MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
MUZIKI WA LEO UMESHINDWA KUWA BORA KAMA ZAMANI
My fellow citizens natumaini mko poa.
Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi. Kwa siku kadhaa nilikuwa kimya hadi wengi wenu mkawa mnaniuliza nini kimenipata. Niwatoe hofu kwamba niko salama kabisa ila kwa sasa nimeona niongeze elimu kwa kujiunga na shule ya uongozi ya Komredi Polepole ambayo haina ada. Jumamosi hii Mwalimu Polepole atatufundisha kuhusu ujamaa na kujitegemea. Hiyo shule kwakweli ni madini matupu yanatolewa. Komredi Polepole adumu.
Kama wiki mbili zilizopita boss wa label ya Koffi Central ambaye ni ndugu wa damu wa Koffi Olomide aitwaye Tutu Robert, aliulizwa na shabiki anadhani ni albamu gani ilikuwa bora zaidi kwa Koffi Olomide na kundi zima la Quartier Latin? Tutu Roba akajibu yeye anaona kiufundi kwa maana ya tungo na mambo ya kimuziki albamu ya V12 ya mwaka 1995 ilikuwa bora zaidi. Hii albamu ndo yenye wimbo Andrada. Ila albamu zilizompa Koffi tuzo nyingi ni Loi na Effrakata. Kwangu mimi komredi Tutu Roba alijibu kisomi sana. Na pia nakubaliana nae kwamba ile albamu ya V12 ilikuwa bora mno. Hadi leo Andrada au Etat Major ya Extra Musica ikipigwa bar huwa inaleta vibe la hatari hadi kwa vijana wa umri mdogo.
Baada ya kusoma majibu ya Tutu Roba nikajikuta naenda mbali na kutafakari zaidi kuhusu muziki. Nikajiuliza kwanini albamu ya V12 iwe bora kuliko zingine zilizotoka miaka zaidi ya 20 baadae? Nikaachana na Koffi na kuanza kurudi kwenye miziki mingine hasa USA. Nikaona kwamba wanamuziki wa leo bado hawajaweza kuvunja rekodi zilizowekwa na wababe wa enzi hizo kwenye utamu wa muziki. Wanamuziki wa leo labda rekodi waliyovunja ni kutengeneza pesa nyingi kuliko kipindi kingine ila kiufundi bado. Kwa mfano kwenye slow jams kuna wakali wa leo ambao wana nyimbo tamu kuwazidi Mariah Carey, Whitney Houston, Boyz II men, na wakali wengine wa zamani. Au kwenye pop kuna mtu aliyeweza kuvunja utamu wa nyimbo za MJ? Tukija kwenye hiphop kuna mambo ya ovyo sana. Tungo nyingi za kishenzi mno. Unaweza google lyrics za vijana wa leo ukaona ushuzi unaoimbwa. Hadi leo hii wimbo wa SEYA ni hitsong ya kwenye sherehe hasa harusi.
Na sio wanamuziki wapya tu hata wakongwe waliokuwepo zamani hadi leo wameshindwa kutoa vitu vikali kama walivyowahi kuvitoa mwanzoni. Je tatizo ni nini? PESA. Tatizo ni pesa. Hii kitu imetuvuruga. Yaani mtu anaimba chochote ili mradi ataingiza pesa. Raia nao hawajali tena maadili wanachotaka ni burudani tu kwa namna yoyote.
Na kwa tulipofikia hakuna kitu tunaweza fanya kubadilisha hii hali zaidi ya kuacha tu watu wajiimbie wanavyoweza cha msingi wanapata riziki. Ni tatizo la dunia nzima sio Tanzania tu.