DOKEZO Mvua ikinyesha Stendi Kuu ya Magufuli, maji yanatuama sehemu ya kuegesha mabasi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nimejiuliza hivi Wakandarasi wanaojenga vituo vya mabasi huwa wanachaguliwa kwa kuangalia vigezo gani?

Nasema hivyo kwa kuwa vituo vingi huwa vizuri vikiwa vipya tu baada ya muda changamoto mbalimbali zinaanza kujitokeza.

Vingine huwa vinakuwa vibovu au havikidhi vigezo kuanzia mwanzo kabisa, mnakumbuka Stendi ya Kibaha ile mpya, wakati wa uzinduzi wake Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais aliweka ngumu kukizindua kwa kile kilichodaiwa hakikukidhi viwango stahiki.

Baada ya hapo nije kwenye hoja ya sasa, mfano Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi Mwisho hapa Dar es Salaam, nashangaa mvua zikinyesha maji yanatuama ndani ya eneo la mabasi na hata mahali yanapopaki mabasi kunajaa maji pia.

Ninachojiuliza waliojenga hawakujua kama kulikuwa na uhitaji wa njia za maji maeneo hayo?




 
Hamna banaa hiyo iko incorparated na design kwa ajili ya machinga wanawe na wafuge samaki
 
Tz kila kinachofanyika ni tktk tu
Alafu utasikii ohh hii stendi ndiyo
Bora kwa africa

Ova
 
Ila yamependezea macho, shidaa ni ukiwa hapo live, ukute yali dizainiwa hivyo kupapendezesha, nani anajua😉.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…