Wenye uwezo wa kufanya hili ni serekali ya CCM iliyopo madarakani and we all know what they will say, we have heard it before- 'tupate ridhaa ya wananchi!' as if wakati wa kuunda huo muungano kulikuwa na kitu kama hicho.
Umenipa pakuanzia!
Ni kweli kama mtoa hoja alivyosema kuwa wazanzibari deep down their heart hawaupendi muungano. Hawaupendi muungano kwakuwa wanaona hawafaidiki nao. Kisiasa mtaona wanafaidika lakini ukiangalia kwa makini utaona wana point.
Rais wa zanzibar hana tofauti na Mhe Kandoro yule mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Zamani Rais wa zanzibar alikuwa makamu wa rais siku hizi hakuna hilo! mnajua kwa nini? Hii ni choyo ya CCM wanajua kuwa hawashindi ZNZ ikija tokea CUF wakiwazidi maarifa wakashindwa "kuchukua kuweka waa" Seif au mwingine yeyote wa CUF awe Rais wa ZNZ then awe makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano! hilo haliwezekani kwani wao CCM tu ndio wamezaliwa katika dunia hii watawale!
Wenyewe wazanzibari wana ZNZ yaani Zanzibar Nzuri Zamani
Wa bara wanaosema Zanzibar wananyonya mapato ya Tanzania bara au uchumi wake unategemea Bara si kweli ila naamni kama Bara inafaidika sana na Muungano kuliko Zanzibar na nina hoja. Misaada yote inayoipata Tanzania inakuja kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania yaani Zanzibar ikiwamo maana haiji kwa serikali ya Tanganyika. Kwa taarifa yenu misaada hii haifiki hata Chumbe! inaishia Dar es Salaam!
Ukiangalia hati ya muungano kuna yale mambo 11 ya awali katika yale mambo suala la mgawanyo wa pesa zipatikanazo mafuta na gesi ya asili halikuwepo limekuja kuongezewa tu baada ya kungundulika zanzibar ina neema hiyo! ndio rafiki zangu wazanzibari wanahoji mbona madini hawakuyaweka tugawane mapato pia?
Zanzibar ni nchi ikiyokuwa imepiga hatua kubwa sana wakati inaingia katika muungano.
Msiojua Zanzibari ni nchi ya kwanza kuwa na taa za bara barani barani afrika, ya kwanza kuwa na television ya rangi barani afrika.
Kwa maana hiyo Muungano umeirudisha Zanziba kimaendeleo pengine bila la Muungano Zanzibar ingekuwa Brunei
Kareme baba aliwahi kusema "muungano ni kama koti ukiona linakubana livue" sasa ni hiari yao wabara na wazanzibari kulivua au kulifumua makwapani!
Naomba kuwakilisha hoja!