Mvua Morogoro: Shule zilizo maeneo hatarishi zatakiwa kufungwa kwa muda

Mvua Morogoro: Shule zilizo maeneo hatarishi zatakiwa kufungwa kwa muda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kunyesha kwa mvua kubwa Mkoani Morogoro kuanzia usiku wa kuamkia Januari 13, 2022 hasa katika maeneo ya Kihonda, Mafisa na Soko Kuu la Kingalu.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando amesema hakuna taarifa ya kifo ila kuna uharibifu wa mali na kuwa shule ameagiza Walimu Wakuu wafunge shule zilizo maeneo hatarishi hadi hali ya usalama iwe nzuri.

Mvua hizo zimesababisha mafuriko, nyumba kubomoka, vitu kusombwa, Watoto kuokolewa baada ya kubebwa na maji, pia kujitokeza kwa foleni ya magari katika Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma.

Naye, Kaimu kamanda Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Morogoro, Emmanuel Ochieng amesema wameokoa watu 48 waliokuwa wamezingirwa na maji katika maeneo ya Kata ya Kihonda, kati yao Watoto ni 39 na Watu Wazima 9.
 
Yapaswa kuwa makini kwani maji ni hatari haswa kwa wanafunzi. Pongezi kwa mkuu wa wilaya .
 
Majengo Yanatumiwa Na Watu Wengi Lazima Yahakikiwe Iwapo Bado Ni Imara Kwa Matumizi Ila Hali Tete Mpaka Barabara Kuu Ilifungwa
 
Aibu mafuriko mpka mjini miundombinu mibovu


Sasa soko kuu pale si lipo karibu na mfereji mkubwa umejengwa


Huko mafisa sawa ni uswahilini uliopo katika ya mji hakuna plan ya nyumba
 
Back
Top Bottom