Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
"Karume baba alitumia raslimali za taifa kunufaisha watu, mchango mkubwa ukitokana na karafuu, zao ambalo zaidi ya asilimia 90 ya uzalishaji wake hutegemea kisiwa cha Pemba.

Hadi anauawa, Zanzibar lilikuwa moja ya mataifa machache, ingawa ndani ya Muungano, yaliyokuwa na fedha nyingi za kigeni na uchumi unaokua na kuimarika. Itakumbukwa ni kipindi hicho, Zanzibar iliikopesha fedha Bara."
 
There is a completly diferent MIND SET in Zbr and Tnky. If we are big enough and bold enough to accept facts/reality ,you will not have any problem knowing the reason for the Union.It was formed out of a neccessity that was obvious to Mwalimu but not so obvious to the common man on both sides.(The threat of aligning to the Commuinist block;that it is now history.)Today, Zbr would be much better off on its own,economically. Aid will pour in from the Islamic states,and the Western Block.It could well become another Singapore,if it were to break away.

Wawe kama Singapore, labda tunasoma hadithi za Abunuwasi na Bulicheka. Maendeleo yanaletwa na kufanya kazi, tatizo la Zanzibar wanatafuta mchawi - hakuna mchawi bali wao wenyewe wakae chini na Wapemba wasuluhishe matatizo yao. Hayo yaliyotokea Musoma yalikuwa kati ya Zenji na Pemba, huwezi kufanya muafaka bila kuonana jicho kwa jicho na mbaya wako.

Kwanza wamependelewa sana lundo la viongozi wao wanaweza kulibeba? Bara tuko millioni karibu 40 lakini hatuna hata wabunge unaoweza kulinganisha kwa uwakilishi na wenzetu.
 
Wawe kama Singapore, labda tunasoma hadithi za Abunuwasi na Bulicheka. Maendeleo yanaletwa na kufanya kazi, tatizo la Zanzibar wanatafuta mchawi - hakuna mchawi bali wao wenyewe wakae chini na Wapemba wasuluhishe matatizo yao. Hayo yaliyotokea Musoma yalikuwa kati ya Zenji na Pemba, huwezi kufanya muafaka bila kuonana jicho kwa jicho na mbaya wako.

Kwanza wamependelewa sana lundo la viongozi wao wanaweza kulibeba? Bara tuko millioni karibu 40 lakini hatuna hata wabunge unaoweza kulinganisha kwa uwakilishi na wenzetu.

Ungozi wa mafisadi unategemea Zanzibar Block katika kupita ,maana ukiwaweka unaowataka pale Zanzibar basi kupita katika kinyanganyiro chochote inakuwa ni rahisi ,mbinu hizi ndizo zinazofanya wenyewe wazenji waseme wanachaguliwa viongozi na waTanganyika wakiamini Watanganyika watakuwa Mabwana na kuwatumia viongozi kutoka Zanzibar vile wanavyotaka kupitisha au kupinga maamuzi ndani ya Chama chao kunategemea zaidi hili block la Zanzibar ,ndio ukaona mafisadi hutumia vyombo vya dola kuibatilisha halali na haramu kuifanya ndio halali.Mambo ambayo yalikuwa yafanywena watu wasio na dini lakini leo wengi naona dini imewashinda wamebaki na majina tu na ibada za kiwongo wongo.
Ila ndio tunakwenda nao kama vile tunawaona ndio viongozi watakatifu ajabu nguo waliyoivaa wasiombe akatokea mtoto mdogo atawaumbua.
 
cha ajabu wanaotaka muungano na hasa toka bara hawako tayari kueleza kwa nini tuendelee kuwa na hili jambo

Hii ni kama ndo ikishindikana kila mmoja anatazama lwake
Kuna mjadala mwingine motomoto ambao unaendelea kama huu wenye heading ya leo ni siku ya muungano!Na nimeuliza maswali kama haya na nina subiri waungwana huko wanipe majibu!
 
