Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Rev Kishoka unafahamu kuwa Tanganyika ilikuja lini ?
Nikisema kuwa Coastal area yote ya East Afrika ilikuwa ni Zanzibar utakubali ?wakati huo Tanganyika haipo wala haijulikani ,Tanganyika iliitwa hivyo kuanzia juzi juzi tu 1921 sijui utanikubalia ?
Sasa kwa kukutahadharisha tu sio kukutisha maana mtu mzima hatishwi lakini Zanzibar ina historia ndefu sana sasa unaposema kuwa Zanzibar sio Nchi ,mimi huwa naweka hesabu ya mmonyoko kuwa mwanzo ilikuwa nchi kubwa lakini ikamomonyolewa na bado inaendelea katika hali hiyo mpaka watabakia watu na mwisho hata hao watu watakuwa hawapo maana ikiwa sasa hivi wamasai wanasema ni WaZanzibari ingawa hawajakosea lakini kwa hapa tulipofikia hata waishio Dar hawawezi kusema ni WaZanzibar watu ambao walikuwa ndani ya mipaka ya Zanzibar .hebu jikumbushe kutokana na hii ramani ya Zanzibar wakati hata haijajulikana kama kutazaliwa Tanganyika ambayo vizazi vyake vya leo vinaona aibu kujiita au kujiona ni WaTanganyika wanataka au bado wanang'ang'ania kudai asili yao ya Uzanzibari ,Unajua Mtanganyika unaweza kumwita mzanzibar lakini Mzanzibar huwezi kumwita Mtanganyika na ndio hapo ikawa WaZaznibari hawakubali kuondolewa UTaifa wao na pia kanchi kao kalichobaki kumegwa na watoto wa juzi.

mapzanzibar.gif

Following your argument, here, then we should become one country, one nation without bara au visiwani, without Tanganyika na Zanzibar!

Unguja should become Mkoa just like Kigoma and so is Pemba like Mtwara.
 
Zanzibar inahitaji kuwepo kwa Muungano kuliko Tanganyika, mpende msipende!
Bw. Kishoka. Suala hili kama angalikuwepo Mwalimu Nyerere ningekwambia muulize. Jee ni nani anauhitaji sana Muungano. Tanganyika au Zanzibar? Halafu pitia hulka za Mwalimu Nyerere. Unakumbuka jinsi gani alivyowakaripia ( au alivyowa-fix) wanaochezea Muungano huu.
 
Mimi Mtanganyika nakuulizeni mnaojiita WaZanzibari, je nyinyi ni Wazanzibari wa upande gani? Pemba au Unguja? maana hata hizi hekaya za ukoloni wa Muingezera, serikali ya SMZ na mengine bado yanapiga chenga ukweli kuwa Pemba na Unguja ni sawa na maji na mafuta ndani ya Mtungi!

Ikiwa CUF na wapemba wanaamini walipata Uhuru December 12 1963 halafu Waunguja wa ASP-CCM wanadai hawatambui Uhuru na mamlaka ya Sultani na kusema Mapinduzi ya January 12 1964 ndio siku hasa ya Uhuru wa Zanzibar, mnategemea nini mkijitenga kutoka Muungano na kudai kuwa na nchi/taifa lenu?

Je kama nyinyi ni Wazanzibari wa Unguja na Pemba wakakataa kutawaliwa na kutaka kuwa na nchi yao pekee yao, mtapeleka jeshi na kuleta udikteta na kuendelea kupuuzia historia kama mnavyofanya sasa hivi kuwapuuzia Wapemba kwa ubavu wa SMZ kupitia CCM?

Zanzibar inahitaji kuwepo kwa Muungano kuliko Tanganyika, mpende msipende!

Waarabu wa Pemba hujuwana kwa vilemba....Iwe ccm ama hata CUF ama hizbu!

Kama wanataka nchi yao na mpango wa ccm utakamilika tu.

Nimejiuliza kama muungano ukivunjika leo...Je kesi za Ufisadi zitasimamiwa na sheria zipi?

Za Tanganika ama Zanzibar?

AMA KESI INAKUFA?

