Zanzibar yamtikisa Kikwete
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
KUPANDA kwa kasi kwa joto la kisiasa katika Kisiwa cha Pemba, kunaonekana kuwa ni dalili za mwanzo za kutikisika kwa Rais Jakaya Kikwete, na pengine kukwama kwa ‘ndoto' yake ya miaka miwili iliyopita ya kuweka historia ya kupatikana kwa ufumbuzi wa kile alichokiita Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar.
Matukio ya hivi karibuni, yamechochewa na uamuzi wa vikao viwili vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukataa mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya pamoja ya muafaka iliyokishirikisha chama hicho tawala na mahasimu wake wakubwa wa siasa za Zanzibar, Chama cha Wananchi (CUF).
Tukio la kwanza lililoonekana kumgusa moja kwa moja Rais Kikwete ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ni lile la wazee 12 wa kutoka Pemba, iliko ngome kuu ya kisiasa ya CUF, kuandamana hadi katika Ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) zaidi ya wiki moja iliyopita.
Jambo ambalo linaonyesha dhahiri kushtushwa kwa serikali, na pengine Rais Kikwete na hatua ya wazee hao, ni uamuzi wao wa kuwasilisha waraka maalum kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon ya kutaka Kisiwa cha Pemba kipatiwe fursa ya kuunda serikali yake itakayokuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika barua yao, wazee hao, ambao tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amewataja kuwa ni wanachama wa CUF, wanasema wamefikia uamuzi huo kutokana na kuendelea kutengwa na kusahaulika kihuduma kwa kisiwa chao.
Siku chache tu baada ya wazee hao kuwasilisha barua hiyo, maofisa usalama walivamia kisiwani Pemba na ‘kuwanyakua' baadhi ya watu waliokuwa katika msafara huo wa kupeleka barua UN na kuwahoji kwa siku kadhaa, kabla ya juzi kuwaachia huru kwa dhamana.
Tukio hilo la wazee wa Pemba kuandamana hadi UNDP, lilikuja siku moja tu baada ya wanachama kadhaa wa CUF kupitia katika utenzi walioimba wakati wa maandamano ya chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita, kusema kwamba walikuwa wamefikia hatua ya kuwa tayari kujitoa mhanga ili kushinikiza kufikiwa kwa muafaka wa kisiasa Zanzibar.
Maandamano hayo ya pili ya CUF kama ilivyokuwa kwa yale ya wazee 12, yanatajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni kielelezo cha wazi cha kuendelea kuwapo kwa hali ya hatari kisiasa katika visiwa vya Unguja na Pemba, tangu Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, ilipoyakataa mapendekezo ya kamati ya pamoja ya vyama hivyo viwili ya kutafuta muafaka wa kisiasa visiwani.
Aidha, katika hali inayoonyesha kutaharuki kwa serikali na pengine CCM, ni kauli zilizoanza kutolewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho, kila mmoja akizungumza lake.
Katika hatua moja, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba akiwa ameambatana na makada wengine wa chama hicho, hivi karibuni walilazimika kuitisha mkutano na wanahabari na kuirushia lawama CUF kwa kukwamisha mazungumzo hayo.
Katika mkutano huo na wanahabari, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale-Mwiru alimtupia lawama kada mwingine wa siku nyingi na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba kwa kutoa maoni kuhusu muafaka huo, ilhali yeye akiwa si mjumbe wa vikao vya juu vya chama hicho tawala.
Kauli ya Kingunge ambayo imepokewa kwa upinzani mkali, ilikuja baada ya Warioba kukaririwa akisikitishwa na uamuzi wa CCM kuamua kuitisha kura ya maoni ya Wazanzibari kujadili kuhusu kuundwa au kutoundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo.
Ingawa Kingunge alielekeza hoja kwa Warioba, ukweli ni kwamba pendekezo la kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ikivishirikisha CCM na CUF, kwa mara ya kwanza lilitolewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1995.
Mwalimu alitoa pendekezo hilo kutokana na waliokuwa wagombea wawili wa urais wa Zanzibar, Salmin Amour Juma (CCM) na Maalim Seif Sharif Hamad kuchuana kwa kura chache.
Katika uchaguzi huo, Salmin alishinda kwa asilimia 50.2 wakati Maalim Seif ambaye ameendelea kugombea urais wa Zanzibar hadi mwaka 2005 aliibuka na asilimia 49.8 ya kura zote zilizopigwa.
Ukiacha hayo, matukio ya karibuni yanayochochewa na msimamo wa CCM kukataa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, yametafsiriwa na CUF na baadhi ya wachambuzi wa mambo kuwa, ni kielelezo cha wazi cha CCM ‘kumuangusha' kisiasa Rais Kikwete, ambaye wakati akilihutubia Bunge mwishoni mwa mwaka 2005, alieleza bayana dhamira yake ya dhati ya kumaliza mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ambaye kimsingi yeye ndiye chaguo la urais wa Zanzibar kwa wanachama na wapenzi wa chama hicho, hivi karibuni alieleza bayana kushangazwa na hatua ya Kikwete kuyaacha mambo yaharibike kinyume kabisa na ahadi alizopata kuzitoa yeye mwenyewe siku zilizopita.
"Rais anapaswa ajue kuwa heshima ya ofisi yake na uadilifu wake binafsi ameutia doa kubwa kutokana na kushindwa kusimamia kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa kwa Watanzania kupitia hotuba yake ya Desemba 30, 2005 bungeni, na pia ahadi aliyoitoa na kuirejea mara kadhaa kwa marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika ziara zake za nje ya nchi kila mara pale alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa Zanzibar," alisema Maalim Seif, Aprili mosi mwaka huu katika tamko rasmi la chama chake kuhusu uamuzi wa CCM.
Ingawa Rais Kikwete anaonekana kukubaliana na uamuzi wa chama anachokiongoza, baadhi ya wachambuzi wa mambo wamekuwa wakimtaja Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuwa chanzo kikuu cha kukwama kwa jitihada ambazo awali zilianza kutoa dalili njema za mafanikio.
Tanzania Daima katika toleo lake la Machi 7, mwaka huu, siku chache tu kabla ya CCM kukutana Butiama na kuja na azimio lililoibua utata huu wa sasa, lilipata kuandika likimtaja Karume kuwa kikwazo cha kupatikana kwa suluhu ya kudumu visiwani.
Ikikariri taarifa za ndani kutoka Ikulu ya Zanzibar na vyanzo vingine kadhaa vya kuaminika, Tanzania Daima liliandika: "Karume ndiye kiongozi pekee kwa sasa anayesababisha ndoto za Rais Jakaya Kikwete za kuona hali ya utengamano ikipatikana visiwani." Siku chachte tu baada ya Tanzania Daima kuandika taarifa hizo, viongozi wa juu wa CCM walikanusha wakisema viongozi wote wa juu wa chama hicho, Rais Kikwete na Karume walikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa suluhu ya kudumu inapatikana visiwani.
