Kutengana sio suluhisho katika mgogoro wa sasa!
 

Hiyo ameweka article ya Bunge kuratify muungano lakini sio mkataba wa muungano, hakuna sahihi ya mzee karume hivyo haiwezekani ukawa ni mkataba wa muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…