Muziki wa taarabu ulipotokea hadi kufika Afrika ya Mashariki

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Mwaka 1850 wakazi waliokuwa wakiishi katika pwani ya afrika mashariki kuanzia mto juba nchini Somalia mpaka msumbiji, walikuwa wakiimba mashairi yao yenye kusifu viongozi wao na familia zao.

Tukimaanisha kuwa thamani ya muziki au kazi za mziki wenye radha ya pwani ulikuwepo hata kabla ya mwaka 1850. Na kuna ushahidi wa kutosha juu ya uwepo wa mashairi ya kiswahili hata kabla ya ujio wa waarabu.

Licha ya kwamba mashairi hayo ya waswahili yaliathiriwa sana na tamaduni za kiarabu lakini bado lugha ya kiswahili ilikuwepo na ilitumika katika mashairi ,mfano mzuri ni Fumo lyongo na utenzi wa "mwana kupona".

Historia ya chimbuko la muziki wa taarabu ipo kama ifuatavyo; wakati Zanzibar ikiwa chini ya Sultani Said Sayyid, kuanzia miaka ya 1840, kulikuwa na mabadiliko makubwa katika utamaduni wa waswahili.

Na ifahamike kuwa masultani baada ya kazi walipenda sana kuimbiwa mashairi na kulikuwa na taratibu za kualika watu mbalimbali kuja kuburudisha masultani wa Zanzibar ndani na nje ya Zanzibar.

Ndipo miaka ya 1970, alialikwa mwimbaji wa taarabu kutoka misri ambaye alipata nafasi ya kuwaburudisha masultani wa Zanzibar, Kijana huyo toka misri ambaye jina lake halikufahamika, aliweza kukonga nyoyo za masultani wa Zanzibar, kwani aina ya muziki huo ulikuwa ni mzuri sana.

Masultani walitokea kuupenda sana muziki huo uliokuwa ukiimbwa na Kijana huyo kutoka misri, kwa namna ulivyokuwa ukiimbwa na namna ya watu wanavyocheza kwa polepole, huku kukisikika ala za mziki zilizokuwa zikitoa sauti Nzuri na zenye kukonga nyoyo za wasikilizaji.
Na mara baada ya mwaliko huo kwisha Kijana huyo alirudi kwao misri huku akiwa na zawadi nyingi alizopewa na Sultani wa Zanzibar wa wakati huo.

Mambo yakaja kubadilika Zanzibar chini ya Sultani Barghash kwenye miaka ya 1870, ambapo alimwagiza Kijana aliyefahamika kwa jina la Muhammed Ibrahim, kwenda misri kujifunza mziki huo wenye kukonga nyoyo za masultani.

Na aliporudi aliwafundisha Vijana wengine na wakaunda kundi la taarabu hapo hapo Zanzibar miaka ya 1890,

Na wakati huo kundi la Kijana huyo likizidi kuendelea kisiwani hapo, kukaibuka Vijana wengine waliotokea kuupenda mziki huo na kuanza kujifunza zaidi.
Mpaka kufikia miaka ya 1905, kuliundwa kundi jingine la taarabu lililojulikana kama Akhwan- safa.

Kundi hilo lilihusisha wanamuziki wa kiarabu na walitumia lugha ya kiarabu, na walikuwa wakitoa burudani maeneo ya Darajani klabu,katika mji wa mawe( stone Town), watu Wengi walilipenda kundi hili la mziki wa taarabu na kusikika kila kona ya mji hapo Zanzibar.
Mambo hayakuishia hapo ,kwani miaka ya baadae hasa kwenye miaka ya 1908, kukaundwa kundi jingine lililofahamika kwa jina la "Naadi Shuba " ambalo pia lilikuwa na wanamuziki wa kiarabu waliotokea visiwa vya Komoro na wao pia walitumia lugha ya kiarabu .

Kama ilivyo kwa makundi yaliyotangulia, kundi hilo lilipendwa sana kwa sababu lilitumia lugha ya kiarabu ambayo ndio waliyotumia watawala wa maeneo hayo. Mabadiliko makubwa yalikuja kutokea kwenye miaka ya 1920, baada ya kuundwa kundi la taarabu lililohusisha wanamuziki wa kiswahili, kundi hilo lilikuja kupendwa sana na watu Wengi pale Zanzibar na afrika mashariki kwa ujumla. Na sababu ya kupendwa ni kutokana na matumizi ya lugha ya kiswahili ambayo inaeleweka na wakazi Wengi waliokuwa wakiishi kisiwani hapo.

Kundi hili lilianzishwa na mwanamuziki mkongwe wa taarabu aliyefahamika kama Siti Binti Saad ( aliyezaliwa katika kijiji cha kisaumi na baadae kuja mjini baada ya kugundulika kuwa na sauti Nzuri kwa ajili ya nyimbo za taarabu).

Mwanamuziki huyu alipendwa kutokana na sauti yake na uwezo wa kuimba kwa lugha tatu, yaani kiswahili, kiarabu, na kihindi.

Yeye akiwa na kundi lake, waliweza kurekodi albamu yao ya kwanza Mwaka 1930 huko nchini India ,na jambo la kufahamu ni kwamba kulikuwa na mabadiliko ya mambo yaliyokuwa yakiimbwa kwenye mBi wa taarabu.

Kwa mfano wakati huo (1930), mziki wa taarabu ulikuwa ukiimba mambo ya mapenzi lakini kipindi cha Uhuru (1905-1960) ulitumika kisiasa zaidi.

Na mara baada ya Uhuru mziki huu, uliweza kufika maeneo ya Tanzania bara hasa yale maeneo ya pwani kama Dar es salaam na Tanga, ambayo kwa Tanga kulikuwa na mwanamuziki kama Bi shakira, na kusambaa kwa mziki huu Tanzania bara kulitokana na uwepo wa wanamuziki mahiri wa taarabu kama kina Bibi kidude.

Kwa ujumla mpaka sasa mziki wa taarabu hasa wa kiswahili unapendwa sana na baadhi ya watu nchini Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla. Na wanamuziki wa taarabu kwa sasa na hata hapo awali wanaheshimika na kujipatia mafanikio makubwa katika maisha yao.

Mafanikio hayo yanakuja Kutokana na kuwa na mashabiki Wengi ambao hugharamia kununua CD za mziki wa taarabu au wakati mwingine kuhudhuria matamasha ya mziki wa taarabu. Wapo wanamuziki Wengi sana Baadhi yao ni Khadija kopa ( malikia wa taarabu) mzee yusufu( ameacha mziki) na Isha Mashauzi.

Hiyo ni historia fupi ya TAARAB kutoka lugha ya kiarabu hadi kiswahili na tumepata kufahamu na kuondoa sintofahamu ya miziki wa taarabu ilitokea wapi.
 
Kama ilivyo kwa makundi yaliyotangulia, kundi hilo lilipendwa sana kwa sababu lilitumia lugha ya kiarabu ambayo ndio waliyotumia watawala wa maeneo hayo.
Mabadiliko makubwa yalikuja kutokea kwenye miaka ya 1920, baada ya kuundwa kundi la taarabu lililohusisha wanamuziki wa kiswahili, kundi hilo lilikuja kupendwa sana na watu Wengi pale Zanzibar na afrika mashariki kwa ujumla. Na sababu ya kupendwa ni kutokana na matumizi ya lugha ya kiswahili ambayo inaeleweka na wakazi Wengi waliokuwa wakiishi kisiwani hapo.

Kundi hili lilianzishwa na mwanamuziki mkongwe wa taarabu aliyefahamika kama Siti Binti Saad ( aliyezaliwa katika kijiji cha kisaumi na baadae kuja mjini baada ya kugundulika kuwa na sauti Nzuri kwa ajili ya nyimbo za taarabu).
Mwanamuziki huyu alipendwa kutokana na sauti yake na uwezo wa kuimba kwa lugha tatu, yaani kiswahili, kiarabu, na kihindi.
Yeye akiwa na kundi lake, waliweza kurekodi albamu yao ya kwanza Mwaka 1930 huko nchini India ,na jambo la kufahamu ni kwamba kulikuwa na mabadiliko ya mambo yaliyokuwa yakiimbwa kwenye mBi wa taarabu.
Kwa mfano wakati huo (1930), mziki wa taarabu ulikuwa ukiimba mambo ya mapenzi lakini kipindi cha Uhuru (1905-1960) ulitumika kisiasa zaidi.

