Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
KONGAMANO LA KUADHIMISHA MIAKA 44 YA MUUNGANO
CHUO KIKUU DAR ES SALAAM.
Umetolewa na Juma Duni Haji
Chuo Kikuu cha Dar es salaam .26.04.2008.

UTANGULIZI.

1. Nashukuru kualikwa kushiriki mjadala wa Kustahiki kuwepo au kuto kuwepo Muungano wetu (feasibility of the Union). Nimetakiwa nizungumze juu ya vipi siasa za muwafaka wa Zanzibar zinavyo au zitavyo athiri kuwepo kwa Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar.

Miaka miwili iliyopita nilialikwa katika maadhimisho kama haya ili nije kutoa maoni yangu juu matatizo ya Muungano ambayo wenzetu huyadogoza na kuyaita kero za Muungao. Leo nimepata tena nafasi kama ile. Hoja ya leo inahusiana sana na mjadala uliopita kwani kama ninakumbuka vyema nilisisitiza sana hapa kwamba tatizo linalouponza Muungano ni tabia ya kujiona Serikali ya Muungano ndiyo yenye nguvu kwa Zanzibar na kwamba uendeshaji wa siasa za Zanzibar huamuliwa kwa maslahi ya upande mmoja wa Muungano bila kujali athari za upande wa pili.

1.1 Hivi ninavyozungumza tumo kwenye kukwama kwa kusainiwa kwa muwafaka wa tatu wa Zanzibar ambao ulitegemewa utoe suluhisho la kudumu la Mgogoro wa kisiasa Zanzibar nap engine kupunguza kero za muungano
1.2 Ni vizuri kuzingatia kwamba muwafaka wa tatu umekuja kwa sababu miwafaka miwili mengine ya 1999 na ule wa 2001 haijasaidia kumaliza mgogoro wa Zanzibar kwa sababu wale waliopo kwenye madaraka wamekataa kuitekeleza kwa maksudi. Kwa mfano katika muwafaka wa 2001, kwa mujibu wa sheria iliyotungwa baada ya kutiwa saini muwafaka huo, Mhe. Amani Karume alitakiwa kuteuwa wawakilishi wawili tu kuingia katika Baraza la wawakilishi kutoka CUF. Hili lilimshinda. Sisi mpaka leo tunajiuliza jee kuteua wawakilishi nako kunahitaji fedha za nje za msaada wa wafadhili.

KUVURUGWA KWA CHAGUZI KWA KUTUMIA VYOMBO VYA DOLA.

2. Kwa hivyo suala la kuuliza ni kwa nini kila baada ya miaka mitano kunatokea mgogoro wa kisiasa Zanzibar?

Mgogoro wa kisiasa unatokea kwa sababu hakuna utashi wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki huko Zanzibar. Mimi ninaamini kwamba na huku bara hali ni kama hiyo. Matatizo ya huku yanafichika kutokana na ukubwa wa nchi na wala si usafi wa chaguzi zenyewe.

Vurugu za kuharibu uchaguzi kila baada ya miaka mitano mara zote husindikizwa na viongozi wa CCM na vyombo vya Serikali ya Muungano hasa vyombo vya ulinzi, jeshi la polisi, majeshi ya ndani na hata ya kuazimwa majeshi kutoka nchi jirani pamoja na kutumiwa usalama wa taifa kuendesha chaguzi hizo.

Kila ikifika uchaguzi vyombo vya Serikali ya Muungano ndivyo husindikiza na kulinda makundi haramia ya vijana wa CCM maarufu kwa jina la Janjaweed wanaosaidiwa na vikosi vya SMZ, kuhujumu utaratibu mzima wa kuendesha uchaguzi huru na wa haki. Tafadhali angalieni takwimu nilizozileta kwenu juu ya mwendo wa uchaguzi wa 2005 zenye kuthibitisha maelezo haya. Vurugu huanza tangu wakati wa kufanya makisio ya uandikishaji kama ilivyooneshwa hapa chini


Jimbo Pop. 2005 48 % as Voters ZEC Estimate. Registered voters
Uzini 19,049 9,144 10,117 14,101
Muyuni 17522 8,411 11,506 9,785
Makunduchi 16,501 7,921 7,269 10,839
Donge 18,584 8,920 9,561 11,634
Bumbwini 17,856 8,571 9,314 10,904
Chwaka 21,785 10,457 11,620 13,773
Kojani 25,575 12,276 9,556 10,469
Mgogoni 21,560 10,349 6,689 8,329
Chambani 17,741 8,516 8,356 6,404
Mkoani 19,484 9,352 9,487 8,319
Chanzo : ZEC 2005.
Mfano mzuri wa vurugu za uandikishaji zinaonekana katika vituo vya jimbo la Uzini Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja, ambalo ni moja kati ya majimbo makubwa ya CCM.

VITUO Name of the Camps Estimates Registered % Registration
UBAGO SCHOOL UBAGO TPDF 441 1402 317.91
MACHUI SCHOOL MACHUI JKU&FFU 696 1060 152.3
POSTA KAE PWANI UNGUJA UKUU NAVY 1268 2076 163.72
TUNGUU SCHOOL TUNGUU FIRE BRIGADE 520 556 106.92
MARUMBI SCHOOL MARUMBI NAVY 561 876 156.15
DUNGA BWENI SCHOOL DUNGA JKU&FPDF 1520 2106 138.55
JENDELE SCHOOL JENDELE JKU 907 1366 152.81
CHEJU SCHOOL CHEJU PRISON 971 1163 119.77
BAMBI SEC. SCHOOL BAMBI JKU 1336 2125 159.06
JUMLA 8220 12730 154.87

Uandikishaji wa aina hii huanza kulalamikiwa mapema hata kabla kupigwa kura. Haya hufanyika chini ya ulinzi wa polisi wa Muungano na vikosi vya SMZ.



KUVURUGWA KWA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGIA KURA

Hali ya daftari la wapiga kura la Zanzibar haliwezi kuitwa daftari maana, kuna watu waliozaliwa mwaka 2005 wamepewa vipande vya kupigia kura.
Majina ya mitaa kama Forodhani Muembeladu na mtaa wa Mbuyuni pia yamepewa vipande vya kupigia kura. Kuna majina yaliyorudiwa mara mbili mbili na kuna majina yasiyo baba wala babu kama vile ni majina ya Adama na Hawa manabii wa Mungu, na baadhi ya majina kukosa tarehe ya kuzaliwa Mengi ya majina haya ni ya watoto wadogo.

Daftari la aina hii haliwezi kutoa matokeo yenye kukubalika. Kuongeza wapiga kura hewa kumeongeza nafasi ya kumpa Karume kura zake kuonekana nyingi kumbe sehemu kubwa si kura za watu isipokua ni nambari zilizoandaliwa kwa lengo la kutoa ushindi bandia kama inavyonekana hapa chini katika baadhi ya matokeo ya majimbo ya uchaguzi.