Maana toka wacanada warudi bongo kutoka dodoma..Basi na ccm nao wameenda zenji na Migiro kama naibu katibu mkuu wa UNA...Kaja likizo na kaenda kuwatembelea na ujumbe wa UN kuwa muafaka ni lazima kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Binafsi sijuwi ratiba ya Bunge ila nakumbuka walisema kuwa mijadala ya madini na EPA itapangiwa muda wa kujadili...Sasa sijui ni kabla ya bajeti hii kupitishwa ama ni baada ya muafaka kupatikana.

Tunabasubiria!
 
Nadhani Zanzibar ni kama zile US wanaita states ambazo zina utawala wao chini ya magavana, zinatunga hata sheria zao, zinakusanya hata kodi, na bado si nchi. Ziko katika muungano.
Muungano wetu wakuu umeshathibitishwa kuwa na mapungufu mengi katika kuu practice na viongozi wetu walishalikili hili.
Ndio sababu muungwana kaunda mara wizara mara kamati na kadhalika ili kuona ana mend shida iliyopo. Hata hivyo matatizo ni mengi kiasi kwamba iko wazi tunaitaji KATIBA MPYA.

Wakuu,

What is a state? Zanzibar is a state and Tanganyika is a state and so is Tanzania a state (nchi moja ya Muungano wa nchi mbili, ile ya Zanzibar na Tanganyika). Hata kama Zanzibar haitakuwa na serikali yake, bado ni nchi.

Dola ni mamlaka. Mfano unaotoa wa Marekani utakusuta. 50 States za Marekani, maanake ni nchi 50 zilizo katika nchi moja ya Muungano - Federal. Lakini hizo States bado ni nchi na zina mamlaka yake.

Kama kweli tunautaka huu Muungano ni lazima tukubali ukweli tuunde huu Muungano kwa namna itakayowaridhisha Wazanzibar na Watanganyika. Vinginevyo, hata kwa miaka 100 tujue utavunjika tu. Hapana atakayekubali kupunjika katika ubia.

I think G55 were right, and so are CUF and CCM (Zanzibar). Muundo wa Shirikisho ndio utakaokuwa imara. Zanzibar na serikali yake, Tanganyika na serikali yake na kisha tunakuwa na serikali ya shirikisho. Na hii ndio siri ya mafanikio ya Marekani.

Can you imagine nchi 50 ziko kimya na sisi nchi 2 tu, kelele kila asubuhi? Huu mtindo wa nchi moja na serikali mbili, haungii akilini hata kidogo.
 
Hivi CUF ni chama kwaajili ya Zanzibar au Tanzania?
CUF ni kwa ajili ya Tanganyika na Zanzibar na Tanzania na ndio ukaona sera yao ni serikali tatu na ndio wameanza na kuitafuta moja ,msemo wetu wa kiswaili unasema mtaka mawili moja humponyoka hivyo CUF wameanza na moja mpaka kijulikane CCM hawajui hesabu eti unaanza na mbili kuelekea moja sasa hapo utaona lazima moja itaponyoka ,yaani kama wangelianza na tatu kuelekea moja basi mambo yangekwisha kutimia wangeua moja moja.
 
Tanganyika mbona ilishakufa siku nyingi sana. Ilinichukua miaka kadhaa mimi kujua what was Tanganyika, lakini nilijua kuna ZNZ at the age of five. Tuliozaliwa baada ya muungano huwa tunaisikia Tanganyika shuleni tena darasa la nne. Sasa kwa wale mnaozungumzia serikali 3 mna maana kwamba Tanganyika itafufuliwa upya au tutaendelea na Tanzania bara???
 
jANA UNGUJA PALICHIMBIKA BAADA YA KUKUBALIANA KUTOKUBALIANA, ILA MJADALA HUU UNAWEZA KUVUNJA MUUNGANO AMA UKAWA CHACHU YA KUANDIKWA KWA KATIBA MPYA .....
 
jANA UNGUJA PALICHIMBIKA BAADA YA KUKUBALIANA KUTOKUBALIANA, ILA MJADALA HUU UNAWEZA KUVUNJA MUUNGANO AMA UKAWA CHACHU YA KUANDIKWA KWA KATIBA MPYA .....