Na mara baada ya Uhuru mziki huu, uliweza kufika maeneo ya Tanzania bara hasa yale maeneo ya pwani kama Dar es salaam na Tanga, ambayo kwa Tanga kulikuwa na mwanamuziki kama Bi shakira, na kusambaa kwa mziki huu Tanzania bara kulitokana na uwepo wa wanamuziki mahiri wa taarabu kama kina Bibi kidude.

Kwa ujumla mpaka sasa mziki wa taarabu hasa wa kiswahili unapendwa sana na baadhi ya watu nchini Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla.
Na wanamuziki wa taarabu kwa sasa na hata hapo awali wanaheshimika na kujipatia mafanikio makubwa katika maisha yao.

Mafanikio hayo yanakuja Kutokana na kuwa na mashabiki Wengi ambao hugharamia kununua CD za mziki wa taarabu au wakati mwingine kuhudhuria matamasha ya mziki wa taarabu. Wapo wanamuziki Wengi sana Baadhi yao ni Khadija kopa ( malikia wa taarabu) mzee yusufu( ameacha mziki) na Isha Mashauzi.
Hiyo ni historia fupi ya TAARAB kutoka lugha ya kiarabu hadi kiswahili na tumepata kufahamu na kuondoa sintofahamu ya miziki wa taarabu ilitokea wapi.
= ladha.
 
sio kwa ubaya lakini huu mziki bwana ni wa watu wa pwani mwanzo nilidhani kwa wanawake tu lakini nimekuja kukuta uku zanzibar vidume vinakula taarabu halafu safi tu 😀
 
Mwaka 1850 wakazi waliokuwa wakiishi katika pwani ya afrika mashariki kuanzia mto juba nchini Somalia mpaka msumbiji, walikuwa wakiimba mashairi yao yenye kusifu viongozi wao na familia zao.

Tukimaanisha kuwa thamani ya muziki au kazi za mziki wenye radha ya pwani ulikuwepo hata kabla ya mwaka 1850. Na kuna ushahidi wa kutosha juu ya uwepo wa mashairi ya kiswahili hata kabla ya ujio wa waarabu.

Licha ya kwamba mashairi hayo ya waswahili yaliathiriwa sana na tamaduni za kiarabu lakini bado lugha ya kiswahili ilikuwepo na ilitumika katika mashairi ,mfano mzuri ni Fumo lyongo na utenzi wa "mwana kupona".

Historia ya chimbuko la muziki wa taarabu ipo kama ifuatavyo; wakati Zanzibar ikiwa chini ya Sultani Said Sayyid, kuanzia miaka ya 1840, kulikuwa na mabadiliko makubwa katika utamaduni wa waswahili.

Na ifahamike kuwa masultani baada ya kazi walipenda sana kuimbiwa mashairi na kulikuwa na taratibu za kualika watu mbalimbali kuja kuburudisha masultani wa Zanzibar ndani na nje ya Zanzibar.

Ndipo miaka ya 1970, alialikwa mwimbaji wa taarabu kutoka misri ambaye alipata nafasi ya kuwaburudisha masultani wa Zanzibar, Kijana huyo toka misri ambaye jina lake halikufahamika, aliweza kukonga nyoyo za masultani wa Zanzibar, kwani aina ya muziki huo ulikuwa ni mzuri sana.

Masultani walitokea kuupenda sana muziki huo uliokuwa ukiimbwa na Kijana huyo kutoka misri, kwa namna ulivyokuwa ukiimbwa na namna ya watu wanavyocheza kwa polepole, huku kukisikika ala za mziki zilizokuwa zikitoa sauti Nzuri na zenye kukonga nyoyo za wasikilizaji.
Na mara baada ya mwaliko huo kwisha Kijana huyo alirudi kwao misri huku akiwa na zawadi nyingi alizopewa na Sultani wa Zanzibar wa wakati huo.

Mambo yakaja kubadilika Zanzibar chini ya Sultani Barghash kwenye miaka ya 1870, ambapo alimwagiza Kijana aliyefahamika kwa jina la Muhammed Ibrahim, kwenda misri kujifunza mziki huo wenye kukonga nyoyo za masultani.