Hata hivyo, siku chache tu baada ya kumalizika kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM na kuja na ‘Azimio la Butiama', kile kilichoandikwa na gazeti hili kilithibitika.
Taarifa za maandishi ambazo vyombo kadhaa vya habari vilizinasa kutoka ndani ya vikao hivyo, zilithibitisha kwamba, Karume ndiye aliyetoa pendekezo la kutaka uamuzi wa kutaka kuundwa kwa serikali shirikishi Zanzibar, itakayohusisha vyama vya CCM na CUf, ufikiwe baada ya kufanyika kwa kura ya maoni itakayohusisha wananchi wote wa visiwani.
Pendekezo hili la Karume ambalo liliridhiwa na CCM, ndilo ambalo leo hii limeirejesha Zanzibar katika hali ile ile tete ambayo mwaka 2001 ilimlazimisha Rais mstaafu Benjamin Mkapa akubali CCM itie saini muafaka wa pili na CUF.
Hata hivyo, kwa Mkapa, kama inavyotokea sasa kwa Kikwete, muafaka huo ulikwama hata baada ya yeye mwenyewe (Mkapa) siku ya kutiwa saini kwake, Oktoba 10, 2001 kusema alikuwa akikosa usingizi kutokana na tatizo hilo la Zanzibar.
Kukwama kwa muafaka wa tatu kunakuja wakati jumuiya ya kimataifa ikiwa na shauku kubwa ya kuona muafaka wa kisiasa visiwani unapatikana haraka.
Desemba mwaka jana, Balozi wa Marekani hapa nchini, Mark Green wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jumba la Patterson iliyofanyika visiwani humo, alisema wananchi wa taifa lake wana shauku kubwa ya kuona mchakato wa usuluhishi Zanzibar ukimalizika haraka na kwa amani.
"Watu wanaweza kusema kuwa 2010 bado iko mbali, lakini tuko karibu kuingia 2008 na kufumba na kufumbua, uchaguzi ujao utakuwa umewadia.
"Ni lazima tujikumbushe kuwa mazungumzo ya muafaka kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama cha Wananchi cha CUF yalianza Zanzibar takriban mwaka mmoja uliopita, yaani tarehe 17 Januari 2007," alikumbusha balozi huyo.
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 53 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Hakuna tatizo wala anayekwamisha.
Lipo tatizo moja,rais wetu kama wanvyosema watu ni dhaifu sana na visheni yake ni ndogo.
Huyu si mwanasiasa kiasili bali ni rubani wa ndege.
na mwasiti, iringa, - 18.05.08 @ 10:40 | #11634
ndugu mwandishi umesema vizuri hasa kuchambua hatua ,muelekeo wa suala hili la mpasuko.
Watanzania tuna jukumu la kulilia na kulinda MUUNGANO NCHI YETU .tusikubali chama au mtu ye yote kutuharibia jamhuri.Mhe.Rais Kikwete na Mhe.RAIS KARUME mnalo jukumu pekee hapa la kuonyesha njia ;njia sahihi na ya haki.
tamkeni msimamie njia.
na hao KUFA au CUF lazima waheshimu katiba na utawala bora ikiwemo matkeo ya uchaguzi,wafuate na kutumia taasisi zilizopo nchini kutoa hoja kama BARAZA,BUNGE,;na vikao vya vyama.wala cuf wasitishe watu na kukimbilia vyombo vya nje kama vile UNDP na UN.tunajua cuf wanafaidi mno Muungano ukifa hao cuf watajuta.watazama.
Mashirika ya nje kama UNDP wasichochee taabu nchini kwa kutumiwa kama kichochoro cha uchochezi wa wachache.UNDP IKOME kuchukua mani na kuwasiliana na watu kwenye mambo ambayo ni ya kupitishiwa Wizara ya mambo ya nje.UNDP watuombe radhi watanzania kwa hili la cuf.
na nani, mikoani, - 18.05.08 @ 09:28 | #11644
Jamani tusilaumiane kwa hili la Unguja na Pemba.Tuje kwenye asili ya visiwa hivi.Tujaribu kuwafundisha hitoria wananchi na wanafunzi, ili waelewe nini maana ya mapinduzi.Nini maana ya Afroshirazi paty na ZPP.Hivinivyama ambavyo vilikuwepo toka awali.AFROSHIRAZI Ndiyo CCM.ZPP Ndiyo CUF.Nafikiri hili litaeleweka hata kama litakuwa na dosari.Kinachotakiwa hapa ni serekali ya mseto au mtu anataka cheo.Tuwe wwawazi.Tusipandikize chuki kwa wananchi kwa kutaka vyeo.Kusikika na umaarufu kimataifa. Jamani tuwe wakweli.CUF kama ni chama cha wananchi kwanini kisichague kiongozi mwingine? Kwani nilazima awe maalim Seif.Mimi siko katika chama chochote, kiwe cha hawa mafisadi .Ila nasema kwa mtazamo wangu.Tuangalie ya huyu kiongozi. Kwanini linapotokea jambo lolote la CCM Kujichanganya ,basi trip lazima ifanyike yakwenda kulizungumzia nchi nyingine?why.Inamaana hawa wazee wenyechama cha CUF hawana maamuzi?maamuzi lazimayatoke kwa wanaokifadhili?hili linanitia mashaka kuwa kinaongozwa nje ya nchi na sio ndani ya nchi ya tz.Na CUFhuku bara ni kiinimachotu na nikwasababu wanasema kuwa chama chochote lazima kiwe kinatambulika bara na pwani au visiwani,Ndiyo maana akachaguliwa Pro,Lipumba ,ambae yupo kama kivuli cha maalim Seif kudhihirisha u CuF wake.lakini lengo lake ni kutaka kutawala kisiwa kijitenge, kiwe na serekali yake.Wakati hilo halita wezekana.Kuwagawa wananchi kwa kiitikadi kutaleta maafa tena kama nyuma ilivyokuwa.Ninawaomba viongozi na wazee wa kipemba na kiunguja mjaribu kulisuluhisha hili lisiwe kisiaa zaidi liwe kwa ajiliya maslahi yawananchi,kuwaokoa na adha ya kiitikadi.hawa nimafisadi kama ya chama tawala yanatumiamlango wa nyuma.Hawa walikuwepo madarakani.Wananchi msikubali kugawanywa kwa sababu ya itikadi ya mtu.Mnyazi Mungu tuepushie ya Somaloa na Burrundi ndani ya nchiyetu AMINA