Kukubaliana kutokubaliana ni hatuwa muhimu ya Muungano wetu. Tatizo ni kukataza mmoja kutokubali hilo ni tatizo ndani ya tatizi. Cha kufuata sasa ni kumtafuta msuluhishi yaani mahkama ya Katiba kuondowa kutofahamiana huko, natuanze tuliko ili tukutane katikati na suluhisho litapatikana.
 
Wiki ijayo nataka nikatembee nchini Zanzibar, sijui ofisi za balozi zao naweza kuzipataje wakuu?

Kwa bahati mbaya uhusiano wa nchi ya Zanzibar na nchi yako Tanzania una mgogoro kwa hivyo hawana uhusiano wa kibalozi na kama wewe ni mwananchi wa Nchi ya Tanzania usiyoitambua Zanzibar huwezi kwenda huko kwa vile Serikali yako haiitambuwi Zanzibar na hivyo haiwezi kuwa na uhusiano wa kibalozi nao. Safari yako hairuhusiwi kama wakati ule Watanzania walipokuwa hawaruhusiwa kusafiri South Afrika na Israel.Nchi haiachi kuwa nchi eti haina mabalozi na kama ubalozi ni kigezo Tanzania ni robo nchi kwani kati ya zaidi ya nchi 160 duniani ina Balozi chini ya 30 jee hiyo si robo? Tanzania ni robo nchi kwa mtizamo wako. Kalakabagho!!!!!!!
 
Kukubaliana kutokubaliana ni hatuwa muhimu ya Muungano wetu. Tatizo ni kukataza mmoja kutokubali hilo ni tatizo ndani ya tatizi. Cha kufuata sasa ni kumtafuta msuluhishi yaani mahkama ya Katiba kuondowa kutofahamiana huko, natuanze tuliko ili tukutane katikati na suluhisho litapatikana.
WaZanzibari wamekwisha sema watu wawili hawawezi kuamua kama Zanzibar ni nchi au si nchi ,yaani hata wakiamua basi maamuzi yao hayatatambuliwa kwanza watu hao wawili wamechaguliwa kutoka mfumo wa Chama kimoja hivyo wafanye wafanyavyo bado kutakuwa na zuluma.
Juzi kuhusu makubaliano ambayo yalihusisha vyama viwili tu ,tumeona ni jinsi gani mambo hayakukubalika na kufika chama kimoja kusema tukawaulize wananchi hata Raisi alisikika akinukuu maoni ya Chama chake.
Je jambo hili ambalo linahusu Utaifa uwananchi uzalendo halihitaji kuulizwa wananchi ,watu wawili tu ambao wote wanawakilisha Chama kimoja?
Tukirudi tulikotoka tutaona kuliundwa tume ambayo suluhisho walilokuja nalo ni ulazima wa Serikali tatu ,Tume hiyo iliongozwa na Mstahiki au Mheshimiwa Jaji Nyalali ,bado halikutekelezwa ,ila ndio mazoea ya tume zinazotokana na utawala unaongozwa na katiba iliyotokana na mfumo wa Chama kimoja.
Bado mbali ya tume hiyo wananchi walihitajiwa kuulizwa kwa sababu linagusa Utaifa na Uzalendo wao na kwa sasa Muungano huu hauna faida kabisa hasa ukiangalia nchi imevamiwa na viwavi Jeshi ambao ni mafisadi ,WaZanzibari wamesikika kwenye Baraza lao la Wawakilishi kuwa Zanzibar hawana wala hakuna ufisadi japo upo ni wa kudokoa dokoa tu maanna feza waliyonayo ikipungua shilingi tu inakuwa rahisi kujulikana hivyo kudai Zanzibar sio Nchi ni hila za mafisadi hawa viwavi jeshi kunusa harufu ya dizeli na kuona lazima waondoke na mapipa.
 
Haya ya Spika kujipa mamlaka asiyokuwa nayo ya kuamua ni mambo gani yanastahili kujadiliwa bungeni na yepi hayastahili ndiyo yanazidi kuongeza matatizo ya huu muungano, maana kulijadili hili kutasaidia kuweka wazi kila kitu, lakini wanaamua kuyafunika tu na baadaye yakileta kasheshe basi wanakurupuka bila kutojua wafanye nini.

Date::7/21/2008
Spika auzima mjadala wa mafuta na gesi kuwa chini ya muungano
Na Ramadhani Semtawa, Dodoma
Mwananchi

WAKATI joto la Zanzibar kuwa nchi au si nchi bado likiwa juu, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta, amelazimika kuzima hoja ya Mbunge Habib Jumaa Mnyaa (CUF-Mkanyageni), aliyaka kuibua mjadala wa kwa nini mafuta na gesi ni masuala ya muungano.

Spika aliuzima mjadala huo baada ya Mnyaa kuuliza swali la nyongeza kwamba, kufuatia katiba kuwa na utata kuhusu uhalali wa nchi ya Zanzibar hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akaagiza wanasheria wakuu wa Muungano na Zanzibar kukutana ili kuliweka sawa suala hilo, ni vema Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja atoe tamko kwamba mafuta na gesi, si suala la muungano au lijadaliwe pia katika hoja ya kuhusu uhalali wa visiwa hivyo kuwa nchi.

Mnyaa pia alisema Ibara ya Nane, nyongeza ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambayo ilinukuliwa na Ngeleja haitoi maelezo ya moja kwa moja kuhusu suala la mafuta na gesi zaidi ya kutaja nafasi za Baraza la Wawakikilishi na Bunge la Jamhuri katika maliasili hizo.

Kutokana na utata huo, alisisitiza kwamba kama madini si mali ya muungano pia maliasili ya mafuta na gesi isiwe ya muungano na kumtaka Ngeleja atoe tamko hilo.

Baada ya swali hilo na kabla ya kumpa nafasi Waziri Ngeleja, Spika alisimama na kusema: "Hilo swali lako si la waziri, liko chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo inashughulikia muungano". Baada ya jibu hilo alimaliza kipindi cha maswali na majibu na kufanya ukumbi kuwa kimya huku Mnyaa akiwa ameduwaa.

Awali katika swali lake la msingi, Mnyaa alihoji vigezo vinavyotumika kusema madini si ya muungano na wakati huo huo mafuta na gesi kuelezwa kuwa ni mambo ya muungano.

Pia alihoji ni tarehe na mwaka gani mafuta na gesi yamekuwa ya muungano hivyo, kumtaka waziri aeleze kwa kina utata huo.

Akijibu swali hilo, waziri Ngeleja alisema kigezo kilichofanya madini yasiwe ya muungano na mafuta na gesi kuwa ya muungano, kimewekwa bayana katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 (Ibara ya nane na nyongeza ya kwanza).

Ngeleja aliongeza kwamba, mambo yote ya nchi yanafuata mwongozo huo ambao ni katiba na kuongeza kwamba shughuli za utafutaji na uzalishaji mafuta na gesi hutekelezwa chini ya Sheria ya Utafutaji na Uzalishaji Mafuta ya mwaka 1980 (Petroleum, Exploration and Production Act, 1980).

Aliongeza kwamba, pamoja na maliasili madini kuwa si ya muungano, mapato yake yanakwenda moja kwa moja kwenye Mfuko Mkuu wa Mapato ya Serikali, ambao ndiyo unagharamia uendeshaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Waziri Ngeleja asisitizo kwamba, mafuta na gesi vimewekwa chini ya muungano tangu kutungwa kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano na ambayo imebainisha mambo ya muungano na yasiyo ya muungano.

Katika siku za karibuni muungano umeanza kutikisika, kutokana na kuibuka mjadala mzito kuhusu Zanzibar kuwa nchi au la kwa mujibu wa sheria, ambao uliibuliwa baada ya Pinda kusema bungeni kwamba Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kauli hiyo, Wazanzibar ndani na nje ya Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa waliendeleza mjadala huo.

Hata hivyo, Pinda aliwaagiza wanasheria wakuu kutoka Zanzibar na Muungano, kukutana na kupata tafsiri sahihi ya kitaalamu kuhusu jambo hilo.
 
Kama kawaida...... wanafanya vitu kiusanii hata na vile visivyostahili usanii....
 
Ameahirisha tatizo tu, bado lipo na litaendelea kutuandamana mpaka tutakapolishugjhulikia
 
Hawa jamaa washazeeka, hawajali maslahi yetu bali yao tu. Watakufa na kutuachia matatizo.
 
Normally kitu unapojaribu kukizima kiasanii ndo kinaibuka na kuwa kikubwa.
Ni kama jina la utani ukilichukia ndo lasambaa ila ukitake easy litafifia as time goes.
Mungu ibariki serikali ya Jam ya Watz
 
duh mbona wazee mnalalama saaaaaaana, hebu toeni alternatives basi ya nini kifanyike na kwa namna gani huku tukiwasidia wenzetu kimawazo na kwa kuwatia nmoyo pale inapobidi!, i'm really sick and tired of this kushutumushutumu tuuu all the time,
tena kushutumu kwenyewe siyo constructive "crticism".

hili Taifa gani la ulalamishi lalamishi tuu tunakusudia kulijengal,mara Jk vile, mara Jk hivi,mara Sitta hivi, mara Sitta vile,alichokifanya Sitta kipo ndani ya uwezo wake kama Spika sasa badala ya kumlaumu tu semeni mlitaka afanyeje, na kwa namna gani, na kwa nini hivyo mnavyotaka afanye ni bora kuliko alivyofanya.
Watu wa kushutumushutumu tuu ni wanafiki na ni hatari pia kwa maendeleo yawe ya Taifa au ya kwao wao binafsi.
lets get real people, stop whinning and do the right thing
 
duh mbona wazee mnalalama saaaaaaana, hebu toeni alternatives basi ya nini kifanyike na kwa namna gani huku tukiwasidia wenzetu kimawazo na kwa kuwatia nmoyo pale inapobidi!, i'm really sick and tired of this kushutumushutumu tuuu all the time,
tena kushutumu kwenyewe siyo constructive "crticism".

hili Taifa gani la ulalamishi lalamishi tuu tunakusudia kulijengal,mara Jk vile, mara Jk hivi,mara Sitta hivi, mara Sitta vile,alichokifanya Sitta kipo ndani ya uwezo wake kama Spika sasa badala ya kumlaumu tu semeni mlitaka afanyeje, na kwa namna gani, na kwa nini hivyo mnavyotaka afanye ni bora kuliko alivyofanya.
Watu wa kushutumushutumu tuu ni wanafiki na ni hatari pia kwa maendeleo yawe ya Taifa au ya kwao wao binafsi.
lets get real people, stop whinning and do the right thing

Gamba la nyoka..naomba ucheki kwenye hiyo thread ya Bubu hapo aliponza kabla ya kutoa news...nafkiri ametoa suggestion...kuwa lingeongelewa ma kujadiliwa kwa uwazi zaidi na siyo kama ilivyofanyika.....sijui labda sijakupata vizuri
 
duh mbona wazee mnalalama saaaaaaana, hebu toeni alternatives basi ya nini kifanyike na kwa namna gani huku tukiwasidia wenzetu kimawazo na kwa kuwatia nmoyo pale inapobidi!, i'm really sick and tired of this kushutumushutumu tuuu all the time,
tena kushutumu kwenyewe siyo constructive "crticism".

hili Taifa gani la ulalamishi lalamishi tuu tunakusudia kulijengal,mara Jk vile, mara Jk hivi,mara Sitta hivi, mara Sitta vile,alichokifanya Sitta kipo ndani ya uwezo wake kama Spika sasa badala ya kumlaumu tu semeni mlitaka afanyeje, na kwa namna gani, na kwa nini hivyo mnavyotaka afanye ni bora kuliko alivyofanya.
Watu wa kushutumushutumu tuu ni wanafiki na ni hatari pia kwa maendeleo yawe ya Taifa au ya kwao wao binafsi.
lets get real people, stop whinning and do the right thing

Mkulu watu wanlalamika klwa hawasikilizwi, inaonekana wewe si mtanzania au mkazi wa tanzania kwani karibuni miaka 10 iliyopita kuna malalamiko kuusu swala la muungano na mambo yake huwezi kuniambia kuwa hujawahi kusikia hata watu wa kawaida wanatoa maoni yao, kwani hata mimi bianfsi nilashapata nafasi ya kutoa maoni yangu na wengine wengi kupitia kwenye majukwaa tofauti, lakini viongozi wetu wameamua kuziba masikio kama hawasikiii kinachoendelea au kuona kuwa hawa wananchi ni wapumbavu.

