GE2025 Mvua yatibua uzinduzi wa kampeni za Chama cha Kijamii (CCK)

GE2025 Mvua yatibua uzinduzi wa kampeni za Chama cha Kijamii (CCK)

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Unaweza kusema mvua imetibua uzinduzi wa kampeni za Chama cha Kijamii (CCK) zinazoendelea leo Jumamosi, Agosti 30, 2025, katika viwanja vya Kwa Tesha, Mbagala Kijichi jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, licha ya mvua hizo, wafuasi wa chama hicho waliendelea kubaki kwenye matenti yaliyokuwa uwanjani wakisubiri mvua ipungue ili kuendelea na shamrashamra za uzinduzi wa kampeni hizo.

Waandishi wa habari waliokuwa wakirekodi matukio ya kampeni hiyo walijikuta katika wakati mgumu kwani vifaa vyao vya kazi ikiwemo kamera vilikuwa katika hatari ya kulowa na mvua lakini walifunika na miamvuli na kazi ikaendelea.

Katika uzinduzi huo, CCK inamnadi mgombea wake wa urais David Mwaijojele pamoja na mgombea mwenza wake Masoud Ally Abdallah, huku kaulimbiu ya chama hicho ikiwa ni "Mabadiliko ni sasa, Mabadiliko ni sisi."

Aidha mkutano huo uliokuwa uanze saa 8:00 mchana lakini hadi kufikia saa 10:30 jioni ulikuwa bado haujaanza huku wagombea wakisubiriwa kufika katika eneo hilo.


Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom