Mvua inayonyesha inataka kuniharibia zoezi la upauji

Planet FSD

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2019
Posts
455
Reaction score
948
Habari ya muda huu wakuu?

Nina kajumba kangu ambako nilikuwa nimemaliza kupaua jana. Nilipanga jumatatu nikafate mabati ili nije kumalizia lakini naona leo mvua inanyesha, jambo ambalo limenikosesha raha kwa sababu kwa ufuatiliaji wangu humu nimeona watu wengi wanasema mbao zikinyeshewa afu zikakauka zitapinda.

Nimemuuliza fundi amenihakikishia tuko salama, zikinyeshewa siku moja sio mbaya. Je, hili ni kweli wadau? Anasema labda mvua inyeshe mwezi mzima ndo hapo zinaweza kupinda.
 
Hata zikinyeshea mwezi, haina shida.
 
Habari ya muda huu wakuu? Nina kajumba kangu ambako nilikuwa nimemaliza kupua jana. Nilipanga jumatatu nikafate mabati ili nije kumalizia lakini naona leo mvua inanyesha, jambo ambalo limenikosesha raha kwa sababu kwa ufuatiliaji wangu humu nimeona watu wengi wanasema mbao zikinyeshewa afu zikakauka zitapinda. Nimemuuliza fundi amenihakikishia tuko salama, zikinyeshewa siku moja sio mbaya. Je, hili ni kweli wadau? Anasema labda mvua inyeshe mwezi mzima ndo hapo zinaweza kupinda
Yuko sahihi ondoa hofu.
 
Usiwaze kabisa hazina shida mvua yenyewe ni ya kupita inasindikiza baridi tu wala msimu wake
 
Habari ya muda huu wakuu? Nina kajumba kangu ambako nilikuwa nimemaliza kupua jana. Nilipanga jumatatu nikafate mabati ili nije kumalizia lakini naona leo mvua inanyesha, jambo ambalo limenikosesha raha kwa sababu kwa ufuatiliaji wangu humu nimeona watu wengi wanasema mbao zikinyeshewa afu zikakauka zitapinda. Nimemuuliza fundi amenihakikishia tuko salama, zikinyeshewa siku moja sio mbaya. Je, hili ni kweli wadau? Anasema labda mvua inyeshe mwezi mzima ndo hapo zinaweza kupinda
Usijal Mkuu, haziwezi kupinda kwa mvua ya 1 week
 
Ahsanteni sana wakuu. Nimewaelewa. Mmenisaidia kucalm down.
 
Kapicha ka nyumba basi ili tuone hatua uliyofikia tukupongeze
JamiiForums384951428.jpg
 
Habari ya muda huu wakuu? Nina kajumba kangu ambako nilikuwa nimemaliza kupua jana. Nilipanga jumatatu nikafate mabati ili nije kumalizia lakini naona leo mvua inanyesha, jambo ambalo limenikosesha raha kwa sababu kwa ufuatiliaji wangu humu nimeona watu wengi wanasema mbao zikinyeshewa afu zikakauka zitapinda. Nimemuuliza fundi amenihakikishia tuko salama, zikinyeshewa siku moja sio mbaya. Je, hili ni kweli wadau? Anasema labda mvua inyeshe mwezi mzima ndo hapo zinaweza kupinda
Kuna jamaa aliagiza mabati nje ya nchi, wakati akiyasubiri alikuwa ameshapita mbao tayar,,,,, zilinyeshewa tangu September mwaka jana amekuja kupaua May this year
 
Ndio kuna mda utapiga bati vizuri ila sasa wakati zinakauka zitaweka mawimbi nishawahi ona hii. Alafu mbao zina dawa sasa zikinyeshewa na mvua dawa inapungua especially dawa hizi zinapigwa juu ya mbao. Jitahidi sana upaue mafundi wanaangalia kula usipofanya hivyo baadae misumari itaachia baadhi ya sehemu. .
 
Kuna nyumba nimeiona ina miezi 7 haina bati na mbao hazijapinda
 
Back
Top Bottom