Jimbo Watu/005
(a) 48% watu (b) Makisio / ZEC
(c) Registered
(d) Kura / Karume
(e) % (e)/(d)
% (e)/(b)
Bumbwini 17,856 8,571 9,314 10,904 6,189 57 89
Kitope 20,210 9,701 10,714 10,378 8,099 78 83
Donge 18,584 8,920 9,561 11,634 10,124 87 106*
W/Kas’B’ 56,650 27,192 29,589 32,916 24,412 74 90
Chwaka 21,785 10,457 11,620 13,773 11,161 81 107*
Koani 25,726 12,348 13,167 15,639 10,664 68 86
Uzini 19,049 9,144 10,117 14,101 12,486 89 137*
W /Kati 66,560 31,949 34,904 45,513 34,311 79 107.4*
Muyuni 17,522 8,411 11,506 9,785 7,741 79 92
Makunduchi 16,501 7,921 7269 10,839 8,659 80 109*
W/Kusini 34,024 16,331 18,776 20,624 16,400 80 100.4*
Source: ZEC election data. 2005


MATOKEO YA UCHAGUZI 2005.

Pamoja na kuvurugwa kwa utaratibu mzima wa uchaguzi na nguvu nyingi kutumika bado matokeo yaliyotolewa na ZEC yamezaa ulalamishi. Maana katika kipindi cha mwezi mmoja, yametolewa matokeo aina mbili tafauti.
MAELEZO MATOKEO CCM CUF
Kama Yalivyotangazwa na
ZEC baada ya uchaguzi ZEC 1 239,832
53.2% 207733
46.1%
Baada ya kurekebishwa
Mwezi mmoja baadae ZEC 2 241,899
53.6% 205,872
45.6%
TAFAUTI +2067 -1861

Ushindi huo wa Mhe. Karume uliambatana na kufichwa fomu za uchaguzi kura kuonekana tafauti katika vituo na ulisukumwa na nguvu za dola zilizojumlisha :
(i) Tume ya Uchaguzi ZEC
(ii) Masheha, (iii) Polisi, (iv) Jeshi la wananchi, (v) KMKM
(vi) JKU, (vii) Jeshi la Magereza (viii) Fire Brigade (Zima moto) (ix) Volantia
(x) Usalama wa taifa (xi) Janjawee (xii) TVZ (xiii) Redio Zanzibar na (xiv) vyombo vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Baada ya nguvu hizi mtu angetegemea kwamba, ushindi wa Mhe. Amani upindukie asilimia zaidi ya 80. Lakini bado matokeo yaliyotolewa na ZEC hayajaonesha tafauti kubwa kati ya washindani hao wawili. Kwa maelezo mengine ushindi huu wa CCM usingewezekana kama nguvu zisingetumika na utaratibu wa uchaguzi ungefuatwa. Kwa ufupi hivyo ndivyo chaguzi za Zanzibar zinavyokua.

HISTORIA YA MAUAJI ZANZIBAR NA MCHANGO WA CCM NA SMT KATIKA MAUAJI HAYO

3. Mhe. Kikwete anajua kwamba CUF ilishinda chaguzi zote tatu za 1995, 2000, na 2005. Anajua kwamba wafuasi wa CUF wameuliwa na polisi wa Muungano, na kwa mara ya kwanza Tanzania kuzaa janga la wakimbizi. Lakini bado viongozi wa CUF wamerudi na kukaa na wauaji hao kuzungumza ili kumaliza uhasama wa siasa wa Zanzibar
4. Kinachosikitisha ni kwamba viongozi wa CCM na wa Serikali ya Muungano hawapendi kuona wazanzibari wanasikilizana.Wanafurahia tuendelee kugombana kwa kutumia siasa za wagawe ili uwatawale. (Divide and Rule).
5. Kiongozi mmoja mkubwa wa CCM kutoka bara wakati tukianza mazungumzo, amefika hadi kutwambia kwamba nyinyi CUF mara hii hamna uzito wa hoja kwenye mazungumzo kwa sababu hakuna wazanzibari waliokufa , bora mazungumzo ya 2001 mulikua na hoja ya msingi. Sisi tulishangaa sana kusikia kauli ya kiongozi wa Muungano akisema hivyo. Baada ya NEC kuyakataa makubaliano tuliyofikia, ndipo tulipozinduka na kuelewa kiongozi yule alikusudia nini.

6. Ushahidi wa kueleza haya ni jinsi Mhe Kiwkete na CCM walivyolichukulia maskhara suala hili la Muwafaka. Mhe. Kikwete ndiye kiongozi wa nchi , na pia kiongozi wa chama chake, vipi anashindwa kufanya maamuzi ya kuona amani inapatikana Zanzibar. Badala yake anakuja na lugha ya kisanii na kuepuka hoja ya msingi ya kukamilisha makubaliano yaliyofikiwa yatakayoandaa mazingira mazuri ya kufanyika uchaguzi huru na wa haki hapo 2010.



PENDEKEZO LA CCM L A KURA YA MAONI.

7. Kura ya maoni inayopendekezwa na CCM inatafuta jibu moja kati ya mawili yafautayo. La kwanza ni aidha watu wengi kukubali mfumo mpya wa Serikali shirikishi na la pili la watu wengi kukataa serikali shirikishi. CUF wanauliza kama wengi watasema wanataka, jee kuna uhakika gani wa Mhe Karume kutekeleza maamuzi hayo akiachiwa peke yake. Maana muwafaka wa 2001 alishindwa kuteua wajumbe wawili wa baraza la uwakilishi kutoka CUF, vipi atakubali kutekeleza kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa hivi sasa kabla kupiga kura ya maoni. Na kama watu wengi watasema hawataki Serikali ya umoja wa kitaifa, jee hali hiyo itakua imetoa jibu la ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo wa Zanzibar?. Maana chanzo cha mgogoro imetokana na SMZ kubaki wasshindani na wasimamizi wa chaguzi na hivyo kuvuruga utaratbi mzima wa uchaguzi huo. Katika hali zote mbili, kura ya maoni haiwezi kusaidia chochote kati ya hayo mawili kwenye mazingira ya sasa ya CCM kubaki peke yao katika Serikali.

UFUMBUZI WA KUDUMU UTAPATIKANA VIPI?

8. Mheshimiwa Kikwete anajua kwamba bila uchaguzi huru na wa haki 2010 ni kurudia vurugu na mauaji mengine visiwani humo. Hiyo Serikali ya umoja wa kitaifa hapo 2010 huwezi kuipata bila uchaguzi huru na wa haki 2010. Vipi utapata uchaguzi huru 2010 bila kutekeleza muwafaka kwa kushirikiana pamoja hivi sasa?

9. Mhe. Kikwetet anajua kwamba Karume hakushinda uchaguzi wa 2005 na hivyo Serikali iliyopo madarakani hivi sasa siyo halali, vipi anakubali kufanya kura ya maoni kwa kutumia Serikali isiyokubalika na wananchi, chini ya Tume ya uchaguzi isiyokubalika na chini ya daftari lisilokubalika?

