Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
We sema hutaki muungano kwenda huko na bichwa ka yai! Wakat mataifa makubwa makubwa yanaungana we hutak muungano muone na kitambi chake cha gongo na mbege nyoooo!
 
Watanganyika mbona mmelala?

Visiwani washaanza kupika kampeni kila sehem makanisani, misikitini, kwa ma sheha , kila wilaya na kitongoji na mtaaa

sisi CHADEMA hawataki kutoa tamko vipi?
 
Wakuu hiyo hicho kitufe cha kukubali au kukataa kikuwapi? nataka nikaukatae muungano.
MOD pliz kama possible weka vitufe vya unautaka au la tupige kura.
 
Serikali zote mbili za muungano na ya mapindduzi ni lazima wakubali ukweli kwamba muungano ni tatizo litakalodumu kama uhasama wa Israel na Palestina, Wakubali wafanye jambo sahihi waueweke muungano kwenye mtihani, waitishe kura ya maoni ili muungano upate uhalali wa kuwepo au kuvunjwa.
 
UAMSHO kazi yao kuamsha daku, watu washaamka washakula daku wanasubiri swaumu. wengine wameanza kufunga tayari. Maoni ya Muungano wa MKATABA yanaongoza kwa asilimia 70 kwa mikoa miwili ambayo imeshatoa maoni Zanzibar. UAMSHO wamefanya kazi sio mchezo. Lazima wafanye kazi maana wanalindwa na SMZ. Kule mkoa wa kusini Unguja mkoa maarufu wa wahafidhina, SHURA za UAMSHO zikiendeshwa na CCM ambao walikataa kupiga kura ya NDIO wakati wa kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa. UAMSHO wamewazindua sasa ni vinara wa Kutaka Zanzibar huru. Ya Zanzibar hamuyajui we nyie. Mnasoma Tanzania daima na kuangalia ITV tu. UAMSHO wanafanya sober talks na mawaziri wa SMZ na viongozi wastaafu, hawajitokezi hadharani tu kaka.

Amani Karume: Nakuulizeni wana CCM nyinyi mnaogopa kuamshwa daku? basi msijali wala msiwe na wasi wasi, UAMSHO wanawaamsha waliolala waamke wale daku. Kwani hata ambae hakuzoea kuamshwa kula daku anaamka mwenyewe, siku anayosahau anawaona waamsha daku watu muhimu.

Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza
 
Lula wa Ndali Mwananzela




Toleo la 253
8 Aug 2012
















WAMEIBUKA watu wanadai Muungano wa “kimkataba”. Miongoni mwa hawa ni pamoja na mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar mzee Hassan Nassor Moyo ambaye amewahi kuwa Waziri Bara na Visiwani.
Pamoja naye wamekuwapo viongozi wa kidini na wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao nao – kama watu waliosahau – wanapigia panda “uhuru wa Zanzibar” na kuwa wanataka Muungano wa “kimkataba”. Bado hawajataka kile ambacho sisi watu wa Bara tuko tayari kuwapa – Zanzibar nje ya Muungano. Hatuutaki Muungano wa “kimkataba”!
Sasa, ukiangalia hoja za hawa wanaotaka Muungano wa Kimkataba utaona kuwa zinavutia watu wasiotaka kufikiri tu au ambao wanafikiri kwa kutumia vionjo kuliko chembe za ubongo ambazo Mwenyezi Mungu amewajalia.
Situkani hapa wala sibezi, naelezea ukweli ambao mtu yeyote ambaye anaweza kutumia ubongo wake anaweza kuufikia bila kuhangaika sana. Wanaosema wanataka Muungano wa kimkataba wanataka tuamini kuwa Muungano uliopo sasa ni wa kimahaba (a romantic union).
Sasa mambo ya mahaba kwa kweli hayahitaji makubaliano yenye nguvu ya mkataba. Mambo ya mahaba yanahitaji watu kukubaliana kihisia tu kuwa pamoja na kufurahia maisha yao pamoja bila kuwekeana makubaliano ya aina yoyote.
Muungano wa kimahaba kimsingi ndio unawafanya watu wawe pamoja mwanzoni na wakiamua kuupeleka mbele uhusiano wao huingia katika mahusiano ya kimkataba yaani ndoa.
Wanaodai kuwa wanataka Muungano wa kimkataba maana yake ni kuwa hawatambui Muungano uliopo ambao ni wa mkataba. Hawa wana sababu kubwa tatu ambazo wanazitumia kuhalalisha mtazamao wao: kwamba, Baraza la Wawakilishi halikuridhia wala kutunga sheria ya kutambua Muungano isipokuwa Bunge la Muungano tu; Abeid Karume aliingia makubaliano ya Muungano akiburuzwa na Julius Nyerere huku Mwanasheria wake Mkuu akiwa hana taarifa na kuwa makubaliano ya awali yalivunjwa baada ya kuongeza mambo kwenye orodha ya Mambo ya Muungano.
Nina uwezo na ningeweza kuzijibu zote hizo zote tatu ili kuonyesha kuwa zina makosa makubwa. Lakini kwa vile si lengo langu kuutetea Muungano pendekezo langu nikuwa Wazanzibari wanaotaka “Muungano wa Kimkataba” wamepotea. Sisi watu wa Bara (najua sizungumzii wote wa Bara!) hatutaki Muungano nje ya huu wa mkataba ili tuingie mkataba mwingine ambao hauwezi kuwaridhisha Wazanzibari hawa.
Tutaweza vipi kuwa na mkataba mpya wa Muungano ambao hautaweka orodha ya Mambo ya Muungano – kwani ukiweka tu mambo ya Muungano tutajikuta pale pale tena.
Tutaweza vipi kuingia makubaliano ambayo yatafanya Zanzibar iwe sawa kwa kila hali na Tanganyika bila Tanganyika kujikuta inabebeshwa mzigo mkubwa? Najua wanaopenda “mkataba” huu mpya watataka Tanganyika na Zanzibar zigawane nusu kwa nusu nafasi mbalimbali (za utawala, ubalozi) na hata mapato mbalimbali.
Lakini nina uhakika pia watu hawa hawatopenda kuchangia nusu kwa nusu kuendesha serikali hiyo ya Muungano. Nitapenda tuwe na mkataba mwingine pale ambapo Wazanzibari wanaotaka kugawana “nusu kwa nusu” wawe tayari kuendesha serikali ya Muungano nusu kwa nusu!
Lakini zaidi ni kutambua vile vile kuwa Muungano uliopo tayari ni wa kimkataba njia pekee ya kutoka hapa ni ama kufanya marekebisho makubaliano hayo au kuyavunja. Binafsi napendekeza kuwa wakati umefika kwa Wazanzibari kuyavunja wao wenyewe kabla sisi watu wa Bara hatujawasaidia kuyavunja makubaliano haya.
Haiwezekani watake “Zanzibar huru” na wakati huo huo kutaka “Muungano wa kimkataba”. Haiingii akilini kwa sababu kama Zanzibar itakuwa “huru” na “full sovereignty” itaweza vipi tena kuingia kwenye mkataba?
Je, kuingia kwenye mkataba mwingine wanafikiria itawezekana bila kusalimisha hakimiya hiyo (without surrendering some sovereignty)? Yaani wawe huru halafu wajiunge bado na nchi nyingine? Si tutarudi hapa hapa tulipo sasa? Yaani, pale ambapo Zanzibar iko huru sana na wakati huo huo bado imeungana.
Wanaotaka Muungano wa Kimkataba wanaitaka Zanzibar na bado wanataka Muungano. Hawawezi kuwa na vyote viwili. Sasa kama nilivyosema huko nyuma sisi watu wa Bara tutawasaidia kutoka kabisa kwenye Muungano kwani tayari tumeshawahi kuwa na muungano wa kimkataba na kamwe wenzetu wameshindwa kuridhika. Tanganyika imekubali kufa ili Zanzibar ipate uhai lakini katika uhai wake Zanzibar inaibeza Tanganyika. Wanatuambia “ifufueni Tanganyika”.
Na bahati mbaya wapo watu wa Tanganyika wanaofikiria Zanzibar ikiondoka itarudi Tanganyika; haiwezekani. Nchi yoyote itakayopatikana baada ya Zanzibar kuondoka haiwezi kuwa Tanganyika!
Kwa vile hadi hivi sasa hakuna Mzanzibari hata mmoja – kati ya wale wanaotaka kuvunjwa Muungano – aliyeleta hoja Bungeni ya mswada wa sheria ya kura ya maoni inaonekana labda tuwasaidie.
Tumesubiri kwa muda wa wiki kadhaa kuona kama kuna Mzanzibar mpinga Muungano ambaye ameweza kuthubutu kuleta mswada wa aina hiyo kwenye Baraza la Wawakilishi au hata kwenye Bunge la Muungano ili Wazanzibari wapige kura ya kuamua kuhusu Muungano. Hakuna aliyejitokeza. Na kushangaza zaidi pamoja na yote wanayosema kuhusu kutaka Zanzibar hakuna Mzanzibari aliyeanza kampeni ya kutaka Wazanzibari walioko kwenye taasisi na idara za Muungano kuachia nafasi zao kususia Muungano ili warudi kujenga Zanzibar yao “mpya”; hakuna ambaye amejitokeza kutaka Wazanzibari walioko Bara wawaunge mkono katika kuukataa Muungano.
Ndiyo maana tumeanza hii kampeni ya Let Zanzibar Go. Tuiache Zanzibar iende. Na sisi watu wa bara na wale wengine ambao wanaamini bora Zanzibar ijitoe inabidi tuwasaidie kujitoa (kwani hawana ujasiri wa kuamua kujitoa kiukweli).
Njia pekee ya kufanya hivi ni kwa wananchi wa Bara wanapotoa maoni juu ya “muundo wa Muungano” wasikubali kutaka “serikali tatu”. Kwa sababu serikali tatu ndio MUUNGANO WA KIMKATABA huo.
Watu wa Bara wadai serikali moja, taifa moja! Kama serikali mbili za sasa hazifai na haziwekani kwa hakika serikali tatu itakuwa ni mzigo mkubwa. Njia iliyobakia ni kudai serikali moja na taifa moja.
Kwa sababu kama Muungano wa sasa ambao ni wa mkataba hautakiwi tena, bali Muungano mwingine wa kimkataba basi hakuhitajiki kuwapo kwa Muungano mwingine wowote.








