Mvua za kujaza mabwawa ya umeme ndo nitabiriwa kuanza kuanzia Desemba 1?

Mvua za kujaza mabwawa ya umeme ndo nitabiriwa kuanza kuanzia Desemba 1?

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825

Tahadhari mvua kubwa mikoa saba nchini​

Dar es Salaam. Baadhi ya maeneo katika mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro na Mtwara yanatarajia kupata mvua juu ya kiwango kwa siku mbili kuanzia leo Desemba 1, 2023, hivyo wakazi wa maeneo hayo wameombwa kuchukua tahadhari.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya utabiri wa hali ya hewa wa siku tano zijazo kuanzia Novemba 30, 2023 uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo iliyotolewa Novemba 30, 2023 inaeleza kuwa, mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma inatarajiwa kupata mvua hiyo, Desemba Mosi.

Huku siku siku inayofuata, mikoa ya Morogoro, Ruvuma na Mtwara nayo inatarajiwa kupata mvua hizo.

“Mvua hii itasababisha baadhi ya makazi kuzungukwa na maji na kuathiri baadhi ya shughuli za kiuchumi.

TMA imekuwa ikitoa taarifa kila wakati kwa wananchi kuhakikisha hatua muhimu zinafuatwa ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Mwananchi
 
Kwa hapa Dar tumeichoka sasa, kwanza hatuna dili nayo inyeshee huko huko
 
Tanesco ni wahuni tu, sina hamu nao, na hili joto wanakulaza usiku masaa sita bila umeme hawana huruma.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom