Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Spika Sitta ameuliza muda mfupi uliopita mbona wanaodai serikali ya TANGANYIKA bungeni ni wabunge kutoka ZANZIBAR?
 
nafikiri wakati umefika watanganyika tirudie historia yetu.. Hakuna haja ya ya kung'ang'ania utanzania wakati hakuna faida tuipatayo huko. Jaribu kulinganisha ni zipi faida za muungano na hasara zake kwa mwananchi wa kawaida. Hawa jamaa wamezoea kutunyonya, tumekuwa tukiwaachia na sasa wanatudharau. Imgine bidhaa zizalishwazo Tanganyika leo hii hugaiwa kwa bei ya kutupwa huko zanzibar. mchele kutoka kyela huuzwa kwa bei ndogo kuliko kule kyela kwenyewe unakolimwa, mfuko wa simba cement znz bei ndog kuliko hata Tanga unakotengenezwa, hali kadhalika kwa umeme. wapo wamejazana tele wakifaidi vinono vya watanganyika, wanasoma mlimani na vyuo vingine vya tanganyika bure kwa gharama za walioa kodi wa tanganyika ilhali serikali yao haichangii lolote kwenye HESALB.Tumewalisha vya kutosha sasa wameshiba ndio wanaanza kutudharau. Ushauri wangu ni kwamba tuanze na yafuatayo:-

kwanza tujenge dhana ya utanganyika niongoni mwetu ili vizazi vyetu vijitambue kwamba ni watanganyika na sio watanzania bara.

pili tugomee hali yeyote ya udhalilishaji na uoneaji kama uliondikwa mwanzoni mwa mjadala huu

tatu tutetee maslahi ya watanganyika popote pale bila uoga pale inapoonekana wazanzibari wanataka tugawane vyakwetu.

Kwa kufuata hayo kwanza baadae ukweli utakuja kuoneana kuwa muungano hauna manufaa kwetu kwa wakati huu na tutauvunjilia mbali
 
Masikini Tanzania yangu........unyang'au unaneemeka, uzalendo unazikwa.....

Tanzanianjema
 
Kama unaona muungano hauna maana na Tanganyika ndio suluhu ya unayoona kuwa ni udhalilishaji na usumbufu, ni vyema ukafutilia mjadala wa bunge wa wizara ya sheria na katiba kwa siku ya jana na leo.......

Tanzanianjema
 
nafikiri wakati umefika watanganyika tirudie historia yetu.. Hakuna haja ya ya kung'ang'ania utanzania wakati hakuna faida tuipatayo huko. Jaribu kulinganisha ni zipi faida za muungano na hasara zake kwa mwananchi wa kawaida. Hawa jamaa wamezoea kutunyonya, tumekuwa tukiwaachia na sasa wanatudharau. Imgine bidhaa zizalishwazo Tanganyika leo hii hugaiwa kwa bei ya kutupwa huko zanzibar. mchele kutoka kyela huuzwa kwa bei ndogo kuliko kule kyela kwenyewe unakolimwa, mfuko wa simba cement znz bei ndog kuliko hata Tanga unakotengenezwa, hali kadhalika kwa umeme. wapo wamejazana tele wakifaidi vinono vya watanganyika, wanasoma mlimani na vyuo vingine vya tanganyika bure kwa gharama za walioa kodi wa tanganyika ilhali serikali yao haichangii lolote kwenye HESALB.Tumewalisha vya kutosha sasa wameshiba ndio wanaanza kutudharau. Ushauri wangu ni kwamba tuanze na yafuatayo:-

kwanza tujenge dhana ya utanganyika niongoni mwetu ili vizazi vyetu vijitambue kwamba ni watanganyika na sio watanzania bara.

pili tugomee hali yeyote ya udhalilishaji na uoneaji kama uliondikwa mwanzoni mwa mjadala huu

tatu tutetee maslahi ya watanganyika popote pale bila uoga pale inapoonekana wazanzibari wanataka tugawane vyakwetu.

Kwa kufuata hayo kwanza baadae ukweli utakuja kuoneana kuwa muungano hauna manufaa kwetu kwa wakati huu na tutauvunjilia mbali

Mtenda akitendewa, Hujihisi kaonewa.
 
