DOKEZO Mv Magogoni imechoka

DOKEZO Mv Magogoni imechoka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Moshi25

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,555
Reaction score
4,118
Kiukweli Mv Magogoni imechoka imechakaa Ina mwendo wa jongoo inatia aibu sana hii nchi. Nusu saa nzima kutoka Kigamboni hadi Kivukoni. Yani wakati ukipanda unatabasamu unaona naenda paleee mjini pazuri ila muda unaenda unagundua kuwa hufiki mwisho hadi baada ya saa moja Sasa unajaa upepo taratibu na wakati ukishuka tayari umenuna umechukia una hasira na Kila alie mbele yako!!
Kivuko hiki kwasasa kupaki tu robo saa.

Kweli maendeleo si kitu chetu. Li kivuko limechakaa limejaa kutu tunalo tu hadi lizamishe watu ndo tuseme limechoka!

Kawaida ya watu weusi na maskini ni hivi yani wanasubiri siku Mv Magogoni ifikie mwisho wa matumizi kwa kuzimika katikati ya bahari na kutoboka na kujaza maji na kuua wapiga kura wa Bimkubwa!

Soma: Hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni

Hivi Bakhresa Hana uwezo wa kujaza SeaTaxi kumi hiyo Mv Magogoni ibebe magari tu mbona duniani tunateseka sana? Kuna majitu bongo yanayofanya maamuzi siku yakifa ni jehannam direct maana yanajali pesa kuliko uhai za watu!

Bimkubwa Samia tunakupenda sana na kukuombea sana tunaomba utupie macho Mv Magogoni iwekwe injini mpya au waitupie makumbusho ya taifa. Haifai inatia aibu sana nchi tajiri kuwa na mavivuko yamejaa kutu na injini za boda boda!

Watu wanachelewa makazini na wagonjwa sidhani kama wanatoboa wakiona tu kivuko Mv Magogoni wanaingia kwenye COMA! maana kuvuka tu saa nzima!
 
Mbona niliskia linapelekwa taratb ili Azam apige pesa
 
Back
Top Bottom