Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Lakini ni sisi ndiyo tunaoutaka muungano zaidi kuliko wao. Ndiyo maana CCM inashindwa kutatua suala la Zanzibar. Kama hatufaidiki kwa nini tunazidi kung'ang'ania muungano wakati wenzetu hawataki. Sijawahi hata siku mmoja kusikia kiongozi wa bara akitamka wazi kuwa hatutaki muungano lakini Wanzanzibar wako too open kuwa muungano hauna faida kwao tena.
 
Mtikila kasema mara kibao.
 
sisi kina nani? u mean CCM bara ndo wanataka muungano zaidi? as far as am concerned wananchi wa kawaida hatuna mshawasha wowote na muungano.
 
Wengi wao hapa wanabishana kama nani zaidi, bara au visiwani

Mmeshindwa kujadili kitu cha msingi.

Huwa najiuliza kuna nini huko visiwani mpaka tukung'ang'ania hivi? Nchi yetu Tanganyika ina kila kitu lakini tukisikia tu visiwani wana uwezo wa kuwa na kitu hiki basi hata kulala macho hatulali.

Tumekua kama watoto wadogo ambao tumepewa kila aina ya toys lakini kesho tukimuona mtoto mwingine ana toy moja tu ambayo hatuna tutawalilia wazazi ili tununuliwe.

Kuna alamasi, dhahabu, Tanganite (siyo Tanzanite), chuma, makaa ya mawe, magadi,phosphate,gesi, mpaka uranium. Kama hizi zitakuwa ni suala la Muungano basi na mafuta nayo yanastahili yawe ni suala la Muungano vinginevyo La. Kwa bahati mbaya ulipitishwa uamuzi kuwa mafuta ni suala la Muungano na kuyaacha kuyafikiria madini mengine. Ni sahihi (kama wanavyoona Wazanzibari) kutengua uamkuzi huo na kusema mafuta si suala la Muungano kama yalivyo madini mengine. Hiyo ndiyo haki na usawa.
 
Mzee Mwanakijiji umenikuna! Hawa Wazanzibari wanaota ndoto za mchana za utajiri, sasa wameipata. Ooh Mafuta ya Zanzibar ni ya Zanzibar; mara Ooh zama za kutishana zimeisha, Ooh mafuta ya Zanzibar hayaendi bara mpaka dhahabu ya Mwanza igawiwe Zanzibar! Hawa wala tende wana matatizo kweli kweli! Wanasema hayo huku bara tukilipia starehe zao zote kwa fedha itokanayo na pamba, mpunga, chai n.k. Zama za kuwabeba Wazanzibari zimekwisha - tuwaachie Zanzibar yao ndogo kama wilaya ya Pangani lakini yenye Rais, Waziri Kiongozi, Naibu WK, mawaziri na manaibu wao 40, wakurugenzi na makatibu wakuu zaidi ya 100, viongozi wa siasa zaidi ya 5,000! Kisiwa cha viongozi! Kalagha bhao!

Wacha mtizamo finyu huo. Unajua kuwa wanaosababisha Zanzibar kuwa na viongozi wengi ni nyinyi Bara katika Muungano wenu huu wa kisanii. Kwani Zanzibar inalazimika kuteua viongozi ili wameze ku-match katika vyombo vyenu hivyo mlivyounda Wizara za Muungano, Bunge, CCM, na makorokoro tele tu ambayo hayana faida na Wazanzibari. Jenga hoja.
 
Mr.Zero said:
Lakini ni sisi ndiyo tunaoutaka muungano zaidi kuliko wao. Ndiyo maana CCM inashindwa kutatua suala la Zanzibar. Kama hatufaidiki kwa nini tunazidi kung'ang'ania muungano wakati wenzetu hawataki. Sijawahi hata siku mmoja kusikia kiongozi wa bara akitamka wazi kuwa hatutaki muungano lakini Wanzanzibar wako too open kuwa muungano hauna faida kwao tena.

..Population ya Watanganyika ni zaidi ya milioni 30. wakati Wazanzibari wako millioni 1 na ushee.

..kwa msingi huo, kwa kila Mzanzibari 1 kuna Watanganyika karibu 30.

..Watanganyika, ndani ya Tanganyika, hawawezi kuona athari[mbaya au nzuri] za Muungano kwa kiasi kilekile kama Wazanzibari wanapokuwa kwao.