na mtzmwenyeuchungu, tz, - 18.05.08 @ 09:47 | #11650
HUYU JAMAA WA JUU CHIZİ KİDOGO YEYE ANAJUA WAZİ KWAMBA CCM HUWA HAWASHIDİ ZNZ NA UCHAGUZI UPO KARIBU 2010 SİMBALİ HIVYO UNATAKA WATU WAENDELEE KUFA.NAKUPA KUPA HONGERA NDUGU MWANDİSHİ KWA UPEO WAKO MPANA
na mimi, ughaibuni, - 18.05.08 @ 09:49 | #11651
Binafsi sioni umuhimu wa kura ya maoni Zanzibar kwani kiujumla matokeo ya chaguzi zote 3 zilizopita zinaonesha haja ya kuwa na Serikali ya Mseto. Kura ya maoni ni kupoteza gharama na inaweza kuzua mtafaruku mwengine wa watu kulalamika kuibiwa Kura. Ingawa hatujui matokeo yake lakini watu watafuata maelekezo ya vyama vyao na "gap" itazidi kuongezeka. Tatizo kubwa bado ni viongozi wetu kutokubali kukubaliana. nakumbuka mara baada ya kutiwa saini Muafaka wa pili wanachama wa vyama hivi viwili waliandamana pamoja wakiwa na picha ya viongozi wa vyama vyote viwili hali ilikuwa ya kutia moyo sana kiasi ambacho mapenzi baina ya wazanzibari yalipatikana bila kujali wanatoka wapi hili lilifanyika bila ya kura za maoni naamini Seif na Karume wakiwa na nia ya dhati mnaweza kuandika historia ambayo vizazi vijavyo vitakukumbukeni naamini mnaweza. Dunia imebadilika hatuwezi tukaegemea sababu za kihistoria kwa kuhofia kufanya mabadiliko ya manufaa. Sisi vijana tunahitaji kuhamasishwa maendeleo na sio kukumbushwa nani ni nani. Muda bado upo na mnaweza kuonesha njia nasi tuko nyuma yenu.
na Mzanzibara, Zanzibar, Tz, - 18.05.08 @ 10:00 | #11653
Mtz mwenye uchungu sikubaliani na maoni yako ya kufananisha CUF na ZNP na CCM na ASP. Sioni kiunganishi chochote hapo. ASP na ZNP ni vyama vilivyopita na wakati wake umepita. CCM na ASP ni vyama vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria zilizopo sasa ambazo ni tofauti na sheria zilizokuwepo huko nyuma. Pili kama chama bado kinamuona Seif anastahili kugombea hiyo ni hiyari yao wala hawaingiliwi. Kuwa na nguvu CUF Zanzibar ukumbuke kuwa Zanzibar ni ndogo na Elimu ya Uraia inaweza kumfikia kila mmoja kwa urahisi tofauti na bara. Bado Upinzani popote pale uwapo unahitajika ili kuwa na changamoto kwa Serikali hivyo ni vyema ukaimarishwa zaidi na Bara. Sote tunayaona matunda ya Wabunge wachache wa upinzani ambao wamekuwa chachu ya mageuzi ndani ya Bunge. Hivyo kuhusisha hali ya sasa na Historia haitusaidii sasa tuna Tanzania wakati ule tulikuwa na Tanganyika na Zanzibar. Lete hoja za kujenga na ambazo zinasaidia kizazi hiki na kijacho
na Mzanzibara, Zanzibar, Tz, - 18.05.08 @ 10:16 | #11654
MIMI NABAKI KATIKA BUMBUAZI!! NAONA MWAKA 2010 SI MBALI. CUF HAWANA SUBIRA YA MWAKA 2010
EBU WATOA MAONI NA HASA WANAOSISITIZA MUAFAKA UFANYIKE WAKATI HUU KAMA WANA CUF, NAOMBA MTOE MAELEZO YA MSINGI KWA NINI WASISUBIRI 2010?
KWA UPANDE WANGU NAONA WASUBIRI 2010:
-CCM INA ILANI NA SERA ZAKE ZA MIAKA 5.
-KAMA NI KUGAWANA MADARAKA LAZIMA KUWEPO MABADILIKO KIKATIBA.
KWA NINI WANA CUF HAWANA SUBIRA??
WAPALESTINA WANA SUBIRA, MANDELA KUWA RAIS WA AFRICA KUSINI ALIKUWA NA SUBIRA, MUGABE NA KAUNDA WALIFUNGWA HIVYO NA KUONESHA SUBIRA.
SASA WANA CUF PEMBA WANAKOSA KUWA NA SUBIRA. SISI WATANZANIA KUPATA MAFANIKIO KISIASA, NA KIUCHUMI HATUPENDI KUSUBIRI. TUNAPENDA KURUKA HATUA. KWA HIYO SI RAHISI KUSONGA MBELE KWANI TUTAKOSA MSINGI MZURI.
INASIKITISHA SANA KUONA VISIWA VYA ZANZIBAR VYENYE WATU WACHACHE WANASHINDWA KUAFIKIANA SABABU YA KUCHOHEWA NA WATU WACHACHE.
na Madaha - 18.05.08 @ 10:18 | #11655
PEMBA KUJITENGA NA KUINGIA KATIKA SHIRIKISHO NI SAHIHI KABISA.MATATIZO YOTE YATAISHA NA TUTAKAA KWA AMANI.TUNAOGOPA NINI? AU PEMBA KUNA KITU GANI TUNAKING'ANG'ANIA ? INAONEKANA PEMBA KUNA JAMBO,NA JAMBO HILO LIPO CHINI YA ARDHI. KAZENI UZI WAPEMBA,NAJUA MUMESOMA,NIMEKUWA NANYI CHUO KIKUU DAR UHANDISI BAADHI YENU MIAKA YA 80.NA MKO WENGI NA TUNAJUA UWEZO WENU. MSICHOKE,NYINYI NI MATAJAIRI NA MUNGU AKIPENDA BAADA YA MIAKA 20 WABARA ,WAUNGUJA NA HATA WENGINE AFRIKA MASHARIKI NA YA KATI WATAKUJA KUHEMEA PEMBA.
