Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
under_age,

..tufafanulie kuhusu hii hoja yako ya Tanganyika kuitawala Zanzibar kiuchumi.

..kuna Wazanzibari wengi tu wametajirika/wanatajirika huku Tanganyika bila kubugudhiwa.

..Wazanzibari hao wanaweza kurudi kwao na kuwekeza kiuchumi.

..vilevile Zanzibar ina wizara yake ya fedha, mamlaka yake ya mapato na kodi, wizara ya utalii, viwanda, etc etc.
Unaposikia Uchumi wa Zanzibar umemezwa au Tanganyika alieavaa koti la Utanzania na kusanya fedha ya kodi na kuwaachia mafisadi wachote bila ya kuhojiwa usifikiri wanaokusudiwa ni watu mmoja mmoja au matajiri uchwara wanaomiliki vihiace na vifuso vya kubebea mchanga hapo utakuwa unapotea na njia ya kurudi haipo.
Uchumi wa Zanzibar umebanwa na njia zake kuu zote zimewekewa mabouncer ambao ikifika jioni wanapanda boti kurejea Dar kwenda kugawana fedha na kilichobaki ndio hupelekwa Serikalini(TZ muungano).
Sasa unaikuta serikali ya Zanzibar haina mapato ambayo yatawezesha kulipia mishahara ya wafanyakazi walio serikalini seuze walio staafu,serikali haitaweza kuendesha shughuli za maendeleo,mashule,mahospitali mabarabara na kuhudumikia ,sasa unategemea hii serikali iapate wapi fedha ?
kama unasema kuna watu wazanzibari walioko Tanganyika na ni matajiri au wametajirika ,fahamu ya kwamba hao hawakai bure na kusubiri mafao ,ukubwa wa utajiri waliokuwa nao kodi wanayolipa inaingia katika mfuko wa serikali ya Tanganyika ndani ya Tanzania na sio Zanzibar ,biashara wanazofanya hazina uhusiano na wizara zilizoko Unguja income tax yote inabaki huko huko,sasa sijui umenielewa ?
 
Hebu tuambieni ni wapi katiba ya ZNZ inasema ZNZ sio nchi, Hebu tuambie niwapi hiyo Katiba ya huo Muungano inasema ZNZ sio nchi, wanachosema ZNZ ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano, jee ni sehemu kama nini ?.

Hivi mtu akichukua vipande viwili vya chuma cha aina moja na kuviunganisha, kikawa kimoja, hivi vile vipande huwa sio chuma?. Na jee inakuaje vitu viwili vaimbiwe vimeungana halafu kufanya kimoja, halafu kimoja kibakie, lakini kiambiwe sio tena kitu.

Hakuna Muungano ,wala katiba ya Muungano, kilichopo, ni Tanganyika kuitwala ZNZ.

Halafu huo unaoitwa Muungano, si ulikuja kwa makubaliano (mkataba) sasa mbona nyinyi, huo hamuutaji, mnashikilia katiba katiba. Leteni hadharani basi huo mkataba wa Muungano, halafu mtuonyeshe hapao paliposema kwamba ZNZ sio nchi ?.

Wazanzibari Hawaitambui hiyo katiba ya Muungano, wanachokijua ni Mkataba wa Muungano wa Karume na Nyerere ambao haukutekelezwa tokea day one, na hakuna cha kudai haki wala nini kutoka Tanganyika. Hayo mtayajua nyinyi.

Wazanzibari wanachotaka, ni kwamba Mkataba wa Karume na Nyerere upelekwe katika baraza la wawakilishi, na ikionekana kwamba umekiukwa ,basi nikutangaza kwamba hakuna cha Muungano.

Mimi nawapa challange kama mnaamini ZNZ sio Nchi, wekeni hadharani mkataba wa Muungano, mbona hili hamlitaki, mmeshikilia katiba ,Katiba viraka.

Katiba ya ZNZ,kwa ZNZ ndio iliojuu, na ndio yenye haki ya kuamua lolote kuhusu ZNZ ,kuhusu lolote. Baraza la wawakilishi ndio lililojuu kwa ZNZ na ndio lenye haki ya kuamua lolote kuhusu ZNZ. Kwa hiyo na huo muungano wenu, basi sasa lazima baraza la wawakilishi liutolee maamuzi,na maamuzi yenyewe ni kutangaza kwa ulimwengu kwamba hakuna cha muungano wala nini.

Katiba ya muungano hatuitambui, pakuanzia ni mkataba wa Nyerere na Karume kama upo,kama haupo ndio hivyo tena itakua pono kwa ubua.
 
Pakacha,Ngekewa,Fundi Mchundo,Mwiba,

..mimi naomba kuelekezwa hizo kasoro au kero za Muungano ni zipi.

..naomba pia mtueleze njia ya kuzitatua.

..wako wanao-suggest tuunde tuwe na serikali tatu.

..sidhani kama mazingira ya serikali 3 yataipa madaraka na nguvu zaidi SMZ. zaidi nafikiri madaraka ya serikali ya TGK yatakuwa kama ya serikali ya SMZ sasa hivi.

..pia nadhani serikali 3 zitaongeza gharama na matumizi ya serikali. mzigo huo itabidi ubebwe na wananchi wa Tanganyika kwasababu wao ndiyo wanaowakilisha majority ya population ya Muungano.

..kitendawili kikubwa ktk Muungano huu nadhani ni udogo wa Zanzibar, kieneo, idadi ya watu, na kiuchumu. katika mazingira kama hayo kila upande hauishi kulalamika kwamba haupati a fair deal.

Mimi ni muumini mkubwa wa Serikali mbili na mfumo tulio nao sasa hivi ndio muafaka. tuwashukuru waliobuni mfumo huu. Tatizo ni kuwa kile kilichobuniwa sicho kinachotekelezwa. Kwa mfano mfumo huu uliobuniwa na Mwalimu Nyerere hausemi kuwa Zanzibar sio Nchi. Lakini leo Mheshimiwa Pinda anasema Zanzibar si Nchi. Sasa tatizo ni la utekelezaji na watekelezaji (akiwemo Mh. Pinda na wenziwe ). Serikali ya Jamhuri ya Muungano isijifanye Baba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima iwe na madaraka yake kamili, kama tulivyokubaliana katika article za Muungano. Sasa Pinda haelewi hivyo - ina maana watendaji wake wengi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano hawaelewi hivyo. Hii ni kasoro. Kikwete simama Kidete kurekebisha hii. Wazanzibari siyo wakorofi lakini panapouma wanasema ukweli.
 
under_age,

..tufafanulie kuhusu hii hoja yako ya Tanganyika kuitawala Zanzibar kiuchumi.

..kuna Wazanzibari wengi tu wametajirika/wanatajirika huku Tanganyika bila kubugudhiwa.

..Wazanzibari hao wanaweza kurudi kwao na kuwekeza kiuchumi.

..vilevile Zanzibar ina wizara yake ya fedha, mamlaka yake ya mapato na kodi, wizara ya utalii, viwanda, etc etc.
kuhusu suala la wazanzibari kutajirika bara hiyo ni individual effort ambayo haimo kwenye ajenda ya muungano ,hata wabara wapo ambao wametajirika zanzibar na sio wabara tu hata wakenya wamejenga baadhi ya vihoteli na kutajirika, hapa hatujadili individual effort ambayo kila mmoja wetu ana uwezo wa kutajirika popote kutokana na jitihada zake ,bali tunaongelea system as a whole inayounda muungano ambao zanzibar inalazimishwa na system hiyo ili iwe tegemezi. umetaja wizara ya fedha , to me its like a joke , hivi naomba unieleweshe waziri wa fedha wa zanzibar ana mamlaka gani kimataifa ?na yule anaeitwa wa muungano naomba unielimishe anawakilisha upande gani wa tanzania?, hichi ndicho ninachokiongelea kila siku kwamba zanzibar tumepewa vivuli vya wizara na tanganyika wakabeba wizara halisi huku wakizipa jina la wizara za tanzania, na hivyo kuvifanya vitu kama misaada na scholarships kutolewa kwa jina la tanzania, na huku inathibitiwa na tanganyika huku zanzibar ikiambiwa ina serikali yake na wizara zake, wizara ambazo hazina mamlaka yeyote nje ya mipaka.
 
mwiba,under-age,

..jaribu kuchunguza shughuli na mamlaka ya zanzibar revenue board na tra-znz.

..fedha zote zinazokusanywa na vyombo hivyo viwili zinawasilishwa kwa SMZ.

..waziri wa fedha wa tanzania anawakilisha pande zote za muungano[tanganyika na zanzibar]

..kabla hatujamchambua waziri wa fedha wa zanzibar, labda tungechambua mamlaka iliyomteua--Raisi wa Zanzibar. Je, Raisi wa Zanzibar ana mamlaka gani kimataifa?