JMushi1,
Mkuu naingia hapa pamoja na kwamba sikupenda maanake hili jukwaa zito zaidi na pengine naweza vuruga kilichoanzishwa hapa.
Swali lako gumu sana kulieleza kama mtu hufahamu maana..
Swali lako linaweza jenga hoja nyingine ya kujiuliza hivi Uhuru wa nini ikiwa wananchi wengi hawapendi Uhuru huu tuliokuwa nao?. Je, kuna haja ya kurudi kwa mkoloni!..
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ndoa ambayo haiwezi vunjwa pasipo sababu ati kutokana na utashi wa watu kama tunavyovunja ndoa zetu Bongo. Huwezi kuvunja ndoa hiyo hiyo Ulaya hata kidogo na pengine unaweza kujiuliza hizi sheria zote na taratibu za nini ikiwa mtu hataki kuishi ktk ndoa... taraka inatosha kila mtyu ajikate! - sii rahisi hivyo mkuu.
Swala la Zanzibar ni zito kuliko maamuzi ya mtu mmoja ktk ndoa na kama kweli Zanzaibar hawautaki Muungano (kulingana na madai ya wengi) how come wanapoambiwa ifanyike referendum wanachomoa?..
Mkuu, hiyo Kariakoo yote leo hii imevamiwa na Wapemba, mshikemshike wa kuvunja Muungano una hasara kubwa sana kwao kuliko kuulinda..nina hakika kura za kuvunja muungano zitawashindwa!
Sasa sema KATIBA ya Muungano huo ndio ina utata mkubwa na sielewi kwa nini hadi leo hii bado tumekubmbatia sheria za Ulinzi wa Mapinduzi yale wakati wananchi wa Zanzibar wamekwisha tambua hilo kuwa ni moja ya maisha yyao na wataishi nalo kama kumbukumbu ya Kitaifa.
Unless kweli hizi hoja zinazopikwa kila mara na mbaadhi Wapemba wanasiasa ndizo zinazojenga imani ya CCM kuwa Zanzibar bado haiko salama.
 
..mkandala,

..muungano kuvunjika hivi sasa ni suala la when zaidi kuliko why and how!

..wakati mwengine ukweli si mzuri,na huu ndio haswaa,si mzuri hata kidogo.
 
Muungano ni kama ndoa..na kama ikishindikana kuishi pamoja basi tupeane talak kila mmoja atazame ustaarabu wake.

Muungano haukuwepo na unaweza usiwepo.Kwa wazanzibari wengi wao be it CUF au CCM deep down wanaamini kuwa muungano hauna faida kwao, na zaidi ule mkutano wa Butiama ambao CCM ZNZ walimtisha JK kuwa kama anataka kuwasikiliza hao CUF basi na wao watarudi ZNZ kivyao.Na hapo bado hatujazungumzia 60/40

Bara nao wanaona kuwa watu wa ZNZ wanaishi kwa income support ya kodi wa watu wa Bara sasa je mnasemaje wana JF tuuvunje huu muungano?

Maoni yenu Tafadhali


JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY

Kwa maoni yangu, nadhani itakuwa vema na haki kuuvunja huu Muungano. Muungano huu hautoka kwa Mungu bali ni mawazo ya binadamu wawili ambao nao wameshatangalia, hivyo hata wenyewe unaweza kufa vilevile.

Siioni faida yeyote ya muungano kama nikitoka shopping Znz nalipishwa ushuru kwa ajili ya gari, redio au tv mpya kama vile nimenunua Kenya.

Sioni faida ya muungano kama mtanganyika mimi nikitaka kufungua biashara Znz iwe isuue wakati kuna wapemba kibao huko kwetu wanafanya biashara yao bila bughudha.

Sioni faida ya muungano pale niliyeungana nae hanithamini na ananiona mtu duni eti kwa vile yeye tu 'anauarabu fulani' hata kama ni 0.01% ya uarabu basi yeye ni bora zaidi.

Hizi ni sababu nyepesi sana ambazo kwa upande wangu ni bughudha. afadhali mara mia nitafute visa au kugongewa passport kuliko kujua eti niko ndani ya muungano.
 
...Today, Zbr would be much better off on its own,economically.Aid will pour in from the Islamic states,and the Western Block.It could well become another Singapore,if it were to break away.

I wonder how zbr could become another singapore through aid from islamic states as you have put it. that is dependence, which has put this country wehere it is today. and the continued dependence threatens our countries into becoming colonies again
 
Dar si Lamu,
Noo mkuu hilo nakukatalia kabisa!.. Huwezi vunja Muungano kwa maneno hatupo Urusi hapa...Hata hao Albania wamepiga kura kutaka kujikata na Tibet wananchi wanaonyesha ari ya kujikata kinachotakiwa ni sheria tu. Sio rahisi hivyo hata kidogo msijaribu kuwahadaa wananchi hali nyie mnakaa Ulaya mafichoni!

