Muuza CD/DVD za uchochezi akamatwa mkoani Simiyu

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
4,258
Reaction score
1,416
Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limemkamata mtu mmoja akiwa anauza CD/VCD/DVD za uchochezi wa kidini.

Polisi mkoani humo wamesema walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu mtu huyo kujihusisha na uuzaji huo wa CD za uchochezi. Walipokwenda walimkuta mtu huyo akiuza CD hizo ambazo zinawahimiza waislamu kuwadhuru Wakristo.

CD hizo zilionesha watu wanaosadikiwa kuwa waislamu wakiwa wamevalia kijeshi huku wakiwa na silaha za moto.

Ndani yake alisikika mtu mmoja akiongea kwa lugha ya Kiswahili akiwahamasisha waislamu kuwadhuru Wakristo.

Source: Star TV Habari 11.03.2013 (20:00).

My take:
Natoa pongezi kwa jeshi la Polisi mkoani Simiyu kwa kazi nzuri waliyoifanya. Polisi mikoa mingine waige mfano huu wa Polisi Simiyu ili kuleta amani nchini mwetu.
 
Polisi wakiamua kufanya kazi ya kuzuia na kutoa mafundisho kwa wanaodharau amri halali ya dola, wanaweza.
Cha msingi na sisi raia tuwe polisi jamii, tuisaidie polisi kuwastua endapo kutakuwa na uhalifu wa amani wa aina hiyo!
 
Huyu nae wamuhoji wamuachie kwa dhamana, kama alivyoachiwa Mch Mtikila jana!
 
Huyu nae wamuhoji wamuachie kwa dhamana, kama alivyoachiwa Mch Mtikila jana!
Inategemea na kesi aliyoshitakiwa.
Pili inategemea kama hao wadhamini atakuwa nao na watakidhi vigezo vya dhamana.
 
Inategemea na kesi aliyoshitakiwa.
Pili inategemea kama hao wadhamini atakuwa nao na watakidhi vigezo vya dhamana.
Alichokosea huyo muuza CD hakuwa na hata CD moja inayoonyesha viongozi wa Chadema wakipanga mauaji naamini kama angekuwa nayo hata Audio tu inayokashifu Chadema asingekamatwa na Policcm maana Maccm yapo tayari hata kama utachoma makanisa yooote wakati huohuo ukikashifu Chadema....Pale Boko jamaa hata leo wapo wanachochea chuki ila kwakuwa wanamtukana Slaa mpaka leo hawajaguswa kabisa
 
Siku zote jina "Christ" huwa linampa wakati mgumu shetani, hao wanaompinga wakristo wanatumwa na nguvu za shetani
 
very good,polisi isicheke nao awe mkiristo au mwislam kamata weka ndani!
 
serikali ilijipa likizo, naona inaanza kurudi kwa mwendo wa kinyonga
 

Mbn hueleweki? mtoa mada anazungumzia cd,dvd za nn na ww unaongelea nn? ndo maana umefeli ujiandae kurisiti, hayo unayoyayungumza c ungeyaleta kama ww uliyaona umesubiri gari ingine ipite ndo urukie kwa mbele b straight 2ze topic mkuu
 
Kwanza kabisa aliekamatwa ni muhusika mwenyewe amerekodi au ni mmachinga tu anaganga njaa tu mitaani?
Kama ni chinga basi polisi isaidiwe na huyo jamaa wahusika wote wanaoonekana kwenye hiyo Cd wakamatwe haraka sana
Lakini serikali yetu hii ilivyo DHAIFU nna wasiwasi sana hata wahusika hata wakijulikana hawatashikwa kwani hata Ilunga mchocheaji wa hadharani kabisa hajashikwa lakini muuza Cd asiyekuwa na kosa mganga njaa atafungwa
 

Unatoa pongezi bila kujua kama mtu huyo kaadhibiwa kisheria au la?!? Utasemaje utakapomuona mitaani kesho? Mkuu una ugonjwa wa Kitanzania wa kuridhishwa na vitu vidogo sana. Mie nitatoa pongezi nitakaposikia amefungwa jela kifungo si chini ya miaka mitano.
 
Mkuu kufungwa jela hiyo ni hatua ya pili ambayo haiwezi kutimia hadi hatua ya kwanza ya kukamatwa ifanyike.

Kwangu mimi hatua ya kukamatwa ni muhimu zaidi ukiilinganisha na hiyo ya pili au ya tatu kama itakuwepo.
 
Hakika nashukuru sana Wana-Jamiiforums kwa kutoa malalamiko yao hapa jamvini na pia nashukuru sana vyombo vyote vya Usalama kwa kutusikia kuhusu kuzagaa kwa mihadhara, kanda na mengine yanayokusudia kuharibu ama kuvuruga amani hapa Tanzania. Mkifanya vizuri namna hii mtapata support toka kwa wananchi na Imani ya wananchi kwa vyombo vya usalama itarejea.
 
miaka kumi inakaribia kwisha sijui wanaiachaje nchi....walifikiri kugusa vitu sensitive kama ubaguzi udini ni vitu rahisi kuvinyamazisha baada ya kuvianza...
Ninawasiwasi taifa litakuwa vipandevipande...maana makanisa yanachomwa na viongozi wa dini wamekuwa kama Albino hivi wanasakwa na kuuawa...
 
2015 ndo hiyo inakuja sidhani kama kosa lililofanyika litakuja kujirudia jipangeni saana kila mfumo una mwisho wake! Jipangeni upya
 
Polisi wakiamua kufanya kazi ya kuzuia na kutoa mafundisho kwa wanaodharau amri halali ya dola, wanaweza.
Cha msingi na sisi raia tuwe polisi jamii, tuisaidie polisi kuwastua endapo kutakuwa na uhalifu wa amani wa aina hiyo!

Wakiamuua kufanya kazi wanaweza ila hawana ubavu wa kuzuia mikutano ya CCM au shughuli zozote za Magamba
 
...Ndo wanashtuka leo kwamba DVD hzo zinasababisha uchochezi? Sissy!
 
Ili usije hukumiwa kwa kukosa maarifa, ni muhimu sana kufahamu vifungu hivi:
TAZANIA PENAL CODE
CHAPTER XIV
OFFENCES RELATING TO RELIGION
125. Any person who destroy, demage or defiles any place of insult to worship or any object which held sacred by any class of persons with the intention of thereby insulting the religion of any class of any persons or wuth the knowledge that any class of persons is likely to consider such destruction, damage or defilement as an isult to their reliogion, is guilt of misdemeanour.

126. Any person who voluntarily causes disturbance of any assembly lawfully or religion ceremony is guilt of misdemeanour.

127. Every person who with the intentions of wounding the Tresspassing feelings of any person or isulting religion of any person, or with the knowledge that the feelings of any person is likely to be wounded , or that religion of a person is likely to be insulted thereby, commits any tresspass in any place of wordhip or in any place of sepulture or in any palce set apart for performance of funeral rites or as depository of remains of dead, or offers any indignity to any human corpse, or causes disturbance for any person assembled for the purpose of funeral ceremonies, is guilt of misdemeanour.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…