Muuzaji wa konyagi feki arusha atiwa mbaroni

Muuzaji wa konyagi feki arusha atiwa mbaroni

Democrasia

Member
Joined
Feb 1, 2008
Posts
79
Reaction score
3
Jana mchana majira ya saa saba eneo la Tengeru nje kidogo ya mji wa Arusha bara bara ya Moshi kuna mfanya biashara maarufu hapo ajulikanaye kama KIMARIO kutoka ROMBO amakamatwa na zaidi ya katoni mia tano (500) za konyagi ambozo ni FEKI zimekuwa zikiwadhuru kweli wananchi hasa maeneo hayo ambayo yamekuwa yakiuziwa kinyaji hicho.
Sasa wasi wasi wangu ni kwamba, Kwa kuwa tuko bongo na Bongo yetu hii utasikia jamaa kaachiwa huru na kesi inaendelea
Naomba walio karibu wafuatilie kesi hii nami nitakuwa natoa update kila siku wakuu

.........naomba kuwasilisha.........
 
unataka kusema alikuwa anauza machozi ya simba?
 
Dah huyu kweli anahatarisha maisha yetu tunaomba kesi yake isomwe haraka na afungwe maisha jela maana akitoka ataendeleza kamchezo haka, inasikitisha sana siku hizi hata Valuu nazo zimezagaa sana feki bora kunywa bia tu wanashindwa kutengeneza feki.
 
Tena inasemekana "machozi ya kenge" siku hizi ukinywa mchana kweupe unapoteza kabisa site(kuona) ,zimezagaaa sana upcountry kama kanda ya ziwa ndo usisemee ...Value, Nyagi nyingi feki especially kwenye viloba package.
 
Dah huyu kweli anahatarisha maisha yetu tunaomba kesi yake isomwe haraka na afungwe maisha jela maana akitoka ataendeleza kamchezo haka, inasikitisha sana siku hizi hata Valuu nazo zimezagaa sana feki bora kunywa bia tu wanashindwa kutengeneza feki.
kama unataka usinywe ki2 feki ni bora ujinywee bia tu kama ulivyosema maana kuna viwanda vingi vya majumbani vya kutengeneza konyagi na pombe nyingine kali na watengenezaji hao hawana hata mpango wakuacha.hivyo kukamatwa kwa kimario sio mwisho wa safari ya vinywaji feki.
 
kaaazi kwelikweli. hii yote ni kutaka kutajirika haraka. huu ni ufisadi mkubwa sana, kwanza mbaya sana kwa maana unahusisha maisha ya watu! Ni mbaya sana, tunauwana kila siku, kansa za vibofu, figo, koo, zimezidi siku za karibuni, hii inaweza kuwa mojawapo ya sababu!!
 
Na hizo zilizokamatwa ziko wapi? Manake rafiki zangu wa Jeshi la Polisi na wenyewe ni memba wa klabu ya Machozi ya Simba.

Baada ya muda kesi ikishasahaulika zinabakizwa hapo katoni mbili kama kizibiti nyingine mtaambiwa ziliteketezwa
 
Kwa kweli hii inasikitisha sana, nimewahi kwenda kituoni polisi kijenge arusha saa nne usiku na kushuhudia askari wakiwa kwenye negotiations za kuuza lita 40 za machozi ya simba ambazo zlikuwa ni kidhibiti walichokamata siku hiyohiyo kwa mtu mwingine! what a disgusting situation
 
kaaazi kwelikweli. hii yote ni kutaka kutajirika haraka. huu ni ufisadi mkubwa sana, kwanza mbaya sana kwa maana unahusisha maisha ya watu! Ni mbaya sana, tunauwana kila siku, kansa za vibofu, figo, koo, zimezidi siku za karibuni, hii inaweza kuwa mojawapo ya sababu!!
Kwani hizo ambazo si feki hazihatarishi afya ya mnywaji!?
 
Back
Top Bottom