..zanzibar leo hii inaweza kabisa kuamua ku-dissolve serikali yake, kama walivyofanya watanganyika, na tukawa na serikali moja ya Tanzania.

..siyo kweli kwamba misaada toka nje inathibitiwa na serikali ya muungano. wafadhili wanapotoa msaada huelekeza ni miradi ipi wameamua kusaidia. kama mradi uko zanzibar fedha hupelekwa huko moja kwa moja.

..kama unakumbuka wafadhili waliwahi kuifungia misaada SMZ wakati ule wakati wa utawala wa Dr.Salmini. huo ni ushahidi tosha kwamba kuna misaada ya Zanzibar ni tofauti na misaada ya Tanzania Bara.

..wazanzibari mmepewa serikali yenu wenyewe, vilevile mnao uhuru wa kuendesha shughuli za kiuchumi huku bara bila kubugudhiwa.

..wazanzibari waliotajirika huku bara wangeamua kuwekeza huko zanzibar hali ya uchumi na maisha ingebadilika kwa kiwango kikubwa sana. msingejikalia tu mkiota na kusubiri kuchimba mafuta.

Pakacha,

..suala la zanzibar ni nchi au la linategemea tafsiri na uelewa wa katiba na sheria.

..wazanzibari wamepiga kura, kuna Raisi, serikali, bunge,mahakama, wimbo wa taifa, etc etc. kwanini hamjiamini na kuridhika mpaka msubiri kuambiwa na Mizengo Pinda kwamba Zanzibar ni nchi?

..nadhani kauli ya Mizengo Pinda imekuzwa bila ya sababu yoyote ya msingi.
 
ZANZIBAR HAKUNA WAZIRI WA FEDHA au hulijui maana naona unaanza kutuburuza.
 
Mwiba mbona huo mkataba unaudai kwa watanganyika tu.....nadhani mkataba jinsi unavyotakiwa pande zote mbili zinazoingia mkataba zinabaki na nakala yake, sasa kwanini watanganyika ndio walete huo mkataba na sio wazanzibari waitoe ile nakala yao tuione...

Hebu tuambieni ni wapi katiba ya ZNZ inasema ZNZ sio nchi, Hebu tuambie niwapi hiyo Katiba ya huo Muungano inasema ZNZ sio nchi, wanachosema ZNZ ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano, jee ni sehemu kama nini ?.

Hivi mtu akichukua vipande viwili vya chuma cha aina moja na kuviunganisha, kikawa kimoja, hivi vile vipande huwa sio chuma?. Na jee inakuaje vitu viwili vaimbiwe vimeungana halafu kufanya kimoja, halafu kimoja kibakie, lakini kiambiwe sio tena kitu.

Hakuna Muungano ,wala katiba ya Muungano, kilichopo, ni Tanganyika kuitwala ZNZ.

Halafu huo unaoitwa Muungano, si ulikuja kwa makubaliano (mkataba) sasa mbona nyinyi, huo hamuutaji, mnashikilia katiba katiba. Leteni hadharani basi huo mkataba wa Muungano, halafu mtuonyeshe hapao paliposema kwamba ZNZ sio nchi ?.

Wazanzibari Hawaitambui hiyo katiba ya Muungano, wanachokijua ni Mkataba wa Muungano wa Karume na Nyerere ambao haukutekelezwa tokea day one, na hakuna cha kudai haki wala nini kutoka Tanganyika. Hayo mtayajua nyinyi.

Wazanzibari wanachotaka, ni kwamba Mkataba wa Karume na Nyerere upelekwe katika baraza la wawakilishi, na ikionekana kwamba umekiukwa ,basi nikutangaza kwamba hakuna cha Muungano.

Mimi nawapa challange kama mnaamini ZNZ sio Nchi, wekeni hadharani mkataba wa Muungano, mbona hili hamlitaki, mmeshikilia katiba ,Katiba viraka.

Katiba ya ZNZ,kwa ZNZ ndio iliojuu, na ndio yenye haki ya kuamua lolote kuhusu ZNZ ,kuhusu lolote. Baraza la wawakilishi ndio lililojuu kwa ZNZ na ndio lenye haki ya kuamua lolote kuhusu ZNZ. Kwa hiyo na huo muungano wenu, basi sasa lazima baraza la wawakilishi liutolee maamuzi,na maamuzi yenyewe ni kutangaza kwa ulimwengu kwamba hakuna cha muungano wala nini.