Muungano sio hauna faida bali hauna faida kwa WaTanganyika na WaZanzibar ,wanaofaidika ni wale unaowasikia wakisema na wengine wakiapa au kuapishwa kuwa wataulinda Muungano,hao ndio wanaofaidika,kwani si umeviona hivi vita vya maneno ni baina ya vigogo na magome wenyewe kwa wenyewe,mimi na wewe tunapoiga debe tu ,tukijibanza kila mmoja upande wake,yaani kama tupo kwenye ngumi na tunashangilia au kusema mpige kichwa ,mrukie ,mwangushe.
Wenyewe wanajua wanachopigania,zaidi wanaopambana kama umefuatilia tokea mwanzo ni CCM Butiama against CCM KisiwaNdui au wahafidhina,hao ndio wanaofaidika ,wengine au vyama vingine vinatazama tu anaelemewa wanajaribu kumnyanyua nafikiri uminielewa.
 
msikonde haya mambo yatapatiwa ufumbuzi mapema tu

JK yumo akipanga mikakati ya kulikabili hili
 
vilevile naona umekimbilia suala la kugawana na unataka mambo yawe 50 kwa 50.

..ungefikiria KUCHANGIA sidhani kama ungekuja na hiyo hesabu ya 50 kwa 50.

..Watanganyika tuko milioni 30, wenzetu Wazanzibari ni milioni 2, hatuwezi kuwa na mgao wa 50/50, zaidi hatutugemei mchangie lolote lile kwa asilimia 50%. sijui kwanini mnakuwa wagumu kuelewa kitu kirahisi kama hicho.

Naona hao wapigania ukombozi wa Zanzibar hili wamelikwepa!!!!!!
 
Muungano unatakiwa marekebisho ili bara wapate nafasi wanayostahili kwenye manufaa ya muungano huo..Sambamba na visiwa vya Unguja ,Pemba nk...Lakini Muungano kuvunjika ni NDOTO YA MCHANA SAA SITA!
 
Muungano unatakiwa marekebisho ili bara wapate nafasi wanayostahili kwenye manufaa ya muungano huo..Sambamba na visiwa vya Unguja ,Pemba nk...Lakini Muungano kuvunjika ni NDOTO YA MCHANA SAA SITA!
Muungano kuvunjika ni jambo ambalo huwezi kulitegemea labda unaweza kufananisha na kikombe au gilasi inayokuponyoka bila ya kuitegemea na hata harakati zako za kuidaka huwa hazina wakati utaona imeshafika chini na kuvurugika unabaki kutafuta fagio na kukusanya magae.
Ukiitazama Russia hakuna alietegemea kama itasambaratika na kwa nguvu ambazo Mrusi anazo si mimi wala wewe tuliokuwa na mategemeo kama vijinchi viduchu viduchu vingeweza kujipapatua ndani ya Shirikisho la Rusia ,lakini Mungu si Asumani vinchi hivyo vimejipapatua na leo vina viti ndani ya Umoja wa Mataifa ,sasa tofauti kubwa utakayoiona ni kuwa Zanzibar ni Nchi ambayo ilikuwepo kabla ya Tanganyika au iliasisiswa kabla ya Tanganyika ni rahisi sana kujipapatua ndani ya Muungano ambao upo wazi na unajulikana kuwa hizi ni Nchi mbili na zote viti vyake katika umoja wa Mataifa vipo wazi kwa maana siku wakiamua kujikata basi hawatahitaji kuomba kujiunga na Umoja huo maana viti vyao havijafutwa wala hakuna aliepeleka maombi ya kuvifuta ili kibakie cha Tanzania (Nchi ya kubuni).
Tuchukulie wale wenye sera za serikali tatu ,hawa ni kuwepo kwa Tanganyika ,Zanzibar na Tanzania,hawa wanadai kuwa ni lazima iwepo Tanganyika ,iwepo Zanzibar ndipo ipatikane Tanzania bila ya kuwepo Nchi mbili za asili hakuna la maana katika Muungano huu ni ubabaishaji tu.
Sasa ikiwa wenye mrengo wa serikali tatu watafanikiwa kuwashawishi WaTanganyika na WaZanzibar kuwaondoa mafisadi madarakani basi viti vyao vya umoja wa mataifa watavichukua tena na kuwakilisha nchi zao wala patakuwa hapana pingamizi si FIFA wala Olympic wala Kagame Cup.
 
Spika Sitta ameuliza muda mfupi uliopita mbona wanaodai serikali ya TANGANYIKA bungeni ni wabunge kutoka ZANZIBAR?
Kwa sababu wabunge wa Bara wamekaa kama watu wa mfalme Suleimani yule nabii aliekufa huku amekaa kwenye kiti na bakora yake,wao wakawa bado na woga wa kufanya kazi bila ya kusita mpaka mchwa walipokula ile bakora na Nabii kuanguka wakaona kumbe alikwisha kufa kitambo.
na ndio hivyo bado wabunge wanawoga wa kuitetea Nchi yao kama walivyofanya akina Kikwete na wenziwe waliojulikana kama kundi la G55 ,walipotishwa na Nyerere basi mpaka leo bado wanaona Nyerere yupo hai ,hivyo wanaogopa kunyanyua sauti zao kuirudisha mada ile ndani ya vikao vya bunge,sasa wasubiri mpaka mafisadi wameimaliza nchi na kuiangusha ,hapo ndio wataanza kuulizia. Ipo wapi Tanganyika.
 
Zanzibar ni Nchi ambayo ilikuwepo kabla ya Tanganyika au iliasisiswa kabla ya Tanganyika ni rahisi sana kujipapatua ndani ya Muungano ambao upo wazi na unajulikana kuwa hizi ni Nchi mbili na zote viti vyake katika umoja wa Mataifa vipo wazi kwa maana siku wakiamua kujikata basi hawatahitaji kuomba kujiunga na Umoja huo maana viti vyao havijafutwa wala hakuna aliepeleka maombi ya kuvifuta ili kibakie cha Tanzania (Nchi ya kubuni).

Viko wazi vipi? Kwa mtazamo wako kujiunga na Umoja wa Mataifa ndiyo panacea wa matatizo yetu yote? Mbona Eritrea na Ethiopia wako lakini kila kukicha wako kooni kwa mwenzie! Sitashangaa kuwa tukitengana tukaja gombania kisiwa cha Bongoyo!!!!!
 
Date::8/14/2008
Mbunge: Shamuhuna adhibiwe, suala Zanzibar si nchi laibuka tena Bungeni
Na Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi

MBUNGE wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, ameitaka serikali kumuadhibu Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Ali Juma Shamuhuna, kwa kuonyesha utovu wa nidhamu wa kumkosoa hadharani Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusiana na kauli yake kuwa Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya Pinda kutoa msimamo huo kuwa Zanzibar si nchi, Shamuhuna alidai katika tamko lake ndani ya Baraza la Wawakilishi, Zanzibar ni nchi huku akibeza wale wanaodai tofauti.

Dk. Makyembe ambaye jana alikuwa akichangia hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2008/09, alisema kitendo kilichoonyeshwa na kiongozi huyo wa juu wa serikali ni utovu wa nidhamu na kimeonyesha fedheha kubwa kwa serikali.

Hata hivyo, Dk. Mwakyembe ambaye hakutaja moja kwa moja jina la kiongozi huyo ambaye hivi karibuni alisimama na kupingana na Waziri Mkuu Pinda kuhusu hadhi ya Zanzibar, alisema kwa waziri kupingana na tamko la Waziri Mkuu ni utovu wa nidhamu wa kupindukia.

Alisema kilichotokea ni fedheha kwa serikali kwa kuwa Waziri Mkuu alishatoa tamko bungeni, lakini kichekesho kinakuja pale waziri anasimama na na kumkejeli.

Pia Dk. Makyembe alihoji serikali ipo wapi na usiri wa serikali ikiwa ni pamoja na vyombo vya mawasiliano kama vimeenda likizo kwa kushindwa kumshughulikia waziri huyo ambaye alionekana wazi kumkejeli Waziri Mkuu ambaye amekuwa akifuata katiba na tayari alikwisha agiza wanasheria wa pande zote mbili kulishughulikia suala hilo.

"Waziri wa Zanzibar kumkosoa Waziri Mkuu ni utovu wa nidhamu kwa viongozi wetu, mimi hapa sioni kama kuna mgogoro wowote wa kikatiba ninachoona ni fedheha kubwa kwa serikali yetu, baadhi ya viongozi wa serikali. Ninachoomba adhibiwe, asipoadhibiwa mimi sioni ajabu siku moja Rais akinyooshewa kidole machoni," alionya Mwakyembe.

