Mvua ya samaki hunyesha nchini Honduras.

Mvua ya samaki hunyesha nchini Honduras.

Hii habari hunifanya nikumbuke kwenye miaka ya 98 bro yetu akitoka machungani saa7 mchana alikuja na kambale mkubwa sana akidai kamuona tu huko mlimani baada ya mvua kubwa kunyesha. Hakuna aliyeamini na samaki yule alitupwa wakiambatanisha na imani za kishirikina.

Kwa maelezo yake alikuwa anachunga mara mvua kubwa ikaanza kunyesha hadi maji kuanza kuteremka kwa wingi kwenda bondeni na baada ya mvua kukata tu haikuchukua muda mrefu sana kukata basi akawa anaenda kuswa ng'ombe wao walikuwa2 na jamaa mwingine yeye aliogopa hata kumchukua.

Wakiwa wanaenda ghafla wakamuona yule kambale kwenye matuta na hapakuwa na chanzo cha maji labda waseme huyu alikuwa anafuata maji. Wakaanza kushauriana na kila mmoja alikataa kumchukua na mwisho kabisa bro akaamua aje naye hadi nyumbani.
 
Hili tukio linatokea kila mwaka kwa miaka zaidi ya 100, wanasayansi hawajapata conclusive answer.

Sasa anatokea mwanasayansi kutoka Namtumbo na kuanza kubisha 😅😅😅
 
Ni kweli kabisa hayo matukio hutokea na umeandika vizuri kabisa kuwa kati ya mwezi Mei na Jul kuna kuwa na mvua kubwa na dhoruba kali; Kimsingi hao samaki husombwa na hiyo dhoruba kutoka baharini na kutupwa mitaani

Natumaini unajua nguvu ya dhoruba ya cyclone ile yaweza kunyanyua hata gari sasa ikitokea baharini yaweza kunyanyua maji mengi kwa mstari wa kwenda juu ambapo hayo maji huambatana na kila kiumbe kilicho kwenye eneoo husika.... baadae yakiangua ndio hapo samaki nk nk hyonekana mitaani
HILI NDIO JIBU SAHIHI HONGERA MKUU
 
Back
Top Bottom