na ibraka, dar, - 18.05.08 @ 10:24 | #11656
mambo ya zanzibar yataamuliwa na wazanzibar wenyewe si ****** wa njena vibaraka wa kiarabu na mabasha zao, na wewe mwandishi pia unafanya upotoshaji hujui chochote kuhusu zanzibar na una mapenzi makubwa na hicho chama chako cha cuf na kila wanachoeleza wao mnakikubali kwa urahisi hii inakuwaje lakini au na nyie mnajirahisisha mpate kupandwa
na ali, zanzibar, - 18.05.08 @ 10:41 | #11659
Nduguyangu Madaha suala si kuwa na subra hadi 2010 kama ni subra imeshafanywa sana tokea 1995. Suala hapa ni kigeugeu cha CCM na kuibua mambo mapya kama Kura ya Maoni. Ni bora wawe wa wazi waseme tunakubali Serikali ya Mseto lakini hadi 2010 bila ya kura ya maoni hapo kidogo wataeleweka. Utawaamini vipi iwapo watang'ang'ania kura ya maoni na matokeo yakawa mfano 50.2% hawataki mseto halafu ukasema wananchi wameamua ina maana 2010 kutakuwa hakuna huo mseto tatizo linabaki pale pale! Tulipokuwa tunazungumzia kuwepo kwa vyama vingi wakati wa Mzee Rukhsa kura za maoni zilionesha ni 20% tu ndo wanaotaka vyama vingi lakini Serikali ikaona busara kwamba hiyo hiyo asilimia ndogo wapewe Rukhsa ya kuanzisha vyama vingi kwa hiyo kimsingi ndugu yangu busara inahitajika zaidi na iwepo nia ya dhati basi tatizo hilo linaweza kumalizwa kwa urahisi wote hao ni wazalendo wanaoipenda nchi yao na wanaweza kushirikiana kuijenga
na Mzanzibara, Zanzibar, Tz, - 18.05.08 @ 10:46 | #11660
Ndugu yangu Ali kuwa mstaarabu kidogo na wacha kutumia ****** hayasidii. Tumia hoja kuonesha udhaifu wa mwandishi na sio ******. Dunia ya leo hakuna matatizo ya kisiasa ambayo utayawekea mipaka kwamba wengine hawahusiki hususan kama yaliwahi kumwaga damu huko nyuma kama wewe hujali maisha ya raia wengine wanawake na watoto basi dunia inajali kasumba za uarabu hazisaidii hapa kwani kina Machano, Juma Duni, Jussa na wengineo ni Wazanzibar na waUnguja halisi
na Mzanzibara, Zanzibar, Tz, - 18.05.08 @ 10:57 | #11664
WAZANZIBAR KAZENI KAMBA, CCM HAIWEZI KUKUPENI HAKI ZETU MEZANI. MAKAMBA NA KIKWETE NI WASANII. NI JAMBO LA AJABU TAIFA HILI LIMEWAPA UOGOZI HAO WATU WASIONA VISION. NIAMBIENI MAKAMBA HANA SHULE ATAPATA WAPI VISION
MAALIM SEIF , USITETEREKE KUNA SIKU DUNIA ITAKUSIKIA
na ANDREW, unguja, - 18.05.08 @ 11:21 | #11667
Bwana Madaha huelewi nini kuhusu Muafaka, Muafaka haujaanza Jana au juzi, Huu ni Muafaka wa tatu na inaonekana tutakuawa na miafaka mingi ijayo. Shaka hapa ni dhamira ya kweli ya kutatua mgogoro huu, ambayo kwa namna yoyote ile CCM na hasa Mh. Raisi Kikwete ndio wenye jukumu kwa kiasi kikubwa kutatua mgogoro huu. unaposema kuwa mwaka 2010 haupo mbali hivyo CUF wasuburi uchaguzi ujao nafikiri hujajua kuwa ni chaguzi ndizo zinazolalamikiwa na mambo yanayoongelewa sana katika miafaka yote hii ni kuweka mazingira yasiyoleta shaka katika chaguzi, hivyo kwenda kwenye uchaguzi wowote bila ya kurekebisha mambo haya haitawezekana kuwashawishi Cuf kuwa uchaguzi ujao utakuwa huru na haki tupu na hivyo wao CUF wakishinda watepewa Mamlaka. na hili Nd. Madaha halipo Zanzibar tu hata huku Bara, ila Zanzibar sote tunajua kuwa Nguvu ya CCM na CUF zinakaribiana sana, na pia tunajua kuwa sio Zanzibar tu bali Bara (Tanganyika) na hata sehemu kubwa ya Africa walio madarakani wanafanya hila nyingi ili kukaa madarakani(mifano ipo mingi),hivyo tukikaa na kusubiri chaguzi bila ya kufanya jitihada yoyote tukiamini kuwa chaguzi zetu zitakuwa huru na haki tunajidanganya! uzoefu unaonyesha hivyo Zanzibar, Bara na hata Afrika pia. Kwa maoni yangu msimamo wa CUF ni katika harakati za kufanya chaguzi zetu zijazo ziwe bora zaidi kuliko ilivyo leo! na kumbuka hata hao Wapalestina, Mandela na dhulma yoyote ile haijawahi kuvumiliwa kwa kusubiri eti Madhalimu watatoa haki wakipenda, tumeona harakati za ANC,PAC hata sisi(Tanzania) tulivyokuwa nyuma yao kukataa dhulma waliokuwa wakifanyiwa na Makaburu, natunaona pia harakati mbalimbali zinazoendelea huko Gaza na Ramallah. ni vipi Nd. Madaha useme kuwa tusubiri na kutumbua macho tu kusubiri hatma?
na A.S. Mbweni, DSM, - 18.05.08 @ 11:30 | #11669
mimi nakwambieni huyu karume ndio sababu zote za matatizo ya sasahivi zanzibar nyinyi hata hamumuoni kupewa uraisi tu kamuondoa waziri wa fedha nakujieka yeye mwenyewe na wakati huo huo ni raisi na huyu ndio aliye sababisha yale mauwaji ya watu 20 kule pemba nakusababisha wanawake na watoto wadogo kurepiwa,watu kuvunjiwa majumba yao,wengine kukimbia, lakini tujiulize kwa nini huyu anaogopa mseto? anasema waarabu watarudi kwani wakirudi itakuwa nini hao waarabu familia zao wameishi miaka mingi kuliko hiyo familia yake huyo babaake anayekula marungu ya moto hivivisa alikuja zanzibar kama baharia mwaka 1958 na waraabu walikuja zanzibar zaid ya miaka mia mbili(200)toka 1788 na kama hawa waarabu ni watu wabaya kwani yeye kaowa muarabu na sio mmalawi inakotoka uko wake, hebu karume tueleze huyu m'ke wako unaye mmwagiya kinyesi yako ni nani? ku..ma..mako wewe masharubu kama kambare..ole wako mara hii ikifika wakati wa uchaguzi uchukuwe familia yako urudi kwenu malawi au tutaenda kumuwasha kibiriti ma..ma..ako bifatuma karume anyeishi pale maisara tumeshakuonya!