Alisema endapo Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi wa Baraza la Mawaziri akiamua jambo na kulitolea ufafanuzi, hairuhusiwi kwa waziri yoyote kupinga maamuzi hayo, kwani kwa kufanya hivyo ni kutoheshimu kiongozi huyo na ni utovu wa nidhamu.

Mjadala wa Zanzibar si nchi au la umezidi kuchukua sura mpya kila kukicha.

Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge Samuel Sitta, jana tena alimuokoa tena Waziri Mkuu Pinda, kutumbukia katika mjadala wa ama Zanzibar ni nchi au la, baada ya kuweka msimamo kwa kutaka wabunge wasiulize tena hoja hiyo katika Bunge linaloendelea.

Sambamba na hilo, Spika Sitta alijikuta akilazimika kujibu maswali ya wabunge waliokuwa wakionekana kuendeleza hoja hiyo ya Zanzibar ni nchi au la, huku pia akimtaka Katibu wa Bunge, asirudie kupanga wabunge wengi kutoka visiwani Zanzibar katika orodha ya wabunge wanaotaka kumuuliza waziri mkuu, maswali ya papo kwa papo.

Aliyeibua tena mjadala huo alikuwa ni mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Sulemain Khalifa, ambaye alitaka kauli ya serikali kuhusu azimio la mkutano wa 16 lililoazimia pamoja na mambo mengine, kuundwa kwa serikali ya Tanganyika lililotolewa mwaka 1993 na kuomba alisome lote, jambo aliloruhusiwa na spika.

Hata hivyo, badala ya kumruhusu Waziri Mkuu Pinda ajibu swali hilo, spika Sitta alisimama na kusema:, "Mimi nalitafsiri hili ni kama njia ya kwenda katika hoja ya kwanza ya Zanzibar si nchi au la, wakati Waziri Mkuu ameshalitolea maamuzi jambo hili lisingestahili kwa wakati huu, hapana silikubali hata kidogo, mheshimiwa Waziri Mkuu wala usijibu hili,"alisisitiza Sitta na kuongeza:

"Zanzibar kuna serikali, kuna Rais, kuna Baraza la Mawaziri, hivi hii hoja ya Zanzibar si nchi ina kitu gani kwa Wazanzibari? Kutaka serikali ya Tanganyika basi suala hili litoke kwa Watanganyika wenyewe, leo Wanzanzibari wanataka serikali ya Tanganyika kwa nini, kuna kitu kinajificha hapa, hawa wenzetu wana hoja gani hasa wanayoimaanisha," alihoji Spika Sitta.

Mara baada ya Spika kujibu hoja hiyo, Mbunge wa Mkanyageni, (CUF) Habibu Mnyaa, alisimama na kutaka kuuliza swali, lakini kabla ya kufanya hivyo, aliuulizwa, na wewe unaenda huko? na kisha Mnyaa akamjibu kuwa hapana yeye alikuwa akiuliza swali lingine.

Hata hivyo, hali haikuwa kama alivyoahidi kwani alionekana kutumia ujanja kwani baada ya kupatiwa nafasi, alihoji ni chombo gani kinatambulika kisheria kinachounganisha Muungano, jambo lilofanya ukumbi mzima kutamka kuwa ni 'yaleyale'.

Kufutia swali hilo, Sitta alisimama kwa mara nyingine na kulazimika kutoa ufafanuzi tena na kusema katika utaratibu kama hoja ikishajibiwa na kutolewa maamuzi katika mkutano unaoendelea, haistahili kujadiliwa tena.

Sitta alisema ni dhahiri kabisa jibu lililowazi Makamu wa Rais anatoka Zanzibar ambaye ndiye mwakilishi wa Zanzibar, kwani hata wakati Rais anaposafiri yeye ndiye anamkaimu hivyo kuendelea kuhoji suala hilo haileti maana.

Mara baada kujibu hoja hiyo, wakati huo Waziri Mkuu akiwa amesimama katika eneo lake la kujibia maswali, Spika alimwita mbunge mwingine, Dk Tarab Ally Tarab, mbunge wa Konde (CUF), ambaye aliuliza swali lililofuata na kushangazwa jinsi Katibu wa Bunge alivyopanga orodha hiyo ya wabunge wanaotakiwa kumuuliza maswali Waziri Mkuu, kwa jinsi wote walivyotoka visiwani Zanzibar.

