Date::7/24/2008
Waziri Mkuu Pinda akiri hoja ya Zanzibar ni nzito kwake
*Asema wanaoendeleza hawamtakii mema
*Aitwisha CCM mzigo ili itoe tamko rasmi

*Spika atumia kiti chake kuzima mjadala'

Ramadhan Semtawa na Michael Uledi, Dodoma
Mwananchi

HOJA kwamba Zanzibar si nchi imemfika shingoni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; na sasa amekiomba chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuitolea kauli kwa sababu kwa jinsi linavyochukuliwa kwa watu hawamtakii mema.

Pinda ambaye mara mbili ametoa kauli katika Mkutano wa Bunge wa 12 unaoendelea kwamba Zanzibar si nchi, jana hakutaka kusema lolote juu ya maswali matatu yaliyokuwa yanamwelekeza kwenye hoja hiyo kwa kile alichosema kwamba, "Mheshimiwa Mnyaa hanitakii mema."

Kauli ya Pinda ilitokana na swali la Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Juma Mnyaa, aliyeuliza swali la mtego kwamba: "Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa una uzoefu wa kufanya kazi Ikulu kwa muda mrefu na kwa kuwa wewe ni mwanasheria, hivi Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Article of Union (Mkataba wa Muungano) kipi kiko juu?"

Baada ya swali hilo, Pinda ambaye amejizolea umaarufu kwa kujibu maswali ya wabunge kwa utulivu na umakini, alianza kushusha pumzi kisha akasema: "Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mnyaa hanitakii mema, leo (jana) nimesikia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imezima maandamano dhidi ya Pinda, sasa sikutaka sana kuliendeleza hili.

"Chochote nitakachokujibu nitakuwa nikizidi kuendeleza malumbano juu ya jambo hili, tayari niliagiza wanasheria wakuu wakae na kuliangalia hili, sasa kuanza tena kulijadili, ahaa?"

Hata hivyo, Pinda alisema kutokana na mwelekeo wa mjadala huo kuchukua taswira tofauti, ni vema sasa CCM ikalichukua na kulijadili kisha kulitolea kauli.

Baada ya hayo, Mnyaa alisimama tena kutaka kuuliza swali la nyongeza ndipo Spika alipoingilia kati na akasema: "Unataka kuuliza swali hilo hilo, kama unataka kuuliza hilo itakuwa ni sawa na vurugu, kwani tayari Waziri Mkuu amekwishasema linashughulikiwa na wanasheria wakuu."

Kama watu waliokuwa wameagana kuibua hoja ya Zanzibar si nchi, baada ya Mnyaa, aliibuka Mbunge wa Konde (CUF), Dk Ali Tarab Ali, alisimama na kuhoji mantiki ya kauli ya Pinda ya kuagiza CCM ichukue suala hilo na kulitolea kauli kwani si la kisiasa bali ni la wananchi.

Dk Ali pia aliuliza kwamba kwa kuwa suala hilo ni la wananchi kwa nini kusiwepo mjadala wa kitaifa kuhusu Muungano kabla ya mambo hayajaharibika huko mbele?

Baada ya swali hilo, kabla ya kumpa Waziri Mkuu nafasi ya kujibu, Spika alizima tena mjadala huo akisema kanuni ya 53 (8) iko bayana kwamba, jambo likishaamuliwa katika mkutano uliopo, mbunge haruhusiwi kulijadili tena.

Spika aliongeza kwamba Waziri Mkuu alipojibu swali kama hilo wiki iliyopita na kuagiza wanasheria wakuu wa SMZ na Bara, walichukue suala hilo na kuliangalia kisha kutoa tafsiri ya kisheria wabunge walipiga makofi wakishangalia wakionyesha kuunga mkono na kuongeza kwamba: "Kwa hiyo ruling (uamuzi) yangu ni kwamba hilo nalo haliendelezwi tena."

Pamoja na Spika kuzima mjadala huo, aliibuka Mbunge wa Chambani (CUF), Salim Hemed Khamisi, akijaribu kuibua suala hilo kwa mlango wa nyuma, lakini hoja yake ikaonekana kushindwa kugusia suala la Muungano hasa kama Zanzibar ni nchi au la.