Katiba ya muungano hatuitambui, pakuanzia ni mkataba wa Nyerere na Karume kama upo,kama haupo ndio hivyo tena itakua pono kwa ubua.
 
Msiwe na shaka na maneno ya Mbuzileeni. He is right in a wrong way, ni prototype ya Bw. Pinda. Katiba alizonukuu zina vifungu vingi mno, sio hicho kimoja alichochomoa dondoo yake hiyo maarufu. Angeisoma katiba kwa ujumla wake, kama mwanasheria mahiri angeona pale ambapo wanasheria mahiri wenzake wamepaona. Katiba ambazo tayari zinajipinga zenyewe haziwezi kuchukuliwa kamwe kuwa ndio vitabu vitukufu vya rejea (Basic Documents) kama wanavyofanya wao. Hilo la awali na la msingi katika mada hii.

La pili, ambalo angepaswa kulisemea kama kweli Mbuzileeni hana ajenda ya siri dhidi ya Zanzibar. Angeangalia issue kubwa katika jambo hili ambayo ni Muungano sio Katiba, wala sio maneno Zanzibar si Nchi au kinyume chake. Mtu yeyote wa kawaida (layman) akinasibisha Zanzibar na Katiba ya Muungano, jibu lake ni kuwa Zanzibar si nchi. Kwa sababu hiyo Katiba (sio Muungano) imeiua Zanzibar kwa makusudi kinyume na (Makubaliano ya) Muungano. Na hio ndio main issue hapa. Na hapa ndipo wasomi wanapomparamia Pinda, kama mwanasheria, kuwa si mweledi wa mambo, jambo ambalo kama yeye ni mwanasheria ni muhali kulifanya. Kosa hilo hilo analirudufu Mbuzileeni. Lazima nae tumshangae mara tatu!!!

Jambo la tatu, Mbuzileeni angeangalia mamlaka na mfumo mzima wa SMZ tangu baada ya Muungano kupitia kufa kwa Karume, kufa kwa ASP, pale 1977 hadi leo. Mfano: Mwaka 1967, miaka mitatu kamili baada ya Muungano, Zanzibar ilijiunga na East African Community baada ya kuasisiwa, kama Zanzibar, chini ya sheria za Zanzibar huru, kinyume na anavyodai yeye kuwa watu hawaijui historia yao. Anajicheka mwenyewe. Cha ajabu, baada ya Karume kufariki, Jumuia hiyo ilivyovunjika, pale 1977, ilivunjika ikiwa na memba watatu (Zanzibar ndani ya Tanzania). Hapa panazaliwa lile suali tata: Mgao wa Zanzibar kwenye EAC umeyeyukia wapi, Zanzibar kwenye hazina ya SMZ au hazina ya SMT? Still, kusema hazina ya SMT pia ni tata, kwani SMT, ni Zanzibar na SMT, kwa vile kutaja Tanganyika ni uhaini. Limetajwa hilo pia na Mbuzileeni.

Jambo la nne ambalo kwalo Mbuzileeni tumshangae ni kuwa: yeye binafsi alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa SMZ, kwa nini alipokea uteuzi huo wakati hakuna nchi wala dola ya Zanzibar. Je alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kitu gani, Mkoa wa Zanzibar, Wilaya ya Zanzibar, Kaya au Serikali ya Kijiji? Hili inabidi alitolee ufafanuzi mwenyewe. Je kukubali kwake kuteuliwa na Rais wa Zanzibar na baadae kufanya kazi hiyo kwa ajili ya Zanzibar alivunja katiba ya Muungano? kwani kufanya hivyo ni miongoni mwa vile alivyoviita "Vitendo vya watawala wa Zanzibar kuvunja katiba"
 
Hivi nyie watu humu haya niliyoandika ni upuuzi ama nini? Watanzania tumezoea mpaka kitu kitendeke ndiyo tuanze kulalamika. Haya mambo yataingizwa kwenye katiba ya muungano. Hivi ni kweli watu humu ndani mnayaunga mkono au hamna la kusema. Najua Mkandara unayaunga mkono how about the rest?