"Leo katibu amewapanga wale wale, kweli usirudie mchezo huu, hoja hii imeshajadiliwa, lakini hawa wenzetu bado wanaturudisha nyuma," alisisitiza Spika na kuhoji kama Wanzanzibari hao wana hoja gani iliyojificha ndani yao mpaka wakashupalia suala hilo la kuundwa kwa serikali ya Tanganyika badala ya kuwaachia Watanganyika wenyewe.

Dk Ally alimuuliza Waziri Mkuu Pinda, atawahakikishia vipi wananchi wa Zanzibar kila raia mwenye sifa za kupiga kura atapatiwa haki hiyo na kudai kuwa yeye kama mbunge alinyimwa haki yake ya kupiga kura mwaka 2005 katika uchaguzi mkuu baada ya kushindwa kuona jina lake katika daftari la wapiga kura.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alishindwa kujibu swali hilo na kusema kuwa swali hilo linaleta utata kwa kuwa ukilitazama tu unagundua halina maana kwa kuwa muuliza swali alionekana wazi kuficha baadhi ya vitu ambavyo aliamini ni kutokana na Spika kukataza hoja ya Zanzibar isijadiliwe hivyo kumtaka muuliza swali aliweke vizuri swali lake.

Naye Mbunge wa Chambani (CUF), Salimu Hamisi, alimuuliza Waziri Mkuu kwa nini viongozi wa siasa wanaingilia matokeo ya uchaguzi na kutoa mfano wa Tume ya Uchanguzi Zanzibar (ZEC), kuwa ilishawahi kukiri inaingiliwa katika matokeo yake, je, serikali inasemaji kuhusina na hilo na Waziri Pinda alimjibu kuwa inaonekana muuliza swali kuna kitu ameshindwa kusema kwa kuwa hana hakika mbunge huyo alikuwa anataka kusema nini hasa.

Kwani serikali ya Zanzniaba ina tume yake ya Uchaguzi na kama imekiri kuingiliwa basi zipo njia za kupeleka malalamiko hayo huko.

Hata hivyo, mara baada ya kipindi hicho cha maswali ya papo kwa papo kuisha, Mbunge wa Mkanyageni, Habibu Mnyaa alisisimama na kuomba muongozo wa Spika kwa kutumia kifungu namba 68 (7), na kusema kwa kuwa si kazi ya Spika kujibu maswali ya wabunge inakuaje mbunge aulize swali na kujibu Spika? na kwamba hakuridhishwa na majibu hayo hivyo kuomba muongozo afanyaje ili maswali yao yaweze kujibiwa na mtu anayestahili.

Sitta alisimama tena na kumjibu mbunge huyo kuwa ni kweli kazi ya spika si kujibu maswali ya wabunge, lakini inapotokea hoja imeshatolewa ufafanuzi na spika akaona kuna baadhi ya watu wanaendeleza usumbufu, kiti alichokalia ni imara hivyo hataruhusu mambo hayo yatendeke.

''Kiti ni imara na tutaendelea na msimamo huo huo, nawaomba wenzangu akiwemo Naibu Spika, Wenyeviti, Job Ndugai, Zuberi Maulid na Jenista Mhagama, wote tuwe na msimamo huo huo,'' alisistiza Spika Sitta.

Mjadala kuhusu hadhi ya Zanzibar uliibuka katika mkutano wa Bunge unaondelea baada ya Pinda, kusema Zanzibar haiwezi kujiunga na Jumuiya za kimataifa kama ile ya Kiislam (OIC) au Afrika Mashariki (EAC), kwani si nchi.
 
Kwani Pinda amekuwa Mungu mpaka asikosolewe hadharani kama kakosea? 😕
Hao mafisadi waliokupua mabilioni ya shilingi mpaka leo bado hawajaadhibiwa kwa sababu ya kutaka kuwalinda ili kulinda hadhi ya chama cha mafisadi na serikali yake ya kifisadi, lakini mtachukua hatua za haraka ili kumuadhibi Mbunge kwa kumkosoa 'kiongozi asiyestahili kukosolewa hadharani'!!! Endeleeani kutoa adhabu kwa wale wasiostahili na kuwalinda mafisadi lakini mkae mkijua za mwizi ni arobaini.
 