10. Mhe. Kikwete anajua kwamba bila CCM na CUF kufanya kazi pamoja kuanzia sasa katika serikali ya pamoja kwa kutekeleza Muwafaka huu hakutakua na uchaguzi huru na wa haki 2010. Kwa hivyo kizingiti cha muwafaka wa sasa kipo penye tatizo la utaratibu wa namna ya kupata uchaguzi huru na wa haki hapo 2010 ili tuepuke mgopgoro mpya.

11. Lakini badala yake Mh. Kikwete amekwenda Butiama kuzaa mgogoro ndani ya mgogoro, eti kura ya maoni: aulizwe nani chini ya usimamizi wa nani ili upate jibu gani ambalo hivi sasa halipo?
12. Imani huzaa imani. CUF chama cha wananchi kilionesha imani kwa kuiachia miwafaka miwili ya 1999 na ule wa 2001 itekelezwe na Serikali ya SMZ, bila sisi kushiriki maana CUF hatuna nguvu za Dola. CCM na Serikali zake kwa maksudi walikejeli miafaka hiyo na matokeo yake kwa mara ya tatu tunazungumza muwafaka mwengine.
13. Hivyo chama chetu CUF kimesimama na kauli kwamba kama hakuna imani ya kufanya kazi pamoja hivi sasa, hakuna matumaini yeyote ya kutekelezwa muwafaka huu.
14. Na kama CCM inakataa kufanya kazi pamoja hivi sasa hakuna matumaini ya kuwepo serikali ya pamoja hapo 2010. Hiki ndiyo kipimo kikubwa cha kuupima uongozi wa CCM kwa wao kuonesha kwamba wako tayari kumaliza mgogoro wa Zanzibar. Mheshimiwa Kikwete na CCM wamefeli mtihani huu mdogo.

USANII WA KISIASA.

15. Waraka wa CCM uliofikishwa kwenye NEC umethibitisha kwamba agenda mpya kuhusu kufanywa kura ya maoni ameipeleka Mhe Kikwete kwenye NEC baada ya kujadliwa katika Kamati Kuu. Inashangaza baadae Rais anarudi kuwaambia wakazi wa Dar es salaam kwamba hoja ilitokana na mjadala. Mhe. Kikwete anafanya usanii wa kisiasa, na matokeo ya usanii wake ni janga kwa wazanzibari waliochoka mateso kwa kutopewa nafasi ya kuchagua kwa hiari yao viongozi wanaowataka bila ya sindikizo la Serikali ya Muungano

KIKWAZO CHA MIGOGORO YA ZANZIBAR

16. Kwa hivyo wazanzibari wote wanaamini kuwa viongozi wa Muungao ndiyo kikwazo cha ufumbuzi wa matatizo yao ya kutosikilizana ili kujenga nchi yao. Kwa sababu kila unapofika wakati wa uchaguzi huletea majeshi kusaidia chama cha CCM lazima kishinde.
17. Kwa mfano wakati Mhe. Mkapa akijitayarisha kwa uchaguzi wa 2005 alisema bila kificho kwamba atafanya kila lililo katika uwezo wake kuhakikisha kwamba CCM inashinda Zanzibar na Bara. Ndipo akatuletea vikosi vya polisi na majeshi kunajisi na kupiga wafuasi wa CUF, huku jeshi hilo chini ya Kamanda wa Mkoa wa mjini magharibi aitwae Kizuguto,likiwalinda vikundi haramia vya CCM vifanye vitakavyo.
18. Hapo 2001 wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi,Rais mstaafu Mzee Msafi Banjemin Mkapa alipeleka askari aliowaita Ngunguri, kule Zanzibar na wakawaua wazanzibari wasiopungua 45 na baadae Rais akarudi kujisifu kwamba tusifanye mchezo maana hiyo ndiyo maana ya Mapinduiz daima .Baada ya kuwaua wazanzibari wale Mhe. Mkapa alikuja kwenye mkutano wa hadhara pale jangwani na kuwapa vyeo askari waliowaua wazanzibari hao. Hivyo ndivyo Serikali ya Muungano inavyowafanyia wazanzibari.

Tulitegemea matukio yale yawe fundisho kwa Mhe. Kikwete. Hali iliyojidhihirisha kule Butiama ni kwamba yale yaliyotoke kule Zanzibar 2001 na 2005, hayajamshtua na wala hatajali yakitokea tena 2010.
19. Kwa miaka 15 sasa Chama cha wananchi CUF kimeonesha uvumulivu mkubwa sana ili kuepusha wazanzibari wasianze mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Viongozi wetu wa kitaifa wamefika kiwango cha kutukanywa hadharani na wafuasi wao pale walipowakataza wasijibu fujo. Wamekua wakifanya hivyo kwa maslahi ya taifa. Kila mara tumekua tayari kuacha kudai hoja z msingii ya kurejewa uchaguzi ulioharibiwa kwa maksudi ili kulinda umoja wa wazanzibari. Viongozi wa CCM na Muungano wao bado hushikilia misimamo ya chama chao.

20. Hivyo athari za siasa za muwafaka wa Zanzibar kwa Muungano ni sawa na kuweka kijinga cha moto kwenye jaraha la moto la mateso ya wazanzibari, na kwa wazanzibari ni ushahidi mwengine kwamba Muungano huu hauna faida kwao isipokua kuwakandamiza na kwa kutumia nguvu za Serikali ya Mhe. Kikwete na CCM.

AHADI NA MALENGO YA MAPINDUZI YA 1964 NA UBAGUZI WA KIHAFIDHINA

21. Mapinduzi yalikua na lengo la kuwaunganisha wazanzibari wawe kitu kimoja. Baada ya miaka 50 wazanzibari wamegawika zaidi kuliko walivyokua kabla Mapinduzi. Huku ni kupotosha lengo la mapinduzi ya 1964.,

22. Wachunguzi wa kitaalam wanabainisha kuwa iwapo historia ndiyo inayotizamwa katika kuueleza muundo wa kisiasa wa visiwa viwili vya Unguja na Pemba kwa kudhani kuwa kila kisiwa kimekuwa ngome ya chama kimojawapo peke yake, basi utafiti wa kitaalamu unaotokana na hali halisi hauoneshi hivyo. Huko Pemba ambako ndiko kisingizio kikubwa cha wahafidhina wa Zanzibar wanakokueleza kuwa CCM haiungwi mkono ukweli ni kwamba katika uchaguzi mkuu wa Julai 1963 chama cha ASP kilipata asilimia 44 ya kura zote za kisiwa hicho.