Hivi wew mkuu ukileta mjadala ni lazima kila mtu achangie? Hoja haziendi kwa kulazimishana
 
we have to do what we have to do.
ni lazima watu (viongozi) wanaowakilisha pande za muungano wa kae wajadili upya huu muungano?
Tunaogopa nini?
Kama hautekelezeki, uvunjwe, uundwe upya, au nchi zibaki zimetengana.
Au bado viongozi wa bara wanaogopa Zanzibar haiwezi kujiongoza? ni kanchi kadogo (angalia rwanda)
hakana rasilimali kama bara?
mimi siamini naona kama kuna woga wa ukomunisti au ualkaeda.
Wanaogopa nini kukaa?
 
Tukirejea hotuba ya Muungwana wakati anazindua Bunge baada ya kuchaguliwa, moja kati ya mambo muhimu aliyotuahidi ni kushughulikia kero za Muungano. Kwangu mimi huu ni wakati muhimu wa yeye kufanya jambo kubwa kuhuisna na ahadi yake hiyo. Na kwa ushauri wangu, analopaswa kulifanya ni kulipeleka suala hili sasa kwa wananchi walijadili na kufikia muafaka wa nini wanakitaka kuhusiana na Muungano.
Tusihofu kuwa Muungano utavunjia au ukivunjika nani ataathirika zaidi. majadiliano yawe ya wazi ambayo kama wananchi wanapenda kuuvunja Muungano waachwa wafanye hivyo kwa jinsi ambayo wataiona inafaa bila kuathirika.
 
Akijibu swali la Mbunge wa Bububu, Cosmas Masolwa (CCM), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhammed Seif Khatib, alisema ni miaka 44 sasa mambo hayo hayajaendeshwa kimuungano na hajui sababu.
Suala la Bandari ni miongoni mwa kero 22 za Muungano ambazo zimekuwa zikizungumzwa kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi kutokana na sababu mbalimbali. Sababu gani hizo ?
Akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo aliyetaka kufahamu sababu za kuzuia utekelezaji wake, Khatib alisema hata yeye hafahamu na kwamba labda serikali zote zimeridhia.
"Mimi siwezi kujua sababu za kutotekelezwa kimuungano kwa sababu serikali zote mbili zimekaa kimya…labda wameridhia," alisema Khatib

Huyo ni Waziri wa Nchi wa Muungano tena ofisi ya Raisi anashindwa kukwepa suali na anasema hajui,sasa kama yeye hajui ni nani alipaswa kujua.Eti jamani serikali ni kitu gani ?
 
Huyo ni Waziri wa Nchi wa Muungano tena ofisi ya Raisi anashindwa kukwepa suali na anasema hajui,sasa kama yeye hajui ni nani alipaswa kujua.

Umesahau neno Makamu! Kuna tofauti kubwa.
 
mwiba,under-age,

..jaribu kuchunguza shughuli na mamlaka ya zanzibar revenue board na tra-znz.

..fedha zote zinazokusanywa na vyombo hivyo viwili zinawasilishwa kwa SMZ.

..waziri wa fedha wa tanzania anawakilisha pande zote za muungano[tanganyika na zanzibar]

..kabla hatujamchambua waziri wa fedha wa zanzibar, labda tungechambua mamlaka iliyomteua--Raisi wa Zanzibar. Je, Raisi wa Zanzibar ana mamlaka gani kimataifa?

..zanzibar leo hii inaweza kabisa kuamua ku-dissolve serikali yake, kama walivyofanya watanganyika, na tukawa na serikali moja ya Tanzania.

..siyo kweli kwamba misaada toka nje inathibitiwa na serikali ya muungano. wafadhili wanapotoa msaada huelekeza ni miradi ipi wameamua kusaidia. kama mradi uko zanzibar fedha hupelekwa huko moja kwa moja.

..kama unakumbuka wafadhili waliwahi kuifungia misaada SMZ wakati ule wakati wa utawala wa Dr.Salmini. huo ni ushahidi tosha kwamba kuna misaada ya Zanzibar ni tofauti na misaada ya Tanzania Bara.

..wazanzibari mmepewa serikali yenu wenyewe, vilevile mnao uhuru wa kuendesha shughuli za kiuchumi huku bara bila kubugudhiwa.

..wazanzibari waliotajirika huku bara wangeamua kuwekeza huko zanzibar hali ya uchumi na maisha ingebadilika kwa kiwango kikubwa sana. msingejikalia tu mkiota na kusubiri kuchimba mafuta.

Pakacha,

..suala la zanzibar ni nchi au la linategemea tafsiri na uelewa wa katiba na sheria.

..wazanzibari wamepiga kura, kuna Raisi, serikali, bunge,mahakama, wimbo wa taifa, etc etc. kwanini hamjiamini na kuridhika mpaka msubiri kuambiwa na Mizengo Pinda kwamba Zanzibar ni nchi?

