Mvua zinanyesha nchi nzima, mavuno kwa wingi yanavunwa na kelele za "Bashe Funga Mipaka" zimekwisha

Kuanzia Bashe amekuwa Waziri wa Kilimo msimamo wake ilikuwa ni kutofunga mipaka ili wakulima wapate bei nzuri ya mazao yao. Humu JF kuliandikwa nyuzi nyingi za kulaani kutofunga mipaka na kutabiri njaa kutokea Tanzania.

Kati ya Machi na Mei mikoa mingi sana wamevuna na bei zimeshuka chini. Na sasa tunapata mvua za kutosha kuanzia Mei hadi mwisho wa June 2023.

Wako wapi wale waliokuwa wanatoa macho kumuambia Bashe afunge mipaka ili chakula kisitoke?

Mkuu ni hii mvua inayonyesha leo hapa Dar ndio imekufanya uje na huu uzi?
 
Alikata miti zaidi ya Milioni 4. Halafu kumbuka kilawaida June siyo mwezi wa mvua. Mvua za vuli hunyesha katika miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba na mvua za masika hunyesha katika miezi ya Machi, Aprili na Mei.

Kitendo cha kupata mvua za masika mwezi June ni ishara ya mabadiliko ya tabia nchi. Athari za miti iliyokatwa bado zipo
Unazungumzia mabadiliko ya Tabia Nchi au Mabadiliko ya hali ya Hewa? Wewe ni Kiazi
 
Mkuu ni hii mvua inayonyesha leo hapa Dar ndio imekufanya uje na huu uzi?
Mvua zimenyesha sana mikoani kuanzia April hadi leo kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Mwanza, Arusha kwa ile niliyokuwa na uhakika.
 
Acha upotoshaji wa kijinga, kukatwa kwa miti wote tunaelewa kunaleta mabadiliko ya tabia nchi. Na mabadiliko ya tabia nchi sio lazima mvua isinyeshe tu, bali inaweza kunyesha kupita kiasi, awa ikanyyesha bila kufuata ratiba halisi, vimbunga nk. Labda useme wale wanaotoa elimu ya kuwa kukata miti kunasababisha ukame na mabadiliko ya tabia nchi ni waongo. Tukikubaliana kwenye hilo uje uendelee na huo utetezi wako wa Magufuli kukata hiyo miti.

Kama mimi upotoshaji wangu niwa kijinga basi wewe ulichoandika ni upu.mbavu bila kujua kama ni upu.mbavu!
 
Ungekuwa mkulima usingeandika huo utumbo.

Kulima sio sifa, na unatakiwa uelewe kwamba sio kila mahali hizivua zina impact, kwingine ni too much kwa mazao yanaoza, mwingine zimechelewa mazao yalikauka na hawajui zitaendelea kwa mda gani. Kqa kifupi wewe na ukulima wako ni vilaza. Haya kapalilie matikiti maji huko.
 
Mvua zimenyesha sana mikoani kuanzia April hadi leo kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Mwanza, Arusha kwa ile niliyokuwa na uhakika.
Mkuu mvua ni kweli zimenyesha, ila hilo neno sana hebu liondoe. Kuna sehemu nyingi tu hizo mvua zimenyesha bila mtiririko mzuri, ni kweli kuna siku zimenyesha nyingi hadi mafuriko, lakini sio kwa mtiririko mzuri wa kilimo. Mfano halisi ni huko Arusha. Ninakuambia hili nikiwa na ushahidi na nisemacho.

Huko Kanda ya kaskazini mvua imenyesha kwa mwenendo mbovu, ambao imegeuka kutokuwa rafiki kwa kilimo. Kwahiyo usidhani kama sehemu ilenyesha nyingi siku fulani, basi hiyo ni dalali ya mvua sahihi kwa kilimo. Ndio maana nikakuambia hii mvua ya leo Dar ndio imekufanya ufikie hitimisho hilo?
 
Kuanzia Bashe amekuwa Waziri wa Kilimo msimamo wake ilikuwa ni kutofunga mipaka ili wakulima wapate bei nzuri ya mazao yao. Humu JF kuliandikwa nyuzi nyingi za kulaani kutofunga mipaka na kutabiri njaa kutokea Tanzania.

Kati ya Machi na Mei mikoa mingi sana wamevuna na bei zimeshuka chini. Na sasa tunapata mvua za kutosha kuanzia Mei hadi mwisho wa June 2023.

Wako wapi wale waliokuwa wanatoa macho kumuambia Bashe afunge mipaka ili chakula kisitoke?
Hawaachagi ulalamishi hao
 
Hazina impact kwa nyie mnaoishi mijini kufanya kazi za kuuza ice cream, kusuka nywele wadada, kuuza viatu vya mtumba barabarani nk

Wwkulima wanajuwa walime nini

Uko sahihi kabisa mkulima wa matikiti
 
Kajionee Ifakara.
Huko unaambiwa Punga linaogelea mimaji hadi Mamba wamesogea Mashambani.
 
Kuanzia Bashe amekuwa Waziri wa Kilimo msimamo wake ilikuwa ni kutofunga mipaka ili wakulima wapate bei nzuri ya mazao yao. Humu JF kuliandikwa nyuzi nyingi za kulaani kutofunga mipaka na kutabiri njaa kutokea Tanzania.

Kati ya Machi na Mei mikoa mingi sana wamevuna na bei zimeshuka chini. Na sasa tunapata mvua za kutosha kuanzia Mei hadi mwisho wa June 2023.

Wako wapi wale waliokuwa wanatoa macho kumuambia Bashe afunge mipaka ili chakula kisitoke?
Unaonekana huna uelewa kabisa wa masuala ya kilimo.

Mazao makuu ya chakula kwa Watanzania ni mahindi, mpunga na maharage.

Mvua za sasa hazina msaada wowote kwenye mazao hayo, tena zinaharibu kabisa kidogo kilichokuwa kimepatikana. Mahindi kidogo yaliyopatikana, sahizi yamekauka na mengine hayajatolewa mashambani. Hayo sasa, kama mvua zitaendelea yataozea mashambani.

Siafiki suala la kufunga mipaka lakini ukweli ni kwamba mwaka huu kuna upungufu mkubwa sana wa mazao makuu ya chakula, na huenda, zaidi ya mwakajana. Bei jinsi zilivyo kwa sasa, tena wakati wa mavuno, ni juu zaidi kuliko mwakajana muda kama huu.

Mvua za sasa, kama zina msaada itakuwa ni kwenye mazao kama viazi vitamu na mihogo, ambavyo siyo mazao makuu ya chakula.
 
Hazina impact kwa nyie mnaoishi mijini kufanya kazi za kuuza ice cream, kusuka nywele wadada, kuuza viatu vya mtumba barabarani nk

Wwkulima wanajuwa walime nini
Hakuna.mkulima anayeweza kulima sahizi eti kwa sababu ya mvua zinazonyesha. Wanaolima sahizi wanategemea kumwagilia, siyo hizi mvua za siku chache.

Kwanza hizo mvua zipo tu Dar. Maeneo mengine karibu yote ni kukavu kabisa. Hakuna mvua. Tabora hakuna, Mwanza hakuna, Shinyanga hakuna, Same hakuna, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, ni manyunyu kidogo sana, Singida, Dodoma hakuna.
 
Alikata miti zaidi ya Milioni 4. Halafu kumbuka kilawaida June siyo mwezi wa mvua. Mvua za vuli hunyesha katika miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba na mvua za masika hunyesha katika miezi ya Machi, Aprili na Mei.

Kitendo cha kupata mvua za masika mwezi June ni ishara ya mabadiliko ya tabia nchi. Athari za miti iliyokatwa bado zipo
Kumbe ikikatwa miti mingi mvua zinanyesha sana.
 
Acha upotoshaji wa kijinga, kukatwa kwa miti wote tunaelewa kunaleta mabadiliko ya tabia nchi. Na mabadiliko ya tabia nchi sio lazima mvua isinyeshe tu, bali inaweza kunyesha kupita kiasi, awa ikanyyesha bila kufuata ratiba halisi, vimbunga nk. Labda useme wale wanaotoa elimu ya kuwa kukata miti kunasababisha ukame na mabadiliko ya tabia nchi ni waongo. Tukikubaliana kwenye hilo uje uendelee na huo utetezi wako wa Magufuli kukata hiyo miti.
Nitashangaa kama we jamaa una ELIMU hata ya form six.
 
Back
Top Bottom