Dah hii GOT mim season 1 tuh ilinishimda.. [emoji28]
Game of Thrones waliipenda wachache kisha ikawa trend sababu dunia imejaa wafuata trend ndo maana ikapata wafuasi wengi, ni kama suruali za modo au skin jeans kwa madem zilivyoingia trend miaka fln. Mm ulevi wangu ni movie, naangalia kuanzia movie za ki-asia, kiafrica, kizugu etc.... lakini sijaona chochote cha kushangaza kwenye GOT, Nadhan kati ya watu walioangalia movies nyingi na mm nipo, sababu kila wiki lazima niangalie movie au drama mpya
Nitakupa dramas hapa ambazo hata waandishi nguli wa movie wanazinyooshea mkono, movie hata kama unajua nn kinafuata bado unakua anxious na kama hujui nn kinafuata basi utatetemeka kabisa
1)Gangs of London
Nimeanza nayo sababu ni movie underrated saaana
2)Billions.
Hii kama hauna akili usiangalie, ila kama una akili utaona season 7 hazitoshi. Imejaa power games, politics, manipulation, spying etc... kama ulipenda house of cards basi jua kwenye power play na politics hio ni cha mtoto kwa billions
3)Breaking bad na Better call saul.
Nmeziweka sehemu moja coz zinahusiana, storyline matata sana
4)Peaky blinders.
Kama ww unapenda hardcore movies hii sio ya kuacha. Kamuangalie Thomas Shelby mule ujifunze maana ya mwanaume wa shoka ni nini.
Hii sitoipa namba kwa sababu ni drop in kwa wanaopenda movie za kiasia, wape pause wakorea kaangalie wachina kwenye Princess Agents, Joy of life na Nirvana in fire (1&2) BTW Princess agents ndio most watched chinese drama huko youtube na baadhi ya streaming sites. Hizo dramas storyline zao zimeenda tofauti kabisa na tulivyozoea wa-asia wanavyoandika na kuigiza achilia mbali Cinematography ya humo
5)Ozark.
Ngoma nyingine Underrated labda sababu akili mingi zimetumika mule.
6)Prison break.
Hapa sitoongea mengi, sikatai prison break ilipata nayo umaarufu kwa sababu zile zile kama za GOT coz ilikua Trend na kama usingeijua basi ulikua huna cha kuongelea na marafiki, tofauti ni kwamba Prison Break ili-deserve huo umaarufu, GOT haikudeserve.
7)Snowfall
Another underrated drama, ila ukiiangalia hutowahi kujutia muda wako
Mwisho nimalize na drama ambayo walianza na story vzr lkn wakaja ku-fuckup mwishoni nayo ni Money Heist, bora wangeishia season ya pili pale wakaiachia hio drama Legacy.
Kwenye zilizo bora size ya kati Unaweza kuongezea na hizi Top Boy, Zero Zero Zero, Tulsa King