23. Katika kipindi cha miaka takriban 50 ya utawala wa ASP/CCM matokeo ya kura za urais yameshuka na kutoa sura mbaya sana ya kibaguzi kama inavyoonekana hapa chini. Kura za ASP/CCM kutoka Pemba zimeshuka kutoka asilimia 44, hapo 1963 na kufika asimia 16 tu 2005. Si hivyo tu ila kilicho kibaya ni kwamba katika kila kura 100 za ushindi wa CCM mchango wa kura za Pemba katika ushindi huo umeshuka mpaka kura 9 tu katika uchaguzi wa 2005.


CHAMA/VYAMA Oktoba 1995 Oktoba 2005
Unguja Pemba Unguja Pemba
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) 144,408 20,863 217,209 22,413
69% 17% 72% 16%
Mchango/Kisiwa katika ushindi 87% 13% 91% 9%

24. Wahafidhina wa CCM walipaswa kujiuliza hali hii imesababishwa na nini. Si kingine isipokua siasa mbaya za kibaguzi na ukandamizaji, kama zinavyothibitika katika mfumo wa Serikali ya SMZ hivi sasa. Hivi ninavyozungumza Serikali ya Zanzibar ina umbo lifuatalo


Wadhifa Unguja Pemba Jumla
Mawaziri 14 1 15
Naibu Waziri 5 1 6
Makatibu Wakuu 13 2 15
Naibu Makatibu Wakuu 12 0 12
Wakuu wa Mikoa 4 1 5
Wakuu wa Wilaya 7 3 10
Wakuu wa Idara 83 17 100
Wakuu wa Polisi 18 0 18
Wakuu wa Vikosi vya SMZ 5 0 5
Kamati za Baraza la Wawakilishi 5 1 6
Jumla 166 26 192

Nyote munaelewa kwamba hata Pemba wapo wanachama na viongozi wa CCM wenye uwezo na waliosoma kuweza kuteuliwa kushika nyadhi hizo. Lakini kwa makusudi kabisa viongozi wanaojidai kulinda Mapinduzi wamewaacha. Kweli haya ndiyo malengo ya Mapinduzi ya 1964? Mapinduzi ya 1964 yalitegemewa kuwatoa watoto wa wakwezi na wakulima kutokana na mateso ya utumwa na maonevu, mateso ya kukosa elimu na pia mateso ya kubaguliwa. Leo watoto wa wakwezi na wakulima wanagombanishwa wenyewe kwa wenyewe. Wamefanywa watumwa wa hiari chini ya ulinzi wa Polisi .

21 Kwa mwenendo huu ile Falsafa ya Mwalimu ya Pan-Africanism ni ndoto ya alinacha, maana kama nchi mbili zinaendeleza ubaguzi mbaya kuliko ule wa Makaburu, vipi tutaweza kujenga umoja wa waafrika. Ni aibu
22 Vijana waliokoseshwa elimu huchukuliwa katika makambi na kufundishwa chuki za kuwachukia ndugo zao. Vijana kutoka Makunduchi, vijana waliokata tamaa ya maisha, wakiongozwa na askari wa KMKM, JKU, Magereza na Polisi walikwenda katika kisiwa cha Tumbatu au Pemba na kuwanajisi ndugu zao, kuvunja nyumba zao na kuwalazimisha wakimbie katika makazi yao. Kosa la watumbatu na wapemba wale ni kukipigia kura chama cha CUF
23 Mateso haya yalifanywa chini ya usimamizi wa Polisi na mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, ambae pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Mhe. Haji Omar Kheri. Huyu si mwarabu, huyu ni mtoto wa kitumbatu aliezaliwa Tumbatu na kusoma Tumbatu Baada ya kupata bahati ya kuwasaidia jamaa zake amewageuka na kuwafanya vikaragosi,walokosa heshima. Hapo ndipo CCM na Serikali ya Muungano ilipowafikisha wazanzibari. Haya ndiyo yanatakiwa yaendelezwe hapo 2010 na Mhe Kikwete anayafurahia na kuyakubali.



SIASA ZA KUREJESHWA ARDHI KWA WARABU

24 Kuna wakati CCM ikitumia hoja ya kurejeshwa ardhi kwa waarabu kama CUF itaingia madarakani. Hoja hii sasa haizungumzwi kwa sababu takriban ardhi yote imeshachukuliwa na familia ya viongozi wa CCM na inasemekanahasa Mhe. Karume na familia yake.

SIASA ZA KIHAFIDHINA NA MGOGORO WA MUUNGANO

25 Ni vizuri kueleza pia kwamba hoja pekee inayosimama hivi sasa katika siasa za CCM Zanzibarna Jamhuri na katika Serikali ya Muungano ni ubaguzi. Nusu ya wazanzibari hubaguliwa kwamba wao asili yao ni warabu, au hubaguliwa kwa kuambiwa kwamba wao ni vibaraka wa chama cha ZNP. (Zanzibar Nationalist Party.) Pale wanapotaka kututukana au kupinga kile wasichokitaka viongozi wa CCM wanapenda sana kuitumia hoja hii hata kufikia kiwango hawajali kwamba hua wanajitukana wenyewe. Wakati wa Mkutano Mkuu Mhe. Salim Ahmed Salim alibaguliwa kwa asili ya uarabu mbele ya watoto na wake wa waheshimiwa hao ambao ni warabu wakiwepo hapo kwenye mkutano.
26 Hoja hii ya ubaguzi huunganishwa na kunasibishwa na chama cha zamani cha ZNP ambacho ndicho kilichopinduliwa. Viongozi wa wahafidhina Wanashindwa kujiatambua kwamba wengi kati ya wale watetezi wakubwa wa sera hii ya kihafidhina kama akina Muhamed Seif Khatib inasemekana kwamba mwenyewe alikua kijana wa umoja wa vijana wa ZNP aliekua ni mpika tarumbeta ya bendi ya vijan hao.

MATATIZO TA ZANZIBAR KIUCHUMI.