..vilevile Watanganyika hawashindwi kuwabeba Wazanzibari. kuna mikoa na hata wilaya huko kwetu ambazo ni kubwa kuliko Zanzibar.

..huku Tanganyika malalamiko kuhusu Muungano yatatokana na WANASIASA na siyo wananchi wa kawaida.

..itakapotokea kwamba mwanasiasa wa Tanganyika anaona maslahi yake yanakwazwa na Mzanzibari, au Muungano, basi kampeni za kuvunja Muungano zitaanza kusikika toka bara.
 
Wacha mtizamo finyu huo. Unajua kuwa wanaosababisha Zanzibar kuwa na viongozi wengi ni nyinyi Bara katika Muungano wenu huu wa kisanii. Kwani Zanzibar inalazimika kuteua viongozi ili wameze ku-match katika vyombo vyenu hivyo mlivyounda Wizara za Muungano, Bunge, CCM, na makorokoro tele tu ambayo hayana faida na Wazanzibari. Jenga hoja.

Muungano UFE ,Maana ya muungano umepotea badala ya kutusaidia unaturudisha ktk marumbano ambayo hayana faida na yanaturudisha nyuma.

Angalia muafaka ulivyochukua mda na pesa nyingi.

Waacheni wazanzibar wakalime karafuu na Nazi zao na wakanunue majenerata ya umeme.

Nyie watanganyika nendeni mkachimbe madini yenu,gesi na mkalime pamba,chai,kahawa zenu.

mtu ukiona somo linakua gumu na gharama unajaribu UJINGA.
 
Mwenzenu kuna siku nilitaka kupigwa na rafiki mmoja mwenye asili ya Pemba. Yeye alikuwa anadai Zanzibar ( specifically) Pemba kuna mafuta mie nam-bishia na kumwambia nijuavyo kuna "potential" ya mafuta akaja na hoja hizo hizo za tafiti za miaka 1950 still hizo sites kuzifungua kakuta neno "potential" lakini wapi hatimae almunusra tushikane mashati.

Back to the article kweli siasa SI_HASA sasa baina ya hao "wawakilishi" na Mr Raeding sijui nani ni mtaalam.

Kazi kweli kweli

Masatu,

Umesema vema kabisa; ila tu ni kwamba with current oil & gas prices, hiyo "potential" ya economically viable deposits imeongezeka sana ... ndiyo maana Shell wanasubiri kwa hamu kuanza exploration tena .... wanasubiri kupewa go-ahead baada ya kujua "haya mafuta" ni ya Muungano au ya Zanzibar. Huyo mscot nadhani ameongea zaidi "kiushabiki wa kisiasa", kuliko "kiutaalamu".
 
Nafikiri hapa kwa hali ya sasa tatizo lilopo ni wanasiasa wa bara (Tanzania Bara) kwani utaona kabisa wazanzibar including Karume hawataki muungano, sasa kwa nini tunawang'ang'ania? mtu hataki kuishi na wewe tatizo ni nini? kama mafuta wanayo si basi na sisi tutaendelea kuishi bila shida. Vikao vikubwa vya chama hawa jamaa wanatishia kuvunja muungano, kule Butiama swala la muafaka kati ya CCM-Zanzibar na Cuf, Karume kaongea kwa jaziba mpaka analia anamwambia coton man (Muungwana) kama anataka muafaka basi yeye anarudi Zanzibar na nchi yake. Sasa kweli hapo kuna muungano? na wajumbe wote wa Zanzibar wakawa wanafoka kama nguruwe kapigwa mkuki. It's time tufanye referendum Zanzibar, kama wanataka kuwa nasi au lah
Nionavyo mimi kama Rais ataendelea kutoka CCM hili limuungano litaendelea kuwepo hivyo hivyo kigumugumu lakini huwezijua labda ndio maana walikwenda Butiama kumwambia Mwalimu "Ukisikia tumevunja Muungano usitulaumu, si unaona wenzetu wa huko walivyochoka na 'jimuungano' hili" Koti lishawabana waachiwe walivue. Sawa? Sawasawa.
 