Siku zote wananchi wanapowakilishiwa hoja ya kuvunja Muungano na wakaipokea kwa kura zao ndipo unaweza kuona dalili za kuuvunja Muungano kuliko hizi hadithi za viongozi ambao kwa kila hali wanatafuta nafasi zao kuiba pia.
Nina hakika dawa ya kupoza yote haya ni Takrima ya sharing power zaidi ya maslahi ya Zanzibar!..
Hivi wewe hujawahi kujiuliza kitu kimoja..
Ikiwa hawa viongozi wetu wanaona hakuna haki kabisa kwa Wazanzibar wala Muungano hauna maana kwa nini bado wanajipanga kugombea Utawala ktk Jamhuri isiyokuwa na haki Kikatiba!
Maneno yote tunayasikia wakiwa kwelnye chaguzi hizi. Zanzibar inapokonywa Utajiri wake mara hivi then why msiwe straight kama Salmin Amour ambaye leo wote hawa wamemtema baada ya kujichimbia kaburi la Uongozi.
Wafanye kama nchi hizo za Ulaya wanavyofanya.. Toeni Azimio kisha tafuteni kura za wananchi ktk kuvunja Muungano, Wazanzibar wengi wakisema tuuvunje then nitakubali nje ya hapo ni hadithi za wanasiasa ambao wao wenyewe walipokuwa katika madaraka hawakusema Muungano ni mbaya isipokuwa baada ya kutemwa.
Tazama hapa JF mbona watu tunasema ovyo pamoja na kwamba wengine ni wana CCM ama wana Chadema?..nia na malengo yetu ni kitu gani haswa kama sio kurekebisha ama kuondoa mapungufu ya viongozi wetu... kwa sababu tuna nia nzuri na nchi hata kama hatuna wadhifa wala mshiko sio viongozi wetu wanafiki wakubwa.
 
..mkuu mkandala,

..kwa taarifa,

..mi siko ulaya au merekani.

..simdanganyi mwananchi,mi si mwanasiasa.

..halafu,kuna njia mbili juu ya zanzibar:

..1/kuitawala = serikali moja.

..2/muungano kuvunjika = hali hii tuliyonayo inavyoelekea.
 
Bwana Obama mimi nafikiri suala la muungano hatujafikia huko kwa maana ya kuvunja muungano kwani kwa maoni yangu kama kutakuwa na tatizo la kuvunja muungano basi watakaoathirika ni hao wapemba maana kila kitu wanategemea bara kulima hawawezi hata wanapopata nafasi ya kutoka nje ya nchi na wakirudi na vijisenti kama alivyosema AC hawajengi kwao wanajenga Dar
 
Ushauri ni mzuri uvunjwe kwanza halafu ndio tujadiliane namna gani tunataka kungana kwani
yalinisikitisha maelezo kama hayo uliyokwisha yatowa waliyoyatowa CCM Zanzibar kule Butiyama kwa kuwaeleza CCM Bara kama wanataka mseto basi wao watarudi zanzibar na ASP na pale ndipo wakaoneka wasomi wetu kutokea Tanganyika kunyongonyeshwa na kauli zile kama vile kuku aliyowekwa katika gunia liloroweshwa maji walihofia kuachiwa kuachiwa Tanganyiaka yetu huku wakisahau kuwa hatuhitaji zanzibar isipokuwa zanzibar inatuhitajia sisi.
 
Umenipa pakuanzia!

Ni kweli kama mtoa hoja alivyosema kuwa wazanzibari deep down their heart hawaupendi muungano. Hawaupendi muungano kwakuwa wanaona hawafaidiki nao. Kisiasa mtaona wanafaidika lakini ukiangalia kwa makini utaona wana point.

Rais wa zanzibar hana tofauti na Mhe Kandoro yule mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Zamani Rais wa zanzibar alikuwa makamu wa rais siku hizi hakuna hilo! mnajua kwa nini? Hii ni choyo ya CCM wanajua kuwa hawashindi ZNZ ikija tokea CUF wakiwazidi maarifa wakashindwa "kuchukua kuweka waa" Seif au mwingine yeyote wa CUF awe Rais wa ZNZ then awe makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano! hilo haliwezekani kwani wao CCM tu ndio wamezaliwa katika dunia hii watawale!

Wenyewe wazanzibari wana ZNZ yaani Zanzibar Nzuri Zamani

Wa bara wanaosema Zanzibar wananyonya mapato ya Tanzania bara au uchumi wake unategemea Bara si kweli ila naamni kama Bara inafaidika sana na Muungano kuliko Zanzibar na nina hoja. Misaada yote inayoipata Tanzania inakuja kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania yaani Zanzibar ikiwamo maana haiji kwa serikali ya Tanganyika. Kwa taarifa yenu misaada hii haifiki hata Chumbe! inaishia Dar es Salaam!