na sule, znz, - 18.05.08 @ 11:50 | #11672
hili gazeti ni la chama gani?inaonekana ni kama haliko neutral bali linamuelekeo wa upande mmoja. waandishi wetu ni budi wazingatie maadili ya uandishi kuliko jazba.
na ustadh, usa, - 18.05.08 @ 12:27 | #11675
Naona sule huelewi historia ya ZNZ. Ikiwa Karume alikwenda ZNZ mwaka 1958, mbona alianzisha ASP na kushinda uchaguzi 1957? Naona waarabu ni mabasha wako na umezoea kuf...a. Bora uwafuate huko waloko arabuni.
na Sully., Zenj, - 18.05.08 @ 12:35 | #11676
Sule nenda shule. Karume kweli aliwahi kuwa baharia lakini hakwenda ZNZ 1958. Hilo naona ulilimeza wakati unatiwa na ***** wako wa kiarabu.
na Chonjo. - 18.05.08 @ 12:41 | #11678
Naona sule huelewi historia ya ZNZ. Ikiwa Karume alikwenda ZNZ mwaka 1958, mbona alianzisha ASP na kushinda uchaguzi 1957? Naona waarabu ni mabasha zako na umezoea kuf...a. Bora uwafuate huko waliko arabuni.
na Sully., Zenj, - 18.05.08 @ 12:46 | #11679
Huyu MADAHA ni IDIOT MKUBWA inaelekewa upeo wake wa habari za nyumbani na kimataifa ni finyu.Suala la Zanzibar ni time bomb
na alyoundi, uk, - 18.05.08 @ 13:11 | #11681
AMA KAMA NINGALIKUWA NAKUJUWA WEWE MSEMA KWELI, UNAJUWA KWA UPANA NA MAREFU JUU YA MAMBO YALIVYOTOKEA HAPA KWETU.KWANINI HUKAI JUU YA KIPAZA SAUTI UKAWAFUNDISHA HAWA WENGINE WALIOKUWA HAWAFAHAMU YALIVYOKUWA.LAKINI KAMA UNAVYOWAANDIKIA MUNGU ATAWAJAALIA WATAONA NA KUJUA WAKO UMBALI GANI NA NCHI YAO.NAMIMI NAKUSAIDIA MJA TU KUWA MARA HII UCHAGUZI ZANZIBAR[PEMBA ]CHAMA CHA MAPINDUZI[CCM]KITACHUKUWA VITI KARIBU YA NUSU YA VITI VYA PEMBA. TUOMBE UHAI TU.ILI KUONEKANE KUWA NA PEMBA CUF WANAKATA TAMAA NA CHAMA CHAO.
na KINYANG'UNYA, ZENJI, - 18.05.08 @ 13:32 | #11683
WENGI WA WATOA MAONI KUTOKA ZANZIBAR TUPE MAELEZO YA KUTOSHA. SIO TU KUANDIKA HISTORIA YA ZANZIBAR HATUIJUI. MFANO ALYOUNDI HUJASEMA LOLOTE MBALI YA KUMPINGA MADAHA SABABU HUENDANI NA MAPENDEKEZO YAKE. PALE JUU SULLY ELEZA UHUSIANO WA HISTORIA YA ZANZIBAR NA VUGUVUGU LA SIASA WAKATI HUU. SIO KUSEMA HISTORIA YA ZANZIBAR HUMUIELEWI.
na Sammy - 18.05.08 @ 13:40 | #11685
kinachotokea zanzibar ni matokeo ya dharau na kutoheshimiana. aidha ni matokeo ya kutoheshimu taratibu zilizopo na uroho wa madaraka tu.
uchaguzi ulifanyika na wote tunajua kuwa anayeshida ndiye huchukuwa vyote.
sawa watu wanasema ccm waliiba kura wangekuwa wezi vipi waache za pemba!
ushajua wezi sijui vibaka wakiingia kwako waiba hata mboga au siyo.
wote twajua idadi ya waugunja wengi kuliko wapemba sasa kama mtaji wa kura ni wapemba tujuane sasa waunguja wafanzeje? cuf kama wanataka kutawala zanzibar basi waukane upemba kama mtaji wao wa siasa vinginevyo badala ya kushinda kwenye internet na kusambaza ugongo na propoganda waende vyumbani wazaane sana ili idadi yao iongezeke vinginevyo sioni njia.
hivi wao na uchache wao wanapiga kelele hivi fikiria ikiwa kinyume chake.
nasikia pamoja n kupinga ubaguzi wanao mzunguka seif wote yaani walinzi mpaka dreva wote ni wapemba. vipi akiingia ikulu?
na bituro kazeri, mwanza, - 18.05.08 @ 14:14 | #11687
Mzanzibara, kama upinzani wa nguvu unahitajika ili serikali iliomo madarakani iweze kuongoza kulingana na sheria za nchi, sasa hii serikali ya mseto yanini? Nijuavyo mimi serikali ya mseto katka demokrasia ya vyama vingi huundwa pale hakuna chama kilichopata nusu ya kura/viti vya bunge.
Sasa bahati mbaya,labda, Tanzania tumeamua kuunganisha muundo wa uchaguzi wa kimarekani na wa Ulaya. Wamarekani huendesha uchaguzi wa mabunge yao na wa rais tofauti kiasi hutokea chama kitoacho rais kisiwe na viti vingi kwenye mabunge yake mawili(House of representatves na Senate). Katika hali hii rais hutumia veto kupinga maamuzi yanayokinzana na mayakwa ya serikali yake. Watu wa Ulaya wao serikali huundwa kutokana na wingi wa viti katika bunge. Kiongozi wa chama chenye viti vingi huunada serikali ya chama chake tu ikiwa kina zaidi ya nusu ama huunda serikali ya mseto na vyama rafiki ili waweze kupata viti zaidi ya nusu vya wabunge.
Kuchanganya kwetu miundo hii miwili ndio chanzo cha wizi wa kura na vurugu kwenye uchaguzi. Ugumu wa CCM kukubali mseto wao wanaona ni kukubali kuwa walipata kura pungufu ya nusu.
Kama serikali kuundwa itakayojumuisha CU na CCM basi itakuwa ni kwa nia ya kuleta umoja wa kitaifa kuliko mseto. Pengine waondoe hili neno mseto labda wahafidhina wa pande zote mbili watakubaliana.
Ndg Mzanzibara tatizo la mpasuko sasa si wa kisisa tena bali wa kisaikolojia.