Aliuliza maniki ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kuuunga mkono kwa kiwango cha theluthi mbili katika mambo mazito yanayohusu Muungano.

Baada ya kuulizwa swali hilo, Spika alisema ni jambo zuri kabla ya kumwita Pinda ambaye naye alisema: "Hilo ni jambo zuri tu, kwani inapofika katika mambo mazito lazima kuwe na uungwaji mkono wa kiwango cha theluthi mbili kutoka kila upande."

Kufuatia majibu hayo, Khamisi aliuliza tena kwamba kutokana na hali hiyo nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliingizwa kinyume cha katiba mwaka 1994 kwa kile alichodai kwamba wakati wa kufanya mabadiliko hayo ilichukuliwa theluthi mbili ya wabunge wote badala ya kila upande.

Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na Spika ambaye alisema si kweli kwamba ilifanyika hivyo kwani wakati wa mabadiliko hayo alikuwa ni Waziri wa Katiba na Sheria.

Tangu Pinda atoe kauli kwamba Zanzibar si nchi, umeibuka mjadala mkali ambao unaonyesha kuutikisha Muungano, kutokana na baadhi ya wanasiasa kutaka Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Amani Abei Karume, atoe kauli juu ya utata huo.

Kabla ya kufikiwa kwa kauli hizo, tayari Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Iddi Pandu Hassan alikwisha kutoa kauli kwenye Baraza la Wawakilishi kwamba akimjibu Pinda kwamba Zanzibar ni nchi.

Hassan alisema kwamba Pinda alikuwa ameteleza kwa kauli yake, lakini Pinda aliirejea bungeni kwamba hakuteleza ili aliitoa kulingana na sheria za nchi zilivyo. Pinda alisema anafahamu utata unaozungumziwa kuwa ni suala la dola (sovereignty) na kuwataka wanasheria wa SMZ na Muungano kukutana kujadili suala hilo.

Miongoni mwa wanasiasa kwa upande wa CCM waliojitokeza kuzungumzia suala hilo njia ya Bunge ni Mkuu Kitengo cha Propaganda, Hizza Tambwe, aliyemuunga mkono Waziri Mkuu kwamba Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hadi sasa Wazanzibari bila kujali itikadi zao za vyama wameungana kumjia juu Pinda kwa kusema ameshusha hadhi ya visiwa hivyo huku wengine wakienda mbali wakimtaka Rais Karume aitoe Zanzibar kwenye Muungano.

Tayari hali hiyo imefanya pia baadhi ya Wazanzibari kupanga kufanya maandamano kulaani kauli ya Pinda, lakini SMZ imeyazima. Ingawa yalipata kibali cha polisi, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, alikataa kuyapokea kwa maelezo kwamba eneo la Baraza linahitaji utulivu wakati huu wa kujadili na kupitisha bajeti ya serikali ya mwaka 2008/09.

Kutoka Zanzibar, Salma Said, anaripoti kuwa baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesema Zanzibar sio taasisi ya Tamisemi na wala haitakuwa hivyo kwa kuwa ni nchi yenye mamlaka yake kamili na ndio Kituo Cha Afrika Mashariki na Kati Cha Utafiti wa Simulizi za Asili na Lugha za Afrika (EACROTANAL) Zanzibar.

Wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ya mwaka wa fedha wa 2008/09 katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wajumbe hao walisema suala la Zanzibar kuwa nchi haliwezi kuepukwa kwa hali yoyote ile hadi hapo tamko rasmi litakapotolewa.

Mwakilishi wa Jimbo la Koani (CCM) Haji Mkema Haji, alisema kutoka na kuwa Zanzibar kuwa nchi ndiyo maana jengo la EACROTANAL likajengewa Wazanzibari kwa kuwa wanafahamika kuwa wao ni watu wenye nchi kamili yenye mamlaka yake bila ya kuingiliwa na mtu yeyote.

?Mheshimiwa mwenyekiti Zanzibar ni nchi yenye mamlaka na sio Taasisi ya Tamisemi na wala haitakuwa na ndio maana tukatoa nyumba ile ya EACROTANAL haikujengwa Msumbuji wala Comoro imejengwa hapa kwa Wazanzibari,? alisema Haji. Tamisemi ni Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Haji alisema hakuna haja ya kutafutwa mambo ya kisheria kuhusu suala la Zanzibar kwani kila jambo linafahamika, hata suala la kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki linajulikana undani wake kwa kuwa wenyewe ndio walijitoa.

Akitilia mkazo kauli hiyo, Mwakilishi wa Jimbo la Gando (CUF), Said Ali Mbarouk, alisema katika suala la Zanzibar kuwa ni nchi au siyo, hilo halina mjadala linafahamika na Wazanzibari hawatataka kusikia lolote kwa kuwa wanajua Zanzibar ni nchi kamili.

''Katika suala la Zanzibar nchi au sio nchi hilo Mheshimiwa Mwenyekiti hatuna compromise (suluhu)'' alisema Mbarouk huku pande zote zikiwa zinapiga makofi na kuaza mazungumzo ya chini chini.

Kwa upande wake Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Abubakar Khamis Bakari, alisema tatizo la kudhalilishwa Wazanzibari linatokana na wenyewe kwa kushindwa kuheshimiana.

''Tunajidhalilisha wenyewe na hili nalizungumza kwa nia safi kabisa ndio haya yanatotokea?.tunaambiwa Zanzibar sio nchi jamani haya mambo tuyaangalie,'' alisema Abubakar ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Magogoni (CUF).

''Sio mara moja nimeshawahi kumwambia Waziri Kiongozi kuwa yeye sio Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lakini yeye ni Waziri Kiongozi wa Zanzibar ni wa Wazanzibari wote hili nalisema kwa nia safi kuanzia sasa aitwe Waziri Kiongozi wa Zanzibar,'' alisema Abubakar.
 
Huyu kila kitu kwake ni kigumu, na tulijua kuwa kazi ni ngumu ndio maana tulikuwa na matumaini na yeye. Sasa kila kitu kwake kigumu, atafanya busara sana kama atasema kazi imenishinda, aachie ngazi.
 

Kama ulisikia hizi habari basi umepotoshwa katika miaka ile ya mwanzoni mwa themanini bado waasisi hao walikuwa madarakani na wote walokuwa hai walikuwa Wajumbe wa Baraza La Mapinduzi - hao ni kina Said Natepe, Hassan Nassor Moyo, Seif Bakari, Khamis Darweshi, said Idd Bavuai na wengineo, na kwa taarifa ni kuwa wakati huo BLM ndilo lililokuwa na mamlaka ya mwisho. Na hata hiyo hoja yako ya kuwa hawakuwa madarakani haimaanishi kuwa hao waasisi hawakuwa na influence na siasa za Znz na Tz kwa ujumla ni hao hao walompiga vita Salim Ahmed Salim katika kinyanganyro cha Uraisi mwaka 85 na 2005.

Unazungumzia demokrasia ukifikiria wakati tulonao lakioni kama utaulizia yalipotokea haya kama kulikuwa na hiyo demokrasia ya kuwashtaki - unataka ushahidi gani kama ni kuuwawa watu hilo si siri ,kuna ndugu za marehemu hao ambao majina yao machache nayakumbuka kina Hanga, Mdungi Ussi nk walikamatwa na SMZ na hao waasisi wakiwa ndio wadau wakubwa - hao watu hadi leo hawajulikani waliko. Jamaa zao wameulizia waonyeshwe japo kaburi lakini wapi wamegonga ukuta. Au kwako ni kuwa no corpse no murder?

Kwa kukelewesha hiyo ndio nia ya Jumbe na wenzake katika jaribio la kutaka kuvunja Muungano kwa kivuli cha Wazanzibari na narudia sio wote tuko tayari kurudi katika utawala ule lokuwepo baada ya Mapinduzi hadi 1984.

Seif aliyajua hayo na aliwaona Wazanzibari walivyoteseka unajua kuwa kwa Mzanzibari wakati huo kwake aliona kapendelewa kucharazwa mkijeledi na asiswekwe jela? - kulikuwa na msemo maarufu hasa Pemba - pya nsalama kupingwa nsifungwe - sasa fikiria mwenyewe ni hali gani walikuwa nayo wananchi hawa.

Seif alifata sheria za nchi zilizokuwepo kwa kutoa taarifa ya uhalifu ulotaka kufanyika kwani ni muumini wa Muungano akiwa na mtazamo wa serikali tatu na Umoja wa wtz wote lakini msamiati wa CCM (uroho wa madaraka) ndio umekuwa unatumika badala ya kumuona ni mtu mwenye uchungu na Znz na wananchi wake - Analopinga ni kundi wachache(kama walivyotaka kufanya kina Jumbe) kuirudisha Znz katiak janga la utawala wa mababvu usozingatia sheria na vile vile anapinga Bara kutaka kuimeza Zanzibar lakini hapo hapo anaamini katika Muungano wenye kuzingatia maelewano na maslahi ya pande zote mbili - hukuwahi kumsikia akisema hataki Muungano kitu ambacho ana hakika kikitokea na kama Znz kutakuwa na mfumo wa kidemokrasia basi CUF watashinda chaguzi zote, kwani kinachoiweka SMZ madarakani ni serikali ya Muungano kwa kutuma majeshi na kutishia wapiga kura na kufanya mbinu nyengine za kuharibu uchaguzi.

Kama ni mroho wa madaraka kwa nini asitumie nafasi hiyo?
 
Ile kauli iliyotolewa na Tambwe Hiza Ilikuwa ni ya kwake ama CCM BARA, mbona hawa watu hawaeleweki wanakoelekea. Ama ndio tuamini kuwa CCM cha cha wengi, kinanza kupoteza muelekeo. Kwnini, PINDA asieleze kuwa Tambwe hakutumwa na CCM BARA, na jee Upi ni msimamo wa CCM ZNZ.
 
Huyu kila kitu kwake ni cha Kisiasa tu, yeye ameamua kuwasaidia VIONGOZI MAFISADI na jamii yao yote, hawezi hata kupima umuhimu wa nafasi yake. Nahisi hawezi hata Kusoma alama za nyakati.
 
Watanzania - sisi wote ni masikini tu na haya makelele mengine ya kusema hiki au kile ni changu ni ishara ya kufilisika. Tufanye kazi na kuondoa matongo tongo na tuwasulubu mafisadi hadi waelewe kwamba tunahitaji kuondoa umasikini wetu na sio wao kutuhadaa.
 
Acheni kumponda PM wetu
Fuatilia mujadala kwa makini(wabunge wanaohoji juu ya zenj+vyama vyao+dini zao ndani ya zenj na Tanganyika),utapata picha ya nini kinaendelea hapo.

Wazenj(na waislamu walio wengi) wangelipenda kuona zenj ikiingia ktk ulimwengu wa kiislamu + uarabu,kwa bahati mbaya ndoto zao zimebanwa na MUUNGANO.

Ikitokea MUUNGANO ukafa,asilimia kubwa ya waislamu wataihama Tanganyika kwa lengo la kutimiza haja zao chini ya dunia ya kiislamu.

Wakristo wote JF na kwingineko,iweni makini sana,musishabikie issue kama hizi.Tujiweke kamili kwa lolote ndani ya muda wowote.

Migogoro isiyokwisha + yenye ushabiki wa kidini chimbuko lake ni zenj
(uislamu),halina ubishi hili.

Nina hai ya kusema Wa-Tanganyika tukifaidicho ndani ya MUUNGANO ni kero zisizokwisha na hasa zilizobeba chachu za udini.

Pinda relax,kaza kamba,tupo pamoja.
 
Wakristo wote JF na kwingineko,iweni makini sana,musishabikie issue kama hizi.Tujiweke kamili kwa lolote ndani ya muda wowote.[/B
]

Hapa sijakupata vizuri mkuu, hebu iweke sawa hiii?
 
Kwa uelewa wangu ni kwamba Zanzibar si nchi. Hii ni kutokana na muungano ulifanywa na waasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kusema Zanzibar ni nchi ina maana muungano usiwepo. Na hii itamaanisha Zanzibar iwe na maamuzi yake yenyewe bila kuishirikisha Tanzania Bara.

Wazanzibar wanataka Zanzibar iwe nchi. Hapa inabidi busara itumike ya hali ya juu kutatua suala hilo. Kinyume chake damu itamwagika. Lengo la mjadala huu upo chini ya suala la kisiasa. Inaonekana kuna kikundi au kundi la watu wanaotaka kuiyumbisha serikali ya muungano.

Suala hilo ninashauri iachiwe mahakama. Na mahakama inabidi kutoa maamuzi yatakayokubalika na pande zote mbili, zinazotaka Zanzibar kuwa nchi na Zanzibar kuwa sehemu ya Jamhuri ya Tanzania.
 
Pinda alisaidiwa sana na Six baada ya kuingilia hoja. Vinginevyo alikuwa katika wakati mgumu.
Kitu kimoja sijakielewa na nahitaji ufafanuzi kwa kweli kutoka hapa jf ni ile kauli kwamba suala zima la Zanzibar kuwa nchi au la analiacha mikononi mwa CCM.
Je CCM ni nani katika kuamua mstakabali wa nchi yetu? Hili ni jambo la kikatiba wala si la katiba ya CCM ila katiba ya nchi ambayo wote tuna maslahi. Yaani tusio na vyama na nyie wenye vyama. Nisaidieni nielewe jamani!
 

Tumeshaona wengi wa watu wenye msimamo wako wa kuwa Zanzibar sio nchi ndio pia wenye msimamo wa kusema kuwa kulijadili hili ni kosa. Sasa kama wewe umetowa mawazo yako kuwa Zanzibar sio nchi na pengine umetowa sababu zako kwa nini si nchi swali linakuja hapa "kwanini mwengine usimpe uhuru wa kusema mawazo yake kuwa Zanzibar ni nchi na ukamsikiliza nae sababu zake ? Pengine wewe hukuziona hapo kabla.
Wazanzibari wanazo sababu za kudai Zanzibar kuwa nchi kwani zilizouungana ni nchi na kwa lugha rahisi tunasema Tanzania ni Muungano wa Nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar.
Kilichofuata kilikuwa ni makubaliano ya namna tutakavyofanya Muungano wetu na makubaliano yakawa Nchi ya Tanganyika itaendesha shughuli zake kwa kupitia Serikali ya Muungano na Zanzibar itabaki kuendesha mambo yake chini ya jina lake la Zanzibar lakini baadhi ya mambo ya Utaifa yataendeshwa na Serikali ya Muungano.
Wakati wa Uhai wa Abeidi Karume Muungano uliendeshwa hivyo lakini baada ya kifochake taratibu yale mambo waliyowakiendesha Zanzibar yalianza kupunguzwa taratibu kutokana na ujanja au kutumia nguvu.
Hivi sasa basi Wananchi wote wa Tanzania wameamka Kisiasa wamekuwa wakijadili yale yanayowaudhi na kuwakera na Kwa upande wa Zanzibar mbali ya matatizo yao na Serikali yao hili suala la Muungano wameliamkia wakidai haki katika Muungano.
Wananchi wa kawaida hawajui sababu za upande mmoja kuiminya mwengine lakini viongozi wao wanajuwa sababu zao na ndio hawataki kuwaambia ukweli wananchi kuwa Muungano wetu una mushkeli, lakini anaeonewa siku zote ndio mwenyekutafuta mbinu za kujinasua na maonevu.
Ni bahati mbaya sana kwa Viongozi kuwa kauli zao za kejeli ndio zimefungulia mlango kwa wananchi kuujadili Muungano hivyo kuuzima mjadala huu ni kupoteza wakati kwani vizazi vya sasa hivi bado vina malezi mazuri hatujui watoto wetu tutawalea vipi na vipi mjadala kama huu wataucheza .
Kuhusu kuachia mahakama nani atakuwa Jaji ,Mtanganyika au Mzanzibari na watalitolea uamuzi suala gani iwapo viongozi wa sehemu mbili wanatafautiana? Hivyo si dhahiri tukaita process yote batili na tukaanza upya kujadili namna gani Muungano wetu uwe ili sote tukubaliane?
 
CCM itoe tamko gani na tayari imeshatoa tamko rasmi kupitia kwa njaa kali tambwe au wanataka ibadilishe tamko na kusema vinginevyo.
 

Kama Upo Utaratibu Wa Watu Wa Namna Hii Kufungiwa Ungemfaa Huyukwani Anakotupeleka Yeye Ni Kwengine> Tunaweza Kumjibu Lakini Tutakuwa Tunamsaidia Katika Adhma Yake Ya ufisadi
 
wewe huna tifauti na wale wanaoamini zanzimbar ni nchi haya yote yameanzia wapi.au ni fisadi mwibngine anayetaka kuzua udini bara
 

Sijawahi Kumwona Mtu Asiye Na Uelewa Kama Wewe. Ninyi Ni Moja Ya Watu Wanaopotoshwa Na Mashehe Huko Misikitini Wasiojua Kitu. Yaani Kila Kitu Kikitokea Tu Duniani Wanaona Ni Kampeni Ya Kuufuta Uislam.ndo Maana Hata Shule Hamuendi Kisa Uislam Mtausomea Saa Ngapi, Matokeo Yake Mnaona Kama Mnaonewa Wenzenu Wakichuma Mali Kutokana Na Elimu Yao. Wewe Unasema Hivyo Wakati Raisi Wetu Pamoja Na Makamu Wa Rais Wote Ni Waislam, Je Wangekuwa Wakristo Hao Watu Si Ndo Ungejitoa Muhanga Kabisa?

Tell Me, Unaesema Anafanya Kampeni Ya Kuuwa Uislam Zanzibar Ni Jakaya Kikwete? Karume Au Muhamad Shein? Who Is It? Ni Nani? Yaani Nikwambie Rafiki Yangu, Wewe Ni Mtu Uliyepitwa Na Wakati Kishenzi Yaani. Na Akili Kama Hiyo Ndo Iliyojaa Huko Zanzibar, Kila Kitu Mnaona Mnaonewa Na Wabara, Mnaishia Kulalamika Tu Na Maisha Yenu Hata Hayatabadilika, Kisa Nini?mnafikiri Mtu Ana Dili Na Uislam Wenu, Kwaajili Ya Nini? Hebu Futa Hiyo Kauli Yako Haraka Kwasababu Inakuaibisha. Ok?
 

Ukitaka kujua anachosema bikirembwe soma kitabu kiitwacho kanisa katoliki na siasa za Tanzania humo utaona mkakati kwamba baada ya ukomonist kitu gania ambacho kina fuatia
 

Kwa bahati mbaya hujui faida mnayopata kuungangania huo Muungano lakini viongozi wako wanajua faida na bora ungewauliza kwanza kabla ya kufanya jazba.
Jazba ya nini eti Wazanzibari wamesema kuwa mafuta ni ya kwao kama vile dhahabu ,almasi, Tanzanite, Gesi na kadhalika zilivyokuwa si mali ya muungano?
Funua macho na utafakari kwanini kinachotoka upande mmoja kisiwe cha muungano na kinachotoka upande wa pili kiwe cha Muungano huo huo? Na baya zaidi ni kuwa hali hii imekubaliwa kwa kipindi cha miaka 44 lakini upande mwengine ndio umepata neema unaambiwa ni chetu na huku msisitizo ile neema ya miaka44 itaendelea kuwa si ya pamoja. INAKUINGIA AKILINI?
 
Kuna tatizo hapa,Waziri Mkuu inaonyesha amechanganyikiwa na hili si yeye peke yake hata Kikwete ,uongozi wanauchanganya na uanachama, ni kweli kuwa wao ni wanachama wa CCM lakini unaposhika madaraka ya Inchi na kuwa Raisi au Waziri Mkuu au waziri wa aina yeyote ile inatakiwa uwe na tahadhari kubwa ya kuchanganya mambo la si hivyo utakuwa unafanya mambo kama mwenyekiti wa Chama chako au Katibu ,aliposema Tambwe sikuwa na la kusema kwani alikuwa anakisemea Chama chake au alikuwa anawakilisha Chama chake kama alivyo ni mkuu wa uongo wa kisiasa katika CCM,lakini Pinda anaposema tena ndani ya Bunge Tukufu kuwa anaiwachia CCM kuamua au kutoa tafasiri , Pinda kama Waziri mkuu labda angelisema suala hilo anamuachia Waziri wa mambo ya ndani na nje au anawaachia wanasheria wa Serikali zote mbili na angewapa miezi sita ili warudi na jibu.Kusema anawawachia CCM ni kosa la jinai.
Suala la Zanzibar au Tanganyika kuwa Nchi au si Nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano hilo kwa ukweli ulio wazi si suala la kuhusisha Serikali ya Muungano au Serikali ya Zanzibar ,seuze chama cha siasa ambacho kimejaa mafisadi na uongozi unaohujumu Taifa au chama kingine chochote ,labda pengine naweza kusema Bunge la Jamhahuri na Baraza la wawakilishi kwa upande wa Zanzibar wanaweza kwa kiasi fulani kulijadili suala hili na sio kulihitimisha ,bali maamuzi ya mwisho warudi kwa wananchi na kulijadili na ukiangakia ,hakuna cha kujadiliana ila kuna kupanga upya namna ya Muungano lakini sio kusema Zanzibar sio Nchi au Tanganyika sio Nchi ,sidhani kama kuna Mtanganyika anekubali kuambiwa au kusema Tanganyika sio Nchi na wale wanaosema Tanganyika ilipotea kwa kuanzishwa Muungano hao ni maadui wa waTanganyika inafaa wamulikwe ni dizaini za akina Tambwe ambao hawaoni tabu kupoteza uzalendo wao kwa ajili ya maslahi, huku wakiangamiza wengi kwa tamaa zao.
 
Wewe hujui unafikiri kitu gani na unachokiandika sicho ulichokipanga inaonyesha una mgongano wa mawazo na huna coordinasheni ,

Maana kwa uelewa wangu Zanzibar si nchi...1
Muungano ulifanywa na waasisi wa Jamhuri ya Tanzania...2
Kusema Zanzibar ni nchi inamaana Muungano usiwepo......3
Hii inamaanisha Zanzibar iwe na maamuzi yake ...................4
WaZanzibari wanataka Zanzibar iwe Nchi..............................5
Busara itumike kutatua suala hilo...........................................6
Kinyume chake Damu itamwagika.............................................7
Lengo la mjadala huu upo chini ya suala la kisiasa..........................8
Kuna kikundi au kundi linataka kuiyumbisha Serikali ya Muungano.......10.

Sasa hebu nipe majibu.
1 ) Zanzibar ni kitu gani ? Mkoa ,wilaya,tarafa kata ,jimbo au sehemu ?
2 ) Nani aliwapa nguvu waasisi hao kuunganisha Nchi bila ya ridhaa zaW/nchi?
3 ) Hakuna Muungano kama Nchi zinazoungana hazipo ,ndio ukaona ili kuwepo na Muungano basi inahitajika serikali ya Tanganyika ,huu ni Muungano feki uliojaa mazabe .
4 ) Hakuna mZanzibari anaetaka Zanzibar iwe Nchi kwani haijawahi kutokuwa si Nchi.
5 ) Zanzibar ina maamuzi yake ,Raisi ,Mawaziri ,mahakama na Baraza la wawakilishi.
6 ) Suala unalolizungumza halipo kwani halijatolewa kauli na kuthibitishwa rasmi.ni waZiri Mkuu ambae anakurupuka kwa tiketi ya CCM na sio kama Waziri Mkuu maana tumesikia anapozungumza kama Waziri mkuu huwa analikwepa suala hilo ,huzungumza kama CCM ili kuwatosa wahafidhina si unafahamu wana matatizo tokea walipopigwa na chini kule Butiama.
7 ) Damu itamwagika naona umekwenda mbali hivi kitu gani na nani atamwaga damu kwa ajili ya nini ?
8 0 Mjadala huu upo kwa lengo la kisiasa ,unafahamu tokea wahafizina wamchafulie Kikwete kule Butiama na kumwambia awarudishie ASP yao hadi leo mambo hayajakaa sawa na katika gazeti moja la juzi Wahafidhina wa Zanzibar walisema wanahisia za wenzao wa bara kuwawekea ngumu kwa matatizo yale yaliotokea Butiama ,sijui kama uliliona hilo.

Hapa hakuna kundi wala kikundi ila kuna Muungwana na akina kaka kazi wake wa Butiama na kikundi cha Karume ambavyo vimo katika mapambano ya vita vya maneno na kila mmoja anataka kujionyesha kuwa yeye ndio Superior kuliko mwengine ,nani atapwaya ,hatujui ila muda ndio utakaotuwekea mambo waziii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…