Nani kakwambia Wabara wanalishikilia la Mafuta? Kwenye hiyo semina kulikuwa na Mbara hata mmoja? Au huyo Reading ni mzanaki? Kinachowahangaisha nyie akina Ami sasa hivi hata hamkijui! Kusema mwasema lakini chenga mwaliwa! Hayo mafuta mnayotafuta mtayaweka kwenye Mapakacha? Au mnamsubiri Okello aje tena kuwasaidia kuifukuza hii 'mijitu ya bara' kama alivyofanya kwa ZNP+ZPPP=CUF? Habari za mitaani zinasema ndani ya serikali yenu hiyo ya nchi yenu kuna harufu kali ya Abdulrahman Babu!! Ya kweli hayo???
 
Salma Said, Zanzibar

======================================================

My take;
Mimi nadhani zanzibar ikikosa mafuta kero za muungano na mambo ya kudai nchi yataisha.

Mungu Ibariki Tanzania

1CAD8VQY3.jpg
 
linalowakera wazanzibari sio mafuta , hayo mafuta wanayang'ang'ania wabara zaidi kuliko sie wazanzibari. tunachotaka wazanzibari ni HAKI SAWA KWA WOTE. na naomba muamini kwamba watanganyika mnajiona wajanja lakini bado mnawahitaji wazanzibari kwa kukukomboeni . hamna uwezo wa kuleta mageuzi ndani ya ardhi yenu na hilo lipo wazi kwani mpaka leo ccm inajua fika kwamba haina upinzani ndani ya tanganyika na ndio maana inaushikilia muungano ili iweze kuilinda ccm zanzibar. la kufanya ni kuisupport zanzibar katika mageuzi ili mageuzi ya zanzibar yaweze kuwaamsha watanganyika walio wengi ambao wanaonekana kulala na kulemazwa na siasa za nyerere. mafuta sio big deal, tunaomba uadilifu tu.

ni mzenji halisi-----under age
 
Unde_age,
Hivi nani anatawaliwa na mwingine? Kelel za mafuta kwa JK ni sawa na macho ya chura yasivyomzuia Ng'ombe kunywa maji. Baada ya Karume mkubwa tuambie ni rais gani au mwenyekiti gani wa baraza la mapinduzi amepita bila ridhaa ya bara? Leo hii hamlii mnaomba bara iwasaidie kumaliza tofauti? Nafikiri hukijui unachoongea ni kheri unyamaze, na kwa kukufahamisha tu kwa mfumo wa sasa wa CCM wa kumpata mgombea sahau rais kuja kutoka Zanzibar
 
Kuna mtu aliwahi kusema na mimi naona kuna mantiki flani katika usemi huo kwamba muungano umewasaidia Wazanzibari kuwa na mshikamano kwa sababu umewapa kisingizio cha kuelekeza malalamiko yao. Usingekuwepo mwungano hawa wangekuwa wameshapinduana sijui mara ngapi mfano wa Comoro. Na aliyesema haya alikuwa Mzanzibari.
 
wazanzibar wanataka tuwaache na matuta hewa..watakoma baada ya kuvunja muungano...pemba nao wakajitenga na mafuta yao....alafu nao mwisho wa siku wakashindwa kuyapata...

watanganyika msijali ...mafuta tanganyika yameshapatikana kwa wingi.........
 
linalowakera wazanzibari sio mafuta , hayo mafuta wanayang'ang'ania wabara zaidi kuliko sie wazanzibari. tunachotaka wazanzibari ni HAKI SAWA KWA WOTE. na naomba muamini kwamba watanganyika mnajiona wajanja lakini bado mnawahitaji wazanzibari kwa kukukomboeni . hamna uwezo wa kuleta mageuzi ndani ya ardhi yenu na hilo lipo wazi kwani mpaka leo ccm inajua fika kwamba haina upinzani ndani ya tanganyika na ndio maana inaushikilia muungano ili iweze kuilinda ccm zanzibar. la kufanya ni kuisupport zanzibar katika mageuzi ili mageuzi ya zanzibar yaweze kuwaamsha watanganyika walio wengi ambao wanaonekana kulala na kulemazwa na siasa za nyerere. mafuta sio big deal, tunaomba uadilifu tu.

ni mzenji halisi-----under age

zanzibar pia hakuna upinzani ...kuna mgawanyiko..pemba ..CUF,unguja ..CCM...

huwezi kuiita hiyo kuwa ni hali huru ya kisiasa.....ningeita hivyo kama pemba ccm na cuf wangegawana nusu..na unguja vile vile..lakini sasa hatuchekani...
 
