Mvua zaendelea kuwa kilio kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam

Mvua zaendelea kuwa kilio kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam

Sisi ni utalii, ndege ya mizigo, kuwaita mafisadi stupid, misafara mirefu ya bibie, kumsifu sana bibie kupitia TBC, kuwawezesha zenji, kushangilia ya Yanga na Simba, kupiga vipicha na vitoto, na nini sijuwi.
Mambo ya barabara kujaa maji mtajijuwa, tuko biz na hayo!😭😭😭😭
 
Kusifu ni laisi zaidi kuliko hayao uyasemayo
 
Bado mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam zimeendelea kuwa kilio kwa wakazi wake kutokana na adha ya usafiri wanayoipata kufuatia baadhi ya barabara kujaa maji.

Hayo yanathibishwa na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu wanaodai maeneo mengi yaliyokuwa sugu kwa kujaa maji kipindi cha mvua kama Jangwani na Kamata yameendelea na hali hiyo jambo linaloleta kero kwao.

Mvua hizo zilizoanza kunyesha kuanzia alfajiri ya kuamkia leo Juni 5, 2023 zimeleta madhara mbalimbali kwa wakazi wa jiji hili ikiwemo kushindwa kufika kazini kwa wakati.

Wakizungumzia changamoto hizo watumiaji wa barabara jijini hapa wamedai licha ya kujengwa kwa lami zimekuwa zikijaa maji kiasi kwamba hata watumiaji wa vyombo vya usafiri wanaogopa kupita.

“Eneo la Kamata limekuwa sugu limekuwa likitusababishia vyombo vyetu kama hizi pikipiki kuharibika,’’ amesema Joseph Stanley ambaye ni dereva wa bodaboda eneo la Kamata.
Miaka ya zamani Dar ilikua haina hili tatizo, kuanzia miaka ya 1985 ndio hili tatizo la maji kujaa bara barani, kabla ya hapo kulikuwa na miundo mbinu ya kutoa maji bara barani sasa ilipoanza kuziba ndio hili tatizo lilipoanza mpaka sasa limesha kuwa sugu
 
Usifananishe Dar ya mzungu na uswahili wa mtu mweusi
 
Back
Top Bottom