..nadhani kauli ya Mizengo Pinda imekuzwa bila ya sababu yoyote ya msingi.

siasa za nyerere zimewaathiri sana watanganyika, hivi umesoma vizuri hiki ambacho umekiandika, naomba nifafanulie ni vipi waziri wa fedha wa muungano anadeal na zanzibar kama ni nchi kamili, na naomba unipe mgao wa misaada katika muungano huu kipercentage ?na unapoongelea zanzibar kupata misaada uelewe ni misaada gani unayoongelea kwasababu zanzibar haina seat umoja wa mataifa na wala haitambulikani huko,inayotambulikana ni tanganyika inayojiita tanzania, tunachokoseana na huu muundo wa muungano ni pale zanzibar inapochukuliwa kutokana na udogo wa eneo na idadi ya watu ambayo ni completely wrong , ZANZIBAR ILIPOUNGANA NA TANGANYIKA HAIKUWA MKOA ,U GUYS MUST UNDERSTAND THAT, ilikuwa ni dola kamili na hivyo mgao wa the so called muungano lazima uwe 50-50, regardless ya ukubwa wa eneo la tanganyika wala population na ndio maana kila siku nasema kwamba solution ya muungano huu ni serikali 3,. na kuhusu zanzibar kudissolve serikali yake si ndio mtaimeza kabisa.hatudissolve ng'o.

ningependa kuendeleza huu mjadala lakini nataraji kupotea kidogo, ninachokuombeni ndugu zangu watanganyika hasa nyinyi wa jf ambao mnaonekana mna upeo wa uelewa. nyinyi ndio tunaokutegemeeni kutusaidia katika mapinduzi haya ya fikira. nakuombeni msifiche ukweli kwa kujali uzawa wenu. penye haki piganieni haki. mimi sikuenda shule lakini ni suala liliopo wazi kwamba muungano huu hauinufaishi zanzibar. hivyo ni vyema mkaacha ushabiki wa uzawa na mkashabikia haki na usawa wa muungano huu.
 
under-age,mwiba,

..nyinyi sijui mnaishi dunia gani. wizara ya fedha ya ZNZ inaongozwa na Raisi Karume, ambapo chini yake kuna waziri wa nchi wa fedha na uchumi Dr.Mwinyihaji Makame Mwadini.

..pia ZNZ inapata misaada na mikopo kama ilivyobainishwa ktk bajeti ya SMZ.

..ZNZ vilevile inapata mikopo toka vyombo mbalimbali hilo nalo limebainishwa ktk bajeti iliyosomwa na Dr.Mwinyihaji.

..nimeambatanisha habari inayohusu BAJETI YA ZANZIBAR kama ushahidi wa hayo niliyoyaeleza hapo juu.

NB:

..vilevile naona umekimbilia suala la kugawana na unataka mambo yawe 50 kwa 50.

..ungefikiria KUCHANGIA sidhani kama ungekuja na hiyo hesabu ya 50 kwa 50.

..Watanganyika tuko milioni 30, wenzetu Wazanzibari ni milioni 2, hatuwezi kuwa na mgao wa 50/50, zaidi hatutugemei mchangie lolote lile kwa asilimia 50%. sijui kwanini mnakuwa wagumu kuelewa kitu kirahisi kama hicho.


Tanzania Daima said:
Zanzibar yatangaza bajeti

na Saada Said

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) jana ilitangaza bajeti yake ya mwaka 2008/09, iliyoipa jina la Bajeti ya Maendeleo, ambayo kama ilivyo ile ya Muungano, imeongeza kodi na ushuru katika bia, vinywaji vikali na sigara.

Akisoma bajeti hiyo katika Baraza la Wawakilishi jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema lengo la kuifanya bajeti hiyo kuwa ya maendeleo, haliishii kwenye maneno matupu.

Alisema ili kuakisi lengo hilo, serikali imeamua kwa dhati mwaka huu, kutenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo tofauti na miaka iliyotangulia.

"Ni bajeti ya maendeleo, kwa maana kwamba sehemu kubwa ya bajeti imeelekezwa kwenye matumizi ya maendeleo kuliko matumizi ya kawaida kama ilivyokuwa katika bajeti zilizopita," alisema waziri huyo wakati akiwasilisha bajeti hiyo jana jioni.