Unde_age,
Hivi nani anatawaliwa na mwingine? Kelel za mafuta kwa JK ni sawa na macho ya chura yasivyomzuia Ng'ombe kunywa maji. Baada ya Karume mkubwa tuambie ni rais gani au mwenyekiti gani wa baraza la mapinduzi amepita bila ridhaa ya bara? Leo hii hamlii mnaomba bara iwasaidie kumaliza tofauti? Nafikiri hukijui unachoongea ni kheri unyamaze, na kwa kukufahamisha tu kwa mfumo wa sasa wa CCM wa kumpata mgombea sahau rais kuja kutoka Zanzibar
jaribu kusoma tena bandiko langu ,nadhani hujalielewa. sijaongelea nani anamtawala mwenziwe bali nimeongelea kelele za wanamageuzi wa kweli (zanzibar) zinavyozimwa kinyemela kwa the so called muungano ili kuwafanya watanganyika wasiamke milele(wanaojihisi wanamageuzi lakini mpaka leo hawajaleta upinzani wowote kwa the so called mafisadi). ndio nakwambieni ili tanganyika ipate mageuzi ni lazima iisupport zanzibar kuletwe mageuzi (ni jambo lisilo shaka kwamba kuleta mageuzi zanzibar ni five second mission). hili sio jambo lililojificha , mageuzi ya kisiasa tanganyika yanahitaji karne otherwise zanzibar ifanye mageuzi ya kisiasa na watanganyika waamke kwa mabadiliko yatakayotokea zanzibar.nakuomba irudie tena post yangu kwa kituo ,utagundua naongelea nini.
 
zanzibar pia hakuna upinzani ...kuna mgawanyiko..pemba ..CUF,unguja ..CCM...

huwezi kuiita hiyo kuwa ni hali huru ya kisiasa.....ningeita hivyo kama pemba ccm na cuf wangegawana nusu..na unguja vile vile..lakini sasa hatuchekani...
hivi cuf ikichukua madaraka leo! je hayo yataitwaje? mabadiliko ya kisiasa au ya uzawa?, kumbuka kwamba pamoja na mgawanyiko wa uzawa lakini bado cuf na ccm ni vyama vya siasa na vina sera zao, hivyo mabadiliko yoyote yatakayoletwa na vyama hivyo yatakuwa ni mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na si vyenginevyo.
suali jengine?
 
Kamateni hii hapa!!! kwenye wenzetu wako desparate!!!

Date::9/19/2008Mafuta Zanzibar: Hata kidogo katika kinibu tutagawana na mengine kujipakaNa Salma Said, Zanzibar

Wawakilishi wa Zanzibar wamesema "hata kama ujazo wa mafuta yanayoweza kupatikana Zanzibar ni sawa na glasi ndogo ya kupimia pombe (kinibu), mafuta hayo ni mali ya Wazanzibari watagawana ili watakaoweza wajipake mwilini".

Kauli hiyo ilitolewa jana baada ya mshauri, David Reading, kueleza kuwa mafuta yanayowezekana kupatikana kisiwani humo ni kidogo na kupatikana kwake ni kwa gharama kubwa.

Mtaalamu huyo kutoka Uingereza aliitwa kwa ajili ya kuishauri Serikali ya Mapinduzi (SMZ) na serikali ya Muungano namna bora ya kugawana rasilimali itokanayo na gesi na mafuta.

Kauli hiyo ya Reading pia imesababisha wawakilishi kuingiwa na chuki dhidi ya Wazanzibari walio kwenye serikali ya Muungano, wakiwaita kuwa ni vigeugeu mithili ya vinyonga na wasiojali maslahi ya Wazanzibari.

Akitoa maoni yake kuhusu suala la mafuta na gesi asilia kwa mshauri huyo mwelekezi, mwakilishi kutoka Chama cha Wananchi (CUF), Najma Khalfan Juma alisema kuwa hata kama mafuta ya Zanzibar yatakuwa madogo kiasi cha ujazo wa glasi ndogo ya kupimia pombe ya haramu ya gongo (kinibu), Wazanzibari watagawana hata ikiwa kwa ajili ya kujipaka mwilini.