27 CCM inashindwa kueleza kwamba hali ya maisha ya wananchi hivi sasa ni mbaya sana. Ukosefu wa kazi haupungui asilimia 80, hali ambayo imefanya vijana wa kizanzibari kushiriki katika vitendo vya kula madawa ya kulevya na wasichana kushiriki vitendo vya kuuza heshima zao yaani umalaya mkubwa sana.
28 Sekta pekee inayotoa ajira Zanzibar ni uaskari. Aidha uwe askari wa JKU, askari wa KMKM, askari wa Fire Brigade walokosa gari la kuzimia moto, askari wa Valantia, askari wa usalama wa taifa au janjaweed. Hakuna sekata yeyote ya uzalishaji inayotoa ajira labda udereva wa kutembeza watalii. Karibu tutafikia hali ya one man one soldier- yaani mtu mmoja askari mmoja.
29 Hali ya ugumu wa maisha inaashiria kwamba uchaguzi wa 2010 utakua na maafa makubwa sana kama muwafaka huu haukutoa suluhisho lenye kuleta maelewano mapema. Vijana bila kujali itikadi za vyama wenye ukosefu mkubwa wa maisha ya maana wameshindwa kusubiri mabadiliko yenye matumaini ya hali ya uchumi wa Zanzibar kubadilika. Kila siku zilivyopita hali inazidi kuwa ngumu na uonevu na ubaguzi uliokithiri unaendelea na kushamiri. Pale mjini Zanzibar mwenye kuomba naye anaombwa. Hakuna mwenye nacho isipokua wakubwa wa Serikali na baadhi ya viongozi wachache wa CCM . Hata wafanya biashara wamekimbizwa na serikali eti kwa kisingizio kwamba wanakisaidia chama cha CUF.
30 Kwa hivyo kukosekana kwa muwafaka ni kuendelea kuwanyima wazanzibari kujipa nafasi ya kufanya kazi za maendeleo yao na wengi wao wanaamini kwamba sababu kubwa ya hali mbaya ya uchumi ni kukosekana utulivu wa ksiasa, hali ambayo inachochewa na Serikali ya Muungano. Wazanzibari wanaamini kwamba hali hii ya kubaki na hali ngumu inafurahiwa na serikali ya Muungano maana lengo ni kwamba wazanzibari wafike mahali waseme hakuna haja ya kubaki na serikali isiyo manufaa nao.

31 Viongozi wa CUF watafika mahala hawatasikilizwa tena na vijana waliokosa haki na kuteswa kwa kudai haki yao ya kushiriki katika kuchagua viongozi wa nchi yao. Kuna kila kiashirio kwamba maafa yanaweza wakati wowote kutokea, maana njaa haina bwana wala haijui kiongozi na wala haina itikadi
32 Yote haya Mhe. Kikwete anayaelewa vyema. Kilicho cha ajabu ni kwamba ameshindwa kusimama kama kiongozi wa nchi na amebaki kushabikia itikadi za kichama, za kibaguzi zinazowadhalilisha hata wao. Hii ni hatari kwa taifa. Wazanzibari wanauona Muungano ni kikwazo kikubwa cha kupatikana suluhu ya kudumu na hivyo kuwasababishia hali ngumu ya maisha, ugomvi usokwisha katika jamii na kukosa nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

KUKOSEKANA UONGOZI WENYE HEKIMA

33 Kwa hivyo katika kuliangalia suala la kuwepo au kutokuwepo Muungano, lazima watanzania wanahitaji kuzinduka kwamba Tanzania hivi sasa imekosa uongozi wenye hekima wenye uwezo wa kusimamia masuala mazito ya kitaifa. Tafadhali tafautisheni JK ya Julius Kambarage na JK ya Jakaya Kikwete. Hizi ni tafauti ya mbingu na ardhi. Ni hatari sana. Tangu kuingia madarakani Mh. Kikwete inasemekana maamuzi yake mengi yamekua ya kusukumwa, haonekani kabisa kwamba ana uwezo kama ule tulio utegemea hapo 2005 wakati wa kampeni za uchaguzi ingawa CUF tuliwatahadharisha watanzania siku ya ufunguzi wa kampeni zetu kule Tabora 2005.
34 Mgogoro wa Zanzibar unaweza kusababisha kuvunjika kwa amani Tanzania nzima na ndiyo maana CUF inasisitiza wazanzibari kufanya kazi pamoja hivi sasa ili kuandaa uchaguzi huru na wa haki wa 2010. Kama Mhe. Kikwete ataendelea kuona kwamba chama chake ni bora kuliko usalama wa taifa, basi wakati ndiyo utatoa jibu.
35 Mgogoro wa Afrika ya kusini ulikwisha si kwa sababu ya ushupavu pekee wa Mzee Mandela, bali pia ujasiri wa mzee De,clerk kukubali ukweli kwamba lile lenye faida kwa wazungu ndilo lenye faida kwa waafrika. Alimaliza uhasama wa wazungu na wafrika kwa kuzingatia faida ya taifa lao. Baada ya kumaliza mazungumzo Mzee De,clerk hakurudi nyuma ,alisimama kwenye utekelezaji bila kusukumwa kwa sababu alikua na nia njema. Makubaliano ya mika zaidi ya mika 100 ya Afrika ya kusini hayakupigiwa kura ua maoni. Msumbiji walikua na mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa mika 18, makubaliano yao hayakupigiwa kura ya maoni, Kule uingereza kumekua na mgogoro wa Nothern Ireland , umemalizwa kwa kuundwa serikali ya pamoja bila kura ya maoni. Jirani zetu hapo Kenya ambapo Mhe. Kikwete yamemalizika kwa kuunda Serikali ya pamoja bila kupigwa kura ya maoni. Lengo kubwa katika nchi zote lilikua kuweka mbele mstakabali wa taifa. Kuna lipi la jabu lisilowezekana kwa mgogoro wa Zanzibar. Ni ukosefu wa utashi wa kisiasa kwa CCM na Mhe. Kikwete.
36 Inaelekea Mhe. Kikwete alitoa kauli ya kuumaliza mgogoro wa Zanzibar pale Bungeni si kwa nia njema isipokua alikusudia kuiweka CUF katika matumaini (Political engagement) huku akivuta muda hadi ifike 2010 kama maelezo ya kutaka kura ya maoni katika waraka wao unavyoeleza, na ndiyo maana waraka wa CCM wa NEC umeeleza kwamba pendekezo la kura ya maoni ni kwa lengo la kuipiku CUF ili waache kushabikia kudai mambo madogo madogo. Madai haya madogo ni ile haja ya kutaka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hivi sasa kabla 2010.
37 Yeye kama kiongozi wa nchi hii alitakiwa asimame juu zaidi ya ushindani wa siasa za vyama na kuelekeza msimamo wake kwa hekima na kumaliza tatizo. Hilo limemshinda kwa sababu hakua na nia njema.
38 Kuwepo au kutokuwepo Muungano kunategemea jinsi viongozi waliopo madarakani wanavyotoa umuhimu wa kulinda umoja wa wazanzibari na hivyo wa watanzania. Kukataa Serikali ya umoja wa kitaifa hivi sasa ni kuongeza mgogoro Zanzibar na hivyo kupalilia vurugu hapo 2010. Vurugu hizo zikianza Zanzibar hazitaacha kuingia na Tanzania bara. Huu ndiyo mtihani wa Mhe Kikwete na wahafidhina wake.