Akitoa takwimu, Makame alisema katika mwaka ujao wa fedha, fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni sh bilioni 42.8, ambazo ni sawa na asilimia 28.7 ya bajeti yote.

Alisema mipango hiyo inatokana na kukua kwa pato la taifa na kutolea mfano sekta ya viwanda ambayo mchango wake katika pato la taifa ulipanda kutoka asilimia 14.8 mwaka 2006 hadi kufikia asilimia 15.4 mwaka 2007.

Alisema kwa sehemu kubwa, ongezeko katika sekta hiyo lipo katika ukuaji wa sekta ya ujenzi, ambayo mchango wa pato lake umeongezeka kutoka asilimia 7.5 mwaka 2006 hadi asilimia 8.8 mwaka 2007.

Alisema kulikuwa na angezeko la asilimia 34.5 katika thamani ya shughuli za ujenzi visiwani hapa, kutoka sh bilioni 38.3 mwaka 2006 hadi sh bilioni 51.5 mwaka 2007.

Waziri huyo alisema kwa kuzingatia ukuaji wa uchumi na malengo ya mpango wa bajeti ya mwaka 2008/2009, serikali imelenga kukusanya mapato ya ndani yenye jumla ya sh bilioni 134.550.

Katika mapato hayo, sh bilioni 124.709 zitatokana na kodi na sh bilioni 9.841 zitatokana na mapato yasiyokuwa ya kodi.

Kwa upande wa matumizi, alisema kwa mwaka wa fedha 2008/09, serikali imepanga kutumia jumla ya sh bilioni 341.709 kwa kazi za kawaida na miradi ya maendeleo kulingana na ukusanyaji wa mapato.

Hata hivyo, alisema kwenye mipango ya makusanyo na matumizi, inajitokeza nakisi ya bajeti ya sh bilioni 207.159.

Akifafanua kuhusu mapato, alisema kuwa serikali inatarajia kupata sh bilioni 23.407 kama misaada ya kibajeti na sh bilioni 8 kutokana na fedha za misamaha ya madeni, na hivyo kupunguza nakisi ya bajeti hadi sh bilioni 175.752, ambazo zitazibwa kwa mikopo na ruzuku.

Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kupokea mikopo yenye thamani ya jumla ya sh bilioni 72.427 na mikopo ya fungate ya sh bilioni mbili pamoja na ruzuku ya miradi ya sh bilioni 101.325.

Kwa upande mwingine, serikali imeamua kuitumia bajeti hiyo, kutimiza malengo yake ya kuzuia matumizi ya kilevi kupita kiasi.

Utekelezaji wa azima hiyo unajionyesha katika viwango vya kodi zilizopangwa kwa vileo. Dk. Mwadini alisema kuwa serikali imedhamiria kuweka viwango vipya vya kodi ya sh 400 kwa lita ya bia na vinywaji vikali na kodi ya sh 500 kwa kila sigara 1,000 zinazoingizwa Zanzibar.

Dk. Mwadini alisema serikali imechukua hatua hizo kama njia ya kudhibiti matumizi yanayoongezeka ya vinywaji vikali na sigara, kutokana na vinywaji hivyo kuathiri afya za wananchi.

"Kutokana na athari za kiafya kwa matumizi ya bidhaa hizi, serikali imekusudia kuchukua hatua za kupunguza matumizi yake na Sheria ya biashara itapitiwa kwa lengo la kupunguza matumizi yake pia," alifafanua Dk. Mwadini.

Akizungumzia hali ya uchumi, waziri huyo aliliambia Baraza la Wawakilishi kuwa uchumi wa Zanzibar umekua kwa asilimia 6.5, hatua ambayo imetokana na kukua kwa pato la taifa.

Akifafanua, alisema kuwa pato la taifa limekua hadi kufikia sh bilioni 588.5 mwaka 2007. Mwaka 2006, ukuaji wa uchumi ulifikia asilimia 6.1.

Kwa upande wa pato la mtu binafsi, nalo limeonekana kukua hadi kufikia wastani wa sh 518,000 kwa mwaka 2007, ikilinganishwa na sh 459,000 mwaka wa 2006.

"Ni matarajio yetu kwamba kwa mwelekeo huu, kasi ya ukuaji wa uchumi itakuwa kubwa zaidi kwa mwaka ujao na hivyo hali za maisha za wananchi zitakuwa bora zaidi," alisema.

Dk. Mwadini alisema sekta nyingine iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa uchumi wa Zanzibar ni utalii. Alisema kuwa kulikuwa na ongezeko la idadi ya watalii walioingia visiwani humo.