Na aliporudi aliwafundisha Vijana wengine na wakaunda kundi la taarabu hapo hapo Zanzibar miaka ya 1890,

Na wakati huo kundi la Kijana huyo likizidi kuendelea kisiwani hapo, kukaibuka Vijana wengine waliotokea kuupenda mziki huo na kuanza kujifunza zaidi.
Mpaka kufikia miaka ya 1905, kuliundwa kundi jingine la taarabu lililojulikana kama Akhwan- safa.

Kundi hilo lilihusisha wanamuziki wa kiarabu na walitumia lugha ya kiarabu, na walikuwa wakitoa burudani maeneo ya Darajani klabu,katika mji wa mawe( stone Town), watu Wengi walilipenda kundi hili la mziki wa taarabu na kusikika kila kona ya mji hapo Zanzibar.
Mambo hayakuishia hapo ,kwani miaka ya baadae hasa kwenye miaka ya 1908, kukaundwa kundi jingine lililofahamika kwa jina la "Naadi Shuba " ambalo pia lilikuwa na wanamuziki wa kiarabu waliotokea visiwa vya Komoro na wao pia walitumia lugha ya kiarabu .

Kama ilivyo kwa makundi yaliyotangulia, kundi hilo lilipendwa sana kwa sababu lilitumia lugha ya kiarabu ambayo ndio waliyotumia watawala wa maeneo hayo. Mabadiliko makubwa yalikuja kutokea kwenye miaka ya 1920, baada ya kuundwa kundi la taarabu lililohusisha wanamuziki wa kiswahili, kundi hilo lilikuja kupendwa sana na watu Wengi pale Zanzibar na afrika mashariki kwa ujumla. Na sababu ya kupendwa ni kutokana na matumizi ya lugha ya kiswahili ambayo inaeleweka na wakazi Wengi waliokuwa wakiishi kisiwani hapo.

Kundi hili lilianzishwa na mwanamuziki mkongwe wa taarabu aliyefahamika kama Siti Binti Saad ( aliyezaliwa katika kijiji cha kisaumi na baadae kuja mjini baada ya kugundulika kuwa na sauti Nzuri kwa ajili ya nyimbo za taarabu).

Mwanamuziki huyu alipendwa kutokana na sauti yake na uwezo wa kuimba kwa lugha tatu, yaani kiswahili, kiarabu, na kihindi.

Yeye akiwa na kundi lake, waliweza kurekodi albamu yao ya kwanza Mwaka 1930 huko nchini India ,na jambo la kufahamu ni kwamba kulikuwa na mabadiliko ya mambo yaliyokuwa yakiimbwa kwenye mBi wa taarabu.

Kwa mfano wakati huo (1930), mziki wa taarabu ulikuwa ukiimba mambo ya mapenzi lakini kipindi cha Uhuru (1905-1960) ulitumika kisiasa zaidi.

Na mara baada ya Uhuru mziki huu, uliweza kufika maeneo ya Tanzania bara hasa yale maeneo ya pwani kama Dar es salaam na Tanga, ambayo kwa Tanga kulikuwa na mwanamuziki kama Bi shakira, na kusambaa kwa mziki huu Tanzania bara kulitokana na uwepo wa wanamuziki mahiri wa taarabu kama kina Bibi kidude.

Kwa ujumla mpaka sasa mziki wa taarabu hasa wa kiswahili unapendwa sana na baadhi ya watu nchini Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla. Na wanamuziki wa taarabu kwa sasa na hata hapo awali wanaheshimika na kujipatia mafanikio makubwa katika maisha yao.

Mafanikio hayo yanakuja Kutokana na kuwa na mashabiki Wengi ambao hugharamia kununua CD za mziki wa taarabu au wakati mwingine kuhudhuria matamasha ya mziki wa taarabu. Wapo wanamuziki Wengi sana Baadhi yao ni Khadija kopa ( malikia wa taarabu) mzee yusufu( ameacha mziki) na Isha Mashauzi.

Hiyo ni historia fupi ya TAARAB kutoka lugha ya kiarabu hadi kiswahili na tumepata kufahamu na kuondoa sintofahamu ya miziki wa taarabu ilitokea wapi.
kwa hiyo 1970,Zanzibar kulikuwa na masultan?
 
Back
Top Bottom