Nikikubali ntaonekana dhaifu, na akikubali ntakuwa kidume. Pengine kwa jinsi hali ilivyotete Zanzibar demokrasia ya vyama vingisi wazo jema.
na Mtimkubwa, Tz, - 18.05.08 @ 14:18 | #11688
ndugu mtimkubwa uliyonena ni kweli.
hivi watanzania wote hatujui kweli kwamba mbegu za mtama haziwezi kuota mahindi?!. mseto maana yake uchaguzi utupiliwe mbali. kila mtu apate nafasi ya kutawala. kutesa kwa zamu. sasa hii sijui iko wapi duniani hapa? tutakuwatunagundua kitu kipya kabisa . tunaweza tukitaka lakini kwa mfumo uliopo lazima watu wakubali matokeo ya uchaguzi. TUJIFUNZE KUSHINDWA.
na bituro kazeri, mwanza, - 18.05.08 @ 14:35 | #11692
KUNA HAJA YA WAPEMBA KUPELEKA BARUA YA KUJIUNGA KATIKA (ARAB LEAGUE).KWAVILE TANZANIA INAMINI KUWA WAPEMBA NIWARABU NA HAWANA HAKI.
na karim ali, kikwajuni znz, - 18.05.08 @ 14:55 | #11694
kwanza nyinyi munaotoa maoni **** mamazenu na huyo karume ****lamaake na la mkewe na huyo seif **** la mamayake na hao vichogo kina kiwete na kikwapa ****mazenu siasa hamuijui kazi wizi tupale znz lengo kubwa ni kuondoa uislamu tu
na ****, leicester uk, - 18.05.08 @ 15:06 | #11696
Nduguyangu Mtimkubwa ita vyovyote upendavyo mseto au ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa bado zote zina maana moja. Kumbuka Mazungumzo haya yamechukua takriban miezi 14 na moja ya mambo waliyokubaliana ni huo mseto na hata C.C.M wanazungumzia haja hiyo baada ya uchaguzi wa 2010 suala hapa ukisikiliza vyama vyote ni muda gani vianze huo mseto na labda agenda mpya iliozuka ni hiyo kura ya maoni kama pendekezo jipya naomba tusijadili Mseto kwa kuwa hayo ni mambo ambayo vyama wamekubaliana kimsingi una faida hauna hilo ni suala jengine. Sikubaliani na Ndugu yangu ambaye anasema Seif amezungungukwa na wapemba tu ninavyofahamu mimi kina Jussa, Juma Duni, Machano pamoja na Katibu wa Seif na wengineo ni watu wa Unguja halisi nahisi hiyo ni propaganda zaidi kuliko ukweli halisi ulivyo. Si vyema kuitumia propaganda hii ikageuka kama kingunge alivyolishwa maneno ya Uhizbu akakuta majibu yanawarudia viongozi waandamizi wa C.C.M. Wazanzibar ni watu wanaoweza kuishi pamoja na kushirikiana alimradi wakijengewa mazingira ya kufanya hivyo na sio fitna na Ubaguzi wa huyu anatoka wapi na yule wapi. Kuijenga nchi inahitaji mashirikiano ya pande zote naamini inawezekana watu wenye hekima kama Warioba wamelisemea hili na hata baba wa taifa hilo alizungumzia. rais kikwete anapojaribu kuunda serikali (Baraza la Mawaziri) hutizama uwiano wa kimikoa anaweza kufanya vyenginevyo lakini kuonesha kwamba kila mmoja anawakilishwa basi hufanya hivyo kwanini busara hizi zisitumike zanzibar pia?
na Mzanzibara, Zanzibar, Tz, - 18.05.08 @ 15:16 | #11698
MIMI NIMECHANGAZWA NA PINDA HUHUZURIA MKUTANA WA KIUCHUMU MISRI(ARAB CUNTRY).? KWANINI HENDI PEMBA?
na karim ali, kikwajuni znz, - 18.05.08 @ 15:24 | #11700
HAKIKA UKISOMA MAONI YA HUMU UTAJUA KWELI UKO MAMBO SIO SAFI HUMU SI MAHALA PA KUTOA DUKUDUKU LAKO KWA NJIA YA ****** WATANZANIA TOENI MAONI KWA NJIA MOJA AU NYENGINE ZITAWEZA KUSAIDIA KUFIKISHA UJUMBE SI ZANI ****** YATASAIDIA KITU AU NJIA PEKEE YA SIASA
na FELA KUTI, TANGANYIKA, - 18.05.08 @ 15:33 | #11701
Ali, zanzibar nibora ukaanze shule ujifunze lugha ya kutumia katika matandao lugha hiyo unaweza kutumia ukiwa na ***** wako ki/yu.
na Samwel, Beijing, - 18.05.08 @ 15:37 | #11703
Tehe tehe, heeeeeheeeeee!
Loh... Maoni mengine bwanaaa!!!!
na Ndalichako, Dar/TZ, - 18.05.08 @ 15:52 | #11707
ustadh USA unakula nguruwe ondoka tu uko ubongo wako una crack, una mataizo ,soma namagesti mengine, huilo la CCM linaweza kufanya hivi mpaka mshamba kama wewe aweze kuto maoni ya ma'vi kama yako
na ERT, USA, - 18.05.08 @ 16:52 | #11712
Hawa CUF ni chama hatari sana na Watanzania tusiwe wajinga kuilaani CCM kila watendacho. msimamo wa CCM ni kwa Usalama wa Taifa na sio kuonea CUF. Wachunguze sana hawa viongozi wa CUF wanavyo vaa na kufuga ndevu zao. Hawana tofauti na HAMAS(palestina),FIS(ALgeria), HIZBOLLAH(Lebanon) au MUSLIM BROTHRHOOD(misri) ambao karibia vyama vyote hivyo ni vya kidini na msimamo mkali na mbaya zaidi ni VIBARAKA WA IRAN. Kuweka serikali ya mseto visiwani ni sawa na kuunganisha vibaraka wa IRAN na CCM. IRAN ni Nchi hatari sana hapa duniani na imeikosakosa kuninunua Jamhuri nzima ya muungano kwa ncha ya sindano tuu. kuwapa madaraka CUF ndani ya serikali tulivu ya CCM ni hatari kwa nchi nzima maana sasa IRAN itaanza kuwa na sauti ndani ya jamhuri kama ilivyotaka mwanzoni. Yatafumuka madai makubwa sana ya kutikisa nchi kama ilivyokuwa NIGERIA kwa majimbo ya kaskazini ambako wameweka sheria kali sana za kumzuia mkristo kuishi huko. Tutajikuta mapumziko ya kazi yanananza alhamisi mpaka jumapili bila kupenda. maana hawa CUF wapo mpaka BARA. Lazima mtu uangalie sana msimamo mkali wa kidini wa CUF ulivyowekwa kisirisiri kuliko kupayuka hovyo kuwa CCM ni wabaya. kaeni chonjo saa mbaya !lazima tufanye lolote liwezekanayo CUF wasipate madaraka katika jamhuri ya muungano Tanzania. wapo wachache na wakijifanya kuiga waarabu wadaivyo haki bila sheria ya kibinadamu basi nao watakiona . hakuna taifa la midle east kujinyakulia kisiwa cha pemba wala unguja! CCM hongera
na Dzikambani Mawomba, Zimbabwe, Bulawayo, - 18.05.08 @ 17:43 | #11726
kweli hata mimi najiuliza mbona hawa CUF wanamadevu ya kidini hivyo! hujifanya wanadai ulaya na marekani kumbe huko hukutana na majasusi wa irani ili kuwapa hoja za kuiiletea fujo bongo yetu. kuna kitu kiitwacho wahaabis ambao kimejaa ndani ya CUF. naipenda CCM kwa hilo la kuona mbali na sio kingine. wakileta serikali ya mseto tuu baasi CCM yote itatekwa maana mabilioni ya mapesa za IRANi yatajazana kwa kila kiongozi wa CCM ili akubali hoja na kuingia CUF. IRAN isipewe mwanya kuichukua kisiwa kizuri cha pemba na unguja. mara kwa mara serikali za msimamo mkali wa dini mwanamke husota sana anfanywa kama baby factory tuu, CCM tatua kwa busara ya moto. maana moto unaweza kufanya mtumwa wakati mwingi ila siku ukiamua kukutoa duniani huwezi kukataa ingawa una pesa za hongo!
na montenzuma binti salim , bweju na baje,unguja, - 18.05.08 @ 17:54 | #11727
Kwa Wanzazibari...nyinyi ni watu wa dini moja ambao mnatakiwa kupendana na sio kuchukiana...ni jambo la kushangaza kuona mnavyochukiana katika ngazi za juu kabisa. Inapaswa mjue kwamba kuwa na serikali yenu ya Zanzibar haitokuwa suluhishi la matatizo yenu. Jambo la muhimu ni kumaliza tofauti zenu na mrudi kwa Mola wenu aliyewaumba toka kwa Adam na Hawa. Hakuna atakae watetea masilahi yenu bali ni nyinyi wenyewe...acheni dharau na chuki, ubaguzi na dhulma ya nafsi zenu. Kaeni mkijuwa kwamba M'nyezi Mungu haibadilishi jamii mpaka ibadilishe yale yaliomo kwenye nafsi zao...pia mkae mkijuwa kuwa M'Mungu hanashida na utii wenu na ibada zenu iwapo mtachagua kumuasi na kuendeleza dhulma katika ardhi...acheni upemba na uunguja, umagharibi na umkoani...nyinyi ni watu wamoja, damu moja, asili moja na cha muhimu zaidi Dini moja...rudini ma kwenu mukaijenge nchi yenu...acheni kuhamahama dunia nzima...hamisheni utajiriwenu kwenu...acheni kulalamika...jengeni mashule yenu na vyuo vyenu...simamieni masilahi yenu...acheni kuwatutaka watu wa bara kwa matatizo yenu...kumbukeni kuwa wengi wenu mnamakazi, biashara, wake na watoto, mmemiliki ardhi tanzania bara kwa maelfu ya hekari bila kubughudhiwa...pendaneni kama maamrisho ya dini yenu yanavyowataka amasivyo adhabu ya Mola itawasibu hapa duniani na kesho akhera.
na jumaa, Duniani, - 18.05.08 @ 18:18 | #11732
HUKO NYUMA, WATU WA MIKOA YA KUSINI WALIWAHI KUTAMKA, TENA NA MBUNGE WAO NANDONDE KAMA SIKOSEI, KUWA HERI KUSINI ISIWE SEMU YA TANZANIA KWA KUWA ILITENGWA KWA KUTOJENGEWA BARABARA MIAKA MINGI. HAKUNA MTU YEYOTE ALIYESHITAKIWA KWA UHAINI. NINYI WATANZANIA MNAWAONEA WAPEMBA. NA HIYO SI HAKI. KAMA MNA ISSUE YA MSINGI MSEME LAKINI SIO KUWATENGA WENZENU; HILO NI JAMBO BAYA. LITAWARUDIA TU SIKU MOJA. MNGEFANYIWA NINYI WAUNGUJA JE? AU MNGEFANYIWA NINYI WAZARAMO NA WASAMBAA MNGESEMAJE????
na JICKY, UK, - 18.05.08 @ 18:28 | #11733
ndugu mawomba,
habari za huko zimbabwe/ ni bora ukatupasha nini za huko kuliko kutuelezea za unguja kwani naffikiria huzielewi.vipi jirani yako mugabe bado homa imeshamtulia?na yule kijana tsavangari nae yu hai nasikia wanataka kumtoa roho sababu amemuadhirisha mzee wa jongweeeeeee kokoriko.
ya unguja ni ya wenyewe na hao waislam uliowataja usiwaingize katika haya au nawe ndio unaingiza dini katika kueneza chuki
na ustadh, usa, - 18.05.08 @ 18:45 | #11737
Ukiangalia hapa basi utaona wengi wanaotoa maoni yao ni ya chuki tu . sasa angalia hawa hawa ukiwakuta huko mitaani kweli kutakua na salama .ujinga mtupu badala ya kutafa njia ya kutafuta maendeleo sisi ndio kwanza tuko kwenye siasa za chuki .Eee wabentu wenzangu mpaka lini mutaendelea na siasa za chuki . badala ya kutafuta njia ya kuendeleza nchi yetu ili tupa elimu matibabu na kupunguza umaskini. tutaendelea kufa maskini kwa mambo haya .
na EDDY, FRANCE, - 18.05.08 @ 19:29 | #11740
hawa wa Zanzibarndio choo, na sio wa Pemba. sababu hawa hawa ndio wanalalamika kuwa Tanzania Bara inawaonea na wakati haiwaonei, wakati huo huo kwa ukweli wa mambo wao ndio wanawaonea wapemba. Mie naona Wapemba wapate uhuru wao. Tanzania bara bora iisaidie hao jamaa wapate uhuru wao mapema sana. Kuna maana gani kuteseka wakati hakuna sababu? Na msiwatishie kuwa watapata shida,shida wameshapata ni neema tu inawasubiri baada ya kujitenga. PEMBA OYEE. JE UHURU NI 2010?
na COMORO, BAKARI, - 18.05.08 @ 19:35 | #11741
Ukitoka tanzania au kenya au nchi yoyote ya Africa ukenda majuu basi hakuna kuchagua mkenya au mtanzania au nani MANDINGO zote zinztiwa pakacha moja.hapa watu wanabaguana . Hii inaonyesha wazi kuwa bantuz akili finyu. kwasababu yakitokea matatizo basi ni kwa watu wote. huko pemba kuna ccm na cuf na wote wapemba sasa wapemba wakifukuzwa zanzibar watachaguliwa vipi. au watafukuzwa wapemba cuf tu .na wale cuf wazanzibarwatapelekwa wapi
na EDDY , FRANCE, - 18.05.08 @ 19:44 | #11743
EDDY USIWE MJINGA KAMA WAO!!