Akitoa takwimu, alisema kuwa mwaka juzi, waliingia watalii 137,111, lakini idadi hiyo iliongezeka kwa asilimia 4.5 mwaka jana kutokana na watalii 143,265 walioingia.

Kwa mujibu wa bajeti hiyo, sekta ya huduma za jamii ndiyo inayoongoza kwa mchango katika pato la taifa, na Dk. Mwadini alisema kuwa, mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa umeongezeka na kufikia asilimia 43.9 mwaka 2007, kutoka asilimia 43.5 za mwaka 2006.

Lakini mchango wa sekta ya kilimo umeyumba. Dk. Mwadini alisema kuwa mchango wa sekta hiyo umeshuka kutoka asilimia 30 kwa mwaka 2006 kufikia asilimia 27 mwaka 2007.

Hata hivyo, alisema hali hiyo ilijitokeza baada ya sekta hiyo kuonyesha ukuaji mkubwa katika miaka kadhaa iliyopita ambapo ulifikia kiwango cha asilimia 19 mwaka 2005.

Akifafanua sababu zilizochangia mchango wa sekta hiyo kushuka, alisema kulikuwa na sababu kadhaa, lakini nyingi zilisababishwa na wawekezaji.

"Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya wawekezaji wa kigeni kuhodhi maeneo ya ardhi kwa muda mrefu bila ya kuyaendeleza, tabia hiyo inazuia fursa kwa maeneo hayo kutumiwa na wawekezaji wengine walio makini. Hivyo katika mwaka wa fedha wa 2008/09 serikali imekusudia kukamilisha mapitio ya ada za ukodishaji wa ardhi kwa kuweka viwango," alisema.

Kwa upande mwingine, Dk. Mwadini alisema katika mwaka ujao wa fedha, serikali imedhamiria kwa kiasi kikubwa kutekeleza hatua mbali mbali zilizopitishwa kwa kufanyiwa kazi kwa mwaka wa 2007/08, na kuanzisha hatua chache mpya.

Alizitaja baadhi ya hatua zilizopitishwa mwaka jana na ambazo zitatekelezwa mwaka huu, kuwa ni pamoja na ukusanyaji wa ada ya usalama wa anga, ushuru wa kuongeza ujuzi, kukamilika kwa mapitio na kuanza rasmi kutoza viwango vipya vya ukodishaji wa ardhi, utoaji wa ada maalumu ya biashara kwa vinywaji vikali, bia na sigara.

Alizitaja baadhi ya hatua mpya zitakazotekelezwa kuwa ni pamoja na kupitia sheria ya usajili wa majina ya biashara na kuanza rasmi utozaji wa kodi kwenye majengo.
 
.kabla hatujamchambua waziri wa fedha wa zanzibar, labda tungechambua mamlaka iliyomteua--Raisi wa Zanzibar. Je, Raisi wa Zanzibar ana mamlaka gani kimataifa?

Suali lilikuwa na jawabu likawa ZANZIBAR Hakuna waziri wa Fedha ,umekuja na Raisi wa Zanzibar anashughulikia Uchumi na Fedha ,Waziri Ofisi ya Raisi aneshughulikia Uchumi na Fedha ,Lete jawabu ni nani Waziri wa Fedha ? Hakuna Waziri wa Fedha Zanzibar.

..nyinyi sijui mnaishi dunia gani. wizara ya fedha ya ZNZ inaongozwa na Raisi Karume, ambapo chini yake kuna waziri wa nchi wa fedha na uchumi Dr.Mwinyihaji Makame Mwadini.
Usituburuze Zanzibar hakuna waziri wa Fedha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini
Inaonyesha hujui unachokisoma maana maelezo yako hayana coordination na unachokiandika.
 
mwiba,

..wizara ye fedha ya Zanzibar kwa wakati huu iko chini ya Ofisi ya Raisi. Karume ndiye Raisi wa fedha wa Zanzibar, ndiyo maana Mhe.Mwinyihaji anatambulika kama waziri wa nchi ofisi ya Raisi fedha na uchumi.

..hicho siyo kitu cha ajabu katika historia ya nchi zetu. ni suala la muundo tu wa serikali ambao Raisi anaamua kuwa nao.

..mimi nafikiri ungejifunza zaidi kuhusu maana ya Waziri wa nchi/Minister of State, kabla hujaanza kuleta ubishi.
 
Back
Top Bottom