Muuza maziwa aenda jela kwa kulawiti mtoto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Muuzaji maziwa kaunti ya Nakuru amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana wa miaka 8.

Hezbon Mogare, mwenye umri wa miaka 25 alikashifiwa kwa kutekeleza kitendo hicho mwaka wa 2017.

Hakimu mkuu Eunice Kelly akitoa uamuzi wake Jumatano Aprili 3, alisema mahakama ilimhukumu Mogare kifungo cha maisha kwa sababu uhalifu aliotekeleza sio wa kusamehewa.

" Kitendo cha mwanaume huyo kilimtamausha mtoto huyo. Ripoti ya daktari ilionyesha kuwa Mogare alitekeleza kitendo hicho. Hukumu yake itakuwa kama funzo kwa wanaume wengine wenye mazoea kama yake," Kelly alisema.

Mahakama iliarifiwa kuwa mtuhumiwa alimfungia mvulana huyo kwenye nyumba yake kwa siku tatu kutoka Jumamosi Septemba 2, hadi Jumatatu Septemba 4, mwaka wa 2017.

Hata hivyo, mtuhumiwa alikanusha madai hayo akisema familia ya mvulana huyo ilimsingizia tu kwamba alitekeleza kitendo hicho kwani aliharibu piki piki yao alipokuwa akiwafanyia kazi kama kijakazi.

Tuko swahili
 
Ebooh wamnyonge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom