Muziki wa Bongo Fleva umepoteza uhalisia na ladha

Muziki wa Bongo Fleva umepoteza uhalisia na ladha

magnifico

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
11,075
Reaction score
24,634
Namiss ile miaka zinatoka nyimbo kama Siachani Nawe (Baraka Da Prince), Basi Nenda (Mo Music), Sijazoea Masebene (Y Tony). Hizi ngoma hata zikipigwa leo ni kama mpya vile, waimbaji na producers waliumiza vichwa sana.

Muziki wetu hauna utambulisho wetu tena. Ile ladha ya Bongo inapotea kwa kasi kubwa. Mbaya zaidi hata hit song zinazotoka kipindi hiki hazina ubavu wa kusurvive hata mwaka. Siongei kishabiki ila rejea Tetema by RayVanny & Diamond na Uno ya Harmonize kama bado zinamaisha kwenye speaker zako. U-Nigeria umekuwa mwingi ubunifu hakuna tena kwa wote producers na waimbaji.

Sijagusia upande wa Hip Hop huko ndio kabisa wanaita trap siku hizi. Sijui nani aliwadanganya Trap Music is all about "BATA", no more storytelling. Beats za trap nyingi ni tofauti ila zinafanana.(Kama umewahi fanya production utanielewa).

To cut the story short, wanalipua sana kazi zao.
 
Kama nyimbo za kina Baraka de Prince, Mo music eti ndio zilikufanya uone bongo fleva ipo juu na ukaona hao ndo wasanii wa mfano basi nakiri kusema kuwa BADO HUUJUI MUZIKI,,, na una safari ndefu ya kuujua muziki mzuri.

Kamsikilize Q-chillah (hasa katika albamu yake ya kwanza ya Mwana mnyonge), TID wa kipindi kile albamu yake ya Sauti ya dhahabu, Banana Zoro, Prince Dully Sykes, hao ndio wasanii waliokuwa balaa ktk kuleta ladha tamu ya muziki,,, sauti tamu, melodies, lyrics n rhymes.

Nyimbo zao hazikuwa na matusi matusi kama zilivyo sasa na zilitikisa hasa!!
 
tyc,
Keep guessing. Nimeanza kupenda muziki sijapata akili ya kutambua huu unaitwa muziki. Bob Rudala - Nimekuchagua wewe ni moja ya nyimbo nizipendazo. Point yangu sio kuprove mi ni mkongwe, No nataka tu ujue naelewa ninachokisema. Nashukuru kwa kukubaliana nacho.
 
Kila zama na kitabu chake, wako watakaokuja baadae kuzitaja hizi tetema kwamba ndo ilikuwa miziki.

Dah kwangu inaniwia vigumu kukubaliana na hiki ukizingatia kipindi zinatoka hit song tajwa na wadau humu ndani zote tulikwepo na leo imepita miaka ila tulichokisifia kipindi kile ndo tunachosifu leo.
 
Mimi mpaka Leo najiskliziaga old scul too enzi za producer p funk majani na master j album za akina nature akina afande darubini Kali proffesa j awa madogo sikuiz hata siwaelewagi wanaimba nn kila siku kusifia matako tu ya Dada zetu hawana content..mwana fa bdo anatoa mawe huyu mkongwe namuheshimu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imekua too much sasa. Mziki wa zama hizi hauna maisha kabisa.
 
Kama nyimbo za kina Baraka de Prince, Mo music eti ndio zilikufanya uone bongo fleva ipo juu na ukaona hao ndo wasanii wa mfano basi nakiri kusema kuwa BADO HUUJUI MUZIKI,,, na una safari ndefu ya kuujua muziki mzuri.

Kamsikilize Q-chillah (hasa katika albamu yake ya kwanza ya Mwana mnyonge), TID wa kipindi kile albamu yake ya Sauti ya dhahabu, Banana Zoro, Prince Dully Sykes, hao ndio wasanii waliokuwa balaa ktk kuleta ladha tamu ya muziki,,, sauti tamu, melodies, lyrics n rhymes.

Nyimbo zao hazikuwa na matusi matusi kama zilivyo sasa na zilitikisa hasa!!

Miaka kama kumi na... iliyopita huu wimbo ulinipatia mke wangu kipenzi. Nilivyoona hii reply nimekumbuka mbali sana...
Baada ya kuumizwa niliko toka nikaachana na wasichana, rafiki yangu mkuu ikawa ni konyagi(mwenye nguvu) muda wote, kumbe kuna mtu ofisi jirani anaumia juu yangu, haukupita muda nikapata ajali mbaya sana,Mungu mkubwa nikapona.
Alivyo kuja kuniona jirani kiofisi nikamwambia nimepona kufa, akajibu huwezi kufa hadi tuzae mtoto...
Akanizoea sana, akanitamkia lililo moyoni mwake...
Kuna siku nikachukua simu (motorola) yake nikamhamishia kwa Bluetooth wimbo wa busu la pink baada ya kuufuta wimbo wa D'banj maana simu ilikuwa inapokea nyimbo 3 (128mb) tu....
Asubuhi moja akiwa anapiga deki ofisini kwake nilimvamia na kumpiga denda lisilo tarajiwa... Akajidondosha kwenye kiti akabaki amezubaa... Mungu ni mwema tuna watoto wa kutosha...
Ahsante Marlow kwa "busu la pink"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kwangu inaniwia vigumu kukubaliana na hiki ukizingatia kipindi zinatoka hit song tajwa na wadau humu ndani zote tulikwepo na leo imepita miaka ila tulichokisifia kipindi kile ndo tunachosifu leo.

Aisee, ndo maana nasema kila zama na kitabu chake.
 
Back
Top Bottom