Ukiangalia hati ya muungano kuna yale mambo 11 ya awali katika yale mambo suala la mgawanyo wa pesa zipatikanazo mafuta na gesi ya asili halikuwepo limekuja kuongezewa tu baada ya kungundulika zanzibar ina neema hiyo! ndio rafiki zangu wazanzibari wanahoji mbona madini hawakuyaweka tugawane mapato pia?

Zanzibar ni nchi ikiyokuwa imepiga hatua kubwa sana wakati inaingia katika muungano.

Msiojua Zanzibari ni nchi ya kwanza kuwa na taa za bara barani barani afrika, ya kwanza kuwa na television ya rangi barani afrika.

Kwa maana hiyo Muungano umeirudisha Zanziba kimaendeleo pengine bila la Muungano Zanzibar ingekuwa Brunei

Karume baba aliwahi kusema "muungano ni kama koti ukiona linakubana livue" sasa ni hiari yao wabara na wazanzibari kulivua au kulifumua makwapani!

Naomba kuwakilisha hoja!

Basi mzee mie naenda kulala

umemaliza hapo juu sina zaidi la kuongeza

 
Wawe kama Singapore, labda tunasoma hadithi za Abunuwasi na Bulicheka. Maendeleo yanaletwa na kufanya kazi, tatizo la Zanzibar wanatafuta mchawi - hakuna mchawi bali wao wenyewe wakae chini na Wapemba wasuluhishe matatizo yao. Hayo yaliyotokea Musoma yalikuwa kati ya Zenji na Pemba, huwezi kufanya muafaka bila kuonana jicho kwa jicho na mbaya wako.

Kwanza wamependelewa sana lundo la viongozi wao wanaweza kulibeba? Bara tuko millioni karibu 40 lakini hatuna hata wabunge unaoweza kulinganisha kwa uwakilishi na wenzetu.



Moja kati ya mambo yanayosukuma maendeleo ni siasa safi na siasa safi haiwezi kupatikana wakati WATAWALA WA CCM BARA wanaendelea kuwachagulia wazanzibari WATAWALA WAO

kuwalaumu eti wa ZNZ ni wavivu utakuwa huwatendei haki...mbona watu wa bara wakishaanza vita huwa wako mstari wa mbele kuagiza kikosi cha nyuki toka ZNZ?

Uzuri wa ZNZ ni kuwa wao watawala waliwaletea ujinga wanajua namna ya kudela nao na kumwaga damu kwani ni suala dogo sana

wape haki yao wananchi wavumilivu wa ZNZ tatizo ni CCM BARA ni hiyo si siri

Ungeona DVD jinsi wajumbe wa CCM wlaivyokuwa wakimpa vipande JK kule BUTIAMA ungeelewa nina maanisha nini

Naona ZNZ ishakuwa kama ENgland na NORTHERN IRELAND..whawasemwi kwa mabaya na wakisemwa basi wao wanataka kuvunja muungano

Na mtu leo akinuliza je ZNZ inaweza kuendelea wakivunja muungano? Jibu lanu ni YES...kama RWANDA wameweza baada ya vita sioni sababu kwa nini ZNZ isiweze kama ikiwa na siasa safi

they have nothing to lose ila sisi tuna hiyo Pride yetu..na this is hard pill to swallow

 
GAME THEORY,
hakuna mtu anayeweza kusema kwamba Zanzibar bila Muungano wataanguka kiuchumi. Hapana mkuu, binafsi nasema Zanzibar bila Muungano watarudi kuchinjana. Kumwaga damu unakokuzungumzia wewe ndio tishio kubwa la bara na wewe umedhihirisha pamoja na kwamba binafsi nafikiri muda huo umesha pita.
Wapo wengi mtasema inatuhusu nini sisi well kama ndivyo kweli basi msiandike kitu kuhusu Sudan wala Zimbabwe - it's their problem.
Kwa hiyo kabla ujafikia kujipanga kuweza kujijenga kiuchumi ni lazima kwanza tofauiti zao ziwe na usalama wa kutosha na hilo linashindika chini ya Muungano huu huu. waunguja na Wazanzibar ni moto unaosubiri mafuta ya taa. Hilo moja pili, Hao wanaosema kuhusu serikali ya mseto wameshindwa kufahamu kwamba Zanzibar haina chama kimoja tu cha CUF, huo muafaka ulikuwa kati ya CUF na CCM hauhusiani na Muungano kabisa.
Na tatu ningeomba nukuu ya hayo madai kwamba CUF walipeleka ujumbe wao Butiama (kwenye kikao cha kamati kuu ya chama CCM) kuhusiana na kuvunja Muungano, haniingii akilini!
 
