Muziki TZ II: Sikinde Vs Msondo Nani Zaidi?

Muziki TZ II: Sikinde Vs Msondo Nani Zaidi?

Heiwezi kuwa bila bila, we sikiliza kibao cha mpenzi Clara, hadi chozi litakutoka....

- Ni kweli mkuu ukitaka kuhumu bendi hizi mbili, sometiems ni vyema ukaenda kwa song by song, kwa kweli hapo Sikinde in the 90s anakuwa hana mpinzani, I mean kuanzia Taxi, Clara mtoto wa Msimbazi Kota, Tufurahi na wana-Sikinde, Kaka Selemani, Usitumie pesa kama fimbo,

- Msondo walikuwa na nyimbo mbili tu yaani "Punguza chenga zako na dana dana", na "Nilikupeleka kwa wakwe zako"

- Lakini kuanzia 2000 ndipo Msondo wakaanza kuibuka na "Binti Maringo" , "Kalunde", "Ukiwa ni mwema" "Wewe bwana harusi", "Mambo hadharani", Sikinde walijibu na wimbo mmoja tu yaani "Isaya mrithi wangu wa baadaye", Msondo ilikuwa juu, lakini sasa hivi wka maoni yangu wote wako chalii!

FMES!
 
Kwa sie tulioishi Mwenge Kijijini miaka hiyo huku Sikinde wakiporomosha mambo pale Silent Inn, Sikinde ni wazi watakuwa juu. Nyimbo kama Uzuri wa Mtu, Neema, Fikirini Nisamehe, Editha, Nalala kwa tabu , n,k ni timeless classics.

OSS walitema cheche pia na mambo kama Homa imenizidia, Marashi ya Pemba, Somboko amba, n.k
 
Acheni kuzungusha maneeno meeeengi..ya nini kurefusha mada?
Jamani. habari ya nani zaidi ni juu ya mwonja ladha! Unajua mtu anaposikiliza music, huwa anachukuliwa mbali na kukumbushwa matukio ya SIKU ZA nyuma, na hicho ndicho kinamfanya apige kura ya NANI ZAIDI.

Wewe Tusker Baridi, au Morani75, nyie ni lazima mtakuwa mmeacha au kuachwa na akina dada WAREMBO, ndo mana mmaguswa na MSONDO bwna....!!!

Pia kuna vitu kama urafiki na mwanamuziki, Ujirani etc, ambapo mnatajwa kwenye nyimbo zao, si unajua mambo ya....Medi Mpakanjia..Muzee ya Pesa!...Baraka Kapuya...mutu ya watu..
 
Last edited:
Acheni kuzungusha maneeno meeeengi..ya nini kurefusha mada?
Jamani. habari ya nani zaidi ni juu ya mwoja ladha! Unajua mtu anaposikiliza music, huwa anachukuliwa mbali na kukumbushwa matukio ya SIKU ZA nyuma, na hicho ndicho kinamfanya apige kura ya NANI ZAIDI.

Wewe Tusker Baridi, au Morani75, nyie ni lazima mtakuwa mmeacha au kuachwa na akina dada WAREMBO, ndo mana mmaguswa na MSONDO bwna....!!!

Pia kuna vitu kama urafiki na mwanamuziki, Ujirani etc, ambapo mnatajwa kwenye nyimbo zao, si unajua mambo ya....Medi Mpakanjia..Muzee ya Pesa!...Baraka Kapuya...mutu ya watu..

Mkuu Mwaly...., ha ha haaaa..... umenichekesha sana mkuu.... yaani kumbe kusikiliza muziki ni lazima kuwe na matukio yaliyotutokea zamani, sasa ina maana sisi tunaosikiliza mziki wa "NGOMA KUBWA" sababu ya mpangilio wa vyombo, sauti na ujumbe ndani yake hatujui muziki au??

Kuhusu hapo kwenye kulinganisha msikilizaji wa Msondo na kuachika/kuachana nadhani hapo Mkuu umecheza pata potea.... kuna nyimbo nyingi Msondo na bendi nyingine zaidi ya kuvunjika kwa penzi mkuu....

hilo la mwisho ukumbuke kuwa mara nyingi wanamuziki wanaita/imba majina ya watu/kampuni kutokana na misaada au michango waliyopokea kutoka kwa watajwa. mimi Morani sio rahisi waniimbe sababu mimi ni mvuja kingo na muziki wao ni kipenzi changu so siwapendi kwa vile wameniimba....

Hilo lenye nyekundu juu ni kukuonyesha main point kwenye posti yako..... uzuri wa bendi unatokana na "Mwonja ladha".... ulianza nalo hilo lakini ukaharibu na pointi nyingine....

Msondo juu....
 
Acheni kuzungusha maneeno meeeengi..ya nini kurefusha mada? Jamani. habari ya nani zaidi ni juu ya mwoja ladha! .

- Mkuu with all due respect, maana ya kua na elimu ni kwajili ya kuitumia hasa katika ishu kama hizi ili kuepuka mijadala ya Yanga na Simba isiyojali record wala dataz, tunaposema bendi ipi zaidi, kielimu tuna maana inayouza na yenye market zaidi kuliko nyingine, kwa sasa ni Msondo Ngoma,

- Huko nyuma Sikinde ndio walikuwa juu zaidi.

FMES!
 
Field Marshal...usijifanye kwamba si mtanzania .....!!!

How can u talk of market na kuuza zaidi,wakati una uhakika kwamba jamaa

zako waswahili na wahindi wana mitambo ya kurudufu kazi za wasanii

vyumbani kwao? Utapataje data za ukweli za mauzo katika mazingira yetu

haya?

We kiri kwamba unapenda msondo mzee...Poleni na misiba kibao ya wasanii

ndugu..Kunani huko msondo?
 
ukitaka kufurahi kila jumamosi njoo uburudike na wana sikinde oyeee....king enock....walikuwa wapo juu sana enzi zao lakini leo hii choka mbaya.sasa hivi sondo wako juu tu ingawa wanamuziki wengi wamefariki.piga ua talaka utatowa.....
 
Wazee wa Sikinde haoo!

Hassan rehani Bitchuka 'super stereo' kulia na Shaaban Dede wakiwajibika usiku wa kuamkia leo kwenye bwalo la maafisa wa polisi oysterbay jijini dar ambapo kila ijumaa wanapiga nyimbo zao za old skul ili kuwaburudisha vijana wa zamani na wa sasa kwa vibao ambavyo nadra kusikika kwenye shoo zao za kawaida
 
Back
Top Bottom