[h=2]chanzo raiamwema[/h]Muungano
 
Nimefatilia sana mijadala ya Wa znz ya kuukataa Muungano...nikagundua kuwa asilimia 99 ya wa Tanganyika wanataka

Muungano, Kwa sababu kuu zifuatazo kutokana na majibu ya Watanganyika...

1-Mkivunja Muungano tutawafukuza waznz wote bara.

2-Mkivunja Muungano mtapata shida sana (inakuhusu nini?)

3-Mkivunja Muungano hamtakuwa na Amani.

Naomba Watanganyika wenzangu vilaza tusitoe vitisho kwa Wa znz ili kuwavunja moyo jitihada

zao za kutaka nchi yao.....unaogopa nini wa znz wakijiondoa ktk Muungano??
 
Si kweli kwamba Watanganyika wanapenda Muungano, wanaipenda Tanganyika yao kupita kiasi. Wanaopenda Muungano ni magamba kwa sababu wanajua wanafaidika katika kuendeleza ufisadi nchini. Hata Muungano ukifa leo Watanganyika tulio wengi tutafurahi sana kuachana na watu ambao siku zote wanataka kutumia huduma mbali mbali toka bara.

Kwa mfano wana deni la zaidi ya bilioni 50 sasa hivi kwa TANESCO lakini hawataki kulipa hata senti moja. Wengi wa wafanyabiashara wa Zenj wanapenda kufanya biashara bara lakini Wabara wakienda kufanya biashara zenj wanakutana na manyanyaso ya hali ya juu wakati mwingine hata kutishiwa uhai wao ndio maana idadi ya wafanyabiasha wa bara Zenj ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya Wazenj walioko bara.


Nimefatilia sana mijadala ya Wa znz ya kuukataa Muungano...nikagundua kuwa asilimia 99 ya wa Tanganyika wanataka

Muungano, Kwa sababu kuu zifuatazo kutokana na majibu ya Watanganyika...

1-Mkivunja Muungano tutawafuka waznz wote bara.

2-Mkivunja Muungano mtapata shida sana (inakuhusu nini?)

3-Mkivunja Muungano hamtakuwa na Amani.

Naomba Watanganyika wenzangu vilaza tusitoe vitisho kwa Wa znz ili kuwavunja moyo jitihada

zao za kutaka nchi yao.....unaogopa nini wa znz wakijiondoa ktk Muungano??
 
Si kweli kwamba Watanganyika wanapenda Muungano, wanaipenda Tanganyika yao kupita kiasi. Wanaopenda Muungano ni magamba kwa sababu wanajua wanafaidika katika kuendeleza ufisadi nchini. Hata Muungano ukifa leo Watanganyika tulio wengi tutafurahi sana kuachana na watu ambao siku zote wanataka kutumia huduma mbali mbali toka bara.

Kwa mfano wana deni la zaidi ya bilioni 50 sasa hivi kwa TANESCO lakini hawataki kulipa hata senti moja. Wengi wa wafanyabiashara wa Zenj wanapenda kufanya biashara bara lakini Wabara wakienda kufanya biashara zenj wanakutana na manyanyaso ya hali ya juu wakati mwingine hata kutishiwa uhai wao ndio maana idadi ya wafanyabiasha wa bara Zenj ni ndogo sana ulinganisha na ile ya Wazenj walioko bara.

Ni kweli kabisa unayosema...hata mm siutaki huu Muungano...

Lakini fatilia mijadala ya hapa Jf utaona hivo vitisho nilivyotaja......hapo ndio napata wasiwasi

kama kweli Watanganyika hawautaki Muungano !!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Muungano upo kwa maslahi ya magamba na si vinginevyo
 
Back
Top Bottom