KUKOSEKANA VIONGOZI WENYE HEKIMA BARA LA AFRIKA

39 Lakini si shangai, hivyo ndivyo historia ya viongozi wa kiafrika walivyo . kwa kawaida hua hawajifunzi maharibiko yaliyotokea kwa wenegine. Rais Mugabe anaongeza silaha kuua raia zake, wakati anajua ameshindwa hata kuwapatia mkate watu wake ambao anajigamba kwamba anawatetea. Vipi rais atatetea maiti. Rais atetee walio hai.
40 Watu wake wanakufa njaa kwa ukosefu wa chakula. Yeye baada ya kuuona ukweli wa kushindwa kwake anagombana na mataifa makubwa sijui ili aweje. Hivyo kiburi chake kinaweza kushinda kile cha Sadam Husein?.
41 Wafrika tuna tatizo. Watanzania tuna tatizo. Hatuna viongozi na hatupewi nafasi ya kuwachagua viongozi tunaowataka.
42 Lakini si shangai, maana tunajua jinsi tulivyowapata viongozi wa aina ya Kikwete na akina Chenge. Hawa tumewaandaa sisi, hatuna sababu ya kumlaumu mwarabu hapa.
43 Hawa tumewachagua sisi, hawa wametayarishwa na CCM. Hawa ndio vijana wa Mwalimu Nyerere waliouweka Mwenge juu ya mlima wa kilimanjaro na kumwirika pale penye dhuluma, uonevu na ukandamizaji.
44 Tumewachagua wenyewe hawa baada ya kutupa kapero na fulana isiyo hata suruali ya kuficha sehemu zetu za siri. Mimi si shangai wala sitanii, hawa ndio tuliowachagua kwa nyimbo za kwaya zilizoimbwa na Kepteni Komba. Mimi si shangai hawa ndio tuliowachagua kwa harufu ya sahani ya pilau na jagi moja ya pombe ya kienyeji. Mimi si shangai maana hawa ndio tuliowachagua kutokana na sura zao nzuri na uso wenye bashasha bandia.
45 Watanzania tuna tatizo la ukosefu wa uongozi lakini pia tuna tatizo la kuelewa. Kiburi hiki walichonacho kina Kikwete na CCM tumewapa sisi. Walituahidi Tanzania yenye neema wanatulipa Tanzania yenye njaa na ufisadi. Wanatunga sheria za uchaguzi halafu wao wenyewe ndio wanazivunja. Salama itatoka wapi.

KHITIMISHO. HATUNA VIONGOZI WENYE HEKIMA

46 Kwa kumalizia ni vyema nieleze kwamba Muungano umeendelea kuwa na matatizo kwa miaka 44 sasa na inaonekana bado hatukupata Kiongozi wa Muungano aliyetayari kukabili ukweli wa matatizo yaliyopo na kufuata taratibu za kikatiba na kisheria kuelekea kwenye amani na dimokrasia ya kweli. Migogoro mingi ya siasa za Tanzania yametokana na aidha kuwadhbiti wazanzibari mmoja mmoja au kuwadhibiti viongozi wao. Kila mara tafsiri hutolewa kwamba viongozi hao wanahatarisha Muungano. Ni ajabu kwamba maisha yote wenye kuhatarisha Muungano ni wale wanaodai haki zao za demokrasia. Na ndiyo maana muda wote CUF imesimama juu ya kupitiwa upya Muungano huu na Kuundwa kwa Serikali tatu, ya Zanzibar, ya Tanganyika nay a Muungano.
47 Hali ya kisasa iliyomkumba Mzee Jumbe, Mzee Abduwakil na hata akina Maalim Seif na wenzake ni hali ya ukandamizi kwa kujaribu kukwepa ukweli wa mgogoro wa Muungano.
48 Tuna hitaji viongozi wa wapya na chama mbadala kutetea na kushughulikia hali hii. Viongozi waliopo sasa inaonekana hawana uwezo huo na hwenda wakawa wao ndiyo chanzo cha tatizo na kuutia matatizo Muungano wetu. Hatuna sababu ya kuakhirisha tena suala hili.
49 Demokrasia ya kweli Zanzibar itazaa Demokrasia ya kweli Tanzania bara na hivyo Kuimarisha Muungano wa kweli Tanzania na hapo tu ndipo ufisadi na wizi wa mali za watanzania utakapomalizika maana viongozi watatkiwa kujibu uharamia wao mbele ya wananchi.

HAKI SAW KWA WOTE
 
Serikali Zanzibar yaukana mpango wa serikali ya mseto

Salma Said, Zanzibar

NAIBU Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Ali Juma Shamhuna amesema hivi sasa hakuna uwezekano wa kuundwa kwa Serikali ya Mseto kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).


Shamhuna alisema hayo juzi katika Jimbo lake la Donge, Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wazee wa CCM wa Jimbo hilo, waliokuwa wakitaka maelezo ya kina chanzo cha kuzuka mjadala wa Serikali ya Mseto Zanzibar.


Katika maelezo yao wazee hao walionekana kuwa na jazba kubwa wakimtaka Waziri

Shamhuna kueleza ni akina nani waliothubutu kuibua hoja ya Serikali ya Mseto huku

wakijua wazi kuwa suala hilo linahusu maslahi ya watu wote.


''Mheshimiwa Mwakilishi, sisi wazee wako na wananchi wa Jimbo lako, tumekwita hapa leo

utueleze kwa kina, hivi huo mseto ni kitu gani na kwa nini chama chetu tulichokichagua kinataka kushirikishwa na chama tusichokichagua,''
aliuliza Mwanakhamis Khamis Juma.


Akijibu, Shamhuna alisema kwamba serikali ya mseto huundwa kwa kuunganishwa wajumbe wa vyama vilivyokubaliana kuunda serikali baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu, lakini kwa kadiri anavyofahamu yeye suala hilo CCM wameshauri ni vyema watu wa Zanzibar wakaulizwa kupitia kura ya maoni.


''Mheshimiwa tunakwambia na mapema sisi hatutaki kusikia suala la Serikali ya mseto..., mseto tunavyojuwa sisi unakuwa ni wa chakula kwa kuchangaywa wali na choroko au na maharagwe, lakini sio serikali au kama mnataka kutuwekea CCM yetu rehani kwa mseto sawa,'' alisema mzee huyo.


Naye Shamhuna alisema, kwa kuwa wananchi wa Jimbo lake walimwita na kumweleza msimamo wao wa kupinga serikali ya mseto atayawasilisha maoni hayo kwenye Baraza la Wawakilishi na kama kuna watu watakaosema anachafua hali ya hewa na kufukuzwa, atarudi kwa wananchi waliomchagua kufanya nao kazi.


''Seif Shariff Hamad sio Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, kama ni suala la kutafuta vyeo kuwa sasa eti Seif Shariff awe Waziri Kiongozi katika Serikali ya mseto haiwezekani, apate cheo kwa Katiba ipi, maana katiba yenu haizungumzii serikali ya aina hiyo na hata katiba ya Tanzania nayo haisemi hivyo,'' alisema Shamhuna.


Alisema dunia ya leo si ya kulazimishana na pia dunia haikulazimisha Serikali ya mseto kwani hata mataifa makubwa hayana mfumo wa utawala wa aina hiyo.


Katika hatua nyingine, Chama cha CUF kimepanga kufanya maandamano na mkutano wa hadhara Jumapili ijayo katika Kisiwa cha Pemba.


Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Mahusiano na Umma wa chama hicho, Salim Bimani maandamano hayo ni sehemu ya harakati za chama cha CUF katika kutoa shinikizo kwa CCM kukubali na kutia saini makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya pamoja ya kutafuta Mwafaka.


Alisema maandamano hayo yataanza saa 2:00 asubuhi eneo la Machano Mane, Chake Chake na kuelekea katika Kiwanja cha Gombani ya Kale na kwamba yatapokewa na kuhutubiwa na Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba na viongozi wengine wakuu wa chama hicho.


http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5863


My take kwenye hili ni kwamba kwa misimamo hii, naona bado safari ni ndefu kufikia muafaka huko Zanzibar! Misimamo ya kihafidhina kama hii haiwezi kamwe kuleta suluhisho....ambalo kwangu mimi nadhani ni muhimu kwa ustawi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla~
 
wamebadilika toka kwenye kura za maoni kwenda kwenye kusema haya? Ukisikia usanii at its best ndio hapa.
 
Huyo Naibu Waziri Kiongozi alikuwa anaongea na wananchi wa Jimbo lake ambalo ni la CCM na hao wananchi wa jimbo hilo hawawezi kuwawakilisha watu wa majimbo mengine. Waziri huyo huyo anaweza kwenda kule Pemba nako akaongee na wananchi wa kule asikie wanasemaje. Zanzibar si Unguja tu, waende na huko Pemba vilevile. Acheni usanii. Zanzibar bado hawajaukana huo mpango, na kama Katiba ndiyo kisingizio kwani hiyo katiba haiwezi kubadilishwa kukidhi haja ya wananchi????? Kwani kule Kenya walikuwa na cheo cha Waziri Mkuu kabla??? Mbona katiba ilibadilishwa na Rais wa Zanzibar si Makamu wa Rais???? Kaeni chini muongee, suala si Hamad au Karume au Shamuhuna. Suala ni kuleta maelewano within Zanzibar, acheni USANII.
 
Yaliyosemwa hapo ni maoni ya wanajimbo la Donge ambao kwa namna moja hadi nyingine hawapo kwenye Timu ya Muafaka.

Nakubaliana na wewe mkuu katika hili..hawawakilishi mawazo ya wazanzibari wote...lakini kwa upande mwingine, inaleta picha kwamba bado wapo watu wa namna hii...kwa mtu kama Shamhuna kuwa so low na kutoa maneno kama hayo dhidi ya katiba as if haiwezi kubadilishwa, naona ni unazi uliovuka mpaka

Huyo Naibu Waziri Kiongozi alikuwa anaongea na wananchi wa Jimbo lake ambalo ni la CCM na hao wananchi wa jimbo hilo hawawezi kuwawakilisha watu wa majimbo mengine. Waziri huyo huyo anaweza kwenda kule Pemba nako akaongee na wananchi wa kule asikie wanasemaje. Zanzibar si Unguja tu, waende na huko Pemba vilevile. Acheni usanii. Zanzibar bado hawajaukana huo mpango, na kama Katiba ndiyo kisingizio kwani hiyo katiba haiwezi kubadilishwa kukidhi haja ya wananchi????? Kwani kule Kenya walikuwa na cheo cha Waziri Mkuu kabla??? Mbona katiba ilibadilishwa na Rais wa Zanzibar si Makamu wa Rais???? Kaeni chini muongee, suala si Hamad au Karume au Shamuhuna. Suala ni kuleta maelewano within Zanzibar, acheni USANII.

Kabisaa...hii inanipa picha kuwa hata suala la kusema kuwe na kura ya maoni, kuna watu bado hawalitaki kabisa kulisikia...lakini ndo hivo huwezi kusuia mabadiliko daima...lazima ipo siku tu yatatokea
 
Nakubaliana na wewe mkuu katika hili..hawawakilishi mawazo ya wazanzibari wote...lakini kwa upande mwingine, inaleta picha kwamba bado wapo watu wa namna hii...kwa mtu kama Shamhuna kuwa so low na kutoa maneno kama hayo dhidi ya katiba as if haiwezi kubadilishwa, naona ni unazi uliovuka mpaka
Hapo visiwani wanamjua sana Shamhuna na anaeleweka kwa kauli zake zenye utata mwingi, Nina hakika hata mwandishi wa habari hii alimchokoza kwa maswali na kukurupuka na majibu hayo..
 
Ukweli Ni Kwamba Watu Wa Unguja Wana Hasira Na Jk Na Wanaamini Yeye Ndiye Chanzo Cha Hii Agenda,sasa Wameenda Mbele Zaidi Maana Wanamsema Vibaya Eti Huyu Jamaa Kukaa Miaka Miwili Kisiwandui Keshajiona Mnzanzibar Tayari!! Anasema Anatufahamu Sisi Ndani Na Nje,wanamtuhumu Kuwa Anataka Awaletee Rais Wake Baadala Ya Dkt Gharib Billal, Na Ujanja Ni Kumtosa Shein 2010 Ktk U-vp Na Bilal Awe Ndie Vp Wa Jk Na Rais Wa Zenj Awe Atakayemleta Jk.

Huo Ndio Msimamo Wa Waunguja Na Namna Wanavyomungalia Jk Kwa Sasa,all In All Jk Knows Well Kuwa Suguano Lipo Na Yeye Ndiye Mwenye Mpini Kazi Yake Ni Kumuelekeza Wa Kuchinjwa Kibra Wakati Ukitimu. Tunasubiri 2010 Zenj
 
Watasema yote waliyoyaficha.

Huyu aliyesema ni naibu waziri kiongozi kwahiyo anafaamu msimamo wa serikali yake, hawawezi kuruhusu mseto zanzibar hata siku moja na wala haitatokea CUF wakashinda kwa njia yeyote vile kwenye uchaguzi wa kisanduku.
 
Hapo visiwani wanamjua sana Shamhuna na anaeleweka kwa kauli zake zenye utata mwingi, Nina hakika hata mwandishi wa habari hii alimchokoza kwa maswali na kukurupuka na majibu hayo..
Sadakta Kibunango. Wewe hushangai kuwa hata hakuchaguliwa kuwa mjumbe wa NEC-CCM, na hayumo katika CC ya CCM. Shamhuna ni Shamhuna tu, na nanapoona mwanga wa maslahi yake , basi ni hivyo- hovyo. Si Mwanasiasa, bali ni "Opportunist".
 
Ukweli Ni Kwamba Watu Wa Unguja Wana Hasira Na Jk Na Wanaamini Yeye Ndiye Chanzo Cha Hii Agenda,sasa Wameenda Mbele Zaidi Maana Wanamsema Vibaya Eti Huyu Jamaa Kukaa Miaka Miwili Kisiwandui Keshajiona Mnzanzibar Tayari!! Anasema Anatufahamu Sisi Ndani Na Nje,wanamtuhumu Kuwa Anataka Awaletee Rais Wake Baadala Ya Dkt Gharib Billal, Na Ujanja Ni Kumtosa Shein 2010 Ktk U-vp Na Bilal Awe Ndie Vp Wa Jk Na Rais Wa Zenj Awe Atakayemleta Jk.

Huo Ndio Msimamo Wa Waunguja Na Namna Wanavyomungalia Jk Kwa Sasa,all In All Jk Knows Well Kuwa Suguano Lipo Na Yeye Ndiye Mwenye Mpini Kazi Yake Ni Kumuelekeza Wa Kuchinjwa Kibra Wakati Ukitimu. Tunasubiri 2010 Zenj

Well. It is a "Food for thought". Lets see, and digest it.
 
Baada ya kifo cha Kiongozi wa taifa la zanzibar mwaka 1972, kwa kupigwa risasi na Luten Hamud Hamud, raisi nyerere kwa kutumia influence yake aliyokuwa nayo alishawishi na kumteua ndugu Aboud Jumbe kuwa kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar, wakati Aboud Jumbe anateuliwa alikuwa ni waziri wa nchi ofisi ya raisi aliyekuwa anashugulikia muungano.

Mwalimu alimteua Aboud Jumbe kwa sababu walikuwa na element za pamoja kwenye usocialist, umoja wa ulisaidia kupunguza misuguano ya mambo ya muungano yaliyokuwa yameanza kujitokeza wakati wa karume. Aboud Jumbe hakuwahi kukaa zanzibar shuguli zake nyingi alifanyia Dar kwa kuwa alijua kuwa baada ya nyerere yeye ndo mrithi wa kiti cha uraisi Tanzania.

Na kwa kuwa alipigiwa upatu na mwalimu visiwani hawakumpenda , hii iliacha pengo kubwa sana kwenye uongozi wake na wananchi wa zanzibar,

Bwana Aboud Jumbe alifanya kosa la kwanza pale alipokubali kuunganisha vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi, hakujua kuwa ndo alianza kuivua zanzibar uzanzibar wake rasimi na kuingia kwenye Tanzania kama tanganyika ilivyopeza utanganyika wake, lakini kwa kuwa alikuwa anaamini kuwa kuna siku atakuwa raisi wa tanzania hilo alikumpa tabu sana.

Mwaka 1983 mwalimu alimteua Ndugu Edward Moringe Sokoine kuwa waziri mkuu wa tanzania na kutokana na utendaji kazi wake watu wote akiwepo mwalimu walimkubali kuwa anafaa kuwa raisi wa tanzania baada ya mwalimu. Hili lilimshitua sana Aboud Jumbe kiasi cha kuanza kugundua makosa aliyoyafanya, akaanzisha mkakati rasimi wa kurekebisha makosa hayo.

Wakati huo Sharif Seif alikuwa ni waziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar, na yeye kwa kujua kuwa akijipendekeza kwa mwalimu atachaguliwa kuwa raisi wa zanzibar akajenga uasama na Aboud Jumbe akawa ni informa wa mwalimu kwenye shuguli za kila siku za aboud jumbe.

Mkakati wa kwanza ulikuwa ni kuandaa hati ya mashitaka ya kuoji muungano kwa kushirikiana na mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar, hati ambayo haikuwahi kuwasilishwa kwenye mahakama ya katiba ya tanzania kwani Seif Shariff aliiba hati hiyo na kumpelekea mwalimu nyerere akitegemea Aboud Jumbe aondolewe na yeye apewe uraisi wa zanzibar.

Mambo hayakwenda kama alivyotarajia kwani NEC ya CCM ilimteua Mzee Ruksa kuwa raisi wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar na kumwacha Seiff shariff akiwa bado ni waziri kiongozi, kitu ambacho kilimuuma sana na akaamua kuanzisha mgogoro wa chini kwa chini wa serikali ambao haukudumu sana kwani yeye pamoja na kundi lake la The magificient seven walipigwa chini na serikali kwa uhaini na yeye akiwa amefanya kosa kama la Aboud Jumbe la kutaka madaraka kwa gharama yeyote hata kama kumuuza ndugu yako.

Je Seiff alijifunza nini kuhusu matukio haya? au bado anataka uraisi wa zanzibar kwa gharama yeyote hata kama kuwauza wazanzibar? Je kwanini CCM hawataki kuwapa nchi CUF hata kama wananshinda uchaguzi? Kwanini mtu akitaka kuoji muungano anaitwa mhaini ata kama anataka kujua ukweli kuusu muungano? Je kuna hati ya muungano iliyosainiwa na Mwalimu na karume au haipo? Kama hipo kwanini wasiidisplay somewhere watu wakaona na kujua siri iliyopo? Je Jumbe aliwahi kuiona au hakuwa kuiona?
 
jamco_za tunaomba ushahidi wa maelezo yako kwanza ya kuwa hivyo ndivyo ilivyotokea kisha ndio tumchambue seif sharif na makosa yake aliyoyafanya
 
jamco_za tunaomba ushahidi wa maelezo yako kwanza ya kuwa hivyo ndivyo ilivyotokea kisha ndio tumchambue seif sharif na makosa yake aliyoyafanya

Unahitaji ushahidi wa aina gani tena, Iwapo unajua au kusikia au kusimuliwa kuhusu historia ya Madaraka na uongozi baada ya muungano basi hakuna haya ya kudai ushahidi..

Zaidi haya yameelezwa kwa ufupi na mengi kuhusu haya yameuwa yakijadiliwa kwa kina Tangia Jambo hadi sasa Jamii forums.. Jaribu kufanya homework kwa kupitia mabandiko kadhaa yanayomtaja Maalim Seif hapa JF na ukijumlisha na bandiko hilo utafahamu...
 
jamco_za tunaomba ushahidi wa maelezo yako kwanza ya kuwa hivyo ndivyo ilivyotokea kisha ndio tumchambue seif sharif na makosa yake aliyoyafanya

Mkuu,

Hayo hapo ni muunganisho wa mabandiko mengi hapa JF, vilevile kama unaweza kutafuta chanzo cha Shariff kufukuzwa CCM utapata ukweli wa haya na mengine mengi ambayo sikuona kama kuna umuhimu wa kuyaweka hapa.

Swali la kujiuliza, viongozi wetu kwanini wanatawaliwa na tamaa kiasi cha kusaau masirahi ya taifa, leo anaweza kuiba siri za serikali na kuzipeleka sehemu provided kaahidiwa pesa, sio kwamba nanchukia Seiff, ila kwanini hasiachie mtu mwingine agombee uraisi wa zanzibar, au aliweka nadhiri kuwa lazima awe raisi wa zanzibar, na ndo maana alikuwa anautafuta kwa kutumia njia zote.
 
jamco_za seiff shariff inavyoonekana kuna kasoro anazo ambazo wenzake wanazifahamu na ndizo zinazopelekea kutoaminiwa kupewa madaraka ya juu kama yale.
 
Back
Top Bottom