Yap is about time huyo waziri wa Zenj ashikishwe adabu

Na wakati huo huo mafisadi wakiendelea kupeta!!! Mwe!!! Wacha mafisadi waendelee kuwa na viburi vya hali ya juu maana priorities zetu zimekaa kichwa chini miguu juu
 
Hao SMT, kupitia vyombo vyake vya dola ndio wana wajibu wa kuwashikisha adabu mafisadi, Wanasiasa(wabunge) wameshaweka taarifa hadharani.
 
Hivi yeye si ndie aliyesababisha Lowasa kutimuliwa Uwaziri Mkuu ,sababu Mwakiyembe ndie alimkosoa na kumkashifu ,inakuwaje kiongozi anapoelezwa ukweli aseme ni ukosefu wa adabu .kama hivyo ndivyo basi yeye Mwakiyembe nae hana adabu.Huyu si ndie aliesema kuna mambu ameyawacha na kama angeyaandika kwenye tume na kaimati basi serikali au wengine wangeumbuka ,hivyo aliitumia nafasi ya Tume kuwakandamiza wengine na kuwalinda na kuwahifadhi wengine ,Mwakiyembe ameidanganya Bunge na Taifa kwa kutoa taarifa iliyochujwa.Na kwa mtazamo huo uwajibikaji wa WaZiri Mkuu Lowasa ni batili.
Sura za akina Mwakiembe ni hatari na watu wa aina hii ambao ni waongo wa kupindukia ,watu ambao misimamo yao ni ya kujipendekeza hawafai katika jamii na inafaa waepukwe ,watu kama akina Mwakiyembe ni wataka sifa na wako tayari kuua kama walivyowaua akina Lowasa na wenzake kwa kuwaficha na kuyaficha mengine wasiyaandike katika taarifa ya tume aliyokabidhiwa.
Mwenyezi Mungu amemuadhirisha Mwakiyembe kwa kauli yake aliyoitoa kuwa kuna mambo amewacha kuyaandika na kumuonesha unafiki wake ,huyu ni mnafiki nambari one.

Na Tausi Mbowe, Dodoma

MBUNGE wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, ameitaka serikali kumuadhibu Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Ali Juma Shamuhuna, kwa kuonyesha utovu wa nidhamu wa kumkosoa hadharani Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusiana na kauli yake kuwa Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya Pinda kutoa msimamo huo kuwa Zanzibar si nchi, Shamuhuna alidai katika tamko lake ndani ya Baraza la Wawakilishi, Zanzibar ni nchi huku akibeza wale wanaodai tofauti.
Dk. Makyembe ambaye jana alikuwa akichangia hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2008/09, alisema kitendo kilichoonyeshwa na kiongozi huyo wa juu wa serikali ni utovu wa nidhamu na kimeonyesha fedheha kubwa kwa serikali.
Hata hivyo, Dk. Mwakyembe ambaye hakutaja moja kwa moja jina la kiongozi huyo ambaye hivi karibuni alisimama na kupingana na Waziri Mkuu Pinda kuhusu hadhi ya Zanzibar, alisema kwa waziri kupingana na tamko la Waziri Mkuu ni utovu wa nidhamu wa kupindukia.
Alisema kilichotokea ni fedheha kwa serikali kwa kuwa Waziri Mkuu alishatoa tamko bungeni, lakini kichekesho kinakuja pale waziri anasimama na na kumkejeli.
Pia Dk. Makyembe alihoji serikali ipo wapi na usiri wa serikali ikiwa ni pamoja na vyombo vya mawasiliano kama vimeenda likizo kwa kushindwa kumshughulikia waziri huyo ambaye alionekana wazi kumkejeli Waziri Mkuu ambaye amekuwa akifuata katiba na tayari alikwisha agiza wanasheria wa pande zote mbili kulishughulikia suala hilo.
"Waziri wa Zanzibar kumkosoa Waziri Mkuu ni utovu wa nidhamu kwa viongozi wetu, mimi hapa sioni kama kuna mgogoro wowote wa kikatiba ninachoona ni fedheha kubwa kwa serikali yetu, baadhi ya viongozi wa serikali. Ninachoomba adhibiwe, asipoadhibiwa mimi sioni ajabu siku moja Rais akinyooshewa kidole machoni," alionya Mwakyembe.

Alisema endapo Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi wa Baraza la Mawaziri akiamua jambo na kulitolea ufafanuzi, hairuhusiwi kwa waziri yoyote kupinga maamuzi hayo, kwani kwa kufanya hivyo ni kutoheshimu kiongozi huyo na ni utovu wa nidhamu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom