Mvulana huyu kashangaza wengi siku ya jana kisa...

Mvulana huyu kashangaza wengi siku ya jana kisa...

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Pamoja sana wanajf.

Jana 21/10/2018 maeneo ya wilaya ya Ilemela - Mwanza, kuna mvulana au niseme dogo mmoja hivi alishangaza wengi, na hata wengine kuishia kucheka (nikiwemo Nahuja mie).

Tulikuta foleni kubwa ya magari eneo ambalo hata siku moja halina historia ya msongamano wa magari. Watu wakawa wanajiuliza kuna nini, wengine wakaenda mbali zaidi na kuhisi labda kuna ajali.

Baada ya kushuka kwenye magari tuone kuna nini huko mbele kinachosababisha foleni ndefu, oooooops! tukamshuhudia dogo anagalagala katikati ya barabara hali ambayo imefanya magari yashindwe kuendelea na safari.

Wengine wakasikika wakisema, "amekuwa kichaa". Lakini cha ajabu kukawa na vijana wengine pembeni mwa barabara ambao ni rika moja na yule aliyekuwa anagalagala barabarani walikuwa wanacheka sana,hadi machozi na makamasi yanawatoka.

Tukawauliza, vipi huyu wenzenu amekuwaje? wakatujibu kuwa, "ALIBET NA AMESHINDA KIASI CHA TSHS.1,850,000/=" Kijana mwingine akaongezea "JAMAA ALIBET MKEKA MKUBWA"...

Mfyuuuuuuu, watu tukafoka foka hapo, basi akanyanyuliwa wakamuweka pembeni mwa barabara magari yakaendelea na safari.
 
Mi ningekuwa dereva ningemgonga afe ili hela aliyoshinda itumike kwenye mazishi yake maana baadae asisumbue watu
hahaaah. alisababisha foleni ndefu, alikuwa ana galagala kama nyoka. hahahahahah
 
Kuna watu wapo inabidi tu waendelee kuwa na maisha ya umasikini ili waishi kwa amani na utulivu.
Huyo jamaa akipata pesa ndevu si atazikwa?
Mie kwanza niliwaza kuwa anaweza hata kusababisha vibaka nyumbani kwao, maana alishatangaza kuwa ana hela. Na wapambe walikuwa wameshaanza kumwambia wamsindikize home kwao akabidili nguo then waende mjini kuchukua hela kwa kuwa hiyo ni hela ndefu haitolewi na wakala ni mpaka ofisini kabisa kabisa. hahahah
 
Hahaha dah tafuta mawasiliano yake haraka unipatie awe ananiongoza kwenye kubeti
Sijui hata kama yuko salama, maana kulikuwa na kundi kubwa wanamwambia wamsindikize nyumbani kwako akabadili nguo then waende mjini kwenye ofisi kubwa ya hao wanaotoa hela. hahaahh. Kama hawajampora basi watakuwa wamezichea sana jana hizo hela
 
Back
Top Bottom