UJINGA WA KUTOJUA JIOGRAFIA USIUHALALISHE.
TAMBUA KWAMBA WAO WANAPENDA KUPAMBANUA KILA KITU KIWE PEKE YAKE. HAWAJITAMBULISHI KWA UJUMLA KAMA SISI AFRIKA. KWA KUTUCHANGANYA NI KUTOJUA BARA LA AFRICA LINA ZAIDI YA MATAIFA 53. HATA NA SISI WAKATI MWINGINE TUNATUMIA MANENO MZUNGU AU ULAYA. LAKINI NI UMASKINI WA JIOGRAFIA
na SUPER-EDDY - 18.05.08 @ 19:58 | #11746
Maombwa nahisi una chuki binafsi na Uislamu sasa sijui yale madevu anayoweka Fidel Castro utayaitaje? labda na yeye ana ubia na Iran? Hoja zako niza kubuni na wala hazina ushahidi na hakuna mwenye akili timamu akakubali kudanganywa kwa hayo
na Mtunguja, Zenj, Tz, - 18.05.08 @ 20:17 | #11748
UKITAKA KUWAJUWA WATU WAJINGA NA WEREVU HAPA DUNIANI USIPATE TAABU WEWE WAPE KALAMU NA KARATASI TU NA WAPE MADA YOYOTE ILE WACHANGIE.
HAPA TANZANIA KUNA MATATIZO MENGI YALIOJIFICHA NA YALIO DHAHIRI ILA KWA UJINGA TU MTU ANAWEZA KUSEMA WAPEMBA NI WAARABU, WAPEMBA NI WAKOROFI NA CUF NI CHAMA CHA KIDINI AU PEMBA NI MAGAIDI NI MAHAINI
HII NDIO HATARI YA KUMTOWA MTU KWENYE KIKUNDI CHA
TAARABU NA KUMPA UWAZIRI UNATEGEMEA KUTOA MCHANGO GANI KWA TAIFA?
na ikuk, uk, - 18.05.08 @ 20:18 | #11749
Sasa tanzania kuna mataifa mangapi jamani .mimi maoni yangu ni kuwa : tuachane na mambo ya ukabila tuendeleze nchi yetu jamani.tunapoteza wakati wetu kwenye mambo haya wakati .elimu hakuna ukiumwa madawa feki na bantuz kibao zimekimbia nchi kwa shida watu wameacha wazee wao na ndugu zao .tunakufa kwa malaria kila siku wakati haya maradhi kuna kisiwa kiko karibu na tanzania wameondosha kabisa malaria .sisi tuko na siasa tu .Hakuna watu wenye fikra kama hizi huku kwetu .UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU.
na EDDY, FRANCE, - 18.05.08 @ 20:24 | #11750
Kuna watu ukiona wanavyotoa maoni yao basi hutoshangaa ukisikia ccm kampiga cuf au cuf kampiga ccm huo mitaani. badala ya kutoa maoni ya maana wao wanatoa ****** . sasa watu hawa kweli watamchagua kiongozi anaefa au ushabiki tu. ukimuuliza kwanini umempigia kura mtu hawezi hata kujibu
na EDDY , FRANCE, - 18.05.08 @ 20:39 | #11752
Oh,masikini;kuna taarifa kuwa Waunguja wanasambaza vipeperushi kuwataka Wapemba warudi kwao Pemba.Waunguja mmeanza kuwafukuza ndugu zenu Wapemba! Mjue Pemba ndo inawafanya mjulikane kama Zanzibar au jina zuri laTanzania Visiwani.Mjue bila umoja huo,Pemba na Unguja,ninyi ni Waunguja tu,sio Zanzibar! Kanuni inayotawala mazingira duniani (Super Natural Power) siku zote ni kali sana dhidi ya jamii moja ambayo watu wake wanabaguana.Unguja kuwabagua Wapemba mnakaribisha laana ambayo baada ya kuwaondoa Wapemba mtabaki 'kutafunana' nyie wenyewe kwa wenyewe.Tazama laana hiyo inavyowatafuna Waisrael na Wapalestina,na pia koo za Wasomali! Karume na washirika wako ndani ya SMZ funguweni milango ya muafaka ili amani irejee Visiwani. Amani ktk nchi ina 'macho',ikichezewa hutoweka haraka.Zanzibar mbona mmelala? Upemba na Uunguja tija yake ni nini? Mnang'ang'ania vijihistoria ambavyo vitawasambaratisa.Kumbukeni roho mbaya kwa nduguyo si mtaji ila ni hasara tupu! Ohooo,'karagha-baho' braza Karume,waulize Wanyamwezi tafsiri!
na Matiku, Dsm,Tz, - 19.05.08 @ 01:22 | #11758
Oh,masikini;kuna taarifa kuwa Waunguja wanasambaza vipeperushi kuwataka Wapemba warudi kwao Pemba.Waunguja mmeanza kuwafukuza ndugu zenu Wapemba! Mjue Pemba ndo inawafanya mjulikane kama Zanzibar au jina zuri laTanzania Visiwani.Mjue bila umoja huo,Pemba na Unguja,ninyi ni Waunguja tu,sio Zanzibar! Kanuni inayotawala mazingira duniani (Super Natural Power) siku zote ni kali sana dhidi ya jamii moja ambayo watu wake wanabaguana.Unguja kuwabagua Wapemba mnakaribisha laana ambayo baada ya kuwaondoa Wapemba mtabaki 'kutafunana' nyie wenyewe kwa wenyewe.Tazama laana hiyo inavyowatafuna Waisrael na Wapalestina,na pia koo za Wasomali! Karume na washirika wako ndani ya SMZ funguweni milango ya muafaka ili amani irejee Visiwani. Amani ktk nchi ina 'macho',ikichezewa hutoweka haraka.Zanzibar mbona mmelala? Upemba na Uunguja tija yake ni nini? Mnang'ang'ania vijihistoria ambavyo vitawasambaratisa.Kumbukeni roho mbaya kwa nduguyo si mtaji ila ni hasara tupu! Ohooo,'karagha-baho' braza Karume!