"Hata kama watajipaka mwilini au wengine watatumia kama dawa ya kuchulia misuli, itakuwa bora zaidi kuliko suala la mafuta kuwa la Muungano," alisema.

Naye mwakilishi wa kuteuliwa na rais, Ali Mzee Ali, ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, alisukumia shutuma zake kwa mawaziri walio kwenye serikali ya Muungano ambao ni Wazanzibari, akiwaita kuwa ni wanafiki na wanaobadilika kama kinyonga.

"Mheshimiwa mwenyekiti kuna wenzetu ambao wamo katika serikali ya Muungano. Wakija hapa (Zanzibar) wanajifanya ni watetezi sana wa Zanzibar, lakini kumbe ni wanafiki," alilalamika mwakilishi huyo.

"Tabia ya viongozi hao haiwanufaishi Wazanzibari. Viongozi wa Zanzibar wasiwatilie maanani watu wa aina hiyo kwa kuwa wanatanguliza maslahi binafsi.

Baadaye mwakilishi huyo mteule aligeukia vyombo vya habari vya Zanzibar na kusema:

"Kitu cha kushangaza ni gazeti la Asumini ambalo limesajiliwa hapa Zanzibar. Gazeti hili liliwahi kuandika makala ndefu kuelezea umuhimu wa nishati ya mafuta kuwa ya Muungano.

Jambo hili si sahihi kwani Zanzibar hainufaiki na lolote na mapato ya gesi inayozalishwa Tanzania Bara," alisema.

"Ninalo hapa, waheshimiwa wajumbe, gazeti la Zanzibar Leo ambalo limechapisha makala kama ile iliyotolewa katika gazeti la Asumini. Sijui makala hii imepenya vipi mpaka ikatolewa humu; hilo anajua mheshimiwa (Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma) Shamhuna."

Gazeti la Asumini na Radio ya Zenj Fm zinamilikiwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation, ambayo Mkurugenzi wake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Muhammad Seif Khatib.

Mwakilishi huyo alisema mara nyingi wanaojitokeza kutetea maslahi ya Zanzibar wanaonekana wanafanya kampeni ya urais kwa mwaka 2010, huku wengine wakishambuliwa kwa maneno kuwa hawautaki Muungano ama kuwa na ajenda ya siri jambo ambalo anaamini si sahihi.

Ali Mzee aliwataka wananchi na hasa wajumbe wa baraza la wawakilishi kuungana kuwa kitu kimoja katika kutetea maslahi ya Zanzibar na kuachana na watu aliowaita kuwa 'Wazanzibari Maslahi' kwenye serikali ya Muungano.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma aliwataka viongozi wa Zanzibar kutoogopa kufukuzwa serikalini kwa kuitetea Zanzibar kwani mara nyingi mtu anapojitokeza kutetea maslahi ya visiwa hivyo, huambiwa kuwa amechafua hali ya hewa kama ilivyokuwa kwa rais wa zamani wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais, Aboud Jumbe Mwinyi.

"Waheshimiwa tusiogope kunyang'anywa magari," alisema. "Wakitunyang'anya sawa, tutatembea hata kwa miguu lakini lazima tuitetea nchi yetu kwa sababu sisi tumeapa kwa katiba hii (katiba ya Zanzibar) na sio ya Jamhuri ya Muungano."

Akichangia hoja hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji Makame alishabihiana na wenzake, akieleza kuwa katika suala la mafuta hakuna dhamira njema kwa Wazanzibari.

Mwakilishi wa Viti Maalumu (CUF), Zakia Omar Juma alisema umefika wakati sasa kwa Wazanzibari kujikomboa kiuchumi kwa kuungana kutetea mafuta yao kwani mara nyingi Zanzibar inapotaka kujikwamua kiuchumi huwekewa vikwazo na serikali ya Muungano. Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani (CUF), Rashid Seif alisema kwamba inaonekana Zanzibar kuna mafuta ya kutosha na ndio maana watu wa Tanzania Bara (Tanganyika) wanang'ang'ania suala la mafuta kuwa la Muungano licha ya kuwa Wazanzibari wenyewe hawataki.
 
Back
Top Bottom