It could very well be so,

I am not putting that past our journalists. Watu wanakuuliza halafu ukijibu wanaandika kama umesema.Kusema na kujibu ni tofauti kubwa na inaweza kumaanisha north or south pole.

Ndiyo maana magazeti yaliyoendelea huwa wana qualify na statement kwamba "He was responding to a question by......"
 
Huyu mama alitakiwa kunyamaza tu kuhusu hii issue, ama sivyo atajua Tanzania watu hawana akili au adabu, bahati yake hawajaidaka hii.

Siamini huyu undersecretary wa UN hajui hicho kitu wakati wewe mja wa kawaida tu unakijua, unless na wewe umewahi kufanya kazi kwenye taasisi za Kimataifa. Mama Migiro amechemsha big time! Big time!

United Nations, kwa hii statement, imebariki idea kwamba Zanzibar sio nchi. Whether they are right or wrong, the United Nations hapa imejiingiza katika mgogoro wa ndani wa Kikatiba wa member state. Hii ni bonge moja ya diplomatic gaffe on the part of the undersecretary.

Viongozi wa Umoja wa Mataifa huwa hawatoi statement kama hizi vichochoroni vichochoroni kwa sababu kila wanachoongea ni matamko wa UN. I mean, this woman is the undersecretary, she speaks for the body! Goodness gracious!

Nilikuwa proud na huyu Mama Migiro katika hiyo nafasi, lakini sasa hivi najiuliza walimuibua kutoka wapi huyu Mama? Mwanadiplomasia gani huyu?

Yani wenzake Umoja wa Mataifa wakisikia hii kitu watamshangaa ile mbaya.
 


Mama Migiro,

Hakukosea kitu chochote, alichosema ni msimamo wa UN kuhusiana na ishu ya Muungano wa Zanzibar kwa haya maneno hapo juu hakuna alichokosea,

kama alilokosea ni what she did not say na mazingara aliyoisemea ambayo pia it can be debated, lakini asingeisemea kwenye gorund zero, bila ya kuombwa kuingilia kati na moja serikali hizi mbili, otherwise sidhani kuwa hukumu hii nzito ni kwa sababu tu haya maneno, labda kama kuna mengine huko pembeni!
 
Debate yote kwa kweli ni upuuzi tu, na waliozusha hii debate sijui wana lengo gani na sijui wanauwezo gani wa kufikiri. what is it that they want. NI simple kabisa kuwa existance ya Zanzibar kama nchi ili-seize baada ya muungano, so as Tanganyika, na roles na rights karibu zote za nchi zilikuwa shifted kwa Tanzania. Zanzibar ni autonomous part of a Country ambayo inaserikali inayojiendesha, lakini hii haina maana kuwa ni nchi. Haya mambo ya wanafunzi wa for three kudebate sio ya watu wazima na akili zao. Cha kudebtae labda ni status yenyewe na lakini sio kuuliza nini ni nini.
Kama kuna viongozi wanauliza haya basi hawana haki ya kutuongoza kama hata hawajui muundo wa nchi yao ukoje basi hata kuongoza hawawezi.
 

Jambo la kushangaza ni kuwa mnachukuwa kauli na kuwatilia wale wanaoujadili muungano. Si sefu wala Shamuhuna aliyesema kuvunjwe muungano bali hizo ki kauli zenu mnapoambiwa kuwa tunataka Muungano wa haki wa kuheshimiana na kugawana mapato kwa haki.
Kinachoonesha hapa ni nyie kuishiwa hoja na badala yake kukimbilia katika kuwapaka maovu viongozi wa Zanzibar kwa haki yao. Zanzibar ni yao si yenu na kuwa Tanzania iliingia kwa hiari sasa cha ajabu nini kwa hiari ile ile kutaka mabadiliko ya Muungano.

Kuvunjika kwa Muungano kuna mwelekeo wa Bara kuliko Zanzibar.
 

MASLAHI BINAFSI? Hebu na waulizwe Wazanzibari na kuona matokeo yake. Hata wale waliopandikizwa watasema wanataka mabadiliko ya mfumo wa Muungano.
 

Hicho ni kiherehere cha mwandishi na muono wake kuwea Zanzibar si nchi. Kwani katika mjadala huu Zanzibar imedai uanachama au kutambuliwa na UN? Mwandishi amekimbilia kuuliza suala hilo akijuwa kuwa Zanibar imo imo kwa kupitia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Anyway..kama mambo yenyewe ndio haya wazanzibari tuendeleeni kuwa ndugu tu...mtafanyaje na nyie DUNIA haitaki kuwatambueni??

Usidanganyike Zanzibar inatambulika vizuri duniani na unaweza ukashangaa kuona kuwa wengi hawaitambui Tanzania kuliko Zanzibar. UN ni jumuia na ina masharti yake. Zanzibar ikijulikana na UN hata kabla ya uhuru wake 1963 na ndiyo maana ikapata uanachama baada tu ya uhuru wake.
UN wanatambuwa pia kuwa kwa hiari yake Zanzibar ilisitisha uanachama wa UN kwa ajili ya kuungana na Tanganyika na wawili hawa wakajiunga na UN kwa jina la Tanzania. UN itatambuwa pia hiari ya Zanzibar iwapo tutaamuwa kuwa na uanachama TOfauti.

USIPIME!!!!!!
 
Duu!! Kaaaazi kwelikweli

Ukishangaa ya Mussa utapata ya Firauni. Muungano wa Libya na Misri, na ule wa SeneGambia kila nchi kwenye muungano huo walikuwa wanachama wa UN.
Miungano hii bwana!!!!!
 

Kama ilivyotofauti kati ya Quebec na Zanzibar na ilivyo tofauti utaifa wa Canada na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndivyo itakavyokuwa tofauti hapo itakapoitishwa Referendu Zanzibar.
 

Check your records-again.
 
 

Welldone underage. Nilishawahi kusema huko nyuma kuwa utegemezi unaonekana kwa Zanzibar ni ARTIFICIAL kwani umekuwa ukifanywa kusudi. Wakati wa Abedi Karume Masuala ya pesa, elimu, rasilimali na kila kitu kikiendeshwa kwa uhuru Zanzibar na ni wakati huo Zanzibar ilinawirika kiuchumi. Kama kulikuwa na upungufu katika mambo hayo ingefika wakati Wazanzibari wenyewe wangeyatafutia maboresho. Kinachoonekana sasa ni kuibana Zanzibar kwa kila hali ili iitegemee Bara na huku wananchi wakidanganywa kuwa pesa za Muungano (Tanganyika) ndizo zinazoiendesha Zanzibar.
Hali ingekuwa hivyo basi Zanzibar ingepiga hatuwa zaidi badala ya hali ya sasa hivi ya kuzidi kudidimia kiuchumi. Nasema hivyo kwa sababu kulinganisha na udogo wa Zanzibar Serikali ya Muungano isingeshindwa kuipatia maendeleo . Hali halisi ni kuwa Serikali ya Muungano inazuia taratibu njia zote za kuiendeleza Zanzibar huku ikitowa chozi la Mamba.
 
nimeona Azim Dewji ametoa maoni yake na kwa Mtazamo wake kama raia wa kawaida na kama mfanya biashara.....kwenye Guardian ya leo 30/07/2008...full page.
 
Na Mwandishi wetu. Spesho edishon.

Kisumo asizungumze kama yupo kwenye mikutano ya TANU pale Biharamulo.


Akizungumzia maoni ya hivi karibuni yalioandikwa katika gazeti hili juu ya Peter Kisumo kuhusu Zanzibar, Mzee Rashid alisema Kisumo ameonesha dharau kubwa dhidi ya Zanzibar na hakupaswa kulinganisha timu ya mpira na Zanzibar kwa kuwa Zanzibar ni nchi licha ya kuwa hivi sasa kuna mjadala unaoendelea kuhusiana na suala hilo ambalo linahitaji kupatiwa upana wa mjadala ili kuweze kushughulikiwa ipasavyo na kupatiwa ufumbuzi.
"Ni dharau kubwa sana ameonesha Kisumo kwa nchi yetu na pia amemdhalilisha hata Rais huyu (Karume) huwezi kufananisha Timu ya mpira na Zanzibar? Wala huwezi kufananisha wimbo wa taifa na kwaya ? Sio vizuri kabisa amekosea na ni maneno ya kilevi sio maneno ya akili mimi Kisumo mimi ni rafiki yangu kipenzi namualika awe mgeni wangu aje Zanzibar kusiliza maoni ya wazanzibari juu ya suala hili linavyoendelea hapo ndio atajua kinachoendelea hapa visiwani" alisema" amesema huku akionesha masikitiko yake.
Pia maneno ya Kisumo ni kama kwamba anahutubia mkutano wa Chama Cha TANU Biharamulo kuwa kinachosemwa na Chama hicho ndicho kinachotendeka lakini wakati huu ni mwengine ambapo mfumo wa vyama vingi ndio unaochukua nafasi ya demokrasia na sio mfumo wa chama kimoja kama alivyozowea.
"wapo wanaojisahau wakadhani bado kuna chama kimoja Kisumo hana experience wala ujuzi ya kuzungumzia mambo ya kimataifa au kitaifa na ndio maneno yake kama anahutubia mkutano wa TANU chini ya mfumo wa chama kimoja" amesema Mzee Rashid ni Rafiki Mkubwa wa Mzee Kisumo.
Mzee Rashid ambaye ana uzoefu mkubwa wa masuala ya Zanzibar na Tanganyika amewatahadharisha wale wote wanaojaribu kuunyamazisha mjadala huu usiendelee kwa dhana kwamba Chama Cha Mapinduzi kikitoa tamko la kukaripia utamalizika au kufa kabisa.
"Mimi siamini kama mjadala huu unaweza kumalizwa kwa CCM kutoa tamko au kukataza viongozi wasizungumze, hapana babu, huu mjadala uendelee wao wanadhani chama kikisema Zanzibar sio Nchi ndio mambo yatakwisha? Ni hatari kubwa suala hili hayatakwisha Noo" ametahadharisha Mzee huyo.
Akitoa ushauri wake juu ya suala hilo amesema ni vyema kukaitishwa kura ya maoni lakini hata kama wa kuulizwa watakuwa CCM basi waulizwe CCM wa Zanzibar peke yao na Bara peke yao kwa kuwa Zanzibar wakisema hawataki maamuzi na Bara wakasema wanataka mwamuzi awe Mahakama ya kimataifa.

Asha Migiro aumbuliwa ,mzee asema Asha hana ajualo.
Akizunguzia kauli ya Asha Rose Migizo Mzee Rashid amesema hana mamlaka yoyote ya Umoja wa Mataifa hivyo kauli yake haina uzito unaostahiki kwani Migiro alipaswa kutaka mjadala huu uendelee na sio kunyamazishwa huku akikumbusha kwamba Umoja wa Mataifa haujafuta kiti cha Zanzibar kwani hakuna maombi ya Zanzibar wala Tanzania juu ya kufutwa kiti hicho kilichopo katika Umoja huo.
---------------------------
Nilisema hapa hapa kuwa Migiro hana tofauti na Tambwe ...Haya
Mzee amewapa chalenji kina Migiro na wengine kwenu itakuwa Changamoto mkatafute maombi ya Zanzibar au Tanganyika au Tanzania au Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ni lini na ni wapi yalipelekwa maombi ya kufuta kiti cha Zanzibar huko umoja wa Mataifa ?? Kazi kwenu.
 
... ninachoomba ni marekebisho ambayo yatarejesha hadhi ya zanzibar kimataifa...

Heshima mbele mkuu.
Lakini, iwapo Zanzibar itarejeshewa hadhi yake kimataifa, bado Muungano utakuwepo? Kwa misingi gani? Au hoja yako ni kutaka Muungano uvunjwe lakini umeamua kuipresent kivingine?
 
Kumbe migiro hana mamlaka yeyote ndani ya Umoja wa Mataifa .hebu mkimuona muulizeni ni lini Zanzibar iliomba kufutiwa kiti chake cha Umoja wa Mataifa ,mtoleeni uvivu atwambie kama anazo kumbukumbu itakuwa vizuri kuziweka hapa.
 
[17] Tanganyika was a Member of the United Nations from 14 December 1961 and Zanzibar was a Member from 16 December 1963. Following the ratification on 26 April 1964 of Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar, the United Republic of Tanganyika and Zanzibar continued as a single Member, changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964.
Yaani mtaumbuka vibaya sana ,wandugu inaonyesha viti vipo , tena kama haitosho huko inaitwa UNITED OF REPUBLIC OF TANZANIA na si UNITED REPUBLIC OF TANZANIA na kumbe kama nilivhoashiria hakuna Nchi inaitwa TANZANIA. Na katika kufuatilia na kuchunguza mstari kwa mstari kumbe hata katika pasipoti kumeandikwa kimakosa kwenye gamba juu wameandika PASSPORT TANZANIA wakati ilitakiwa iandikwe PASSPORT UNITED OF REPUBLIC OF TANZANIA ndani wameboronga vibaya sana maana nimeona niwaandikie hapa ili mtoe tafasili yake:-
PASIPOTI ilikuwa iwe HATI YA KUSAFIRIA ,maana PASIPOTI hata sijui hii ni lugha gani au kiswahili cha wapi,kimetumika hapa
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kimombo UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ilikuwa iwe UNITED OF REPUBLIC OF TANZANIA.
Sasa kama tunataka tuwe nchi moja hili Tanzania halifai kabisa itabidi litafutwe jingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…