Katika DVD nilioona ya kikao cha CCM Butiama sijaona mjumbe hata mmoja wa CUF na wala sikusema kuwa CUF walipeleka ujumbe ila inshort JK alikuwa kama mbwa aliyelowa maji baada ya wajumbe wa CCM ZNZ kusimama mmoja baada ya mwingine kumpa vipande vyake


Sisi kama bara hatuwezi kungangania kitu ambacho wenyewe pamoja na tofauti zao za kisiasa hawakipendi na wanaamini kabiaasa kuwa its in their interest wao wakiwa huru bila kuingiliwa nasisi kwenye kuendesha nchi yao

Damu kumwagika ni jambo la kawaida kwa Zanzibar (lakini sijasema ni sawa) kwani hata Rwanda walimwaga damu na Kenya nako damu ilimwagika hivyo lets put aside haya mambo eti tukiwaacha damu itamwagika

Deep down wazanzibari wanaamini kuwa kwa sababu wao ni asilimia 99 waislam bara wanaowana kama vile 900 pound gorilla na lazima uliweke in check amasimvyo litaja kukugeukia ...na mfano mzuri ni jinsi wanasiasa wa bara walivyokuwa wakijibu hoja za ZNZ kujiunga na OIC...inshort wanasiasa wa CCM bara waliwaudhi wazanzibari baada ya kupigwa mikwara na Kanisa katoliki sasa hebu niambie kisiwa amvbacho majority ni waislam watajisikiaje wanapewa majibu ambayo hayakuwaeleza wazi kuwa katiba haiwaruhusu kufanya hivyo bali mikwara toka kwa wakatoliki

Najua ni sensitive lakini ndio hali yenyewe hiyo ukizingatia mie binafsi ninayo asili ya huko visiwa vidogo vodogo lakini hiyo ndio popular belief kuanzia Jonzani mpaka Paje ndame
 


Kuvunja Muungano ni kutafuta suluhisho la tatizo kwa urahisi, mimi naamini msemo wa zamani kuwa Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu , kama kweli tunaamini hivyo hakuna haja ya kuvunja Muungano linalohitajiwa ni kukaa pamoja na ktatua matatizo/kero za Muungano na mimi wazo langu ni kuwa na serikali tatu na kuangalia mambo ya kushughulikiwa na serikali ya Tanzania na yapi ya kushughulikiwa na serikali ya Tanganyika na Zanzibar.

Tuiwe wavivu wa kutafuta suluhisho la Muungano na kukimbilia kuuvunja hii na Karne ya 21 na "partnership" ni muhimu katika nyanda zote. Tudai Katiba mpya ambayo ndio njia ya Mkato ya kutatuamatatizo yetu mengi ikiwemo la Muungano.
 
cha ajabu wanaotaka muungano na hasa toka bara hawako tayari kueleza kwa nini tuendelee kuwa na hili jambo

Hii ni kama ndo ikishindikana kila mmoja anatazama lwake



Duh Hii kweli ni hatari!

Watu wanaishiwa point kukiwa hakuna neno mwizi /fisadi . Kushindwa kuelewa umuhimu wa muungano na the need for more muungano barani Africa ,ni tatizo kubwa .Matatizo kama yapo yanatakiwa kutatuliwa sio kukumbiwa escaping problem not solving thr problem.
People try to put brainwash education about this either b'cause they don't know the need for that or just selfishness .
Ila kuna topic zingine hata shuleni wanataka ufanye prerequisite ili kuifanya.Kadhalika hapa inatakiwa watu wajue faida za muungano kwanza kabla ya yote.
 
cha ajabu wanaotaka muungano na hasa toka bara hawako tayari kueleza kwa nini tuendelee kuwa na hili jambo

Hii ni kama ndo ikishindikana kila mmoja anatazama lwake


GAME naomba kwanza uniambie kwanini tuuvunje muungano, ukitoa sababu za kuridhisha mimi nitakuorodheshea sababu ninazoona ni za msingi kulinda muungano!
Mpaka sasa bado sijaona hoja yenye nguvu kutoka upande wa bara inayoweza kunishawishi nikubaliane na kuvunja muungano.
Kuna uwezekano kuwa walioleta muungano walikurupuka, labda hasa wa upande wa sisi bara, kulikuwa na sababu hafifu za kutaka kuungana, lakini pia kuna sababu hafifu za kutaka kuuvunja. Tell me first why do you think Union is useless!
 
Back
Top Bottom