Kama hakuna marekebisho ambayo yatashirikisha wananchi wote wa tanzania muungano utaendelea kuwa bomu ambalo linaweza kulipuka wakati wowote na kuleta maafa makubwa kwa taifa.

Ukweli ni barabara isiyo na kona hata ukisimama mwanzo utauona mwisho bila tatizo lolote lakini ukiona watu wanaanza kukata kona na kwenda vichakani ujue hakuna ukweli kwani maelezo yeyote ya kweli yataleta mgogoro, unapojaribu kuzima kitu bila maelezo ya kutosha unatengeneza maswali zaidi kwa waliouiliza, au unaposema uongo inabidi baadae uandae uongo mwingine kuficha uongo wa kwanza, kisha uandae uongo mwingine kuficha uongo wa pili, ukizidiwa na kama alichafanya spika unamwambia mtu kwa ubabe sitaki kusikia hicho kitu tena.

Kama madini sio swala la muungano kwanini mafuta yawe ya muungano au ndo kusema mafuta sio madini, au madini ya nchi kavu ndo sio ya muungano na baharini ndo ya muungano. Mimi mimi napenda sana muungano lakini katika hili hawa watu wanaonewa inabidi nao wapewe haki yao tuacha kuwa CHAKO CHETU NA CHANGU CHANGU.
 
What aspects of your background permit you to define yourself as a Zanzibari?
• Zanzibar being the country of my by birth and a land where my umbilical cord is lying
• Zanzibar being the country where my parents were born and grew up. The country where in some ways they have contributed towards its development
• Zanzibar being the country where there are numerous tombs of members of my extended family.
• Zanzibar being the country where I grew up and received my basic religious and secular education.
• Zanzibar being the country that I could identify with, in many ways, and that I could easily articulate on its various aspects.
• Zanzibar being the country that consciously and/or unconsciously, objectively and/or subjectively attached with and could dream about and even become nostalgic of.
• Zanzibar being the country that I could be proud of, that I could be sentimental with and going even as far as sacrificing my time, energy and even the best part of my life for its development and social welfare of its people.
• Zanzibar being the country where I could be discriminated against and considered alien by those who are more alien than anybody else, but where I could naturally have the courage to resist without any hesitation against the racist bunch.
• Zanzibar being the country where I could really and genuinely feel at home and at ease.
• Zanzibar being the country where I could find and recall various aspects of my childhood and find my playmates, school mates, etc.

2 In what ways does your upbringing, language, culture, class, religion (or sect), physical environment, legacy, confirms this identification:
• Upbringing: It is one of the fundamental factors confirming my Zanzibari identity. My upbringing in a coastal cosmopolitan Zanzibari society had a major impact in the formulation and development of my system of representation. Despite living abroad for many years, integrating in the process many other non Zanzibari socio-cultural elements, the basis of my system of representation remains essentially Zanzibari. It continues to date to influence in some ways my socio-cultural orientation and world outlook. Through my Zanzibari upbringing I was made to understand life in all its complexities, and to cherish honor and pride. These are some of the ideals that are highly valued by the society that one might find elsewhere, but for me, they reflect my Zanzibari identity.
• Language: I consider this to be an important element of my Zanzibari identity allowing me to differentiate with other Swahili speaking communities in many ways, including accents and colloquial. This is also true to the language used in Zanzibari literature, which I could identify with and feel part and parcel of it, allowing my assertion to the Zanzibari identity.
• Culture: Being part and parcel of the plural coastal societies of East Africa, with a number of socio-cultural similarities, my Zanzibari identity remains relevant by the existence and the performance of a number of customary rites, traditional and moral teachings giving room to some kind of differentiation with other non Zanzibaris. The inculcation of the following norms and values - principal moral foundation of Zanzibari, Swahili identity and culture further confirms my Zanzibari identification: respect (heshima), good behavior (adabu), honesty (uaminifu), ethics (uadilifu) and honour (ari).

Class: This factor does not seem to have any particular importance and to play any role in my identification to Zanzibar, hence to my Zanzibari identity

Religion: It forms an important part of social and moral background of my Zanzibari identity. Although, I am un-practicing Muslim but Islamic elements acquired through my Zanzibari upbringing still have a major impact in my world outlook and my daily life. However, I always make a difference between the Islamic religious practice that I grew up with in Zanzibar and those of elsewhere or the radical Islam. While talking about Islam in terms of Zanzibari identity, I put particular emphasis on tolerance. As a religion that came by dhow, and not imposed by sword, through trade, social and cultural interaction Zanzibar has been for many years characterized by religious tolerance. Zanzibari Islam has been all along open, tolerant and respectful of minority rights, including homosexuals. These elements contribute in my determining of my Zanzibari identity and in my differentiation with other Non Zanzibari Muslims or present Radical Zanzibari Muslims.

Physical Environment (architecture, urbanity, countryside, etc): These factors play a particular role in my taste and appreciation of physical environment of the foreign countries that I am visiting or choose to visit. The Zanzibari architectural background, aspects of Zanzibari urbanity and even countryside consciously or unconsciously remain as my major reference points of appreciation or comparison. In this sense while appreciating and comparing the above elements through the Zanzibari lenses I am affirming my Zanzibari background and by rebound my Zanzibari identity.

Legacy: Although identity is not static and is constantly being negotiated, most of the above mentioned elements remain to date valid and will take time to disappear. They remain the fundamental elements of what I could consider as part of my Zanzibari cultural legacy and identity. They are the elements that I could hardly replace but which I could very well, consciously or unconsciously, enrich with other socio-cultural elements of the foreign society that I am living in.
• Other
3 In what ways these aspects hinder your identification (if any?)
None of these aspects hinder my identification. On the contrary, they are the fundaments providing the intellectual basis for the struggle against cultural hegemony and the efforts of those who are creating confusion among the people in terms of their Zanzibari, Swahili identity and language.
4 Please add any other issues you think would be of interest:
Grew up in a Zanzibari cosmopolitan background facilitated a great deal and made me feel very much at ease mingling with people from other countries with similar plural background or not. For me identifying with Zanzibar goes even further to include a larger Swahili cosmopolitan coastal identity. For Zanzibar belongs to a larger Swahili plural identity of which I am attached and identify with.
 
duh mbona wazee mnalalama saaaaaaana, hebu toeni alternatives basi ya nini kifanyike na kwa namna gani huku tukiwasidia wenzetu kimawazo na kwa kuwatia nmoyo pale inapobidi!, i'm really sick and tired of this kushutumushutumu tuuu all the time,
tena kushutumu kwenyewe siyo constructive "crticism".

hili Taifa gani la ulalamishi lalamishi tuu tunakusudia kulijengal,mara Jk vile, mara Jk hivi,mara Sitta hivi, mara Sitta vile,alichokifanya Sitta kipo ndani ya uwezo wake kama Spika sasa badala ya kumlaumu tu semeni mlitaka afanyeje, na kwa namna gani, na kwa nini hivyo mnavyotaka afanye ni bora kuliko alivyofanya.
Watu wa kushutumushutumu tuu ni wanafiki na ni hatari pia kwa maendeleo yawe ya Taifa au ya kwao wao binafsi.
lets get real people, stop whinning and do the right thing

Ushauri gani ambao utasuikilizwa iwapo watu wanazuiliwa kuyajadili mambo. Kwenye kuyajadili ndio ushauri hutoka sasa tuwashauri kitu wakati wao wenyewe hawaoni kuwa lipo tatizo? Ushauri unakuja katika kukubali tatizo na hawa viongozi wetu wangekuwa tayari kujadiliwa matatizo yanayokabili Taifa basi kusingekuwa na Malalamiko. TUNALALAMIKA KWA SABABU VIONGOZI WETU HAWATUPI NAFASI YA KUJADILI NA KUYATOLEA USHAURI MATATIZO>
 
Back
Top Bottom